gray mgonja akiwa mahakami kisutu leo kabla ya kusomewa mashataka yake sasa hivi. chini akiingia chumba cha mahakama akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi na magereza
KATIBU MKUU WA ZAMANI WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO GRAY MGONJA AMETINGA KIZIMBANI SASA HIVI KATIKA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI YA KISUTU HAPA DAR KUJIBU MASHTAKA MBALIMBALI.
MGONJA ANAKABILIWA NA SHTAKA LA KUITIA HASARA SERIKALI YA BILIONI 11 PAMOJA NA KUTUMIA VIBAYA MADARAKA YAKE.
MGONJA ANATARAJIWA KUUNGANISHWA NA MAWAZIRI WA ZAMANI BASIL MRAMBA NA DANIEL YONA KATIKA KESI YAO.
AMEWEKWA RUMANDE HADI KESI YAKE ITAPOTAJWA TENA DECEMBER 29, 2008 BAADA YA KUSHINDWA KUTIMIZA MASHARTI MAGUMU YA DHAMANA IKIWA NI PAMOJA NA SHILINGI BILONI 5.9 NA WADHAMINI WAWILI PAMOJA NA KUSALIMISHA HATI YA SAFARI NA KUTOTOKA NJE YA DAR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 45 mpaka sasa

  1. Hahahahahahahaaaaaaaaaaaa!!!!!!! Michuzi ndio maana unapenda Fulanzzzzzzz! Nitakusawadia nyingine ukija A- Town. Walahi nitakusawadia. Duh! Amakweli ukila uvute mdomo! Hili lifisadi limefikishwa mahakamani? Aisee basi mambo safi>

    ReplyDelete
  2. Yes,

    Mmoja baada ya mwingine,

    Kudadadadadeki,

    Stars Tupe raha wanamichezo,

    JK tupe raha raia wema,

    Huuuuureeeeeeeyyyyyyyyyy!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  3. Duh!Si ndiye huyu majuzi tu tuliambiwa amestaafu kwa mujibu wa sheria? Wamesubiri astaafu kwanza. Hii kali

    ReplyDelete
  4. Many more are expected! Nasi tunazidi Kuomba Mungu awaweke wazi peupe kabisa!

    ReplyDelete
  5. weweeeeeeeee patamu...

    ReplyDelete
  6. Sssshss hii ni pati ya kimya kimya taratibu kila kitu kimya kimya. AAA nani huyo anapiga honi si apaki kimya kimya. Mafisadi nao wanakamatwa kimya kimya. Duu hii kweli kimya kimya.

    ReplyDelete
  7. Wiziiiiiiiiiiiii Mtupu.

    ReplyDelete
  8. hiki ni kama kiini macho hakuna lolote litakalofanyika atapatiwa dhamana halafu kesi kupigwa dana dana mpaka watanzania wasahau. wataofaidi ni hao maafisa wa mahakama kwa posho pamoja na hongo za kurekebisha masharti ya dhamana kama ilivyofanyika kwa mafisadi wa EPA. tumechoka na michezo ya kitoto

    ReplyDelete
  9. hiki ni kiini macho kingine unafikiri kuna cha maana kitakachofanyika zaidi ya kupewa dhamana? halafu kesi kupigwa dana dana hadi watanzania watakaposahau. Kumetokea nini kwa mafisadi wa EPA? wote wako nje kwa dhamana wanakula kuku. vitu kama hivi vinafaidisha vyombo husika vya mahakama kupata posho na hongo kutokana na marekebisho ya masharti ya dhamana. tumeshaushutukia mchezo huu we need to do more and seen to be doing something.

    ReplyDelete
  10. Hongera JK, ila usisahau wana-Kigoda nao pia IPT, Richmond na Tan Resorce yaani wana-Kiwira. Ukitekeleza hayo utawapiga bao upinzani kabisa!

    ReplyDelete
  11. hapa ndipo misupu aka misoji aka michuzi tunakupendaga, Endeleza libenekeeeeeeeee.

    Libenekeee woyeeeeeeeeeeeee


    Mdau London

    ReplyDelete
  12. Tunaomba isiishie kwa kuwapa mafisadi dhamana na kesi kuisha kiaina, JK we need to see more action.

    ReplyDelete
  13. NAONA JK ANATUPA KARAHA ZAIDI YA KUTURIDHISHA TU KUWA WAMEPELEKWA MAHAKAMANI ...MWISHO WAKE NI NINI???? WADAU NISAIDIENI HATIMA YA KESI ZA MRAMBA NA YONA...??????SIKUWEPO TUTANI NILIKUWA BONDENI RUKWA KUANGALIA SHAMBA LANGU LA MPUNGA..

    MKOMBE...SUMBAWANGA.

    ReplyDelete
  14. Hawa ndio Askari wa Miamvuli awamu ya tatu. Kama sio IMMUNITY, nadhani wangeanzia juu kushuka chini. Angalau JMK anajitahidi, tumpe support!

    ReplyDelete
  15. Huu mchezo ni kiini macho,siamini kama hizi kesi za vigogo wanaotuhumiwa kwa ufisadi zitaisha!Hizi ni mbinu za kujikosha kwa wafadhili tupate misaada,ila mwisho wa siku hawafungwi hawa!Bado inahitajika u-serious wa kutosha ktk hii vita.Namaanisha ukitaka kumuua nyani.....!!

    ReplyDelete
  16. NCHI YENYE UTAWALA WA SHERIA WATU WAKITILIWA SHAKA HUPELEKWA MAHAKAMANI WAKAPEWA NAFASI YA KUJITETEA WAKISHINDWA WANACHUKULIWA HATUA. HIVI WALE WENYE KUSEMA KIINI MACH WANATAKA RAIS YEYE AWE POLISI DPP NA HAKIMU?? TUJIFUNZE KUSHUKURU PALE VIONGOZI WETU WANAPOFANYA KAZI KWA UFASHA NA INAVYOTAKIWA BADALA YA KUMLAUMU NA KUMKEJELI.

    ReplyDelete
  17. Hawa jamaa wa police/magereza vipi?
    Huyo si mtuhumiwa? PINGU ziko wapi?
    Anakaa mahakamani kama yuko nyumbani kwake?

    Kwa usalama wa JAJI, WAFANYAKAZI na WANANCHI wengine, hawa wahalifu wote lazima wafungwe pingu kwani wanastahili hivyo. Walipewa uhuru na dhamana ya wananchi lakini wameitumia vibaya.

    ReplyDelete
  18. Eeeh bwana eeeeh sasa ufisadi noma washikaji!!!
    Hata huyu kaswekwa?
    Kweli JK kiboko atakuchekea weee...
    Kumbe jiwe linapata moto!
    Serikali sasa itapata heshima na sio kama watu walivoanza kusema " ni ya kishikaji.."
    2010 kura yangu anayo wakirudisha bulungutu la wananchi.

    ReplyDelete
  19. Kinachotakiwa ni kwa hatua zaidi kuchukuliwa. kupelekwa mahakamani hakutoshi. ila kwa sasa tunarejesha angalau imani kwa JK kuwa ana mwelekeo, pamoja na kwamba hatma ya waliokatwa haijulikani.

    ReplyDelete
  20. We tata usimwangalie huyu atakufidhadi kabisaaaaaaaaaa! Acha ale chake. hatakama hawavungwi lakini chamoto wamekiona. Hureeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  21. Watanzania wenzanngu, Kinachonipa wasiwasi ni kwamba hizi kesi zitachukua miaka mingi sana. By the time wanamaliza, kama kweli watamaliza, tutakuwa labda na serikali awamu ya sita,maana hii ya tano atachukua JK. Je huyo raisi wa serikali ya awamu ya tano atazipa uzito kesi za mafisadi? au watu wake, au hata yeye, atazihujumu na mafisadi wote wakaishia kushinda na kuachiwa huru? tunamjua raisi huyo atakuwa nani? vipi kama atatoka mtandao wa mafisadi? Mhh!!!!!!!

    ReplyDelete
  22. Naona mambo yanazidi kuwa mambo. Hawa akina Mgonja waliifanya wizara ya fedha na kodi zetu kuwa shamba la bibi. Ngoja vianze kuwatokea puani. Ngoja sheria ichukue mkondo wake ili liwe fundisho kwa walio kwenye madaraka na wanatumia nafasi zao kuhujumu mali ya umma. Inaweza kusaidia angalau hata kidogo maana hali ilikuwa imefikia pabaya. Mtu anaamua tu kufanya jambo lolote analojisikia ili mradi tu ni mali ya umma. Inasikitisha sana.
    Pia ninyi anonymous hapo juu mnaosema kiini macho mlitaka kesi iendeshwe ndani ya masaa 12 tayari hukumu? Mahakama ina utaratibu wake wa kufanya kazi. Kuna DPP kupeleka mafaili mahakamani, watuhumiwa kusomewa makosa yao, ushahidi kuwasilishwa mahakamni,watuhumiwa kujitetea na baadaye wakionekana wana hatia hukumu hutolewa. Hilo linaweza kuwa zoezi hata la miezi sita au zaidi. Hivyo unaposema "kiini macho", mlitaka JK akawakamate watuhukumiwa na yeye huyo atoe hukumu mara moja? Je huo utakuwa utawala wa sheria kweli? Tuipe muda mahakama ifanye kazi zake. Tunawaamini mahakimu, majaji na wote waendesha mashitaka. Tuwe na subira!!
    Mdau

    ReplyDelete
  23. Naaam kazi iendeleee hadi fisadi wa mwisho afikishwe mbele ya sheria. JK kaamua kutimiza wajibu wake kama msimamizi wa maslahi ya Watanzania sio kikundi cha wabadhirifu serikalini. Tumuunge mkono maana vita hii sio ndogo.
    hakuna nafasi ya kukejeli pale mtu anapotimiza majukumu muhimu, wale wasio na imani kwa mazoea yao ya ubabaishaji, wanyamaze wasubiri matokeo. zaidi WATANZANIA tujifunze kuheshimu na kuzingatia taratibu tulizojiwekea za utawala wa sheria.
    Mapambano yaendeleee hadimaadili yarudi na nyumba za serikali zirudi pia!! JK Oyeeeeeeee
    MDAU, Oslo Norway

    ReplyDelete
  24. ...kiina macho kivipi? yaani jamaa wamefanya dili na serikali ili ionekane iko serious? nani atakubali kuchafua jina lake na CV yake kwa ishu kama hizi? career-wise hapo ndo end of the road....hata wewe ukipewa dili kama hiyo ingawa huna umaarufu au CV kubwa ya kuilinda utakubali? sembuse public figures like Yona, Mramba, Mgonja etc..! Jamaa wako serious, hawa wanachinjiwa baharini kikweli kweliii....!

    ReplyDelete
  25. Misupu hebu tuambie ukweli eti na Mzee wa Vijisenti (Chenge) naskia nae amekamatwa na kuzirai! ni ya kweli hayo?

    ReplyDelete
  26. Kidogo inaleta changamoto lakini hizo kesi mwisho wake nini na lini maana watanzania wengi tuna vichwa vya panzi tutasahau na hatutajua hatua zilizochukuliwa. Cha msingi sasa ni kinachofuata nini.

    ReplyDelete
  27. Watanzania wenzangu. Subira ya vuta heri.Kesi huchukua muda kufikia maamuzi na pia ni matarajio yetu haki itatendeka na itaonekana kutendeka katika kesi hizi.
    Mungu ibariki Tanzania

    mdau USA.

    ReplyDelete
  28. NYIKA NA VOME........!!!

    ReplyDelete
  29. Kwa wale wote mnaosema hiki ni kiini macho naomba kuwapa challenge. Ninawaomba mjisimbue kidogo tu na kutumia bongo zenu kufikiria kuliko kuongea haraka haraka. Hivi ni nani katika hawa waliopelekwa mahakamani anaenda pale kwa hiari yake mwenyewe kucheza mchezo wa kuwapumbaza Watanzania? Kupelekwa mahakamani sio mchezo, achilia mbali kuitwa mshatikiwa. Tatizo letu ni kwamba tumekuwa washabiki...tunakurupuka tu, wengi wetu tumekuwa Tomaso yule wa kwenye agano jipya. Ni kitu gani hapa ambacho hakionekani wazi? Hawa jamaa wapo chini ya ulinzi na wanalala rumande. Sheria za mahakama zetu zinaruhusu washtakiwa kupewa dhamana, na kesi ya aina hii ina qualify kwa dhamana kama mshtakiwa atakidhi matakwa ya hiyo dhamana. Mlitaka wakafie gerezani? Mimi siwa support mafisadi lakini naona hata kwa huu ujasiri wa Raisi Kikwete bado wengi wetu tunakatisha tamaa katika hizi juhudi za kupigana na UFISADI. Ni kiongozi gani katika historia ya nchi amewahi kuwafungulia mashtaka vigogo ndani ya Serikali. Jibu ni hakuna. Siku za nyuma tulizoea kusikia mahakimu wa mahakama za mwanzo, makatibu tarafa, wenyeviti wa vijiji, etc., watu wadogo wadogo tu wakifikishwa mbele ya sheria kwa ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma. Sasa tumekuwa tukililia big fish..tumepewa, bado tunapiga kelele eti changa la macho. This is insane!
    Suppose hili ni changa la macho. Ni nani ananufaika? Unafikiri Kikwete ni mjinga kuweka career yake ya Uraisi on the line kwa ajili ya "maigizo"? Tunatakiwa tuelewe kwamba hawa watu waliopelekwa mahakamani wale raia na hawa vigogo ni watu wenye mifuko mirefu. They are all wealthy people. Sifa kubwa siku zote ya watu wenye hela ni kwamba wana EGO. Hawa watu wanaishi kwenye ma mansion zao maeneo mazuri tu, leo hii wanaenda kunyea ndoo gerezani pamoja na kuchanganywa na vibaka wengine..unataka uniambie bado ni changa la macho? Siamini, I think Mr. Kikwete is for real na ninafikiri ni wakati sasa wananchi tuwe na imani.
    -Phatlorenzo, MN-

    ReplyDelete
  30. JK ndio baba lao,piga lupango wote,hao wanaosema ni kiini macho ni chademaanaendeleza siasa zao chafu yadi humu kwenye blogs,ni aibu kwa viongozi wa upinzani mlokuwa mnalalmika kuusu ufisadi now mko kimya hata hamuipongezi serikali kwenye hili,hivi kina ana kilango macelela wako wapi now,mbona wamenyamaza kimya,wao si ndo walokuwa wanangangania mafisadi wachukuliwe hatua,hapo ndtakapojua walikuwa wanaendeleza siasa chafu kwa maslahi yao,asante usalama wa taifa kwa kuzifuatilia hizi kesi kwa ukaribu,JK tupe raha weka ndani wote ili hata hao wanabu kukuhujumu kwa kukuchafua wajue wewe ni rais wa masikini na sio mafisadi.BRAVOOOOOOOOOOOOOOOO

    ReplyDelete
  31. Wale wote tunaojihisi kuwa mafisadi inabidi tuandae pochi ya kutosha, tujiweke sawa kwa ajili ya dhamana. Mambo kwa sasa hivi si mazuri kabisa.

    ReplyDelete
  32. JAMANI TUNAOMBA WANASHERIA TUFAFANULIENI. WENGI WENU HUMU TU MAMBUMBUMBU WA SHERIA. HIVI HIZI KESI ZA EPA NA MIKATABA MIBOVU SI NI KESI ZA UHUJUMU UCHUMI? ZINASTAHILI DHAMANA KWELI? TUNAOMBA KWA KIFUPI MAONI YA WANASHERIA.

    ReplyDelete
  33. Misupu naomba uanzishe huu mjadala! Yusuf Manji wa Yanga yuko wapi sasa? Mbona mgazeti yako kimya?

    Nataka kujua hata kama hali yake bado ni tata

    ReplyDelete
  34. Dah, inanikumbusha picha za kihindi, akina DHARMENDRA, SHASHKAPUR NA DILIP KUMAR!!!!!

    Patam hapo.

    ReplyDelete
  35. mdau anonymous wa Tarehe December 15, 2008 3:13 PM umesahau majina mengine ya mheshimiwa
    MKUU WA WILAYA YA TEGETA A.K.A BALOZI WA ZAIN A.K.A MITHUPU A.K.A MIGRAVY :-) kumradhi kaka michu ila unatufurahisha sana wadau tulio mbali na nyumbani kwa kutupa nyuzi laivu and brekingi!
    MIGRAVY OYEE
    mdau sweden

    ReplyDelete
  36. Mgonja, Mramba na wengineo wamesaini mikataba mingi iliyoliingizia taifa hasara kubwa (kuhujumu uchumi). Kinachoshangaza badala ya kufikishwa mahakamani kwa makosa ya kujumu uchumi (EPA, IPTL, Radar, Ndege ya raisi, Netgroup Solution, nk, nk) wote wanahusika. Sasa kwa nini wanapelekwa mahakamani kwa kosa moja wakati wanayo zaidi ya 10?

    Nadhani hapa hiki ni kiini macho, baadaye utasikia wameshinda kesi kwa vile 'hakukuwa na ushahidi wa kutosha' (baada ya uchaguzi wa 2010). Watanzania kuweni macho na hili changa la macho.

    Wana sheria na Vyama vya upinzani, naomba mpeleke pingamizi mahakamani kutaka washitakiwe chini ya mashitaka ya uhujumu uchumi.

    ReplyDelete
  37. mwali mwali mwali!
    ca-boy

    ReplyDelete
  38. Phat Lorenzo,

    Nakubaliana na wewe kiasi kidogo kuwa sasa tunaelekea Mahali, Lakini kumbuka kuwa hawa wote wanaopandishwa kizimbani ni kundi la pili ambalo halikuwa upande wa muheshimiwa wakati wa uchaguzi. Hawa walikuwa upande wa Mkapa wakiwa na dhumuni la kumuweka Sumai kwenye kiti hicho. Ambao ndio inasemekana walianzisha fyoko fyoko za Richmond Ili kumuharibia Mkuu asipate tena 2010. Na yeye sasa anawarudia na mbio hizi zinamuelekea Mkapa kama ukichunguza vizuri. Kwahiyo mimi naona huu bado ni mchezo mchafu wa siasa tu.

    GZ

    ReplyDelete
  39. Anony wa 3.59 na Phatlorenzo, maoni yeni yameniliwaza kuwa, kati yetu kuna watu wanaofikiri kabla hwajaandika. Pia nimefurahi kuona kuwa mmesema kuwa waTZ tubadilike na ku 'appreciate' mazuri pale yanapofanyika. Mimi naongezea 'Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni'. Kudos to JK, he is for real!

    ReplyDelete
  40. JK BRAVOOOOO!! Umeshaanza kuandikia historia ambayo haijawahi kuandikwa na kiongozi yeyote, si wa Tanzania, Afrika na pengine pia Ulimwengu. Tunaamini kwamba hii ni hatua muhimu sana ya kwanza ili nchi iweze kupiga maendeleo. Bila kuondoa ufisadi nchi haitaweza kupiga hatua zozote za maendeleo.

    HONGERA kwa kazi kubwa. TUNAOMBA mwenyezi Mungu azidi kukupa BUSARA na UJASIRI, kwa kuwa hii vita si rahisi na lele-mama kama ambavyo watu wengine wanadhani.

    NAOMBA watanzania wote wapenda maendeleo, bila kujali itikadi, tukumbuke ule umoja wetu tuliofundishwa na Mwalimu tumuunge mkono Rais katika vita hii.

    MUNGU IBARIKI TANZANIA

    ReplyDelete
  41. Eeeeeeebwana dahh!!!!! OOOOOOOOOi

    ReplyDelete
  42. mbona kabila zilezile???ivi mwalimu alisema kweli eee,,,
    ila twaitaji maelezo
    1.ivi izi kesi ni za kuhujumu uchumi? yaweje dhamana nk?
    2.hakuna sheria/utaratibu/sera nk km uyo mhujumu uchumi alikua kiongozi na sasa yupo ktk kesi aendelee kuwakilisha jimbo?ndio adi awe proven gilty bt hatakiwi apishe uchunguzi uendelee??
    3.miakaunti walonayo uko iliko yaweje? km ametrick kaandika mwanae/ndugu/mtu fulani je?
    INABOA SAAAAANA

    ReplyDelete
  43. Mi naona watu wanacheza, hawana shukurani hata wafanyiwe nini. Hatua aliyochukua JK ni jambo la msingi ni inaonyesha dalili njema. Hakuna mtu aliyetegemea siku moja Mgonja atanyea debe gerezani lakini imetokea.
    JK yupo serious na ndiyo maana amekaa kimya anaonyesha kwa vitendo.Jifunzeni kushukuru kwa mambo madogo maana hata mkifanyiwa makubwa hamna shukurani. Kuwafikisha Mramba, Yona na Mgonja siyo kitu kidogo.Mpeni nguvu JK KWA KUMSUPPORT SIYO KULAAUMU.
    TUPO PAMOJA.

    ReplyDelete
  44. WE ANON WA 8:16 KAMA UMETUMWA KAZI UNAIWEZA,BIG UP

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...