Wasanii wa kundi la Jahazi Modern Taarab mara baada ya kuwasili jana katika uwanja wa ndege wa kimataifa Heathrow terminal 5 London.

Usiku huu kundi hilo litafanya onesho lake la kwanza katika ukumbi wa Silverspoon uliopo pembeni ya uwanja wa kimataifa wa mpira wa Wembley.
jahazi na wenyeji wao mar baada ya kutua heathrow



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Mtanisamehe wote!

    Lakini kuna ulazima wa kupewa "briefing" kuhusu hali ya hewa ikoje huko "waendako" kabla ya kuondoka Tanzania!

    Dar sasa ka-jua ndio hivyo tena. Lakini hapa London ka-baridi ndio hivyo tena.

    Kuwasili na vifulana au vi-T-shirts ni ujuha wa kuonekana kana kwaba ni wendawazimu!

    ReplyDelete
  2. hawa jahazi wanawazim, hajui kama U.K, kuna barid au........

    ReplyDelete
  3. Duuu, wapambe hawakuwaambia jamaa kuwa huko juu winter? Manake wao wametinga vi t-shirt kama vile wanakwenda Diamond Jubilee kuperform!

    ReplyDelete
  4. kumbe nyie wababe sana, yaani mmeshuka uk winter hii na nguo nyepesi namna hiyo! wenyeji wenu wako wapi wasiokupeni onyo juu ya hali ya hewa kwa wakati huu, poleni msije mkashindwa kufanya show shauri ya kuumwa baada ya kupigwa na baridi.

    ReplyDelete
  5. Mbona kama wana mageneza?! Au design ya masanduku?

    ReplyDelete
  6. Wewe Anon 9:15 PM hivi unafikiri ala zao za muziki wangeziweka kwenye masanduku ya kawaida....hivi ni lazima uandike humu? Kama huna la maana kaa kimya!

    ReplyDelete
  7. Hapa nilipo nimo kwenye koti zito la baridi na bado barid ya UK inapenya, nawaonea huruma jahazi, wapambe wao nuksi hawakuwaarifu juu ya winter!

    ReplyDelete
  8. Wewe unaye sema Mageneza , hizo ni cases wameweka vyombo vya mziki, mshamba kweli wewe.

    Na nyie ,Bongo tutanunua wapi hayo makoti wakati kila kitu huku ni cha joto, hata huko huko pia wakati wa summer pia mbona inakuaga ngumu pia kupata sweter , msiwashangae sana walijua wata fanya shopping huko huko.
    kwanini wanunue koti bei mbaya Dar ,wakati wakifika London ni ya ku mwaga?
    Halfu wanjua akishuka ni wako ndani ya airport na hata wakitoka nje ni wanakuwa ndani ya gari so baridi halita wasumua kwani umeiskia ni watapanda mabasi kama nyie mnavyo panda kila siku kwenye kuosha wazee?

    ReplyDelete
  9. Kisa cha kweli.

    Wapi: Moscow Airport

    Nani: Watanzania kwenye ujumbe wa Rais Mwalimu Nyerere. Kimbele mbele cha kuanza kutoka ndani ya ndege na kutayarisha kushuka kwa Mwalimu (maprotokali na walinzi) na huku wamevalia ile ya Mao Suti na viatu vya kawaida.

    Mwalimu kawaambia, "Jamani, hapa ni Urusi! Kuna theluji na barafu! Hamna makoti!

    Wakamjibu: Ni sawa tu, Mzee!

    Wa kwanza akaanza kukanyaga barafu. Akateleza, fyaaaaaaaaa, chini!

    Wa pili akamfuatia. Akateleza, fyaaaaaaaaaaaaaaa, chini, pia!

    Mwalimu kutoka nje anawaona wote wawili wamelowa!

    Kawaambia rudini ndani ya ndege!

    Ikawabidi waletewe makoti ya baridi!

    Ni kisa cha kweli.

    ReplyDelete
  10. duh utafikiri wametoka dafur hawa jamaa.wakimbizi?

    ReplyDelete
  11. NGOJA WATOKE HAPO NJE YA AIRPORT NDO WATAONA CHA MTEMAKUNDE KILICHO MTOA KANGA MANYOYA, WATAHISI KAMA VILE WAKO NDANI YA FRIJI.

    ReplyDelete
  12. jamani nyie mtasema yote,mara wana majeneza mara vifulana,...lakini ni WAKO JUU NA WAKO IN LONDON sasa maneno ya mkosaji,mara hili mara lile kazi kwenu msiopenda maendeleo ya watu hivi ni lini MBONGO AKAMSIFIA MBONGO MWENZAKE, MNABABAIKA NA RANGI NYEUPE EEEHHH
    NDIO MAANA MMEWAJAZA WACHINA TANZANIA WAKO OVERSTAYED KIBAO NA VITU FEKI KILA LEO WANAINGIZA NA WATAINGIZA SANA ....
    Sasa jadili mambo yanayohusu nchi yako siyo ywa wenzenu...WIZI MTUPU.
    MIPODAAAAAAAAAAAA.....LAINIIIIIII

    ReplyDelete
  13. mimi hiyo jezi ya Liverpool tu...hata adidas hawajui hilo toleo. hiyo ndio zanzibar production???/

    ReplyDelete
  14. Ni kweli joto la Dar makoti ya winter watayatoa wapi kama si umbea na ushambenga na WIZII MTUPU!
    Hivi nyie mlivyotoka Dar kwenda Ulaya mlinunua wapi makoti yenye manyoya shingoni kama si WIzii mtupu! Ni duka gani hilo linauza hayo makoti ya winter huko Dar na tena anafanyaje biashara ya makoti ya winter wakati summer ni mwaka mzima huko Dar na anapataje faida kama si WIzi mtupu!

    Ikesha nyie mlinunua wapi maana huku Dar labda uende Manzese ukasagule au uende Tandale au Mchikichini au Tandika na tena kipindi hiki joto la kufa mtu nani anauza hayo madude kama si ujinga mtupu!

    Haya nyie mlivyokwenda huko UK au Europe kwa mara ya kwanza mlishuka kwenye ndege mkiwa mmevalia hayo makoti yenu ya winter kabisa kutokea huko Dar, mliyavaa ndani ya ndege au mlivyoshuka? Wengi wenu mlibeba makoti ya suti tu za kawaida si tunawaona ndani ya ndege, na makoti yenu mliyoshonesha kwa mafundi suti wa kichaga, mkishafika huko London sijui wapi ndio mnaenda Primark, sunday market, upton market kutafuta makoti au kwenye maduka ya charity kwenye bei nafuu. Nani anashuka na koti la wool lenye manyoya la pauni 70 au 100 kutoka nalo Dar kwa mara ya kwanza kabisa anaingia ulaya kama si UDAKU mtupu!!

    ReplyDelete
  15. huyo anony anayesema hawapati baridi eti wapo airport na wakitoka wanaingia kwenye gari,amebugi.ukiwa inside heathrow airport kuna kibaridi na ukitoka nje ndo usiseme na hadi ufike kwenye parking lot ume-freeze.kwahiyo acha kujikosha kuwa hawakupigwa na baridi

    ReplyDelete
  16. huyu alosema eti wako airport na wakitoka wapo ndani yagari hivi ameshafika uk au anaropokwa tu?

    ReplyDelete
  17. mh watanzania mmezidi umbea kwani wao wakipigwa na baridi inawahusu nini?kwani ni nyie si ni wao wataganda mifupa afu mnaopiga kelele hata ndege hamjui inafananaje wapuuzi mtupu!

    ReplyDelete
  18. Wewe, anon wa tarehe December 14, 2008 3:33 pm, kwani ni nani kakwambia kuwa wote wanaoondoka Dar kwenda Ulaya, kwa mfano, huwa wanaoondoka wakati kama huu?

    Eti unasema, utapata wapi makoti ya baridi Dar! Mbona watu wa Dar wanavaa masuti na matai ya winta!

    Wewe fikiria kutoka hapo uwanjani hadi wakatafute hayo makoti ya baridi....wanakufa kwa nyumonia ya kibaridi cha siku nyingi mwilini!

    Wa kulaumiwa ni wote wenyeji wao na wao pia.

    Kabla ya kuondoka kwenda London walipitia "consulate" ya Uingereza hapo Dar, ambako huwa kuna info kuhusu hali ya hewa ya Uingereza wakati wa safari!

    Na hata marubani wa ndege hutoa hali ya hewa ya mahali pa kutua!

    Umbumbumbu (si upumbavu) usipewe nafasi ya kukita hapa bloguni.

    Nina imani kuwa siku nyingine wataamuka wote walio ignorant!

    ReplyDelete
  19. Mimi ndio nime sema kuhusu kuwa ndani ya Airport , usinidanganye ukiwa ndani ya airport ni pale unapo toka ndani ya ndege tuu ndio una sikia kibaridi kidogo ukiingia kwenye terminal sio baridi kihivyo, na hapa ukitoka kwenye parking lot una weza vumilia ile baridi, usinidanganye eti ile baridi kwa muda mchache tu unaweza kufa, nimekaa Chicago kunabaridi sio mchezo , nilipo shuka Ohare sikuwa na koti na mbona sija pata tatizo?

    ReplyDelete
  20. Acheni ujinga baridi inaanzia kwenye ndege!

    ReplyDelete
  21. Hata mimi shaka yangu ni hiyo jezi ya bwawa la maini, jamani wabongo tuepuke kuvaa nguo za kutangaza biashara bila ya idhini za wenyewe, hizo tshirt za KTM tuvae hapa hapa bongo, tutashtakiwa!

    ReplyDelete
  22. wamefikeje apo UK??mdhamini ni nani afu team yao wangapi iyo jahazi
    jamani mboni kuwakomalia wana wa wezenu abt vitop vyao???baridi haiui mtu msijitie mna hurumaaaa,,feki kweli nyie,,
    kwanza ile baridi tu ya ndegeni mtoto wa bongo waweza zimia lzm udate kwanza,,,ingawa ukijifunike vile viblanketi aaaa poa tu

    ReplyDelete
  23. mh kuchamba kwingi kutoka na mavi. afya za wenzeni si mgogoro hebu tusikie atakaye rudi kajeruhiwa na nimoniaaaaa ndo tu comment.
    sasa si nimeona wanaperfom imekuwaje hawasikii baridi au ndo kuna kiyoyozi ja choto

    ReplyDelete
  24. tatizo watanzania waliopo nje wana midomo mno na hawataki kusikia mtanzania mwingine kafika huko maana wanadhani ulaya ni kwa ajili yao tu. lazima wachonge sana maana hawakutegemea kundi kama hilo litakanyaga ardhi ya uingereza, wakati huko ni sawa na kuingia chooni, ni nauli na pesa zako tu.
    pamoja na kashfa zenu zote, zisizo na msingi, lakini wame perform tumeona, hakuna aloumwa wala aloganda kama chizi mmoja alivyosema. Hata nyie mlio huko hamkujua kama mtafika, mkisikia wenzenu wanakuja be proud!!! kua at least watanzania wenzangu wanakuja kutuonyesha show. Mna matatizo gani nyie, kuweni jamani kiakili sio umri tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...