Kwako Bwana Michuzi na wadau wa Blogu ya Jamii, Nami nimeona nisipitwe na mjadala huu wa kuelekea Shirikisho la Afrika ya Mashariki.
Kiswahili VS Kiingereza:
Hawa jamaa wamekuwa wanatusema sana kuwa sisi hatujui Kiingereza, lakini ukweli ni kwamba Kiingereza kwangu mimi si kigezo cha maendeleo,nchi nyingi sana zilizoendelea zimekuwa zikitumia lugha zao za asili, kwa mfano Ujerumani,China,Korea, Japan, n.k, Lugha ni lugha tu, ilimradi inatuwezesha kuwasiliana. Sasa sielewi wao wanaposema kuwa hatujui Kiingereza kwao ina maana gain.
Nakumbuka kuna kipindi nilikutana na bibi mmoja raia wa Kenya, nikawa namuongelesha kwa Kiingereza kwa mshangao yule mama akaniomba niongee Kiswahili sana,nilishikwa na butwaa, kwa sababu nilivyokuwa nasikia kwamba Kenya kila mtu anajua Kiingereza hata kama ni mzee,wakati huo nilikuwa sijafika Kenya bado,niivyofika Kenya ndio nikaja kufahamu ukweli kuwa Kiingereza chao ni cha Kawaida kiasi kwamba hata sisi tunazungumza Kiingereza.
Tofauti za Kiuchumi:
Wao waliamua kuchagua Ubepari nasi tukachagua Ujamaa,kila aina ya uchumi ina mambo inayoambatana nayo. Kwa mfano Ubepari unataka kama mtu unakuwa nacho unakuwa nacho sana na kama hauna hauna sana(kabisa), na hiyo ndio hali halisi iliyopo Kenya, kuna watu wana ardhi kubwa sana na hadi vilembwe vyao vinarithi na kuna watu hata hawajui kama vilembwe vyao vitakuja kumiliki ardhi mfano mzuri ni mtaa wa Mabanda na Kibera pale Nairobi, Tanzania hakuna hasa Dar es Salaam mimi sijawahi kuona makazi kama yale, kama nakosea naomba mnirekebishe.
Kiujumla mimi siwalaumu sana watani wa jadi kwa sababu kila kitu kina faida zake na hasara zake wao walichagua ubepari wamepata faida na hasara za ubepari, sisi tuliochagua Ujamaa tumepata faida zake na hasara zake.
Tatizo letu Watz:
Ukizungumzia kusoma watanzania tumeenda shule karibu sawa na hao ingawa inawezekana wao wametuzidi kidogo kwa idadi ya wasomi. Tatizo tulilo nalo ni aina ya elimu tunayopata, sisi tunasoma ili tuajiliwe wakati wenzetu wanasoma halafu wanaangalia fursa zilipo wakati sisi Watanzania tumesoma lakini hatuoni fursa tulizonazo, kwa mfano ili suala la wao kutaka ardhi yetu kupitia Jumuia ya Afrika Mashariki ni kwa sababu wao wameona fursa(opportunity).
Sisi imefikia hata viongozi wetu kama wabunge na mawaziri hawaoni fursa ambayo nchi inayo ili kujua jinsi ya kuzitumia kwa manufaa ya nchi, hii inadhihirishwa na mikataba ambayo viongozi wetu wamekuwa wakisaini, Richmond, IPTL, AGGREKO.
Tuchukue mfano wa Shirika la ndege la Air Tanzania na tulifananishe na Shirika la ndege le Kenya,ona sisi tulivyoshindwa kuona fursa hadi tukauza kwa Shirika la Afrika Kusini na tuona ambavyo Kenya Airways ambavyo imeuzwa sehemu ya hisa kwa Air FranceKLM na tulinganishe hali ilivyo katika mashirika hayo mawili.
Tumekaa tunalalamika kwamba wao watatunyonya lakini suala linabaki pale pale kwamba hatuoni fursa tulizonazo, angalia mahoteli yanavyopewa msamaha wa kodi(Tax holiday) kwa wawekezaji ambao wamekuwa wakibadilishana utawala, hapa tunakumbuka Sheraton,Royal Palm na sasa Moevenpick na hadi leo sijui wabunge wetu wanafanya nini kuona kwamba fursa hiyo inatumiwa visivyo.
Wenzetu wakenya wazuri sana katika kuangalia fursa zilizopo na kuzitumia, waliangalia Mlima Kilimanjaro wakaona kuna fursa ya kuitangaza Kenya kwa kupitia Mlima Kilimanjaro. Je sisi Watanzania tuliona kwamba fursa tuliyonayo tunaibiwa? Kama tuliona tulichukua juhudi gain za haraka kubadili hali? Tulichukua muda mwingi sana, hata sina hakika kama hiyo hali tumeweza kuibadilisha.
Mfano nakumbuka kuna kipindi mwaka uliopita mwezi kama huu nilienda posta kutaka kulipia kodi ya sanduku langu la posta kwa ajili ya mwakani,niliambiwa kuwa hawajaanza kupokea malipo ya mwakani hadi tarehe 1 Januari ndio wataanza kupokea,mimi nilitaka kuwahi kulipa kwa sababu nilikuwa nataka kusafiri.
Sijawahi kuona taasisi inapelekewa pesa halafu inazikataa, katika uhasibu kuna kitu kinaitwa “prepayment” au malipo ya kabla,sikuelewa kwa nini mfumo huo haupo. Baadae shirika likifa kwa kushindwa kujiendesha tunaanza kutafuta mchawi na kutafuta ubia, watu watakaoshiriki katika kusaini mkataba wanakuwa ni wale wale wanaokataa pesa kwa kutakujua “prepayment”. INASIKITISHA SANA.
Watanzania lazima tufike mahala tukubali kuwa hasara moja wapo ya Ujamaa ni kutokuwa na mawazo ya kibiashara ya kisasa, na TUBADILIKE.
Naomba kutoa wito kwa Watanzania wenzangu kuwa malumbano ya kusema wakenya wanafanya hivi,wanafanya vile hayatatusaidia. Kitu kitakachotusaidia kwa wasomi wetu kuna na mtanzamo wa uchumi wa kisasa katika biashara, utawala,n.k. Tanzania leo hii ina wasomi wengi sana, lakini pale walipokaa hakuna tofauti ya kitu chochote katika kile mtu anachokiongoza au kukifanya.
Wengine ni maprofesa na wengine ni madaktari lakini katika sehemu zao za kazi na shughuli mbalimbali hakuna maendeleo wala ubunifu wowote unaopatikana liwe ni shirika binafsi au Serikali, hakuna jipya inasikitisha sana.
Mdau Mtanzania,
Mdau mimi sioni kama sisi watanzania tunalalamika kumbuka hii debate imeanza kwa wao kututukana kupitia article ya Warig, na sisi tunajibu kwa mapana zaidi, nina wasi wasi umeenda nje ya topic tunayodiscuss kuhusu kujiunga kwa Tanzsania ndani ya EAC
ReplyDeleteJembe
hatimae mtu ana akili ya kuweza kutaja matatizo yetu pia sio kushambuliana kwa maneno ovyo ovyo tu kama walevi.
ReplyDeletejapo sikuwa nafuatilia sana huu mjadala,ila nakupongeza mwandishi wa hii article you have got some point in there,
ReplyDeleteMDAU MAJALIWA MIMI NAONA STORY YAKO HAIKUBALANCE NA WALA HUJAFANYA UTAFITI WA KUTOSHA NI MABISHANO NA MAZUNGUMZO YA MTAANI TU. YOTE ULIYOYAELEZA HATA KENYA YANAFANYIKA HIVYOHIVYO. UMEZUNGUMZIA UJAMAA NDO UMETUFIKISHA HAPA SI KWELI CHINA HADI LEO ITIKADI ZAO NI ZA UJAMAA LAKINI WANKIMBIA KAMA TRAIN YA UMEME NA WAKO MBIONI KUMA NAMBA ONE KWENYE MASWALA YA UCHUMI, RUSSIA THE SAME,KUHUSU TAX HOLIDAY KENYA WANAFANYA THE SAME FDIs WANAZIPA TAX HOLIDAY KAMA SISI TUNAVYOFANYA NA KWA TAARIFA YAKO TU BUSINESS KARIBU ZOTE KENYA NI ZA WAGENI WAZAWA NI WACHACHE SANA NI WALE TU WALIOIBIA SERIKALI NDO WANA BUSINESS. KUONA FUSA NA KUIFANYIA KAZI KATIKA NCHI ZA AFRIKA NI KAZI KUBWA WATU WANAZIONA HIZO FUSA LAKINI WANASHINDA KU CARRY ON KWA SABABU NYINGI KWANZA MTAJI, PILI SOKO KWA VILE WATU WETU WENGI HAWANA PURCHASING POWER. KILA SHIRIKA LINA ACCOUNTING SYSTEM ZAKE NA FINANCIAL POLICY ZAO, HIVYO MTU KUKUKATALIA PREPAID HIYO NI POLCY YAO HUWEZI KUWALAZIMISHA. HATA WASOMI WA KENYA WANASOMEA KAZI NDO MAANA WANATAKA KUJA HUKU KUTAFUTA KAZI. STORY YAKO HAINA DATA ZA KU-BACK UP YUOU ARGUMENTS. KAFANYE UTAFITI TENA. KENYA KUNA RUSHWA KULIKO TANZANIA KAMA HUNA HABARI TENA INATISHA, INGIA KWENYE WEB YA TRASPARENCY INTERNATIONAL UTAONA. WAKUBWA WA WALI WAO WALIHAMISHA MAPESA KIBAO KULETA ULAYA, NDO MAANA HADI LEO NI DARLING OF EUROPE.
ReplyDeleteNA UBEPARI NDO UNAONA SASA DUNIA INAVYOYUMBA, NA KAMA CREDIT CRUNCH ITAFIKA AFRIKA KENYA ITACHUKUWA BIG HIT KWA SABABU YA FDIs KIBAO MASHIRIKA MAMA YAKIFA NA MATAWI YATAKUFA PIA.
ReplyDeleteMzee una point sana kuliko Mashaka na Wenzake. Watu hawachangii sana kwa kuwa umenadika kwa kiswahili. Mswahili si Genius! Kasumba bwana. Ukiandika Imla kwa kingereza unaonekana jiniasi kumbe ni abunuwasi tu. Mzee nimependa sana mangilio wako wa hoja na inaonekana umehitimu vyuo kadhaa. Mtu akisoma UK basi anajifanya hajui kuandika imla kwa kiswahili. Acheni makunyanzi lugha ni lugha bora ujue kuchagua pumba na points.
ReplyDeletewewe majaliwa.CHONDE CHONDE CHONNDEE BABA MAJALIWA,NINAKUOMBA TAFADHALI UACHE USHAMBA NA ULIMBUKENI WA KUTUPWA. YANI WEWE UNAJILINGANISHA NA MJAPANI KISA YEYE ANAONGEA LUGHA YAKE NA YUPO SUCCESFUL?IN SHORT,TANZANIA BADO SANA,TUJIKOMBOE KWANZA NDIO TUANZE KUJIPA KIBURI NA JEURI YA KISWAHILI. HICHO KISWAHILI CHENU KIMAWAPELEKA WAPI SO FAR?CHEKI KENYA THEY SPEAK SWAHILI BUT THE OFFICIAL LANGUAGE IMEWEKWA SWAHILLI N ENGLISH AND THEY ARE DOING PRETTY WELL..WHAT ARE YOU TRYING TO TELL US? IF HALF OF THE POPULATION OF TANZANIA SPOKE ENGLISH TUNGEKUWA MBALI SANA..SIO SIRI MY MANAGER HIMSELF CANT SPEAK PROPER ENGLISH ITS SO DAMN SO BAD.ACHENI USHAMBA NYIE WATANZANIA..NA PUMBA ZENU ALA
ReplyDeleteNI KWELI WATANZANIA NI MBUMBUMBU!!!
ReplyDeleteWEWE MAJALIWA WEWE SASA NAONA UMESEMA UKWELI NA PIA NAKUBARIANA NA DADA MMOJA CYNTHIA MASASI AMEONGEA HUKO NYUMA SISI WATANZANIA TUNA SIASA NYINGI SANA HAWA JAMAA WA KENYA WAMETUZIDI SANA HATUWEZI KUJILINGANISHA NAO SABABU ILIYOSEMWA ETI WATA CHUKUA ARDHI YETU NI YA KITOTO SANA KWANI HATUWEZI KUWEKA SHERIA ZA KUZUIA WASICHUKUE? KAMA MATATIZO YA MUUNGANO NI VITA VYA WENYEWE KWA WENYEWE MBONA ZANZIBAR WANA ISSUE KIBAO NA BADO TUNAWABEBA? HAKUNA LOLOTE SISI NI MAMBUMBUMBU ILA HATUPENDI KUAMBIWA TUNACHEMSHA SANA.HAKUNA CHOCHOTE CHA MAANA HATA UPINZANI WENYEWE UMEDOLOLA NA NDIYO MAANA HAKUNA HAKI CCM INAJUA ITAONGOZA MILELE WABONGO WOTE WAOGA KUFANYA MABADILIKO KAZI KULALAMIKA HAKUNA CHOCHOTE UMBEYA TU UMETUZIDI. MIMI NAWAFAGILIA WATU WANAO PENDA MUUNGANO UTASAIDIA SANA KUWEPO NA CHALLENGE YA MAISHA NA IKIWEZEKANA TUJILEKEBISHE. KILA KIYU TUNAUZA MADINI YA ALMASI, MIGODI YA DHAHABU,MASHIRIKA YA UMMA, RELI, VIWANDA, SASA INACHOBAKIA NI KUM-BINAFSISHA KIKWETE, LABDA SERIKALI ITAPATA HELA KUTULIPIA MISHAHARA, AMA TUIUZE BONGO KWA WASOUTH AFRIKANI. KILA KUKICHA KUNA ISSUE MIFISADI NA FAMILIA ZAO NDIYO INAYO NEMEEKA, KUPEANA MAGARI MAJUMBA YA KIFAHARI NA KUPELEKA MITOTO YAO NJE KUSOMA KWA GHALAMA YA WALALA HOI KISA CHA NINI KUKATAA MUUNGANO? USHENZI KABISA HUU ACHA TUCHEKWE NA KINGELEZA KIBOVU SI UNAJUA NYERERE ALIJAZA MIALIMU YA DARASA LA SABA SASA HICHO KINGEREZA TUNGEKIJULIA WAPI YEYE KAFUNDISHWA NA MAZUNGU SISI WALIMU WA UPE! TUTAACHA KUWA MBUMBUMBU? TOBA UZA NA NCHI KWA MAFISADI USIOGOPE KAKA JAKAYA!
Lete data hapa sio longo longo, huwezi linganisha ATC na Kenya Airways, hivi unajua hiyo Kenya Airways ilitokea wapi? Pili kuhusu elimu wala usijisumbue kutulinganisha na Kenya na Uganda, wao wanatembea sisi tunatambaa, njoo na data bwana.
ReplyDeleteLakini nahisi ni wale wale ambao wanapata mshiko kutoka Kenya ili wakipata madaraka waharakishe shirikisho! SI ndio nyie mnaopata msaada kutoka Kenya? Au sio, kifupi tumetoka katika mifumo tofauti ya kiuchumi wao walianza ubepari moja kwa moja, sie ujamaa na sasa tuko kwenye transitions hatujajua bado tunakwenda wapi! Kwa hiyo wache kwanza wakati tunajipanga tujue tunataka ubepari wa kizungu, wa kichina au wa kiarabu tukishachagua aina ya ubepari tukajua tnakokwenda ndio tutazungumza biashara nyingine!
mdau uliyeandika hii ndio wa kwanza mwenye point kuliko wale wengine wanaotafuta umaarufu tuu na misifa bila kuangalia ukweli...wengine point zao eti wakenya wanafanya wanawake wao prostitute,inasaidia nini katika mjadala kama huu na wengine ndio kusifia tuu,jiangalieni matatizo yenu wabongo sio kulaumu tuu na uwoga bila kufikiria ndio maana mafisadi wanamaliza nchi
ReplyDeleteMdau Mtanzania hapo juu, umeongea ukweli mtupu! Yaani sijui tatizo liko wapi ? ni kweli kabisa kuna wakati unashindwa hata kuona tofauti ya msomi wa kitanzania na ambaye hakusoma katika utendaji wa kazi. Lakini tatizo ambalo mimi naona ndiyo limetuweka nyuma ni jamii kuto kuthamini wasomi wake. Utasikia mara kwa mara,' wewe mwache anajifanya amesoma tutumuonyesha kazi ' anajidai kasoma sasa tutaona, tofauti na hizi nchi ambazo tunaishi huku ughaibuni. Msomi unathaminiwa na watu wanataka kukuiga, na mwajili anataka kujua utaleta mchango gani katika kampuni yake.Na ambaye hakusoma anatakiwa aenda shule wala si kulogana na kukuta kichwa cha kuku kwenye ofisi yako na masizi kwenye kiti. Hili lilikuwa ni tatizo kubwa na bado lina sumbua sana wasomi. Na hili, lili sababisha hasa hiki kizazi ambacho sasa kipo madarakani kutojari sana kuonekana umesoma kiutendaji, na kuonyesha tofauti kati yako na ambaye hakusoma. watu waliogopa kutengwa na kulogwa au kuambiwa ana jidai kasoma huyo. Itachukuwa muda kwa mtanzania kufanya vitu kulingana na Elimu yake. Huku ughaibuni utakuta kuna hata makazi ya watu walio soma tu, utaambiwa hapa wanakaa ma-professor wengi sana nk.
ReplyDeleteAsanteni sana,
Mwakipesile
WATANZANIA WENGI HAWATAKI SHIRIKISHO HILI HAKUNA FAIDA KWETU,TULIKWISHA KUWA NA MAKOVU ILIPOVUNJWA 1977,TUNAHITAJI MUDA KAMA MIAKA 20,KWA NINI TANZANIA SI WAUNGANE WAO KWANZA TUNAMATATIZO YETU YA MUUNGANO WA ZANZIBAR WAKATI HILI HALIJAISHA TUNAINGIZWA KWENYE MUUNGANO MWINGINE,HII HAITUSAIDII
ReplyDelete......ISMA KABENGO,KAMPALA
Nakubalia wewe Mtz kwa asilimia100% Nyie watz ongezeni juudi vinginevyo mtakuwa ni nchi ya mwisho afrika eti, kwasasa tz ni ya mwisho East Afrika kiuchumi ya kwanza ni Kenya ya pili ni Uganda ya tatu Rwanda ya nne Burundi nyie ni wa mwisho japo nyote nchi yenu ina resources mingi sana lakini mme laala tuu na huyo jk wenu mliye mchagueni kwasababu eti ni handsome nikuambieni ukweli watu wengi watalii hawaji kwenu kwasababu hamna kwa kufikia na wanajua mlima kilimanjaro upo Arusha. Watanzania amkeni mpo chini sana jamani
ReplyDeleteMajaliwa jana nilikuwa naangalia program moja ya Ngugi Wa thiong'o a very well known author from Kenya kuhusu maisha yake na kurudi kwake kenya baada ya miaka ishirini na zaidi. Ngugi Wa Thiong'o as kenyan alisema kuwa lugha ya kiingereza sio kigezo cha nchi kuwa na maendeleo. Lugha ya kiingereza ni lugha kama zingine tu kilichozidi ni kwamba imeenea nchi nyingi duniani. Ngugi anaamini maendeleo yoyote yanaweza kupatikana kupitia lugha yoyote na ali comment jinsi lugha ya KISWAHILI inavyokua, kwa mtazamo wangu naona hata yeye anaamini KISWAHILI kinaweza kutumika na nchi ikaendelea. Kama unavyosema si kwamba wakenya wote wanaongea kiingereza wapo wengi tuu ambao wanaongea kiswahili tena kibovu zaidi lugha ambazo wanaziongea vizuri ni za makabila yao.
ReplyDeleteKuna mkenya mmoja alihojiwa akasema watu sio kwamba hawana uwezo wa kufikiri na kufanya mambo tatizo wanalazimisha/wanalazimishwa kufikiri kwa lugha ya kiingereza ambapo mwisho wake inakuwa kikwazo kwa mtu kupanua mawazo yake, hapa unakuta hata wao since kiingereza is not their mother tongue at some point huwa inawapa vikwazo, na hii ni kwasababu wanalazimisha hawataki kukubali kwamba wanaweza kutumia lugha ingine na wakafanikiwa.
Dada mmoja alihojiwa uganda akasema watoto mashuleni wanapigwa ama kuwa suspended kwa kushindwa kuongea kiingereza huu ni unyanyasaji mkubwa.
Amini usiamini baadhi ya wakenya na waganda wanajua vizuri sana kwamba kiingereza is not an issue kwa maendeleo ya nchi ila ni fikra potofu tu ambazo zimesha jengeka kwa baadhi ya watu.
KIDUMU KISWAHILI
MDAU UMENENA UKWELI KABISA WABONGO TUMEKALIA KULALAMA SIO MBUMBUWASIO NA SHULE BALI HATA WASOMI SASA WAMEISHIA KULALALAMA KILA KUKICHA WANAISHIA KUTOFUMBUA MACHO WAJE NA MAMBO MAPYA ,UKIWAKUTA HAO WASOMI WAPO BONGO UTAFIKIRI MSHAMBA FULANI KATOKA KIJIJIN MAANA UNAKUTA NI DR AU ENGINER ANAPAMBANA KUFUNGUA VIBANDA VYA KUUZA SABUNI NA CHUMVI MLANGONI MWAKE BADARA WASHINDE MAABARA WATOE MAVITUZI YA MAANA AU WATUJENGEE MAGOROFA YA MADARAJA MIJINI AU WAPANGE MIJI YETU IWE KTK MPANGO MZURI EBU MIPANGO MIJI YETU MFANO DAR DA UTACHEKA SI ULICHEKI MAJUZI BROMICHUZI ALITUONYESHA MJI WA DAR UNAVYOONEKANA MIPANGO MJIIIIIIII HAHAAH WABONGO TUNAUZIIIII TUNASHINDWA KUANDAMANIA VIONGOZI WETU WAPUUUZI TUWAPIGE CHINI WOTE MAANA HAPA HATA UTAWLA UNACHANGIA CCM INABIDI ITOKE KWENYE UTAWALA NA TUANGALIE CHAMA KIZURI CHENYE WAGOMBEA WAZURI ILA BADO SIJAONA PIA CHAMA KIZURI HADI SASA BONGO YETU KINA OBAMA SIJAWAONA BADO KABISA VYAMA VYA UPINZANI VYOTE NI CCM TYPE MAANA VINAFUFUKA NYAKATI ZA UCHAGUZI TU PAMBAVU KABISA WANANCHI EBU TUANGALIE USTAARABU HATA WA KUUNDA CHAMA KIZURI WASOMI JAMAN MUINGIE MSITUNI MUIKOMBOE TANZANIA YETU INABIDI HAPA TUINGIE MSITUNI TUUNDE WAJESHI KINA MKAPA WALE NI KUSHIKA NA KUINGIZA JERA RADA AMAKULLA NA WAPUUZI WENGINE KINA LOWASA WOTE PIGA SANA WEKA JERA NA KINA NANII WOTE YAAANI INANIUMA DA NATAMAN NINGEKUWA JESHINI LEO HII NIGEASI NITAFUTE WAPAMBE NIPINDUE SERIKALI ILIYOPO MADARAKANI MAANA NAONA WANALETA KINYAA TU MIAKA 47 YA UHURU HAKUNA JIPYA LOLOTE HADI LEO TUNARUDI N YUMA BADARA TY AKWENDA MBELE
ReplyDeletenakuunga mkono ndugu yetu MAJALIWA. ni kweli ulichokisema nami sina pingamizi juu ya hili, kwani viongozi wetu wa sasa na hata wajao(kwa sababu mtu yupo serikalini 40 yrs) unategemea nini kitabadilika?.... hatuwazi mbele hata kidogo ndio mana tunakuja kutafutana baadaye wakati tungeweza kuliweka sawa kama wenzetu Kenya na faida tukaipata baadaye.
ReplyDeleteViongozi wetu kama mnazisoma hizi comments ltakuwa fudisho la kesho na kesho kutwa.
lyimo75@gmail.com
WEWE tmajaliwa MBONA UNAJIFANYA MZUNGU! SISI MALUMBANO NI KAWAIDA YETU KWANI YANACHUKUA NAFASI YA KUFANYA KAZI, TUSIPOLUMBANA TATAFANYA KITU GANIA KINGINE? VINGINEVYO TUKACHEZE POOL AU TUKAIMBE BONGO FLAVA. WAACHE HAO WAKENYA WAFANYE KAZI NA NJAA ZAO NANI ANATAKA MAENDELEO? MBONA SIMU TUNAZO BWELELE. WALIPOTUCHOKOZA HAWAKUJUA KUWA MIDOMO YETU IKO FULL CHAJI?
ReplyDeletehao ha hao wakenya hao mh haaaaaa leteraha mich lete raha lete rah nasisi tukupe zetu aaaaa tingisha kisigino achia kidogo mh ! miena natanzania halo masikio yameziba halooo kajaribuni kwingine HAPA HAMUONI NDANI WACHA WACHA WASEME WATASEMA MCHANA EHHH USIKU WATALALA KAZI MNAYO WAKEYEEEE MPOOOO KATAKATA KATA KATAMWANAGU KATA TARATIBU TARATIBU MPAKACHINI MPAKA CHINI APOOAPOOA HEBU WE MTUTHI NIACHIE NICHEZE WIMBO WA KWETU KWENU HAKUELEWEKI HAAAAAA MICHU NIPERAHA TANZANIA NIPERAHAAAAAAAA
ReplyDeleteao wajapan kwani walilala na kuamka ghafla wakawa matajiri???ni process bwana!!!
ReplyDeleteso ata Tz kiswahili kitatuvusha tuu,sio ati adi kiinglishi ndo uendelee.
bugger
ALUTA KONTINUAAAAA
jaman ATC imekufa 11Dec 08,,,kazi kweeli
Wewe unaesema watanzania mbumbumbu labda wewe ndio mbumbumbu na watu unaowajua wewe, mimi ni MTANZANIA NA SIJIONI MBUMBUMBUMBU hata kidogo matatizo ya rushwa, uzembe, ufisadi n.k nakubali yapo, hayo yanafanywa na ma greedy lakini sina infiriority complex kuwa eti sisi Watanzania ni Mambumbumbu na Wakenya sio mambumbumbu eti kwa vile juzi juzi waliuana kwa kuwa uchaguzi hakueleweka, hiyo wewe tu, ndio mbumbumbu na ukipenda hamia Kenya kaishi huko huko, na wala sioni kama tunalalamika tuna discuss, sasa anaesema Watanzania wanapenda kulalamika huyo nae simuelewi, nyie mlitaka Wakenya kila wanachosema TUKUBALI? HE!!! Jembe
ReplyDeleteMICHU OH MINA LIA MMMMM WATANZANIA TUNACHEKA HAAAAAA.
ReplyDeleteJAMANI WAPAMBE MPOOOOOOO WAPI MIKONOZI UPO UKWENI UTAKWENDA KWELI AU NDO KIMAVI KINAINGIA ?
Mimi sioni sababu ya kuzungumzia IPTL,EPA n.k kwenye topic ya EAC integration na MATUSI ya Getau Warigi! Kila mahali duniani hata hapa Marekani kuna wezi!In Kenya,they stopped one Minister for Corruption,right!Here in the USA,you hear about the Ilinois Governor,right!So,why are you helping Warigi though! Haya ni matatizo ya ndani ya nchi,since no society is perfect!Stick to the EAC issue,NOT internal problems!Insert your Nose to the essay please! I will really appreciate that!
ReplyDeleteChakubanga
Watanganyika wa TANU Mpo....Watanzania wa CCM Mpo...Wabongo wa Vyama Vingi MPO...
ReplyDeleteHii ni nusu ya kutaka kuwakumbusha tulipotoka na tulipo kwa sasa.Na pia nataka niwakumbushe ndugu zangu kuwa kutangulia sio kufika,kuhusu hawa jirani zetu sio kwamba wamepiga maendeleo kuliko sisi kwani maendeleo sio kwa watu wachache kuwa matajiri na majendo mengi ya fahari.Na muangalie sana kwani majengo mengi ya hawa jirani zeti sio mali yao bali watu wa nje na wameyakodisha kwa raia wenye nchi mpo hapo jamani.Kuhusu lugha nadhani sisi ni watu shupavu na mimi nikiwa mmoja wapo ninajivunia lugha yetu na ninaithamini sasa na hasa kwa sasa dunia invyokwenda.Mimi ninaishi nje ya nchi na mara nyingi wenyeji wangu wananiuliza niwafundushe lugha yangu kwani wao wanajua kiingereza tu, pili kwenye state moja marekani inayoitwa Hawaii wanazungumza lugha ya wao na kiingereza, lakini cha kushangaza na kwamba lugha yao imeanza kuenea sana kwenye University haswa kwenye timu za Football na Basketball.Halafu lugha ya kichina na mojawapo ya lugha inayokuwa haraka sana Ulaya na Marekani,Kwani wanafunzi wanaokwenda kusoma china toka marekani imeongezeka kwa kiasi kikubwa sana kwa sasa(wanajifunza kichina).Kwa sasa tuondoe kabisa haya mambo kuwa kiswahili imeturudisha nyuma.Naomba niulize ndugu zangu Maendeleo ni nini? Ni kuongea kiingereza,kuwa na manyumba makubwa mijini,kuwa na viwanda vinavyomilikiwa na watu wa nje,nchi kuendeshwa na mataifa makubwa?Na pia kuacha baadhi ya watu wa chini kuwa na misha mabaya kuliko?Tanzania yetu ni nzuri hatuna makuu tunakuwa polepole kama mwendo wa kobe,tusifanye makosa kama hawa jirani zetu.