MKUTANO WA MAKAMISHNA WAKUU WA SKAUTI WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KUWA MOROGORO TAREHE 10 – 12 DESEMBA 2008,

Chama cha Skauti Tanzania kitakuwa mwenyeji wa Mkutano wa Makamishna wakuu wa Skauti wa nchi za Afrika Mashariki na ya Kati.

Mkutano huo wa siku 3 umepangwa kufanyika mkoani Morogoro kuanzia tarehe 10 hadi 12 Desemba 2008, na utawajumuisha Wajumbe 6 kutoka kila nchi ambazo ni Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Ethiopia na Tanzania.

Sambamba na mkutano huu pia kutakuwa na mashindano ya maskauti ambayo yatajumuisha vikosi [Patrol] 4 kutoka kila nchi wanachama.

Hii ni mara ya tatu kwa Tanzania kuwa mwenyeji wa shughuli kama hii, mara ya kwanza Tanzania kuandaa mashindano hayo pamoja na Mkutano kama huo ilikuwa mwaka 2002 shughuli ambayo ilifanyika mkoani Morogoro katika kambi kuu ya mafunzo ya uskauti iitwayo Bahati, na mwaka 2005 ilifanyika mkoani Arusha.

Mashindano ya skauti kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati pamoja na Mkutano wa Makamishna Wakuu wa Skauti ni jitihada zilizowekwa na Viongozi hawa ili kudumisha Umoja na Mshikamano katika jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki na ya Kati.

Mkutano huo pia utapanga mikakati ya kupambana na changamoto zinazowakabili vijana katika nchi hizo, changamoto hizo ni pamoja na Madawa ya kulevya, Vita dhidi ya rushwa na mapambano dhidi ya janga kubwa la Ukimwi.

Mada zingine zitakazo jadiliwa ni pamoja na mauaji wa albino, katika nchi za Afrika ya Mashariki na Kati.

Mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mkutano huu atakuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mheshimiwa Jumanne Maghembe ambaye pia ni Rais wa Chama cha Skauti Tanzania.

Mkutano wa Makamishna Wakuu wa Skauti hujumuisha wajumbe wapatao 40 wakati mashindano ya maskauti hujumuisha vijana maskauti wapatao 200,
Mashindano ya maskauti yatafungwa rasmi siku ya tarehe 13 Desemba 2008 ambapo washindi katika fani mbalimbali watatangazwa.

LAURENCE H. MHOMWA.
KAMISHNA MKUU.
SIMU: 0784 737230 / 0755 019288

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...