WATANZANIA NAPOLI LEO WALIKUSANYIKA KUTOA HESHIMA ZAO ZA MWISHO KWA MAREHEMU ABDALLAH MJUME ALIYEFARIKI SIKU YA TAREHE 23/11/2008 JUMAPILI ASUBUHI. MWILI WA MAREHEMU UTAONDOKA KESHO KUELEKEA NYUMBANI TANZANIA KWA MAPUMZIKO YA MILELE. MWILI WA MAREHEMU UNATARAJIWA KUFIKA DAR ES SALAAM SIKU YA JUMAMOSI ASUBUHI. JUMUIYA YA WATANZANIA ITALY INATOA RAMBIRAMBI KWA NDUGU NA JAMAA WA MAREHEMU PAMOJA NA WAZAZI KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU CHA MAOMBOLEZO. MUNGU AMLAZE MAHALA PEMA PEPONI AMIN!
jeneza lenye mwili wa marehemu dullah
waombolezaji huko napoli wakumuaga mpiganaji mwenzao
wabongo walionesha umoja wao wa jadi kwa kufika kumuaga mwenzao leo huko napoli
dua ya kumuombea marehemu
GLOBU HII YA JAMII INAUNGANA NA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI WA DULLAH KUOMBOLEZA KIFO CHA MDAU HUYU. MOLA AMUWEKE MAHALA PEMA PEPONI - AMINA






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Ndugu na marafiki wa Dullah poleni sana na mola awape faraja hata katika wakati huu wa Msiba.
    **************
    BTW
    Michuzi ukiangalia picha na habari kama hizi za ndugu zetu wakikusanyika ughaibuni kwa umoja wakinia mamoja kusaidiana na kufarijiana zinatia moyo sana kuliko matangazo na kukutana eti kuchagua viongozi wa mashina / matawi ya CCM- Uingereza.
    Mkutano Mkuu wa CCM (T) kataeni upuuzi huu na mseme kuwa Ofisi za CCM zitafunguliwa nchini Tanzania tu! Ughaibuni watu wanatakiwa kuimba 'Umoja wa Watanzania wa .....' sio nyimbo zisizonadika za kutuletea utengamano!

    ReplyDelete
  2. Mwenyezi Mungu akusamehe akurehemu upumzike kwa amani.
    Tumetoka kwake na kwake tutarejea.
    Wafiwa mungu awape nguvu.

    ReplyDelete
  3. poleni sana ndugu wafiwa na watanzania wote walioshikiki na kufanikisha kuleta mwili wa marehemu.ndugu mwenyekitiA.A.C. tufikishie malalamiko yetu kwa wafungaji watatumaliza.

    ReplyDelete
  4. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi AMIN.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...