Uncle Michuzi na wadau wa glob hii ya jamii,
Kero yangu ni kwa hawa askari wa Halmashauri ya jiji la Dar es salaam,hivi vitu wanavyo wanyanganya wamachinga wanavipeleka wapi???Kama wanavipeleka ofisini basi lazima kutakuwa na utaratibu wa kuvinadi lakini mbona sijasikia hata siku moja tangazo la mnada?Nisaidieni Wadau!
Prosper B.A.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Kwakweli mimi hili linanikera sana, in the first place ni waizi na wanafanya kazi zisizowahusu, kazi zao kuu zingekua kwa mfano 1. kuhakikisha jiji ni safi kwamba takataka zote zimekusanya na usafi umefanyiaka ipasavo, 2. kuhakikisha usalama wa raia mitaani wakisaidiana na polisi kusaka vibaka, wezi, wauza unga, waua maalbino, nk

    ReplyDelete
  2. Wizi mtupu, sera ni ileile ya UFISADI. Kufisidi sio lazima uchukue mabillion, huanzia hata nyumbani kwako...
    Kero hiyo ni ka mchezo kamepangwa, wamachinga na walalahoi waukimbie mji, then, wenye nacho wahodhi jiji. Majumba ya uyoga, makampuni makubwa, nk, yataanzishwa ni kwa maendeleo anyway, lakini kwa kupitia mgongo wako.
    Sera za wenzetu, kwasababu tunataka maendele, yote hayo yangewekwa wazi.
    m3

    ReplyDelete
  3. mnada hufanyika moja kwa moja wakati wa zoezi lenyewe la unyang'anyi mingoni mwa watendaji wahusika(ie mgambo na watumishi wengine wa jiji kwa kadri ya uhusika wao)kwa kujiamulia nini apewe nani.
    Hivyo ndugu yangu ukitaka kusikia habari za minada hii anza sasa kuomba kazi ya mgambo wajiji, ukifanikiwa huenda ukawa ndio mnadishaji mkuu.

    ReplyDelete
  4. wewe unategemea nini kama nchi imejaa mafisadi. kila kitu ufisadi tu.

    Chukua Chako Mapema, hata kisichochako

    ReplyDelete
  5. washauri hao machinga watumie baisikeli kama za bakhresa za kuuza aisikirimu hawatashikwa ng'oo. Huoni wauza dawa za panya wameiga na wanatesa- wanauza dawa za panya mpaka kwenye Bar!!

    Michuzi tusaidie- something is wrong somewhere- kama noma iwe noma mzee!!

    ReplyDelete
  6. washauri hao machinga watumie baisikeli kama za bakhresa za kuuza aisikirimu hawatashikwa ng'oo. Huoni wauza dawa za panya wameiga na wanatesa- wanauza dawa za panya mpaka kwenye Bar!!

    Michuzi tusaidie- something is wrong somewhere- kama noma iwe noma mzee!!

    ReplyDelete
  7. ni vema pia wamachinga na watanzania wote kwa ujumla tukajua haki zetu.Wamaching wananyanyaswa kwa sababu bado elimu kwetu walio wengi ni finyo.Hata bada ya kudhulumiwa mmachinga hajui aende wapi kufatilia haki yake.As long as ignorance ni kubwa,we have a long way to go.Kimsingi,wanachokifanya hawa askari ni utovu wa nidhamu uliovuka mipaka na unyanyasi.Wanapowakamata wanapaswa kuwapeleka mahakamani hawa wamachinga.Kesi ingurume na ni mahakama tu ndo inaweza kutoa uammuzi kama wamachinga ndo wenye haki au halmashauri ya jiji.Hii ni sawa na serikali inapovamia kijiji na kuhamisha watu kwa madai kuwa wamevamia eneo fulani.Ni kosa.Katika hali kama hii,shauri lapaswa kupelekwa mahakamani na mahakama ndo inasema nani yuko katika haki.Kwa hiyo unyanyasaji hupo ni si kutoka serikali za miji na majiji tu bali pia hata toka serikali kuu.The rule of law bado ni tatizo katika nchi nyingi za Afrika.
    {The Son Of Africa.Prince Aba wa Ruba.A little boy among men}

    ReplyDelete
  8. fisadi wa dogo...Hakuna tofauti mmoja alia mezani na wengine wanalia jikoni.....

    ReplyDelete
  9. Hivyo vitu nasikia huwa wanapeleka kwa Kandoro kwaajili ya kuvitunza. Hahahaahahaaaaaaaa!! Wezi wakubwa hao!

    ReplyDelete
  10. SERIKALI YA JIJI INWAPORA WAMACHINGA KWASABABU YA UFISADI.

    1.WIZI/UFISADI
    2.VITU VYAO HAVINA TAKWIMU/HAKIKIWI
    3.WANAUZA VITU BANDIA/FEKI
    4.VILIVYO INAVYOINGIZWA KINYUME CHA SHERIA.
    5. VYENYE VIWANGO HAFIFU.

    ReplyDelete
  11. huu sio mradi wa jiji au kingun---
    mtajaza apo.
    adi siku ifikie wananchi wawapige mawe kila kibosile anayepita mtaani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...