
Jumuiya ya Watanzania Jimbo la Tamil Nadu inawakaribisha kwenye mkutano mkuu wa Kwanza na Uzinduzi wa Jumuiya.
Mkutano huu utafanyika Life Conference Hall, Loyola College, Sterling Road, Nungambakkam, Chennai - 34, tarehe 26 Desemba, 08.
Mgeni Rasmi kwenye uzinduzi huo atakuwa balozi wa Tanzania nchini India, Mh. John Kijazi.
Watanzania wote kutoka nje ya jiji la Chennai, watajumuika na wenzao wa Chennai kwa tafrija ya sikukuu ya Krismasi itakayofanyika tarehe 25, Desemba kuanzia saa 7 mchana!
Wasiliana sasa na mkurugenzi wa mawasiliano kwa ajili ya kujisajili kupitia:
watanzania.tamilnadu@yahoo.com
+919840123784
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...