mfalme mzee yusuf akifanya vituzzz na kundi lake la jahazi jijini london jumamosi ilopita.
Baada ya kuwapagaisha wapenzi wa muziki wa taarab London Jumamosi iliyopita, kundi zima la Jahazi Modern Taarab, siku ya Ijumaa hii litaanza kuwasha moto mjini Leicester ikiwa ni kati ya shoo tatu za mwisho kabla ya kurejea Tanzania Jumatano iyajo.
Kundi hilo linaloongozwa na mfalme, mzee Yusuph, litaongezewa nguvu katika shoo zake baada ya mwimbaji nyota wa kundi hilo, Isha Ramadhani kuwasili jana jioni kuungana na wenzake.Isha hakuwepo katika onesho lililofanyika Jumamosi iliyopita mjini London.
Jahazi ambayo inafahamika Tanzania kuwa ndio kundi namba ‘one’ kwa mipasho na miondoko ya Nakshi Nakshi, linavuma na nyimbo zake kama Msumari unachoma, VIP, Two in One, Kupenda ndio huku na nyingine nyingi.
Ijumaa-19/12/2008 Leicester
Mahali:Lahore Karhi,23-25 Bedford Street South Leicester,
LE1 3JR.
Kiingilio:£15
Muda:Kuanzia saa mbili usiku hadi saa kumi.
Karibu na Jabcentre ya Leicester.
Jumamosi-20/12/2008 Birmingham
Mahali:Afazal Centre,
Newtown Birmingham,
B19-9JA
Kiingilio:£15
Muda:Kuanzia saa mbili usiku hadi saa kumi.
Wasiliana na Bongo Family: 07533512670
Jumapili-21/12/2008 Milton Keynes
Mahali:Spice Launge Discotheaque
3 Savoy Crescent,
Theatre Centre District,
Milton Keynes
MK9 -3PU
Muda:Kuanzia saa kumi na mbili jioni hadi saa tisa usiku.
Kiingilio:£15
Wasiliana nasi :
02083265607,
07861351135

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Mbona hakuna kitu/picha/mchoro kwenye KP leo?

    ReplyDelete
  2. Sasa Balozi vipi tena? naona msiba umekuchanganya, pole sana. Sasa huyu KP leo vipi? mbona naona blank? au mimi tu na macho yangu?

    Mdau
    Cardiff

    ReplyDelete
  3. Mbona huyu Kipanya simuoni, au simuelewi
    m3

    ReplyDelete
  4. Huyu Kipanya mbona hafunguki
    m3

    ReplyDelete
  5. Mbona picha ya kwanza ni diamond jubilee mnasema eti ni london??? huu uongo wa mchana mchana....

    ReplyDelete
  6. mbona picha zote ni za hapa bongo moja ni Diamond na nyingine cjui wapi coz naona bango la tigo nyuma, mbona mnatudanganya huku 2naona

    ReplyDelete
  7. CHANGA LA MACHOZZZ PICHA YA KWANZA NI DIAMOND JUBILEE NA YA PILI NI TRAVENTINE MAGOMENI.

    ReplyDelete
  8. sasa hii vipi? hawa jahazi wanatuletea picha za bongo na kusema ni ukerewe?

    ReplyDelete
  9. Balozi, mzee wa fulanaz...sasa naona msiba wa kijana wako herry umekuchanganya, kulikoni kutuwekeaz 'ze pichaz' ya daimondi jubilii na travetaini na kutuambia ni ukerewe, brother sisi hatujawahi kufika ukerewe, lakini bongo tunaijua kisawa sawa! ,,,,,edit bwana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...