Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Wazo zuri KP lakini kumbuka kwamba kubadilisha pesa pia kutaigharimu TZ mapesa mengi sana

    ReplyDelete
  2. KP NAKUUNGA MKONO MAANA SIJUI UMEFIKIRIA MARA NGAPI, KAMA KWELI WAHUSIKA WANGEKUA NA AKILI NA MAARIFA KAMA YAKO BASI KUSINGE KUA NA MAFISADI NCHINI.

    ReplyDelete
  3. Kubadili fedha cyo issue, waanze na wale waliojidhamini kwa mabilioni ya shillingi...wamezipataje?

    ReplyDelete
  4. hawa watakuwa wameweka fedha zao kwenye account za nje kwa hiyo ziko kwenye dollar

    ReplyDelete
  5. Wewe mdau ambaye kila siku unalalamika waliojidhamini kwa mabilioni nadhani inatakiwa ufanye homework yako. Kwa mfano Mramba amefanya kazi zaidi ya miaka 45 kama leo hii hana vitu venye thamani ya Billion 10 nitamshangaa. Kwa mfano mtu aliyenunua au kugaiwa bure kiwanja miaka ya 80 maeneo ya mbezi leo hii hicho kiwanja thamani yake ni millioni 100 hiyo ni billion 1 upo hapo. Na pengine alijenga nyumba kwa millioni 50 miaka ya 90. Leo hii hiyo nyumba thamani yake inaweza ikawa million 100. Kwa hiyo leo hii akitoa hati ya nyumba mahakamani inakuwa na thamani ya million 200 (billion 2) sasa wewe unayedai wamezipataje nadhani fanya home work yako na mahakama ilitoa hiyo dhamani kwa kuwa walikuwa wanajua wanazo na sio kuwakomoa. Napata hisia wewe ni mtu wa JF ambao mmezidi kulalamika vitu ambavyo hata havi make sense.
    Tumchukulie tena huyo huyo Mramba kati ya miaka hiyo 45, tuchukulie kipindi kati ya 1995 na 2005 (miaka 10). Amekuwa mbunge na waziri na kwa kukadilia kipato chake halali kinaweza kufika million 100 kwa mwaka, kwa miaka 10 hapo ni 10 billion. Ukiondoa vitu vyote na matumizi kama ameshidwa kusave 10% ya kipato chache nitamshangaa sana kwa hiyo naamini kwenye account yake ana zaidi ya billioni 1 na ukizingatia hawa wabunge huwa wanapewa kati ya million 50 na 60 wanapomaliza vipindi vya sitashangaa kama ana 2 billions cash kwenye account sasa hapo unataka aeleze nini? Eti amezipataje wakati kila kitu kiko wazi?

    ReplyDelete
  6. Not a good idea. Tatizo ni vitu viko bei juu. Kama samaki anauzwa kwa mia nyekundu na ukabalisha awe anauzwa kwa mia ya njano bado thamani yake ni mia. Hali ya maisha itabaki pale pale.
    Na kwa taarifa yako hao walioweka hela nyumba haziko kwenye madafu huo unjinga waliacha toka wakati wa Hayati Sokoine labda mumwambie Bush/Obama abadili hela.
    Mdau wenu, XXXX

    ReplyDelete
  7. It will make sense kama hizo pesa wameziweka kama madafu. Kama wanazo kwenye Dola or any other currency kama Euro au Pound sidhani kama itakuwa na effect kubwa kwao. Sidhani kama hiyo ni solution.

    ReplyDelete
  8. wewe anonymous hapo juu shule yako ndogo sana, jaribu kurudi tena shule ufundishwe maana inavyoelekea hata primary school hujamaliza. Milion 100 sio bilion moja, bilioni 1 ni sawa na milioni 1000. usikurupuke tu kuropoka ili uonekane unajua wakati hujui lolote, kwa namna yoyote ile hao mafisadi wakitoa maelezo ya hizo billions zao za dhamana watachemka tu.
    Uwe unajaribu kuuliza kwa wakubwa tofauti ya hesabu sio unajichora tu kwenye blog ya jamii wakati uelewa wako ni mdogo kupindukia

    ReplyDelete
  9. kaka umechemka hapo juu kiasi hata mtoto wa secondary hatakushangaa yaani million 100 imekuwa 1billion? usirudi tena hapa nenda na ukauze labda biashara ya nyanya.inasikitisha kuona kuwa uwezo wako wa hesabu ni mdogo kiasi hicho wengine hata kama hesabu ilikuwa inatutoa knock out in those back in tha days at school lkn hatukuwa vilaza kiasi hicho daaa!!!!

    ReplyDelete
  10. Anonymous wa dec 27,10:13 pm ni mjinga na ndio wale waliopata zero form 4 wakakimbilia ulaya wakizani kuna raha na watayatoa kimaisha matokeo yake kaishia kufanya kazi za dola 15 kwa siku hadi thamani ya bilioni 1 haijui. kufanya kazi miaka 45 serikani hauwezi kusevu bilioni 10 labda angekuwa waziri kwa hiyo miaka 45,nani serikalini aneyepata mshahara wa zaidi ya milioni 20 kwa mwezi? jamani mbona mishahara ya wabunge na mawaziri ipo wazi,au ndo kukaa sana ulaya unashindwa kugagadua mambo ambayo yapo wazi. Asante!

    ReplyDelete
  11. BILLIONI MOJA NI SAWA NA MILLINI ELEFU MOJA SI MIA MOJA, YAANI 1,000,000,000 = 1 BILLIONI NA KUSEMA MRAMBA AMEFANYA KAZI MIAKA 45 SO ANAWEZA KUWA NA 10 BILLINI HUO NI UONGO WA KUFA MTU. TUTOWE MFANO MSHARA WAKE MIAKA YOTE HIYO ALIKUWA ANAPATA 5,000,000. KWA MWEZI, KITU AMBACHO SI KWELI KWANI NINAUHAKIKA KWA MUDA MREFU TOKA AANZE KAZI ALIKUWA HAPATI JUU YA SHS,1000.00 KWANI MIAKA YA 1980s mtu akianza kazi serikalini mwenye degree alikuwa hapati hata shs 1000. TURUDI SASA KWENYE MAHESABU YETU NI HIVI 60, 000,000 KWA MWAKA MIAKA 45 SAWA NA 2 700 000 000 AMEPATA 2.7 BILLIONI SASA HIYO BILLIONI KUMI IKO WAPI NA HII NI INTACT HAKUCHOMOA HATA SENTI TAO KUNUNUA HATA CHAKULA. UNAONA UNGUMBARU WAKO, KABLA HUJASEMA FANYA MAHESABU KWANZA, HATA LEO HII SIDHANI MAWAZIRI WANAPATA 5,000,000 KWA MWEZI!!!!

    ReplyDelete
  12. Kp leo umechemsha.
    Huwezi kumzuia mtu kula chakula chako kwa kuongeza ppilpili au chumvi.
    Dawa kama tunawaafahamu wapeo kibano mpaka waonyeshe ziko wapi.Miaka ya themanini fedha ziliibiwa bot watu wote waliohusika, hata kama walisikia tu huwakutoa taarifa unapata kibano cha saizi yao. kwa mtindo huu zote zilipatikana.

    ReplyDelete
  13. Mi nafikiri kuwa wabongo huwa tunapapara na hatuna mawazo endelevu.Mi nilifikiri kuwa ninyi mnaomkosoa KIPANYA mnakasumba ya kupinga tu na wala hamna fikra mbadala za kuchangia,KIPANYA yeye katoa maoni yake kulingana na upeo wake,mimi ningena ni busara kwa ninyi muwe mnapinga na kuta suluhu mbadala kuligana na mazingira ya tatizo,lakini ni tofauti kabisa....mfano we anonymous 10:13 hizo hesabu unazopiga hapo hata mtoto wa shule ya msingi hawezi fanya madudu hayo.Hoja ya msingi ni kuwa hawa wamejilimbikizia mali kwa kutumia vyeo vyao,isitoshe wako wengi na ushahidi ndio tatizo ili kuwakamata wote,sasa kinachotakiwa ni kuwabaini hawa ili wapeleke mbele ya sheria.Kipato cha Mtanzania kinajulikana hivyo kuhusu mramba kuwa na bil 2 bank kwa sasa sio tatizo,tatizo ni kuwa kazipataje..anonymous 10:13 tuliza akili,inawezekana kabisa huyu Mramba ameweza kusave hiyo 10% ya kipato kutokana na kuwa hela ya matumizi alikuwa anaipata kutoka kwa hao maswahiba aliowasamehe kodi,aliowapa vyeo kwa upendeleo na kusababisha watanzania wengi wakiwa na maisha magumu,sasa huyu anatakiwa afikishe mbele ya sheria ili aseme kuwa hizi bil 2 amezipata kihalali kweli?.Mimi nampongeza kipanya kwa mawazo yake na ni vyema wengine tujifunze kutoa maoni yenye kuleta suluhu zaidi ya kukosoa.CRUX

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...