December 9, 1961 Tanzania bara ilipata uhuru na mwaka uliofuata tukawa jamhuri. Nimeona shamra shamra za sherehe za uhuru kwenye blog yetu ya jamii. Naomba kutoa salamu za uhuru kwa watanzania na wadau wote popote pale walipo duniani.

Naona heshima na fahari kubwa kuwa Mtanzania na najitahidi kila niliwezalo kuitangaza nchi yetu nikiwa huku ugenini.


Mungu Ibariki Tanzania

Mdau Hasheem Thabeet

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. excellent ndiyo tunawataka watu kama nyie muipeperushe bendera ya tanzania.I'm proud of you hasheem

    ReplyDelete
  2. HASHEEM, ASANTE SANA KWA WALLPAPER!!

    -MZOZAJI

    ReplyDelete
  3. Michu mbona hujatuambia kuwa TID kapata msamaha wa Rais. Sasa itabidi ajirekebishe aache ulevi. Mdau ughaibuni.

    ReplyDelete
  4. Safi sana Hasheem...huo ndio uzalendo wenyewe!! Sisi Watanzania pia tunajivunia sana kuwa na Mtu kama wewe huko Ughaibuni! Tanzania inahitaji wazalendo kama wewe katika kuleta Maendeleo...kila mtu akifanya hata juhudi kidogo kwa maendeleo ya Taifa letu tutafika mbali sana!! Watu wamebaki kujilimbikizia mali na kutafuta sifa za kijinga kupitia magazetini na maredioni...Nimeguswa sana na kauli yako kwamba unafanya kila linalowezekana kuitangaza nchi hii...safi sana! Mungu ibariki Tanzania na watanzania wote ndani na nje ya mipaka ya nchi hii

    ReplyDelete
  5. Amen!Kila la kheri na wewe pia!

    ReplyDelete
  6. Hasheem kweli wewe ni mzalendo. safi sana Dogo, endeleza huo moyo wa kuipenda nchi yako, Nami ninajivunia sana mafanikio yako, Ubarikiwe saana.

    ReplyDelete
  7. Keep it up, I tend to believe he will be a national hero in years to come, He will be a real deal once he step in NBA, KEEP IT UP, the young ones are looking up to you.

    We have a true champion at last.

    By Mchangiaji

    ReplyDelete
  8. haaaaaa proud Tanzania. When they cry we lough loud ukiuliza kwaniiiii wanawalilia watanzania now its our turn to show the world we can make it as Tanzanians

    ReplyDelete
  9. Hasheem,
    Wewe ndio tegemeo la vijana Tanzania ktk kuendeleze uzalendo,hasa hasa kwa kujivunia kuwa Mtanzania.
    Ongeza bidii ktk kila ufanyalo na utafanikiwa.
    Mdau
    Mtanzania.

    ReplyDelete
  10. Afadhali na sisi wabongo tupate 'real role model' instead ya kujifananisha na kina Pdiddy na kutia vijiti mdomoni. Wenzetu culture zao na zetu tofauti sie kazi kuiga tu na wengine wana 'wish' wangekuwa 'wanyamwezi'Hongera Hasheem kwa kujivunia utaifa wako
    Mdau UK

    ReplyDelete
  11. HASHEEM WENU
    WETU OBAMA
    NANI ZAIDI
    MTANI WA JADI FROM NAIROBI CITY

    ReplyDelete
  12. Finally... He got it! It only took one msg abt Tanzania, and all over a sudden he is a HERO, a ROLE MODEL and Shining example to be followed.. No one is ranting anymore kwamba ooh atashindwa kwenda NBA, ooh Dogo ana misifa, ooh Aache ulimbukeni kuongea kiingereza yeye Mswahili, ooh sijui nini.. zote zile kumbe zilikuwa kelele za Chura mtoni!!!

    From,
    IloveHasheem.blogspot.com

    ReplyDelete
  13. Ah Mtani wa Jadi weee... ama kweli kitanda hakizai haramu! Hivi angekuwa jambazi mngemkumbatia hivyo nyie jaduong!? Oooh Obama, ooh Mkenya, oooh White house itajengwa Nairobi, ooooh tunamtafutia mwanamke wa kijaluo... oooh si unajua hata wale watoto wake tutawaita majina ya kijaluo....Ole wenu Kenya... ole!

    ReplyDelete
  14. HASHEEM NI MTANZANIA NA OBAMA NI MWA-AMERIKA/USA SI MKENYA HIVI MTAAMBIWA MPAKA LINI? HIVI BAADA YA KUPATA URAIS UMESHAWAHI KUMSIKIA AKITAMKA KENYA!!! MTASHANGAA KWENYE MATAA, KAMA HAMLIJUWI JIJI NENDENI FERRY, MLIDHANI MTASUKUMU TEMBO KWA UBUA, AU MLIDHANI KWENDA AMERIKA/USA ITAKUWA KAMA KUMSUKUMA MLEVI VILE, MTAKOMA UBISHI.

    ReplyDelete
  15. M nakukubali sana dogo we uko proud kuwa mtanzania kuna wapumbavu wakifika huko wakipata chansi kidogo wanajifanya sio wabongo.Wengine hata status(makaratasi) hawana.Ahsanteni!

    ReplyDelete
  16. sisi wakwetu ni kuku wa kienyeji sasa obama si unaona kuku la kizungu hebu angalia mchanganyiko wa hasheem kama ujasikia ni msukuma na mzaramu au mnyamwezi na mkerewe na wote wanatoka proud tanzania ebwana acha tu. ngoma iko kwa wenzetu msomali aliyekimbilia kenya na muisraeli aliye kimbilia us baada ya kibano cha hitler matokeo yake obama huuuuyo aja

    ReplyDelete
  17. sisi wakwetu ni kuku wa kienyeji sasa obama si unaona kuku la kizungu hebu angalia mchanganyiko wa hasheem kama ujasikia ni msukuma na mzaramu au mnyamwezi na mkerewe na wote wanatoka proud tanzania ebwana acha tu. ngoma iko kwa wenzetu msomali aliyekimbilia kenya na muisraeli aliye kimbilia us baada ya kibano cha hitler matokeo yake obama huuuuyo aja

    ReplyDelete
  18. UTAISHIA KUTUMA SALAM KAMA KIPINDI CHA MCHANA MWEMA RADIO TANZANIA CHINI YA SARA DUMBA.
    WATU WALIKUWA WANAITWA MABINGWA WA SALAMU, AKINA NOEL NAMALOWE NA WENZAKE WALIOKUWA WAKIJIFANYA WANASAFIRI KILA MKOA WAKATI WALIKUWA WAKISOTA BARABARA YA PUGU KILA SIKU. LAKINI SALAMU ZIKITOKA...AKIWA MORO, TANGA, TABORA, MWANZA, ETI NA MTWARA WAKATI HUO BARABARA IMEJAA MAHANDAKI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...