
kuku huyu na vifaranga vyake ananikumbusha enzi za young pioneers enzi hizo tukiwa na mashati yetu ya kijani, suruali nyeusi na skafu pamoja na kapelo. hapo kamanda wa gwaride anaaanza kupayuka wakati mguu wa shoto umekita chini na anamalizia mguu wa kulia ukiwa unainuka. unapiga moja, mbili, tatu...unageuka, unarudi tena moja, mbili, tatu, unalamba saluti halafu mguu juu wa....waa...waaa... hadi raha manaake. siku hizi hamna sana mambo kama haya.
wadau hii si blah blah tu, bali pia ni kuwakumbusha kwamba ile globu yenu ya
libenekelataswira.blogspot.com bado ipo hai na inasubiri matirio toka kwenu.
yaani naona wadau mnasahau kwamba hilo si langu mie pekee bali la 'walevi' wenzangu wa masnepu. leteni mavituzzz kama haya kupitia
tuendeleze libeneke. (mdau lilly vipi, umeishiwa nini... hahahaaa!)
au vipi wadauzzzz...
-michuzi
Hapa najua kunguru kafanya vitu vyake, kama sio mwenye kuku kuyala mayai na kubakia vifaranga vitatu tu.
ReplyDeleteMoja mbili tatu, mbili tatu mojaaa.
Hapo umenikumbusha mbali, Mafinga,kwa Afande nusu-mungu, na mkuu wa Kambi,afande Mlai, sijui wako wapi sasa.
emu-three
Sijaishiwa acha kabisa kunichafulia jina Michuzi! Ndio maana ukakosa ndege kwa wasukuma wakati usafiri wa UNGO kibaooo mitaa hiyo kwa watani zetu! Ngoja niingie bush December!Ile camera si unaijua inapiga hadi rangi ya mchanga!
ReplyDeleteMdau Lilly
Poa mkuu, unaomba picha, lakini ulizotumiwa hujazipost na wala hujasema kwanini hujazipost, hivyo sio kitu kizuri unachokifanya, kama unatumiwa picha halafu huzipost na wala hutoi sababu kwanini huzipost inakatisha tamaa wale wenye nia ya kukutumia taswira, ustaarabu ni kumweleza yule aliyekutumia taswira na kumweleza kwamba hazijakaa vizuri au vipi, mie nimesikitika nilizokutumia hujazipost mpaka leo,na nashangaa ninapokuta hapa unaomba watu watume taswira. ni hayo tu,
ReplyDeletewabeba maboksi...nadhara kama hizo ndio mnazikosa kule ukimbizini!!!nasikia kuku kule ati wa mashine!!!
ReplyDeleteMh!... nimepitia young pioneer wakati ule wa TANU, kumbukumbu yangu kuhusu hako kagwaride naona michuzi `umichenka`, ..........heshimaaaaa kulia, pale unapiga zile hatua tatu za kugeuka kulia mguu wa kulia ukianzia kupinda na hatua ya tatu inakita kwa nyuma na kasaluti waaa, halafu kurudi ni hatua mbili si tatu kaka. baada ya hapo nataka kuona soli ya clipper(original chinese) na baadhi ya kofia chini mpaka ile machoooooo mbele! Hapo kaka namuona marehemu mzee Mayagilo akirukaruka kwa raha ya muziki!
ReplyDeleteHii ndio tofauti kubwa kati ya kuku na bata. wakati kuku vifaranga vyake siku zote huvitanguliza mbele kwa ulinzi, kuhakikisha vipo salama. Bata yeye huwa ndio anatangulia mbele kuongoza njia na vifaranga hufuata kwa nyumba.
ReplyDeleteGreat shot jamaa bila shaka atakuwa amedelete kadhaa kupata hiyo iliyotulia hivyo.
Jimmy
Anonym. wa 3.02 PM wamtaka mungu maneno weye, nitakuchambura ka karang!!!!!! Xcschwiiiiii!!!!....@@#??<> kunguru wa Pemba weye.
ReplyDeleteMpiga Box
Huyu kuku si mtetea ni jogoo. Mtetea kaenda kwenye ngoma.
ReplyDeleteBalozi hiyo heading imeniacha hoi. Mmmhu.
ReplyDelete