wote wamewekewa masharti ya dhamana kwamba kila mmoja atoe bilioni 3.9 keshi, wasalimishe hati za kusafiria, wasitoke nje ya dar na kila mmoja awe na wadhamini wawili ambao mahakama inabidi iridhike kuwa ni wa kuaminika.
hadi globu hii ya jamii inaingia mitamboni juhudi za kupata dhamana zilikuwa zinaendelea.
stori kamili inaandaliwa.
stay tuned
Yaani hawa ndio tuliwaamini kwamba watulindie uchumi wetu? Afrika kazi ipo na huyu mwingine si ndio alisemaga kwamaba tutakula hata majani lakini lazima tununue gulf stream
ReplyDeleteJamani wanatia huruma na kaunda suti zao ila wakome ni vizuri sana sheria ichukue mkondo wake
ReplyDeleteWAMEPENDEZA SANA.
ReplyDeleteDamn it. Fedha fedheha. Wamejifedhehesha. Hawana heshima tena waheshimiwa hawa.
ReplyDeleteOmbi kwa bunge na serikali kuanzia sasa ifute title ya Muheshimiwa kwa wabunge na mawaziri wote. Wabunge na mawaziri waitwe ndugu, bwana au bibi kwa sababu imedhihirika kwamba miongoni mwao wapo wasiojiheshimu, wasioheshimu dhamana yao, na wala hawastahili heshima.
Isiishie hapo waburuzwe mahakamani na sheria ichukue mkondo wake. wakibainika kuwa na makosa wafungwe na kufilisiwa mali zao zote walizozipata kwa wizi.
Bado Mkapa.
ReplyDeleteTeh teh teh
ReplyDeleteBwana Michuzi mie naomba Mungu awajalie wasipate dhamana ili huyo Yona aliyesema hakuna wa kumgusa ajue kuwa Mungu yupo na kila jambo lina mwisho wake na mwisho wa regime ya Pesa mbili na huyo Yona ndio hii.
Kwanza majina yao yanaonyesha usaliti. mfano
Pesa mbili = influence ya kupenda hela yani kila anachoearn anaona ni mbili.
Yona= Alitumwa ninawi akakimbilia tarshishi wote wasaliti
Now you are talking!!! Japo najua itakuwa ngumu sana kutumikia kifungo au hukumu itachukua muda mrefu sana. Bila shaka hata japo kitendo cha kuwapandisha kizimbani kitawafariji watz wapenda maendeleo na maisha bora kwa kila mtz. Tunahitaji japo sasa kusikia majina ya masangara ya coy ya Kagoda!!!
ReplyDeleteNi hayo 2.
Duuh!! Mawaziri ndani ya benchi ya korti watuhumiwa!!! Hutajozea kuona haya na wala si utamaduni wetu Watanzania. Taabu moja walimuiga pweza sasa wanajipalia makaa ya moto wao wenyewe!!! Bado hatuwahukumu maana ni watuhumiwa. Jambo la huzuni sana pale kiongozi aliyeaminika na wengi kufikwa na tuhuma kama hizi na hata kufikishwa mbele ya sheria kujibu tuhuma... tumekwenda kubaya sana. Isitoshe wapo ambao walikuwa katika Serikali ya awamu ya kwanza ya hayati Mwl. JK hawa tungetegemea kwamba walifuzu mafunzo ya uadilifu toka kwenye shule ya mwalimu... lakini wapi!!! (dRU)
ReplyDeleteMimi katika vyote vinavyoniuma sana, na si mimi tu hata Mwalimu hili alililamikia ni namna Yona alivyoshinikiza uuzwaji wa NBC. Athari yake kwa maisha ya watanzania kwa kweli ni kubwa sana.
ReplyDeleteTunaomba sheria ichukue mkondo wake kwa kila ovu walilolifanya na iwe ni fundisho kwa wengine wote wanaopewa dhamana ya kuwatumikia watanzania
Kama William Gallas - watu wengine wanatakiwa kutiwa adabu kidogo. Naamini watu hawa wataachiwa pamoja na kwamba kila mtu anajua ni vibaka waliokuhubu. Wakilala Segerea kwa wiki moja ni adhabu ya kutosha kwa sababu siamini kuwa watarejesha pesa - labda wauze hiyo migodi.
ReplyDeleteHaya, yetu macho na masikio!
ReplyDeleteKweli JK umeamua kutafuta dhamana ya wananchi hapo 2010...ukiende pale kerege daniel ana heka kama 200 ivi..ana kijiji makongo juu, damn lazima waonje joto ya jiwe na bado edo na mzee wa vijisenti
ReplyDeleteJK noma,nilijua jamaa anatumia mbinu za kikamanda tu kuhusu swala la epa,hii inaonesha kiasi gani JK amedhamiria kumaliza ufisadi nchi hii.brazo jk, 2010 ushindi asilimia 90.ccm daima
ReplyDeleteHongera JK sasa watanzania tunaanza kukuelewa , kweli sasa hv haumwwangalii nyani usoni.
ReplyDeleteSi mlitaka kujua huyo mdudu aitwae KAGODA?
ReplyDeletePesa Mbili Mramba ndio aliwokesesha wastaafu pesa zao kwa kufanya siri fomula ya malipo na kujichukulia madaraka ya kugawa yeye badala ya ofisi husika kwa mfano EAA wangepeleka pesa ATC walikokuwa wanafanyakazi wastaafu hao EAH wangepeleka THA nakadhalika hapo palijaa ufisadi mno na pesa kuliwa na wajanja wake ni mstaafu kwa uchungu mkubwa....
ReplyDeleteHawatii huruma chochote walifikiri waTZ tutakuwa mabwege hadi lini wao wakila hadi kufanya hospital hakuna dawa watu wanakufa kukosa dawa na wanafunzi kugoma kutokana na kukosa huduma za msingi.... wameleta taabu zote zinazomkabili JK hii leo... UNAWEZA KUMWIBIA MTU SI SERIKALI.... wengine pia wazibuliwe waache ubinafsi na kugombea vyeo ili washibishi matumbo yao tuuuu. MUNGU NDIO HAKIMU WA HAKI
ReplyDeleteDanny Yonah toa mdhamana kwa baba wewe siumejaa hela sio fresh mlinde mzee
ReplyDeleteYAANI HAWA NDO TULIKUWA TUNAWASUBIRI, TUAMBIENI BASI KAMA NI ISUE YA EPA NA STORY ZA KAGODA MAANA MIE NIKO KWENYE HII BLOG MPAKA HABARI KAMILI.....JK OYEEE, HUYU MTU SIO MCHEZO ANAUMA NA KUPULIZA.
ReplyDeleteMmmh time will tell , their face shows confidence can you read their mind?
ReplyDeleteBravo waliofanikisha hilo! Hivyo hivyo! Na wengine, na wengine, na wengine. Tushakula sana nyasi, hadi zimeota viunga matumboni, dege bovu likanunuliwa. We wacha kabisa.
ReplyDeleteKeep it up.
Aluta Continua.
Yaani unasubutu kuwaonea huruma hawa mabaradhuri walioifikisha Nchi yetu hapa tulipo? hawastahili huruma hata kidogo.Ni jeuri ya ufusadi ndiyo iliyokuwa inamfanya atuambie eti tutakula majani lakini hilo lindege lao watanunua,kiko wapi sasa!Hii ni laana hata kwa vizazi vyenu kwa mateso mnayowasababishia watanzania.Eee MUNGU wetu iokoe TANZANIA.
ReplyDeletehiyo ni sawa kabisa haiwezekani uchumi wa nchi umilikiwe na watu wachache
ReplyDeleteKudadadeki sasa tuone jeuri ya ankara hapo, hakyanani jamaa wakichoropoa dhamana kwenye huu msala naandamana World Bank na IMF watutoe kwenye list ya the poorest of the poor, hatuwezi kuwa ni mi-bilionea amongst ourselves halafu tunaitwa maskini wa kutupwa. Hivi hawa hawana Mungu nini? How do they really live and see others wanavyoteseka humu mabarabarani na wanapopita kwenye fuel-guzzling SUVs zao?
ReplyDeleteFolks hav been squandering hii nchi for so long jamani hebu tuamkeni sasa. Keko hapawafai, Segerea ndio ideal place hata kama sio remand prison!
Wadau imekaaje hiyo ya kumuita mtu MHESHIMIWA wakati ni MTUHUMIWA mbele ya Mhe. Hakimu?
ReplyDeleteSafi JK, kwa mtindo huu mafisadi mwaka huu watakoma, na bado. Tuko nyuma yako JK, hakuna kuleana hapa.
ReplyDeleteBig Sam
Wewe anony 25,2008 1:12pm eti 'wanatia huruma'!?
ReplyDelete'There can be no true friends without true enemies. Unless we hate what we are not, We cannot love what we are' quote from Micheal Dibdin's novel, Dead Lagoon.
Kwa kiswahili chepesi wale wote watakaotiwa hatiani na mahakama tuwaogope kama ukoma, hawa bado ni watuhumiwa lakini tuhuma zao ni za kuchukiza yaani kusaini mikataba mibovu n.k hivyo hawakuwa na mapenzi na nchi yao wala kwa wananchi waliowaamini kuwa wana mapenzi mema kuwapatia maisha bora kwa watanzania wote.
Hapo sasa tunaanza kuelewa kwa mbaaaaaali, lakini bado MKAPA,ROSTAM na JK mwenyewe!!
ReplyDeleteMpaka kieleweke!!!
Aaaah...jamani wabongo wenzangu, hii yote dana dana, hawa kesi yao tutasahaulishwa kama haikuwepo vile...mpaka sasa wapo nje kwa dhamana na yule mwingine pale anakunywa kahawa kibarazani wakati watoto wake wakicheza boli bolingo chumba cha chini...bado wanakula raha, 3.9billion shillings is peanut to them, they own hotels, they got big earning vitega uchumi...walahi hawa tutasahaulishwa!...big up JK though, naona unaosha for 2010.
ReplyDeleteHao jamaa walipokuwa matawi ya juu hawakutoa hata peasa kidogo ya kukarabati jengo la mahakama? ona sasa wamekalishwa kwenye mahakama iliyochubuka!! Ok, sheria ifuate mkondo
ReplyDeleteKama kulaga nyasi tulikulaga nao ni vema waonje ladha ya hizo nyasi.
ReplyDeletewadau mi naona tunachezewa changa la macho tu hapa!!!
ReplyDeletewe utamkamataje yona na mramba ukamwacha yule mwingine?
bora,ndo kula nyasi kwa zamu sasa,ila kuvaa kaunda ya zamani sio kigezo cha kufanya tuwahurumie
ReplyDeleteChadema iendelee kuwachua tu
Mheshimiwa mwenzangu,
ReplyDeletePole sana, naomba sana tutunzie mno hii picha ya kwanza katika historia ya Bongo ili tuitumie katika "FROM AWA FAILI" ambayo mimi ni mpenzi wa kolam hiyo katika deile Nyuuuuuuuzi lakini Mwosha huoshwa. Hapo ni Mangi na mtani wake, ingekuwa chingaaas au kina tembooos au pundaaz jamaa wangechonga sana mzee wa t-shet
Chakupewa Mzee wa manzese (Diwani kivuli)
Ni hatua nzuri na ya kupongezwa. Hii itatoa fundisho kuwa cheo ni dhamana na usawa mbele ya sheria. Lakini bado kuna majina na sura za wakubwa wengine tunawahitaji watokee mbele ya haki. Pili wakati hii inaweza kusaidia kurudisha imani kwa serikali ya CCM, lakini kwa upande mwingine itaweza pia kukisambaratisha chama. Ni vigumu watuhumiwa hawa kufa peke yao. na mengi yataweza sasa kusikika na kubwa sana la kutegemea ni kuingizwa kwa CCM yenyewe katika sakata hili kwa namna moja au nyingine. Sijui CCM imejiandaa kiasi gani kupambana na aina yoyote ile ya kuunganishwa katika kashfa hizi. Ila hii ni kazi nzuri a lazima wana demokrasia wote tuiunge mkono na kudai zaidi mapapa wengine wafikishwe mahakamani.
ReplyDeleteWanameremeta!
ReplyDeleteNI VIZURI JK UNAVYOFANYA KUWASHUGHULIKIA MAFISADI LAKINI ANGALIA YASIJE YAKAKUPATA YA CHILUBA (ZAMBIA)
ReplyDeleteMichuzi ,
ReplyDeletePlease tupatie picha wakiwa wanaingia katika karandinga . Nina hasira nao sana hawa watu ndio sababu kila mwaka mamia ya watoto Tanzania wanakufa kwa utapia mlo, magonjwa na kadhalika . I don't feel sorry for them at all cause I firmly believe in reaping what you sow ! Now they are going to face the full wrath of the law....
Hiki ni kiini macho, watu washapigwa changa la macho hapo. Hii yote ni kampeni ya JK kurudi Ikulu 2010. Mkapa yuko wapi?. Maana hawa ndo walikuwa mwaswahiba wake wakubwa na wote wanahusika katika kutumia madaraka yao vibaya. Kama kweli JK amedhamiria kufanya kwli basi tunataka kumwona ka Mkapa ndani ya nyumba.
ReplyDeleteAngalau watanzania wataanza kurudisha imani kwa serikali ya JK, na itakuwa fundisho kwa waliobaki kwenye system
ReplyDeleteHakuna mtu mwenye shaka juu ya hao watu kwani hata nature yao ni wiziwizi tu aka wapenda pesa kuliko hata uhai wa mtu (Wachaga na Wapare) kwa kifupi pipo of Kilimanjaro.Tuhuma nyingi naongezea kama imesahaulika ni kuajiri watu wa kabila lao kwenye sectors na organisations za serikali zilikuwa chini ya wizara ya fedha.Wakabila sana hawa watu. Kama haitaja hiyo, nitafungua mashika yangu mimi binafsi juu ya hawa watu.
ReplyDeleteNdimi mtiifu wa Nchi,
Msukuma
hahah thats funny but this is just some political scam to ease the masses just like the Lowasa case these dudes will prolly be in custody for a few months and they'll be out, besides their bail is 2.9 billion which is chump change compared to what they stole
ReplyDeleteso once again you have been hoodwinked by your stupid governmnet to thinking that they are doing somthing about the corruption lol.
wasiwe wajinga, na wao wawataje waliokula nao ili ngoma iwe dro.na system iwe clean, yaani sasa ivi tukikosa pesa zetu tutawalaani lakini hatuwaachi, ebi yaangalie yalivyo.
ReplyDeleteDuh, hicho chumba kilivyochoka?! Hili ni fundisho kuwa unapokuwa madarakani hakikisha unajali maslahi ya Taifa maana kama wangehakikisha hilo hata hicho chumba kingekuwa nadhifu kwa wao kukaa. Natamani wakakuone huko sero kulivyo!!!
ReplyDeleteHii yote ni kuwatuliza wananchi.. Hamna lolote.. Hizo hela wata kaa nazo na hayo mashtaka yata potea tuu.... Haki ya nani!!!
ReplyDeleteDuh! Hiyo dhamani ni kiboko. Hapo ndiyo nimezima fegi! Ila kama Ester Komu naliweza toa 105ml, sidhani kama hiyo ni hela kwa hawa jamaa!
ReplyDeleteNakumbuka siku moja nikiwa Dodoma tukiwa kijiwe fulani tukibarizi na maofisa waandamizi wa serikali Mramba akawa anafanya utani na baadhi yao,kuna wakati alimwambia mmoja wao..."hivi unajua pesa zoote za nchi hii ni zangu?" kwa nini? akauliza yule ofisa,Mramba akasema "unajifanya una pesa,hizo pesa zina sahihi ya nani?
ReplyDeleteKwa hiyo as long pesa zoote zina sahihi yake basi hawezi kukosa huto tujisenti twa bilioni 3.9
Vinho
to be honest hawa watu nilikuwa sina imani nao yani nilitaka kushangaa wameponea kwenye tundu la sindano mwee Nkiki Mramba odeee
ReplyDeleteSasa wadau hivi mnaona kuna faida ya kuwashitaki hawa watu?
maana kwa upande wangu hakuna kinachorudi tukichukulia mfano wa EPA mpaka sasa hakijaeleweka sembuse hao?
Inauma sanaaaaaaaaa wadau lakini hamna linalifanyika watashtakiwa mwisho wa siku hawana hatia wakati ukweli unaonekana ni wezi
Wananchi tufungue macho
Ehee sasa Mzee JK kinaanza kueleweka watose mmoja baada ya mwingine kam ifuatavyo na listi iendeelee hiyo ya Ufisadi akiwemo na swahiba wako kipenzi yule bwana wa Kimasai. Na tunatak kujua zaidi kuhusu miradi yoote mibove kama ya Rich Monduli na ile kampuni ya Makaa ya Mawe. KILA KIONGOZI AMA ALIEWAHI KUWA KIONGOZI ACHUME ALICHOKIPANDA NA UWAJIBIKAJI UKAMILIKE.MPAKA UFISADI UTAKASWE
ReplyDeleteMengi yamesemwa, na yanaendelea kusemwa, kuhusu ulaji rushwa na ufisadi nchini. Katika hayo yaliyosemwa lililonisikitisha zaidi ni lile la baadhi ya watu kusema na hata kukebehi kuwa Mheshimiwa Ndugu Rais Jakaya Kikwete, na serikali yake, anawaogopa mafisadi na kuwalinda. Sasa yako wapi hayo? Katu Rais haigopi fisadi. Ukweli ni kwamba JK ni simba mwenda pole, anajua afanyalo, kwa nini, kwa namna gani na kwa wakati gani.
ReplyDeleteNakupongeza sana tena kwa dhati kabisa Ndugu Rais pamoja wasaidizi wako kwa kazi nzuri na ya kupigiwa mfano si Tanzania tu bali kila pembe ya dunia kwa kuonyesha utayari na ujasiri wa kupambana na rushwa na ufisadi bila kujali ni nani anakamatwa, ana nafasi gani katika serikali au chama au ana uhusianao gani na watu walioko serikalini. Ukweli ni kwamba vita dhidi ya rushwa na ufisadi siku zote hutegemea utayari na nia thabiti ya serikali iliyoko madarakani ya kupambana maadui hawa wa haki na maendeleo ya nchi. Kwa kazi hii nzuri ambayo inafanywa na serikali yako, Ndugu Rais umeionyesha nia dhati na utayari kweli wa serikali yako wa kupambana na rushwa na ufisadi. Hakika umekata mzizi wa fitina.
Kukamatwa kwa watuhumiwa wa EPA na sasa hawa waheshimiwa wabunge na mawaziri wa zamani ni bishara tosha kuwa serikali ya Kikwete inatekeleza kwa vitendo kanuni na misingi ya Utawala Bora na kuheshimu haki za binadamu. Kuheshimu, kutekeleza na kuulinda utawala wa sheria na haki za binadamu ni miongozi mwa ahadi alizozitoa Ndugu Rais wakati akiomba ridhaa ya wananchi kuingia ya Ikulu Magogoni. Sina shaka hata kidogo kuwa kwa utendaji - kazi wa namna hii wananchi tutamuongezea muda wa pango hapo 2010. Na kwa hakika serikali imedhibitisha kuwa sheria zake ni msumeno hazijali kipato, wadhifa, nasaba au uswahiba kama wengi walivyokwisha kusema kuwa Tanzania ina sheria mbili, ile ya watu masikini kwa upande mmoja na vigogo kwa upande mwingine.
Kazi ya kumkamata mtuhumiwa ni ngumu ikiwa huna ushahadi na wakati huo huo unatakiwa kulinda haki zake za msingi za binadamu kwa kutekeleza kanuni utawala za utawala bora. Hapa pana kizungumkuti cha aina yake. Lakini yote haya yanaweza kufaninya iwapo itatumika hekima na subira kuandaa mkakati wa kukusanya ushahidi dhidi ya mtuhumiwa na hatimaye kumfikisha mahakamani mtuhumiwa ili haki ikapatikane huko. Si kwamba Ndugu Rais alishindwa kutumia madaraka yake kwa mujibu wa katiba kusema 'KAMATA' na watu WAKAKAMATWA! La hasha! Alikuwa na wakati mzuri sana wa kulitoa tamko kama hili wakati akilihutubia Bunge na bila shaka wananchi tungemuunga mkono tena kwa nderemo na vifijo. Lakini yeye pamoja na serikali wakatumia njia nyingine isiyo ya mabavu yenye kuonyesha kukua na kukomaa kwa demokrasia katika nchi yetu. Hili funzo tosha kuwa tukitumia taratibu, kanuni na sheria tulizojiwekea basi tunaweza kuutokomeza ufisadi na rushwa kwa njia ya mahakama kwani ni mahakama tu ndiyo yenye mamlaka ya kumuhukumu mtuhumiwa na kumpa adhabu stahili.
Nakupongeza tena Mheshimiwa Ndugu Rais kwa kutamka wazi kabisa, na kutupa funzo lingine, kuwa serikali yako haitaingilia kwa namna yeyote ile shughuli za mwendesha mashtaka wa serikali au mahakama. Heko Kikwete kwa kusimamia barabara utawala bora. Tanzania itajengwa na wenye moyo na moyo huo unao.
Mungu Ibariki Tanzania
Amani Ramadhani Millanga
KAMA KESI ZA KINA BABU SEYA NA WATU WA UPINZANI KAMA KINA LAMWAI (WASIO WA CCM NA VIONGOZI WA UPINZANI) ZILIVYOPELEKWA FASTA TUNATAKA NA HII IENDE HIVYO HIVYO ,SIO MARA UCHUNGUZI,UNASKIZA MIAKA INAPITA UCHUNGUZI UNAFANYIKA TU MPAKA WATU WANASAHAU,HAKUNA KUTREAT KIHESHIMA TENA,TUNATAKA KAMA CHINA NA THAILAND.HAWA WATU NDIO WANAOWAFANYA NDUGU ZETU HUKO VIJIJINI WAZIDI KUWA MASIKINI NA KUFA KWA KUKOSA HUDUMA MUHIMU KWANI PESA ZOTE ZINAISHIA MIKONONI MWAO.UCHUNGUZI UFANYIKE KWANI HAWA HAWAFIKII HATA ROBO KUNA MAMIA YA MAFISADI BADO HAWAJAFICHULIWA.SO HOO NI WAJIBU SIO SWALA LA KUANZA KUMPONGEZA MTU AU CHAMA FLANI KWA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WATU HAWA.TUSIJE KURIDHIKA NA HILI WATANZANIA BADO WAKO WENGI SANA NYUMA YA PAZIA.
ReplyDeleteSO MAMBO YA KUTOA PONGEZI NI MAPEMA SANA NDUGU ZANGU WAPO WENGI,KUMBUKA HAWA WAWILI TU HAWAWEZI KUMALIZA PESA ZOTE BADO KUNA VIONGOZI ZAIDI TUNATAKA WAFICHULIWE.
Tatizo huko rumande wanapelekwa yao..... ati wakichanganywa na wenzao watawa.... lakini ingekuwa bora wawekwe pamoja kwenye mtondoo... that is where they deserve anyway
ReplyDeleteHiyo ni sehemu tu ya malipo ya dhambi zao. QUOTE. ''HATA MULE MAJANI NDEGE ITANUNULIWA''. mmoja wao alidiriki kuongea hilo
Sasa na yeye ..........apende asipende the truth will be revealed Keep it up JK
sasa hawa wa government wameanza kushikana au kiini macho?
ReplyDeleteWA TANZANIA WENZANGU PUNGUZENI JAZBA ILA HAKIKA MIE BINAFSI NINA MASHAKA NA HII KESI YA EPA KWANI WAMESHAZOEA KUTUFANYA WATANZANIA KAMA KATUNI AU MCHEZO WA KUIGIZA KWANI TUNAENDESHWA NA VYOMBO VYA HABARI HII KESI ITALIPOTIWA SANA KISHA HAKUNA HATUA ZA KIMSINGI ZITAKAZOCHUKULIWA DHIDI YA HAWA WIZI WAKUBWA, HAKIKA INAUMA SANA BABA ZETU NA MAMA ZETU VIJIJINI WANAKUFA KWA KUKOSA MATIBABU AMBAYO NI HAKI YA KIMSINGI KWA KILA MTU. WITO WANGU KWA RAISI TUNAJUA UNAPITIA WAKATI MGUMU SANA ILA IPE UHURU MAHAKAMA ITENDE HAKI STAHILI KUSIWEPO NA SHINIKIZO ZA KISIASA KATIKA HILI LA EPA KWANI WATANZANIA WATAJENGWA KIIMANI IKIWA HAKI ITATENDEKA KATIKA HILI NA C KIINI MACHO - MDAU MTANZANIA HALISI
ReplyDeleteMPAKA SASA HIVI GEMU INAENDELEA VIZURI, INGAWA NDIO KWANZA ROBO YA PILI IMEANZA. HISIA ZANGU NI KUWA MKAPA NA SUMAYE WAKO KWENYE RESERVE LISTI NA WATAINGIA UWANJANI KWENYE DAKIKA ZA MAJERUHI, TUNAFUATILIA KWA MAKINI HII GEMU INACHEZWAJE NA KAMA KUTAKUWA NA USHINDI AU NI MAZINGAOMBWE
ReplyDeleteteh teh,
ReplyDeletecome on! Hata kama ni kula majani tutakula, lazima Mramba afungwe....
Pale mtu na mtani wake wanapokuwa Kizimbani......
ReplyDeleteSAA YA KULA NYASI IMEFIKA!!
ReplyDeleteILA HUU USANII SIJUI UTATUFIKISHA WAPI MAANA KESI YA NALAILA ILICHUKUA MIAKA 10 NA AKAACHIWA SASA HUU USANII WA SASA TUONE UTAISHIA WAPI.
BILA MTU KUPATIKANA NA HATIA, KWENDA JELA NA KUFILISIWA HASHANGILII MTU HAPA.
YETU MACHO
Yani hapa Tz ni wizi mtupu kama masanja anavyosema. Hapa simpi mtu pongezi mpaka nione mwisho manake serikali yetu kwa viini macho ndo yenyewe, na ukitaka kujua ni mafisisadi kweli cheki bil 3.9 wanazipata on the spot kama vile sh. 100, yani inatia machungu we acha tu, halafu eti hakuna hela za kulipia wanavyuo kwa 100% kumbe hela wanazo wenyewe. Kwani hizo bil karibu 8 walizotoa dhamana zinatosha wanafunzi wangapi? Mie nina ndugu yangu anasoma shule moja tena eti inaitwa special school ya wasichana (kilakala), wamekatiwa maji mwezi sasa, hawana chakula any time wanaambiwa wanaweza kurudi makwao, walikatiwa umeme ukarudishwa na sio mara ya kwanza kupata matatizo kama hayo then ukija kuangalia hela wanazo wachache kama hao inauma sana. Hapa mpaka kieleweke wasituzuge."WIZI MTUPUUU"
ReplyDeletehii yote mi naona ni ZUGA tu! Wamenunua ndege...tumeiona....tumekula manyasi....mpaka tumeshiba.....sasa wamekamatwa!! Ndio! Ukigeuza coin....wapi ile Ndege inayotulisha Nyasi? Anaitumia JK kupigia misele viwanja! Angekua na nia ya kweli...kwanza angeitoa hiyo ndege pesa (Shs bilion 50) na kuziongeza kwenye mabilioni yake (bilioni 20 au 21 hivi) Mtaji wa wajasholamaji (wajasiriamali) ungeneemeka mno! Kudos Mr President...but I still got my doubts kwamba hii inawezekana ni kiini macho tu!
ReplyDeleteAahaaa...c'mooon JK...You doin a great JOB big Boi...hebu watembezeni kifua wazi hao, hawana tofauti na vibaka....gwa gwa gwa gwa gwa...am so hepi!
ReplyDeleteHiki ni kibanzi tu!Nanyi jiandaeni kutoa boliti kwenye mboni zenu.
ReplyDeleteI propose something, to get rid of RUSHWA na UBADHILIFU WA MALI YA UMMA, government should set this as holywood story, find a good documentary production team, and make it a priority by showing to our young man and woman in secondary schools across the country as a lesson and as a part of curricula.
ReplyDeleteIf you need to work for your Government you need to save it HONORABLY, and not by squandering our wealth, profiteering, privilege and illegal accumulation of wealth.
THAT WILL BE A FANTASTIC AND GOOD STORY TO TELL.
What do you think WADAU!
Thats the only way SHAMING and DAMNING all those GOVERNMENT FRAUDSTERS!
You better think twice before TAKING OFFICE. Ho
post coment zote watu tunahasira sana eeebo usiminye
ReplyDeleteWatanzania wenzangu, Nina uzoefu wa kutosha na nchi yetu.Jitahidini kufumba vinywa nanyi mtaona.Hakuna lolote wala chochote. Ni mchezo wa danganya toto!!Baba yetu na Mungu wetu ingilia kati uokoe watanzania wako.
ReplyDeleteEee Bwana eee!! JK sasa ana kura yangu ya ndiyo-2010.Sasa kinaeleweka, hawa wajomba waliema tutakula nyasi wakati wao wakitanua!!
ReplyDeleteLiwe fundisho kuwa usimtukane mwnanchi ambaye unachukua kodi yake, unaifuja halafu unamdhihaki.Kilio cha wananchi ndio kimewafikisha hawa jamaa hapo, sio kwamba watu walikuwa hawayajui mambo yao.
Tunawatakia nyasi njema huko Segerea.
Dah, Bongo mambo kidedea, EH?..
ReplyDeleteSa, sijui nibakie hapa Marekani nikimsubiri Obama aapishwe au nirudi Tanzania kimoja.. kweli nyumbani ni nyumbani, mwendo huu kote Tanzania sasa ni nyumbani hivi..
I Love You Bongo, Japo Sijafika!?
===
Buffalo,
New York
IT IS VERY EASY TO TRIGGER THE MINDS OF TANZANIAN VOTERS!
ReplyDeleteASK YOURSELVES MBONA ROSTAM HAJAWEKWA KIZIMBANI WAKATI ISSUE YAKE NI MUCH MORE RECENT ZAIDI YA HAWA EX MINISTERS?
ALL JK IS DOING NOW IS MAKING SURE THE EASILY TRIGGERED MINDS(90% OF VOTERS)WANARUDISHA IMANI YAO THEN THE REMAINING 10%(MIMI NA WENGINE)IS NOT A BIG DEAL SABABU EVEN IF HATUMPI VOTE 2010 ATASHINDA TU.
HAWA JAMAA THEY WERE NOT HIS ALLIES SO ITS NOT A BIG DEAL TO CRUCIFY THEM BUT IT IS A VERY BIG DEAL TO CRUCIFY ROSTAM AZIZ OR A.KINANA HIYO INAITWA USIPIME!
raia mwema
CCM shina la Reading kwanini msiwatafutie hifadhi za kiasiasa?
ReplyDeleteAma kweliTz ninchi ya amani. Nchi nyingine raia wangejichukulia sheria mkononi na kuwaadabisha kiheshimiwa.
ReplyDeleteMie nafikiri hakuna la maana sana zaidi ya kuviwezesha vyombo vya habari kufanya mauzo kwa week hii manake la EPA lilipozzzzzzzzz kidogo sasa jingine la matumizi mabaya ya ofisi na Kesha wii be big day for Vyombo vya habari hasa magazeti.
ReplyDeleteLakini Mie nasisitiza Operetion SANGARA iendeleeee na Hapa DAR twaisubiri kwa Hamu.
Okay...Dhamana ya Shs Bil 3.9 (US Dola Milion 3) CASH..!!
ReplyDeleteTanzania au.!!
kupelekwa mahakamani sawa watafungwa? kama watafungwa na wengineo walioko reserve kupelekwa mahakamani na KUFUNGWA, jk u will need more than bima 4 ur own sekuriti! mtafute Kagame akupe siri!! kasheshe.
ReplyDeleteyampayinka karabaye!!!mshangao wa watu wa nchi jirani hou....
ReplyDeletehii ichunguzwe vizuri pande zote kisiasa na uelewano
KAKA HII SENEMA KAKA!!
ReplyDeleteHATA PICHA UTAONA STARING ANAPIGWA MWANZO MWISHOWE YEYE ANAPIGA MOJA TUU ANASHINDA!!! HII SENEMA HAWA WATATOKA!!
Jamani mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni,JK anastahili pongezi kwani anafanya kazi utaalamu mkubwa na hana kelele mingi.HEBU TUJIULIZE NI RAIS GANI HAPO TZ ALIYEWAHI KUFIKISHA MWAWAZIRI WAKE MUHIMU KAMA HAO MAHAKAMANI???????????NI KIPINDI CHA RAIS GANI BONGO WAZIRI MKUU ALIBWAGA MANYANGA KWA AMRI TOKA KWA MKUU WA NCHI????
ReplyDelete2010-JK Lazima achukue nchi anastahili pongezi katika kipindi hiki kigumu cha nchi na dunia kwa ujumla.Naomba tumpe pongezi na ushirikiano,hiyo migomo wengine wanaiga tu haina kichwa wala kiuno.
Na upinzani hakuna wanakutuongoza hapo anaemshinda JK wote wababaishaji na waganga njaa tuu.
Habari ndo hiyo.....kwikwikwikwi.
Cha Chandu- UK
KAMA NYASI TUMEKULA, NA UMEME TUMEKOSA, NA CHAKULA TUMEKOSA LAKINI HATUKUJALI SABABU NI MKAPA NA SIKU ZIMEWADIA. WAENDA KULA MAJANI NA WAO.
ReplyDeleteNDUGU Amani Ramadhani Millanga NA WATANZANIA WOTE HAPO MLIPO MSIFURAHI MIMBA KABLA MTOTO HAJAZALIWA.
ReplyDeleteHUENDA WEWE NI KATIKA NDUGU WA MAFISADI NDUGU AMANI MAANA KWANZA USITUFANYE SISI WATANZANIA WATOTO WADOGO KWA KUMSIFIA JK.
UKWELI KESI HII JAPO HUENDA NI FILM YA KUIGIZA HADI TUSIKIE JAMAA WAMETIWA NDANI NDIO TUTAJUA NI UKWELI.
SIFA INATAKIWA KUPEWA MBUNGE ALIYEFANYA UTAFITI NA PIA NCHI ZA NJE KUIPA PRESHA SERIKALI YETU VINGINEVYO INGALIKUWA HADITHI YA MITAANI.
WATANZANIA CCM LEO MIAKA 40 NA KITU KITU GANI CHA MAANA ILICHOKIFANYA LEA WASTAAFA WA EAST AFRICAN UNION NCHI ZOTE WAMELIPWA YAANI KENYA NA UGANDA ILA TANZANIA HADI LEO INAWADHULIMU WAHUSIKA HALAFU UNASEMA CCM ICHAGULIWE 2010TENA JK.
HAKIKA KAMA KUICHAGUA CCM BASI KURA YANGU NTAMPA WARIOBA AU SALIM AHMED LA SIVYO NAWASHAURI WATANZANIA WENZENGU WENYE KUPENDA MASLAHI YA NCHI KWA AMAN NA MAISHA BORA NI MUHIMU KUWAPA WAPINZANI ILI NAO TUWAONE.
KWA UPANDE WANGU NAOMBA TUWE KAMA WAAMERIKA TUCHAGUE MTU KWA SIFA NZURI KAMA OBAMA ATAKAYELETA MAENDELEO YA NCHI NA SIYO KWA JAZBA YA CHAMA.
WATANZANIA UMRI UNAKWENDA LINI TUTAPATA FURSA YA KULA MATUNDA YA UHURU KWA KILA MWANANCHI.
NAOMBA TUSIDANGANYWE NA NDUGU AMANI KUWA JK KAFANYA HAKI.
HAKI KUFIKISHWA MAHAKAMANI HII KWANGU NI NDOTO MAANA MAHAKAMA, JESHI, POLISI ZIKO CHINI YA MKONDO WAS SHERIA YA SERIKALI YA AWAMU YA KWANZA YAANI CHAMA KIMOJA.
ILI KUPATA HAKI KATIKA MAHAKAMA NI LAZIMA SHERIA ZOTE ZIBADILIKA NA KATIBA ITENGENEZWE NA VYAMA VYOTE HAPO HAKI ITAPATIKANA.
NDUGU AMANI KUMBUKA MBELE YA MUNGU UTACHUKUA MZIGO MKUBWA KUWAAMBIA WATU HAKI TAYARI WAKATI HADI SASA HAKUNA AJUAYE UKWELI WA MAMBO HADI TUONE HAKI INATENDEKA.
USHAHIDI GANI UNATAKA NDUGU TANZANIA HATUNA WATU WENYE MABILION HATA MTOTO WANGU MDOGO ANAWEZA KUFANYA UCHUNGUZI NI KITU DHAHIRI.
TUNAMUOMBEA JK KWA MUNGU AWE MUADILIFU NA AIPE MAHAKAMA HAKI KAMILI HATA MKAPA ABURUZWE HAPO TUTAJUA NI KWELI NA ITABIDI KUMPA KURA 2010.
MUNGU IBARIKI HAKI AMEN
Si bora hao walioko kizimbani,je nyie watoro mnasengenya nini kutoka kule nje ya nchi...tofauti hakuna...hao wezi,nyie watoro!!!
ReplyDeleteYAANI MI NAONA NI VIZURI HIVYO ILA JK NA YEYE NI MSAFI AU NI UNAFIKI TU.. TUTAONA , MAWAZIRI WANGAPI BADO WAPO TU WANAKULA HELA KITU KINACHONISHANGAZA NI KWAMBA UNATAKA KUJINUFAISHA MWENYEWE BADALA YA KUENDELEZA NCHI KUWEKA ROADS NZURI HEALTH CARE NZURI MAANA UTAKUWA UNA HELA ILA IKITOA EMERGENCY UNASHINDWA KUHUDUMIWA MPAKA UWE AIRLIFTED SAA NGAPI SI UTAKUFA, IT IS ABOUT TIME TUANZE KUFIKIRIA MBALI NA SIYO SASA HIVI. UNAJUA KUWA TUNACHEKWA KILA WAKATI SIYO NZURI , TUNAHITAJI MAENDELEA KAMA HIYO THAMANA ITAENDA SERIKALINI AU KWENYE POCKET YA MTU?? WE NEED CHANGE I MEAN DRASTICALLY CHANGE. TUENDELEZE NCHI YETU BWANA YAANI TUNAWEZA KAMA TUJIKAZA FOR COUPLE OF YEARS HII ITASAIDIA SAANA. NA NAOMBA WATU WAELIMIKE JAMANI ELIMU NI MUHIMU SAAANA, NA KAMA UTAWEZA KWENDA NJE NI MUHIMU PIA KWANI UNAJIFUNZA MENGI UKISAFIRI.
ReplyDeleteAnonymous wa 9:24 uelewa wako ni duni sana. Mimi nipo Bongo, lakini kwa taarifa yako, ninafahamu kwamba watu waliopo nje ya nchi wanakuza pato la Taifa kwa kutuma nyumbani pesa za kigeni wanzozisotea nje huko. Kuna nchi kama India au Kenya, watu waliopo nje wanachangia kiasi kikubwa sana katika uchumi. Fungua bongo yako na upeo wako angalia mambo kwa mapana uweze kusonga mbele. Watu waliopo nje ya nchi siyo watoro ni wachangia uchumi.
ReplyDeleteWanameeeeeeeeeeeremetaaaaaaaa
ReplyDeletewanameremeta ,mafisadi wanameremeta.....
Wanameremeta
Oh now JK sasa tutajenga imani nawe, tulidhani ni changa la macho kwa watanzania! Tulidhani wala nao "the same pot", now you are talking, keep it up!
ReplyDeleteMkimbizi,
The Netherlands
Anon wa 8.25,
ReplyDeleteNakuunga mkono kwa kuwa na dira na mwelekeo mzuri. Kitendo cha JK ni cha kusifiwa ni hatua ya juu mno na inaonyesha transparency ya serikali.
Lakini lazima tumsaidie JK kumpa mawazo hasa katika implementation ya vision yake ya maisha bora kwa watanzania wote aliyoitoa wakati wa uchaguzi.
JK ana nia ya kutimiza hii vision lakini amezungukwa na mafisadi ambayo yamengangana kama kupe, hawakomi na hawaachi tabia zao za ufisadi hadi uwanyofoe kwa nguvu au kuwaua!
Ama mpaka sasa hivi hiyo dira haijatimizwa hata chembe kwa kuwa muda wote anashughulikia mafisadi ambao alidhani wanakaa chini kubuni mbinu za kuleta maisha bora kumbe wanabuni mbinu za kuleta maisha duni kwa mtanzania milele!
JK kwa heshima na taadhima kila kitu kipo bayana ... chama tawala kimejaa mafisadi!...ni wakati wa demokrasia kuchukua mkondo wake...ngatuka na chama chako tawala wapishe wapinzani wenye maana na upeo wa hali ya juu.. wapinzani amkeni .. tafuteni watu watakaoleta mabadiliko na siyo wachovu kama.. freeman, lyatonga, lipumba ...hamfiki popote.....mabadiliko yanahitajika kukisafisha chama tawala. Anatakiwa kiongozi mithili ya Baraka Obama- MUNGU ibariki Tanzania!
HII IMETULIA SANA JK ANAANDIKA HISTOR
ReplyDeleteYES WE CAN!
ReplyDeletehakuna lolote MAFISADI WAKUU TENA KINA ROSTAN AZIZI, MKAPA MNA JK MWENYEWE WAMEJIACHA JAMANI HILO NI CHANGA LA MACHO WATANZANIA TUAMKE
ReplyDeleteSHENZI TYPE KAMA JK ANAKIBURI ROSTAM NAM MKAPA WAONYESHWE HAHA TUNATAKA SURA ZAO HAO
ReplyDeleteMjengwa wewe ndio we kutuletea pic za segerea cjui umefikilia nn kusema hivyo wakat kamera unayo mkonono mwako!!anyway just ike others in africa!!!
ReplyDeleteJuma nature get reaady son!!!!
Jk wewe msafi au ndio nyani haoni kkk!!!
ReplyDeletemichu mboni waminya saana??? eboooo
ReplyDeletewale nyasi???hahahaaaaaa
wezenu wana spesho dayat na executive rooms keko,,segerea hawaendagi ng'o
kalagabaho,,,,,,,
na wewe annon wa" YES WE CAN" hahahaaaaaa unaniacha hoi
hadi mashirika ya umma JK ufisadi wa kutupwaaa wakomboa wapiga kura wako bandarini fika baba unafanyiwa soooo na watu uliwakuta hawana haja na kukujenga ila kukubomolea 'maisha bora kwa kila mtazania' kwa hali hiii haifikiwi piga jicho wanakula hadi nudu kazi hazifanyi huku watu wameshusha paleti
ReplyDeleteMungu ibariiiki tanzaniaaa...wabariki viongozi wakeeee...heshima umoja na amanii......!!
ReplyDeleteMIMI NACHUKULIA HII NI HATUA KUBWA SANA KWA TANZ, MAWAZIRI KWENDA SEGEREA? SIWEZI KUSEMA SANA MPAKA SIKU WATAKAPO FUNGWA NA KUTUMIKIA KITUNGO. BUSH QUEEN.
ReplyDeleteYES WE CAN....
ReplyDelete..and MAY U ROT IN JAIL!for ever n ever Ameeen
ReplyDeleteAlijisemea Joti Lainiiiiiii kama unanawaaaaaaa!, lainiiiiiiiii kama unanawaaaaaaa!
ReplyDeleteYa watawala ni yale yale daima milele
ReplyDelete“KAMA tutaendelea kuchagua watu wa kuahidi neema bila mabadiliko, mapato bila kazi, na utulivu wa kijamii bila kujirekebisha ili kuendana na hali ya kiuchumi, sio tu tutapoteza neema iliyo dhahiri mbele yetu, bali tutakabiliwa na migogoro pia”
Maneno hayo ya wanazuoni hawa wawili yana maana kubwa kwa mazingira yetu Tanzania, ambapo kila baada ya miaka mitano wagombea nafasi za uongozi hubeba furushi la ahadi zisizotekelezeka kwa wananchi.
Na sasa ni utamaduni uliothibitika kwamba kila awamu ya serikali madarakani, kuanzia na awamu ya kwanza (1961 – 1985) hadi iliyopo madarakani sasa, inaingia kwa kauli mbiu na ahadi zake.
Kana kwamba kauli mbiu na vibwagizo ndiyo maendeleo yenyewe, wananchi wamelishwa maneno matupu wakashiba, wakasifiwa kwa amani na utulivu wakati amani hakuna; huku maisha yao yakiendelea kudidimia. Tanzania na Afrika kwa ujumla ni masikini kuliko ilivyokuwa enzi za mwanzo za uhuru. Kipi kimekwenda mrama?
Awamu ya kwanza ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ilianza na kauli mbiu ya “Uhuru na kazi”, na baadaye “Uhuru ni kazi”, kwa maana kwamba Uhuru au kujitawala si “lelemama”; pia kwamba bila kufanya kazi hakuna maendeleo, na maendeleo maana yake ni uhuru.
Tena, maendeleo maana yake ni maendeleo ya watu, na Mwalimu akafafanua hivi: “Maana ukweli ni kwamba maendeleo maana yake ni maendeleo ya watu. Mabarabara, majumba, kuongeza mazao, na vitu vingine vya aina hii siyo maendeleo; ni vyombo vya maendeleo. Kwa Mwalimu, “Majengo pacha” ya Benki Kuu (BoT), Sukari House na barabara za lami zinazotanda nchini nzima, si maendeleo; bali ni vyombo tu vya maendeleo.
Kipi muhimu, kwa mfano, majengo pacha au ujenzi wa mabwawa kwa ajili ya umwagiliaji na kilimo cha ufugaji? Awamu hii iliona uhusiano wa uhuru na maendeleo kama ulivyo uhusiano wa kuku na yai; wawekezaji binafsi waliruhusiwa kuwekeza na kuvuna sehemu ndogo tu ya rasilimali za taifa kama hatua ya muda, wakati taifa likikusanya nguvu kuweza kuvuna lenyewe kwa manufaa ya wananchi wote.
Tena, iliona maendeleo maana yake ni uhuru wa watu wa kuamua jinsi wanavyotaka kuishi, chakula, nyumba, afya, elimu, maji safi na salama, demokrasia, na uhuru wa wananchi kupanga uchumi wa nchi kupitia Serikali walioichagua.
Falsafa hii, ambayo haimo katika msamiati wa Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), lengo lake ni kujitegemea kwa nchi ili kulinda uhuru wa taifa.
Awamu ya pili ya Rais Ali Hassan Mwinyi (1985 – 1995) ilikuja na “Fagio la Chuma”, kana kwamba serikali iliyotangulia iligubikwa na rushwa. Ilianzisha ubinafsishaji uchumi usiojali, ikafuta Azimio la Arusha kwa Azimio la Zanzibar, rushwa ikashamiri, uzalendo na maadili ya taifa yakayoyoma, kila kitu kikawa ni “ruksa” kunyakua. Tanzania ikageuzwa “Shamba la Bibi”, ikawa kichwa cha mwendawazimu kwa kila mtu kujifunzia kunyoa.
Awamu hii iliigeuza nchi uwanja wa majaribio ya kupiga shabaha ya uporaji. Mwinyi hakujua kwamba zile sera za uchumi huria alizozilaki na kuzifungulia mlango, zilikuwa ni matokeo ya mchakato wa miaka mingi katika nchi za ubepari uliokomaa.
Awamu ya tatu ya Komredi Benjamin William Mkapa (1995 – 2005) iliingia na kauli mbiu ya “Uwazi na Ukweli”, Je, ina maana uficho na uongo ndivyo vilivyotawala awamu zilizotangulia?
Mkapa alikuwa mtu wa kimataifa, alifikiri kimataifa, alitenda kimataifa. Hakuwa na muda wa kugusana mabega na walalahoi, mafukara wa Jamhuri hii. Alitaka ubia kati ya (nchi) masikini na (nchi) tajiri. Kwake, ushirikiano wa nchi masikini duniani (South-South) uliwakilisha uvivu wa kufikiri. Nchi za kibepari zikamnasa hima; zikamnesanesa, akafungua milango kwa shetani mnywa damu ya watu, hadi bawaba ya mwisho.
Katika Mkutano wa nchi tajiri duniani (G.8), Juni 1996, nchi hizo zilikubali kuongeza misaada kwa Tanzania ili kuimarisha mpango wa kurekebisha uchumi kwa maelekezo ya WB na IMF. Hatimaye, kwa sababu ya kuwa “mtoto mzuri” wa dunia ya ubeberu, Mkapa aliteuliwa kuwa Mwenyekiti Mwenza wa Tume ya Utandawazi ya Dunia, pamoja na Rais wa Finland, Tarja Kaarina Halonen.
Mkapa alijua athari ya kuingizwa katika zizi hilo; alijua athari za ubia kati ya masikini na tajiri. Alielewa fika nahau ya nchi hizo, kwamba, “aliye na kingi ataongezewa; na aliye na kidogo, hata hicho kidogo atanyang’anywa”.
Kwa nini asijue hilo wakati wanazuoni mahiri wa nchi hizo, wenye kuzihurumia nchi changa, walikwishaonya?. Profesa Paul Kennedy, mwandishi wa “The Rise and Fall of Great Empires”, alikwishaonya katika kitabu chake kingine, “Preparing for the 21st Century”, kwamba “Utandawazi hauna habari wala haujisumbui na maslahi ya asilimia 80 ya mafukara wa dunia hii wasiomo katika mfumo wa kifedha na kibiashara wa mataifa makubwa”.
Profesa Kennedy anashangaa ni vipi makampuni ya kimataifa ya kuhodhi, yenye kutumiwa na kulindwa na nchi mama, yasiyoweza kudhibitiwa na nchi mwenyeji, yanaweza kuwa wabia wa kweli wa nchi masikini zenye njaa?
Tangu lini kukawa na ubia sawa kati ya daktari na mgonjwa; kati ya mbwa mwitu na mwanakondoo?.
Katika kitabu chake “Managing for the Future”, Peter Drucker anasema kwamba, nchi maskini zisikubali kudanganywa kwa njozi za ubia wa maendeleo na nchi tajiri; kukubali hilo ni kujitia kitanzi.
Ni wakati wa awamu ya tatu, mikataba mibovu ya uwekezaji; hususani katika sekta ya madini ilipotiwa sahihi kwa hasara ya nchi. Si kwa sababu Rais hakulielewa hilo, bali ni kwa sababu alisahau utaifa na maslahi ya taifa, akajikweza kuwa mtu wa kimataifa.
Kenichi Ohmae alikwishatuonya juu ya hilo katika kitabu chake, “The Bordrless World: Power and Strategy in Interlinked Economy”: kwamba, “Nchi zinazoendelea zisidanganyike kwamba zinaweza kuwa wabia wa maendeleo na nchi tajiri kwa kuwa tu zina utajiri mkubwa wa rasilimali unaohitaji kuvunwa. Kuamini hivyo, ni kujipeleka kwenye mdomo wa mamba atakayezimeza mwili, mifupa na damu”.
Lester Thurow, ameonya katika “Head to Head: The Coming Economic Battle Among Japan, Europe and America” kwamba, “kwa nchi masikini kufungwa nira na nchi tajiri ni kukalia kuti kavu”.
Awamu ya nne ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete iliingia na kauli mbiu ya “Ari mpya, Nguvu mpya na Kasi mpya”, kana kwamba awamu zilizotangulia zilikosa Ari, nguvu (goigoi) na kasi katika ujenzi wa nchi.
Tofauti na awamu ya pili, ambayo ilidhamiria kufagia matunda ya uhuru, na awamu ya tatu iliyoendeleza ubomoaji wa misingi iliyobakizwa na “fagio la chuma” kwa nyundo nzito, awamu ya nne haisemi “ari” hiyo inajengwa na nini, “nguvu” inatoka au inatokana na nini, na “kasi” hiyo ni kuelekea wapi?.
Awamu hii haina pa kukanyaga; kwa sababu msingi ulikwishavunjwa. Na kwa nahodha asiyeelewa bandari aendayo, hakuna upepo ulio muafaka kwake.
Imesemwa: Maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana, lakini hatuambiwi kwa dira ipi, mfumo upi wa uzalishaji mali na kwa sera zipi-ubepari au Ujamaa? Tunaona katiba, ibara ya 3(1) kwamba, “Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na ya Kijamaa, isiyo na dini, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa. Lakini, mbona yanayotokea sasa yote ni kinyume chake?.
Awamu ya nne iliingia kwa Rais kujitambulisha kama kiongozi wa watu. Amekuwa Rais wa kwanza tangu uhuru kutembelea wafungwa gerezani, ameahidi kupitia upya mikataba yote mibovu ya uwekezaji ili nchi inufaike na rasilimali zake.
Alitembelea nchi jirani kujitambulisha na alitembelea nchi tajiri, bila shaka kwa lengo la kujifunza siri ya maendeleo ya nchi hizo bila kubeza ushauri wa akina Nyerere, Profesa Paul Kennedy, Peter Drucker, Kenichi Ohmae, Lester Thurow, Jeffrey Sachs na watetezi wengine wa ukombozi wa nchi za Dunia ya Tatu.
Bila shaka katika ziara zake amebaini kwamba nchi tajiri zilikwisha komba kabisa rasilimali zake, na kwamba idadi ya watu wake kwa eneo la ukubwa kama lao, ni kubwa kuliko idadi yoyote duniani kutoruhusu kupanua kilimo wala kuratibu shughuli za viwanda na kuepuka uchafuzi wa mazingira.
Ndio maana nchi hizo zimeanzisha uvamizi wa Afrika ili kujipatia madini na malighafi kwa viwanda vyake. Rais atakuwa amejifunza pia kwamba Marekani, ambayo ni mzalishaji mkubwa wa mafuta baada ya Urusi, inaagiza kutoka Mashariki ya Kati ili kulinda hifadhi ya rasilimali hiyo kwa sababu inaelewa kuna kesho.
Kwa nini sisi tumeruhusu rasilimali zetu kuvunwa na wageni kwa fujo kana kwamba tunajiandaa kuhamia mwezini?
Rais atakuwa amegundua kwamba, wakati WB na IMF zinatutaka kuacha kutoa ruzuku kwa wakulima wetu, Marekani inatoa ruzuku ya zaidi ya dola bilioni 200 kila mwaka na nchi za Umoja wa Ulaya huchangia asilimia 60 katika bajeti zake kama ruzuku! Kwa nini mkuki kwa nguruwe katika “ubia” huu wa maendelo?
Licha ya kutojua bandari iendayo, Serikali ya awamu ya nne imefungwa miguu na degedege la ukiritimba wa Chama ulioficha tabaka la wakeketaji demokrasia na maendeleo. Kiongozi mwadilifu kama Kikwete afanye nini anapovutwa shati na mkono mchafu wa kitabaka?
Pengine kuna mantiki katika usemi wa Rais wa zamani wa Marekani, John F. Kennedy kwamba “kiongozi mzuri ni yule anayechukua hatua kwa manufaa ya jamii nzima, hata kama kwa kufanya hivyo kutawafurahisha wapinzani na kuwaudhi marafiki na makada wa chama chake”.
Tusimpuuze pia Cannor Guise O’Brien anavyosema kwenye kitabu chake: “On the Eve of the Millenium” kwamba “mchakato wa kidemokrasia ni zoezi lisilo na kikomo la kutafuta umaarufu. Viongozi wa kidemokrasia ni zoezi lisilo na kikomo la kutafuta umaarufu. Viongozi wanaochaguliwa kwa njia hii; huku wakitarajia kuchagualiwa tena, hutukuza na kuweka umaarufu mbele kuliko mambo mengine.
viongozi wa namna hiyo hawawezi kujitoa mhanga kwa maendeleo ya watu wao kwa hofu ya kupoteza umaarufu wao. Hawafikirii mipango ya maendeleo ya muda mrefu kwa jamii zao”.
Rais Kikwete alikwishawaambia viongozi na marafiki zake “tusije tukalaumiana”; tena kwamba “wasidanganyike na tabasamu lake kwa kuwa hana mzaha kwa mambo ya kitaifa”. Je, ataweza kushi kwa usemi wa Rais John F. Kennedy au ni yale yale ya watawala hadi mwisho wa dahari?