Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Kijana Kamkosea heshima Mzee. Ni kweli hata kwenye sambusa hizo nyama zimo.

    Cheers.

    ReplyDelete
  2. Jaji Mkuu: Baadhi ya mawakili ni matapeli

    2008-12-13 13:47:27
    Na Joseph Mwendapole na Hellen Mwango


    Jaji Mkuu, Augustino Ramadhani, amesema baadhi ya mawakili ni matapeli na wamekuwa wakiwatapeli wateja wao kwa kula njama na upande wa wapinzani wa wateja wao.

    Kadhalika, amewataka mawakili kutowatetea wateja wao ambao hukiri kutenda makosa yanayowakabili mahakamani.

    Akizungumza jana kwenye hafla ya kuwapa vyeti mawakili wapya 64 wa kujitegemea, Jaji Ramadhani alisema baadhi ya mawakili wamekuwa ndumila kuwili na kwamba huo ni usaliti na utapeli.

    ``Hapa kuna suala la uaminifu kuhusu fedha za wateja wenu... Yapo malalamiko kuwa mawakili wachache wanajinufaisha kwa fedha za wateja wao na bila kumung`unya maneno natamka kuwa huo ni wizi,`` alisema.

    Alisema mawakili wana wajibu kwa wateja wao na inawapasa wawe waaminifu kwao.

    Kuhusu washtakiwa wanaokiri makosa, Jaji Ramadhani alisema kama mshtakiwa anakiri kosa, wakili anapaswa kujaribu kupata afueni ya adhabu na ni mwiko kusimama kidete na kudai kuwa mteja wake hana hatia.

    Alisema wakili anao wajibu kwa dhamira yake na kama anaona dhamira yake haimruhusu kushiriki katika kesi fulani basi asijilazimishe bali aiache hata kama itamkosesha donge nono.

    Alisema Tanzania kwa sasa ina mawakili 1,133 lakini mawakili ambao wanafanya kazi ni 761 tu ambao wamehuisha leseni zao mwaka huu.

    Alisema Jiji la Dar es Salaam lina mawakili 704 na kati ya hao mawakili 102 hawajahuisha leseni zao na kwamba mawakili 31 wamepeleka maombi kwa Jaji Mkuu ya kuruhusiwa kuhuisha leseni zao.

    Aidha, alisema ni aibu kuona mawakili 71 bado hawajapeleka hata maombi ya kuruhusiwa kuhuisha leseni zao.

    ``Hivi wakili ambaye anakuwa mzembe kuhuisha leseni yake ambayo ndiyo inampatia maslahi atakuwa makini kuhusu maslahi ya mteja wake?`` Alihoji Jaji Ramadhani.

    Alisema kwa mwaka ujao wakili atakayechelewa kuhuisha leseni yake ataachwa asote mwaka mzima kabla ya kibali cha Jaji Mkuu kupatikana.

    Miongoni mwa mawakili wa kujitegemea walioapishwa jana na Jaji Mkuu ni pamoja na Joseph Holle wa Takukuru aliyewasomea mashitaka mawaziri wandamizi, Basil Mramba na Daniel Yona.

    Mawaziri hao wa zamani walisomewa mashitaka 13 ya kuisababishia serikali hasara ya Sh. bilioni 11.7 kwa kutumia vibaya madaraka yao.

    Wengine walikuwa waendesha mashitaka wa serikali na askari polisi kadhaa.

    ReplyDelete
  3. Mbona masoud anamsema mfadhili wake? wengi tunajua masha kamuendeleza kipanya sasa aangalie asimuudhi.

    ReplyDelete
  4. Anon wa December 14, 2008 10:19 tambua Masha sio mfadhili wa Kipanya, bali mzee Benjamin William Mkapa ndiye rafiki mkubwa wa Kipanya na mfadhili mkuu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...