Ndugu wanachama wote wa CCM Manchester mnaombwa kuhudhuria uchaguzi wa kumchagua katibu atakayejaza nafasi ya ndugu Hamphrey Mhada anayerudi nyumbani Tanzania.
Uchaguzi huo utafanyika katika sherehe ya kumuaga Ndugu Hamphrey Mhada katika ukumbi wa
Manchester Bridge Club.
Namba 30 Palatine Road,
Withington,
M20 3JJ
Jumamosi tarehe 15 mwezi wa 11, saa12 jioni.
Kufika kwenu ndio kufanikisha shughuli hii.
Asanteni
Mwenyekiti
Mwenyekiti
Daudi Mwakimwagile
Nawapongeza sana kwa kuendeleza fikra za Kidumu chama huko UK. Naomba mnifahamishe mikakati yenu ama sera zenu hapa UK, nina maanisha activities zenu. Nitashkuru sana. ningependa kujiunga. Mdau
ReplyDeletejamani
ReplyDeletenafanya kazi Serikalini hapa Bongo tena katika Wizara nyeti sana ya Serikali na hata hapa nilipo natumia computer ya Serikali kuandika hii comment yangu lakini SIIPENDI SIIPENDI na tena NAICHUKIA CCM. Yaani sijui hata nisemeje!!!!!
sasa ninyi mnatuambia suala la uchaguzi mdogo wa CCM Manchester ili tufanyeje!!!!!!!acheni kutuboa bwana na kutuharibia siku asubuhiasubuhi hii
ovyo,hamna kazi!!!!!
Naungana na wewe kabisa.Hata mie nawashangaa sana.Au ndo mnataka kutafuta nafasi za kujiingiza kwenye hicho chama chenu kilichojaa wezi.Kama mtakuwa mmesahau ama mliondoka miaka mingi.Maana ya hicho Chama ni Chukua Chako Mapema.Kama hamna la kusema tafadhali Msitutie Kichefuchefu.Chama Kilikuwepo wakati wa Nyerere na si sasa.
ReplyDeleteWewe unayefanya kazi serikalini; iwapo unaichukia ccm kiasi hicho ni nini umefanya ndani ya uwezo wako kuleta mabadiliko. Au unadhani kuandika kwenye blogu ndio utaindoa ccm madarakani au kuibadilisha matendo yake...!!!
ReplyDeleteWee acha upumbavu, hujui hata kikwete anaisoma hii blog. anon ametoa mawazo yake na ndivyo uwazi aliotufundisha mkapa.Nyie watu wa UK mnadhani mkijipendekeza na CCM ndio mtapata kazi nzuri kwente serikali ya chi chi em bongo??? au ndio mtatanua kama watoto wa mafisadi hapo UK?????
ReplyDeleteNyinyi mnajifurahisha tu na kujiridhisha. chi chi em ina wajanja wake wapo hapa hapa bongo. nyie mtabakia na jina la chama tu na mashati ya kijani kwa wingiiii, ambayo mnajinunulia wenyewe, mambo mengine bwana ujinga mtupu.....
wewe anon 3.56pm una mawazo mafupi, wewe unafanyanini kupambana na matatizo yanayoikumba yetu. Umejunga chama gani? sio ubakie kupiga makelele tu kwenye hii globu. Na pia nakukmbusha kuwa kila mtanzania popote alipo ana haki ya kujiunga na chama chochote sasa watu wakiwa CCM wewe tafuta chama chochote cha upinzani ndio ikomboe nchi yako katka matatizo yanayotukabili, ama sivyo utabaki kupiga kelele tu kwenye blogu hamna unachokifanya
ReplyDeleteWatanzania wa Marekani ndio walinifurahisha pale walipokataa kabisa kufunguliwa kwa tawi la CCM, nadhani haya mambo ya CCM yako UK tu kwa walugawaluga.
ReplyDeleteHivi nyinyi ni watoto wa vigogo nini? CCM inavyoharibu eti bado mnajifanya kuendeleza CCM Uingereza, huo sio Unafiki?. Nahisi nyinyi ni watoto wa vigogo wa Serikali ya CCM Mmepelekwa huko kusoma na Mnataka kuiendeleza ili mje Kugombeza Uongozi CCM na nyinyi mharibu. Mtoto wa nyoka ni nyoka tu.
ReplyDeleteNiache kwenda kubeba box nije kwenye kikao ebooooooo...Acheni hizo nyinyi hivyo ndio vilivyowaleta hapa U.k ushamba wenu ni huko bongo hii nchi ya watu msitake kuleta mambo ya kishamba CCM CCM...CCM kitu gani nyinyi acheni mambo yenu hayo......Kaeni kwanza mufikirie nini mnafanya alafu mkiangalia kuna watu wazima hapo....Kwanza nimalizie kama kuna MENU nitakuja nikitoka box au sio Wakuu.......Pamoja
ReplyDeleteBasi huyo anayerudi bongo....anakwenda kugombea ubunge au ukuu wa wilaya sijui....kaka michuzi watch out wasije wakakuchukulia kiti chako hao....hawakawii kurudi na CV zao ....Katibu wa CCM manchester 2000- 2008......hehehhehehehehheeeh.....
ReplyDeleteWaheshimiwa, wasiwatishe na U-CCM wao wa Uingereza Uzunguni. Kwanza wanamuwakilisha nani???Wenywewe shida tuuuupu.Wabongo tumeamka hata mkija hampati kitu hapa. Subirini Muone jimbo la mbeya vijijini litavyochukuliwa na Chadema.Kama vile TANU na ASP viliungana na kuunda CCM. CCM inatakiwa ibadilike sasa hivi imekosa mwelekeooo .Just Imagine mwenyekiti wake anapigwa mawe!!!!!haaaa!!!sembuse nyie vimbelembele???
ReplyDeleteHuyo jamaa mwanga kweli kweli!! ( ni mawazo yangu tu mungu anisamehe). ana ndoto za kuwa kiongozi huko nyumbani. Anaondoka tu nasikia msiba wa ndg yetu aliyekuwa mbuge wa Mbeya vjj.
ReplyDeleteUsishangae utasikia kaibukia kwenye uchaguzi mdogo utakaotangazwa kurithi nafasi ya marehemu.
Mimi najiuliza sana, hivi hawa jamaa zetu hapa, wenyeviti na makatibu wa tawi na mashina wana agenda gani? kila unayeongea naye ana ndoto kuwa siku akirudi home atakuwa kiongozi. Najiuliza hapa UK kuna course za ubunge na uwaziri? Au huko kwenye matawi na mashina na mizizi mnafundishana hizo kozi!!
Huko nyumbani nasikia hata halmashauri kuu ya sisiem nayo imecharuka imechoshwa wajumbe kuraguliwa na mafisadi, sasa ni wanachama wote watashiriki kuchagua majina ya wagombea udiwani na wabunge, vipi raisi???
Sasa hivi visenti tunavyosevu huku tukavitumie kwa kuwasaidia walala hoi na sio kununulia kura.
Ni hayo tu.
Mdau hapo juu wa November 13, 2008 9:41 AM.
ReplyDeleteUmenifurahiiiiiiiiisha saaaaaaana, leo nimechekaaa sana du!!!!!!eti
Ndugu Hamphrey Mhada anayerudi nyumbani Tanzania. Anakuja zengea nafasi iliyoachwa wazi na marehemu, ama kweli kufa kufaana. tehe tehhhheeeeeeee.
Matani mengine bwana!!!!
Tatizo linakuja pale wanapo jaribu kuwazuga watu. Wanatumia ule ule uzembe wa baadhi ya wanasiasa wa ssm kudanya wananchi. Anyway, nasikia Manchester kuna text meseji inayotumwa kwa wabeba maboxi kuwataarifu sherehe ya kumuaga Katibu wa ssm. Wamekuja hapa kutangaza mkutano utakao fanyika saa ileile ya sherehe ili kuwabamba raia wengine ambao hawataki siasa.Huu ni uhuni wa hali ya juu. Yale yale ya viongozi wetu wa bongo
ReplyDelete