Mambo yameendelea kuwa magumu kwa mawaziri wawili wa zamani Basil Mramba na Daniel Yona baada ya juhudi za kuwatoa rumande kukwama tena jana.


Washitakiwa hao wawili ambao wanadaiwa kuitia hasara ya Sh bilioni 11. 7 serikali, walishindwa kupata dhamana baada ya Mahakama ya Kisutu kugoma kusikiliza shauri lao kwa maelezo kuwa taratibu za mahakama zilikiukwa.


Hakimu Hezron Mwankenja ambaye anasikiliza kesi hiyo, hakuthubutu kuwapandisha kizimbani washitakiwa hao, baada ya kung’amua kuwa hakukuwa na hati ya kuwapeleka mahakamani hapo (Remove Order).


Hakimu huyo pia alisema hata jalada ambalo lilitoka Mahakama Kuu, halikuwa na amri ya Msajili au ya Jaji inayomtaka yeye kusikiliza shauri hilo kwa siku ya jana, kitendo ambacho kilimfanya kugoma kusikiliza shauri hilo.

soma habari kamili kwa
kubofya hapa


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hapo sasa ndipo panaanza kunoga.
    Maafisa wa magereza tuelezeni, ni nani aliyesema watuhumiwa hao watolewe gerezani ? Na removal order ilitolewa na nani ? Nani ilitia saini yake ?
    Au ndiyo kule kufanya kazi kwa kutumia uzoefu tu?
    Hongera hakimu kwa kufuata taratibu za kisheria.Ama sivyo tungeshuhudia sheria ikiburuzwa kama wote hatujui kusoma wala kuandikwa.

    ReplyDelete
  2. Yay! For the Judge. Wamezoea shortcuts kwa vile ni wakubwa na wana hela walizania watafanyiwa kila wanachotaka haraka haraka. Panga foleni kama wengine

    Tukiwa na majudge kama hawa kumi tu Bongo tutafika in no time

    ReplyDelete
  3. Inaonekana jinsi gani tangu Nyerere atuondoke, viongozi wanaonekana tofauti sana na yeye. Mramba anajua sana uongozi ni nini. Mramba na Yona, pia na wote walioiibia nchi waadhibiwe kama wananchi wengine. Nashukuru imefikia hapa leo, sheria zifuatwe wazi na kweli iwe wazi kwa kila mtu. Ninachoogopa ni kupinda sheria kwa ajili ya viongozi wakubwa. Najua sana wanapesa na watapata wanasheria wazuri wa kuwatetea. Serikali haiwezi kufanya kazi kama watu tunaowaamini hawafanyi kazi inayotakiwa. Serikali itatoaje huduma kwa wananchi kama hainafedha na umaskini unaendelea kila siku. Umaskini unakufa kama tutawaadhibu wote wanafanya vitendo kama hivi, hii ni mfano kwa kila mtu na vijana wanategemea kuingia kwenye uongozi baadae. Tusioogope mabadiliko, hii ndivyo inchi inaenda pazuri.

    ReplyDelete
  4. sheria kweli ifuatwe. lakini watu wa mahakama wanapofanya makusudi ku-skip baadhi ya procedure makusudi kwa kuwa hela inahitajika ili wanyooshe mambo yaende YANAVYOTAKIWA nao ni upuuzi

    ReplyDelete
  5. HAYA MAZIMWI YANAJUANA NDIYO SABABU HAYALANI YAKAMALIZANA. MBONA WAHALIFU WADOGOWADOGO WAMEJAZWA RUMANDE BILA YA KUPUNGUZIWA HIZO DHAMANA ZA SHILINGI ELFU ISHIRINI? KWANINI WANYONGE TUSIJITOLEE KUFUNGWA KWA NIABA YA HAWA MAFISADI ILI TANZANIA IJIJENGEE HESHIMA KUWA SHERIA IMECHUKUA MKONDO WAKE? TUPACHIKWE MAJINA YAO KISHA HUKUMU ZITOLEWE BASI, CCM NA SERIKALI YAKE ZIPATE SIFA KAMA WALIVYOMPORA SLAA NA ZITO KUWA SI WAO WALIOFICHUA UFISADI, NA KUSAHAU KUWA WALIWATISHA KUWAPELEKA MAHAKAMANI KWA KUUDANGANYA UMMA KUWA KUNA UFISADI.

    ReplyDelete
  6. Najua serikali yetu ya Tanzania inamatatizo. Vitu ni vingi vya kurekebisha na lazima tuanze mahali, hili swala la rushwa na wizi moja ya tatizo kubwa nyumbani. Tunahitaji viongozi wakweli na wanaojua kinachofanyika, hata Marekani na nchi zingine kuna rushwa bali wenzetu wanafuatilia haraka itokeapo. Kuna mazingira mengi yanachangia rushwa na ninaomba serikali ibadilishe jinsi inavyoendeshwa. Vitu viwe wazi na kila njia kuwe na check and balance. Nchi yetu hatuna systems za open kabisa, mfano ukinunua kiwanja ofisa wengi na wote wanataka uwape pesa. Kwanza umelipia kihalali na umeiingizia serikali pesa then utoe rushwa kupata kibali chako. What is this! Is this suppose to be this way or other wise. Nimenunua kiwanja na mpimaji anataka nimlipe, nitafute gari ya kumpeleka kwenye site, then anataka pesa ya lunch. What hek! It should one office and if I have to pay I should pay one place to Cashier Window. I am sure someone can design something like this, this is just an example to remove loop holes that promote corruption appetites. We have to come up with solutions and increase government revenues and more people will be employed. I belive we can resolve some of these issues. We cann't use the same routes and expect different results. Walk up people!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...