hebu fikiria umejitokea zako vijijini hoi bin taabani na una hamu ya dar kama nini sijiui.
na baada ta kuwasili mwanza mnamo saa saba hivi n usheee na baada ya kupiga sato kwa nguna ya mahindi pale nanihii ukijiandaa kwenda eapoti kukwaa pipa la saa kumi unapigiwa simu kuambiwa kwamba ndege hakuna. toba! hapo vijisenti vyote vya padei umeshateketeza vijijini na huna mwenyeji rock city halafu zama hizi mambo ya kulala ccm hakuna, labda uwe gari.
unaenda ofisi za shirika la nanihii (na jezi yako ya bwawa la maini, kapelo na mawani ya kuazima) unakuta mlango umefungwa kwa ndani na ubao wa kukuambia kuwa pamefungwa unakukonyeza, ila ndani kuna watu. unagonga unafunguliwa baada ya kutishia kutumia 'fatuma' kama hawatofungua. ndani unathibitishiwa kwamba kutokana na hali ya hewa ndege leo hakuna.
dada anayekupokea, ambaye kajaaliwa rangi ya benki na umbo la ki-odemba, ni mkarimu na kastma kea anaijua vilivyo kwani baada ya kupandisha mzuka na kutaka kumpa mtu loba ya roho, anakushusha kwa tabasamu la kufa mtu na kukwambia usikonde, pipa lipo kesho na pa kulala ni juu yao. unashusha pumzi na kujikuta huna la kufanya ila kusubiria hiyo kesho, huku ukishangaa tabia hii imeanza lini katika shirika hili la nanihii ambalo linaaminika na wengi.
basi wadau hayo ndiyo yaliyonisibu mwenzenu na mie leo na hivi hapa nilipo usingizi hauji niko niko tu nawaza ya kesho.
bongo tambarare wadau...nani anabisha??

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. tatizo hutembelei ukanda huo mara kwa mara misupu..ila hata mwanza ni tambarare hiyo ndio California (West Coast) ya bongo na hatubishi kwamba Dar ni NY,,teh teh teh sio mjadala jamani ni maoni tu

    ReplyDelete
  2. hahahaha michuzi kiboko mimi naona ujiunge tuu na ze comedy ili tujue moja!

    ReplyDelete
  3. Pole Balozi wa Nanihii!! Yaliyokusibu ya kawaida katika kampuni zetu za nanihiii sema tu wewe ulikuwa hujakumbwa na kimunga hicho.
    Mie umenikumbusha mbali saaanaaa na huo msemo kuwa hakuna kulala ofisi za CCM, Duuu kweli kaka, zamani Mzee alikuwa Balozi wa nyumba kumi, kasheshe kila wiki lazima mtu abishe hodi anaulizia pa klulala kesho aendeleee na safari zake.
    Wengine walikuwa wezi na wakora tu maana waliondoka na vitu pale home, wengi wao walikuwa waungwana tu wakiyasaka maisha maana lazima mkumbuke enzi hizo basi linapita kijijini kwenda mjini mara mbili lwa wiki, hivyo watu wengi usafiri ulikuwa ni kuunga Azimio (kutembea).
    Imani kwa watu ilikuwa kiwango, hakuna hofu ya wabakaji kama sasa. Enzi hizoo mgeni akifika mtaani lazima alipoti kwa balozi. Enzi hizo hata Bungeni waliita ndugu spika, ndugu waziri!!! Tanzania ilikuwa Tambarare hakuja milima ya Ufisadi na Mabonde ya walalahoi.
    Kazi nzuri na Usafiri salama.

    Mdau toka (Kiabakari -Musoma)safarini Oslo Norway

    ReplyDelete
  4. Michuzi umeniacha njiani. Kiswahili nakijua lakini nimeelewa hadithi nusu tu na nusu nafanya kuguess tu.

    ReplyDelete
  5. issa michuzi msikitini hakuna aliyekatazwa kulala ni free si zambi pengine na pia itakufunguwa macho zaidi inshallah! utapata safari yako tunakusubiri Dar-es-salaam.

    ReplyDelete
  6. Dah, Misupu huyo Dada 'Anauma na kupuliza' kama panya, "Usikonde, Pipa lipo kesho na pa kulala ni juu yako". Kaaaazi kweli kweli.

    ReplyDelete
  7. nimeishi Mwanza kwa muda Mrefu Sana Sasa Naishi NY tatizo ni Usafiri na Sio Mwanza - Kaka Michuzi Asante Sana kwa Picha za Mwanza Mji umebadilika sana

    ReplyDelete
  8. Hivi Michuzi wewe ukiwa kijiweni na umeamua kutoa story live inakuwaje jamani........Nimecheka mpaka basi.....Nakupenda

    ReplyDelete
  9. Wewe kama ulipigiwa simu kukueleza ndege imehairishwa basi mshukuru mola. Mie tarehe 10/11/2008 nilikuwa na tiketi ya precision huyo huyo inaoyoonyesha ndege inatoka Dar kwenye saa 1 asubuhi, kuelekea mombasa, na kunitaka niripoti eapoti saa 11 alfajiri. Nilipofika eapoti hizo saa zao, lahaula! ndege haikuwepo mpaka saa 6 mchana! fikiria umeamka saa 9 alfajiri kuwahi ndege ya saa 6 mchana!

    wakati wa kuridi pia hivo hivo... ndege saa 3 asubuhi... kufika eapoti precision wakawa wamekanseli... KQ wakatuzoa mpaka nairobi (mie nataka kuja dar lakini)na tulikuja kufika Dar saa moja usiku!

    ReplyDelete
  10. Wewe kama ulipigiwa simu kukueleza ndege imehairishwa basi mshukuru mola. Mie tarehe 10/11/2008 nilikuwa na tiketi ya precision huyo huyo inaoyoonyesha ndege inatoka Dar kwenye saa 1 asubuhi, kuelekea mombasa, na kunitaka niripoti eapoti saa 11 alfajiri. Nilipofika eapoti hizo saa zao, lahaula! ndege haikuwepo mpaka saa 6 mchana! fikiria umeamka saa 9 alfajiri kuwahi ndege ya saa 6 mchana!

    wakati wa kuridi pia hivo hivo... ndege saa 3 asubuhi... kufika eapoti precision wakawa wamekanseli... KQ wakatuzoa mpaka nairobi (mie nataka kuja dar lakini)na tulikuja kufika Dar saa moja usiku!

    ReplyDelete
  11. Kaka pole sana,ni kwamba labda tu hujui kinachoendelea ndani ya usafiri wa anga nchini,ni kwamba kuna matatizo makubwa sana katika mashirika ya ndege nchini,ndege zimekuwa zikifutwa mara kwa mara na kusababisha usumbufu mkubwa kwa abiria na bila compersation,ATC ndo balaa,hao prescion nao wamefuata nyayo,wala tatizo si hali ya hewa,tatizo kubwa ni NDEGE ZAO MBOVU.Ukitaka kujua ukweli uliza wanaofanya katika sekta ya usafiri wa anga.

    ReplyDelete
  12. Pole Michuzi, ila umenikumbusha mbali.... kulala CCM. Enzi zile nchi hii ilikuwa nzuri. Pole mdau marehemu Moshi William (TX) msafiri kakiri..

    ReplyDelete
  13. HII STORI BADO HAIJASHA NADHANI.IMEKATIZWA.tena baada ya kuambiwa pa kulala ni juu yao na aleikwambia umesifia kwa "kastama kea" ya nguvu na matabasamu ya nguvu........Je uliweza kufanikiwa kupata pa kulala au ilikuwa ni longolongo tu!
    tunaomba umalizue basi PART 2

    ReplyDelete
  14. Yaani nimecheka mpaka basi!!! michu hujatulia kabisa wewe.. Sasa wewe mtu anakwambia PA KULALA NI JUU YAKO.. wewe bado uko hapo unashangaa!?? Au hukumwelewa nini?

    ReplyDelete
  15. Yaani nimecheka mpaka basi!!! michu hujatulia kabisa wewe.. Sasa wewe mtu anakwambia PA KULALA NI JUU YAKO.. wewe bado uko hapo unashangaa!?? Au hukumwelewa nini?

    ReplyDelete
  16. Da michuzi hii story usimpe my wife wako. Sasa hapo ungewezaje wakati juu yako tena ndio kuna nanihii. Au unafikiri hatukuelewa hiyo pa kulala nijuu yako. Waankijiji wanakuelewa ulikua umechoka lakini ubwedo lazima ukose usingizi....Hi hi hiiiiiiiiiiii-

    ReplyDelete
  17. fulana iyo ndio imekutia nuksi.ukisafiri ichimbie aifai kabisa.Mdau Holland

    ReplyDelete
  18. BWANA MICHUZI ISSA BIN NANIHII....

    NIMEFURAHI UMEIWEKA MADA HII. UNAJUA SHIDA YA NDEGE SI TU KWA TANZANIA WALA MWANZA WALA WAPI. NI DUNIA NZIMA. NA SHIDA HIZI ZINATOKANA NA LABDA MATATIZO YA KIUFUNDI, AU MATATIZO YA HALI YA HEWA.

    KWA MFANO, JANA KUNA RAFIKI YANGU ALISAFIRI TOKA SANFRANSISCO HADI MJI NILIOPO MIE HAPA USA, NA BAADA YA KUFIKA UWANJA WA NYUMBANI, WALIAMBIWA WASISHUKE SABABU KULIKUWA NA UKUNGU NA WALIAMRIWA KURUDI SANFRANSISCO-CALIFORNIA. NA KULE WALIAMUA KUPANDA BASI NA WAKARUDISHIWA NAULI YAO.

    SIKU NYINGINE, MWENYEWE NIKITOKEA WASHINGTON D.C, NILIFIKA UWANJA WA NDEGE KWA MAKEKE ILI NIPANDE PIPA SAA 4 ASUBUHI, TENA NILIKODI TEXI KWA DOLA 60 SEHEMU AMBAYO NINGEPANDA TRENI KWA DOLA 10 TU. CHA KUSHANGAZA NILIPOFIKA EAPOTI NILIAMBIA NDEGE HAIPO SAA 4 NA BADALA YAKE INGEONDOKA SAA 10 JIONI. KWA HIVI MIMI SIONI KUWA BONGO PEKEE NDIO INA SHIDA KAMA HII.

    MDAU,
    USA

    ReplyDelete
  19. Khah! Hana nafasi huyo receptionist wa dirishani mwenye umbo la Duara kama yeye Odemba!? Banana naye huyo huyo. We vipi bana!?

    ReplyDelete
  20. HAO NDO PRECISION KAKA, ME WALINILINICHOMESHA MAINDI HAPO ROCK MASAA 7 PASIPO HATA NA SODA NA BADO KULIKUWA NA WATU WALIOLAZWA MWANZA SIKU 2 NANILIWAACHA WAKIWA HAWAJUI LINI WATAONDOKA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...