Ndugu Watanzania,
Naomba kuwakilisha Dec 20,2008 Watanzania waishio Canton Ohio kwa nguvu na kauli moja waliweza kuuzindua Umoja wao wa watanzania waishio Canton Ohio.
Tukio hili kubwa la kihistoria lilifana sana.Viongozi wa Umoja huu wanapenda kutoa shukrani za pekee kwa kila mwanachama wa umoja huu.Nia na madhumuni ya umoja huu ambao umesajiliwa kisheria under Ohio Laws ni kuwasaidia wana umoja wake katika nyanja zote na zaidi sana kuleta amani kwa wana umoja ndani na nje ya Tanzania. Kuukuza umoja kufika level ya kusaidia jamii nyumbani Tanzania katika hali zote umoja ukaosaidia.
Tukio hili lilifunguliwa rasmi na Mwenyekiti wa Muda Bwana Mohamed Sultan kwa kukata utepe kuashiria ufunguzi rasmi na kuimba wimbo wa Taifa wa Tanzania.
Pia keki iliyotarishiwa kwa bendera ya Taifa iliweza kukatwa rasmi na kulishwa watoto ambao ndio dhumuni kubwa la umoja la kuwajengea mazingira mazuri ya kuendeleza umoja na kujua nini wazazi wao wanafanya wana umoja wanajenga legacy kwa watoto wao.
Tunashukuru kwa tukio hili la kihistoria kufanyika hapa Canton Ohio.Kwa waliofika na ambao hawakufika tunawashukuru sana na pia tunawakaribisha watanzania wote ambao bado hawajajiunga na Umoja huu wa Watanzania Canton Ohio hata walio maeneno ya jirani Cleveland ,Medina,Alliance,Akron,Louisville,Salem,New Philadelphia na Cuyahoga Falls karibuni sana maelezo ya kuhusu umoja yapo.
Karibuni tutakuwa na website yetu itakuwa na information zote.
TAC IDUMU
Katibu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ndugu zangu wa Canton,

    Hongera sana! Afadhali nyie mmeamua kufanya mambo ya maana, maana ndugu zenu wa Columbus wataalam wengi sana mpaka wameshindwa kuanzisha chama. Nadhani Columbus pekee ndo mji mkubwa wenye wabongo kibao ambao hauna chama hai.

    ReplyDelete
  2. Watanzania mliopo Canton hongereeni sana I am proud of you easpecially for the fact that you have decided to form a society to help Tanzanians back home and also to passon a legacy to the kids this is great!

    I hope that Tanzanian in the UK especially will follow suit because what I see now is Tanzanians abroad wishing for their children to imitate western children so they lack manners and they can't even speak Swahili anymore. They think this is developemnt whereas in actual fact the chilcren loose their identity.

    There are many projects to support back home. I just trully hope that whattever project or whomever you support will not just concentrate in the City Dar-es-Salaam but will also spread out to rural villages which are in dire need of your kind of intervention.

    Hope I make sense to you and Good Luck, Once again congratulations and Happy new year!

    Mrs S.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...