ni katika kusherehekea miaka 47 ya uhuru wetu nami najidai na flip video yangu mpya ambayo mdau (jina kakataa nisimtaje) kanidondoseha majuzi. wadau wa taswira nawastua kwamba hii kitu ni bomba sana kwa wanaotaka taswira za video popote pale. zinapatina kwa wingi sehemu mbalimbali duniani, na kodak nao wametoa toleo lao la kodak Zi6 ambalo ni moto pia. zote zinafaa ka shughuli ndogondogo kama hepi besdei, pikniki na kadhalika. usipitwe mdau, kwa maelezo zaidi nenda http://www.theflip.com/products_flip_ultra.shtml
wadau kibao leo wamehudhuria sherehe za miaka 47 ya uhuru wa tanzania bara neshno

Michu tunajua hiyo camera inatoka kwa mshikaji wako Abuu Liongo!!
ReplyDeleteMiamvuli mingine isingeruhusiwa kwenye sherehe za kitaifa.
ReplyDeletesalaam balozi. yaani katika engo zote umeeona uchukue hii yenye mwavuli wa liverpool. ama uchokozi.
ReplyDeleteNdo maana Michuzi unaonekana mweusi kuliko ulivyo. Unashinda sana juani
ReplyDeletehiyo camera video ni dollar 80 walgreens . fake hazifanyi kazi baada ya miezi kadhaaa. michuzi unanichekesha wewewewe
ReplyDelete