supa staa wa filamu steve kanumba akikabidhiwa kitita cha dola 500 na meneja wa duka maarufu la vipodozi la arise beauty supply ili amkabidhi mwakilishi wa mdau sabra nassor wa dublin, ireland, aliyeibuka kuwa mdau wa milioni 5 wa globu hii ya jamii na kupata zawadi
steve kanuma akimkabidhi mdau abdallah ally, shemeji ya mshindi wa shindano la mdau wa milioni 5, sabra nassor, mchana huu huku wafanyakazi wa duka la vipodozi la arise beauty supply wakishuhudia
balozi wa zain akiwa na abdallah ally, steve kanumba na wafanyakazi wa arise beauty supply
steve kanumba akishukuru kwa kujipatia zawadi ya krisimasi ya pafyumu za nguvu toka marekani ikiwa ni kama alama ya shukurani kwa kazi nzito aliyokubali kuifanya ya kumkabidhi mwakilishi wa mshindi wa dola 500 za mdau wa milioni 5 sabra nassor leo
abdallay ally akishukuru kwa niaba ya shemejie baada ya kupokea mkwanja
abdallah ally akila pozi na meneja mkuu wa arise beauty supply, da' rose, na steve kanumba
GLOBU YA JAMII INATOA HONGERA KWA MDAU SABRA NASSOR KWA USHINDI WAKE WA ZAWADI YA DOLA 500 BAADA YA KUIBUKA KUWA MDAU WA MILIONI 5.
GLOBU HII PIA INATOA SHUKRANI ZA DHATI KWA DUKA MAARUFU LA VIPODOZI LA ARISE BEAUTY SUPPLY KWA KUKUBALI KUDHAMINI SHINDANO HILO NA KUTIMIZA AHADI YAKE. TEMBELEA TOVUTI YAKE KWA KUBOFYA HAPA
VILE VILE GLOBU YA JAMII INATOA SHUKRANI KWA SUPA STAA STEVE KANUMBA KWA KUACHA SHUGHULI ZAKE KIBAO NA KUJA KUTOA ZAWADI. HII INAONESHA NI JINSI GANI KANUMBA ALIVYO NYOTA KWA MOYO WA UKUNJUFU NA UCHESHI ALIONAO. MOLA NA AKUPE MAFANIKIO MAKUBWA ZAIDI YA HAYO ULIYOPATA.
-MICHUZI






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Bongo kiboko.. sasa hilo begi la victoria's secret linatafuta nini hapo? Inamaanisha wamenunua vitu huko na kuja kuviuza kwenye yale yale mabegi.

    ReplyDelete
  2. jamani jamani gift bag ya pink ya victoria secret inakuwa gift wrap ya zawadi ya mwanamme? na ndani kulikuwa na products za victoria secret? mana % 98 ya products za victoria secret ni feminine isipokuwa perfume ya" very sexy for men "ndo mana nimeweka 98%.
    sasa amekumbatia kabisa gift bag i hope hatonukia kama mwanamke.
    kaka chunguza ulichopewa ikibidi rudisha uka exchange pls pls.

    ReplyDelete
  3. superstar? are you joking?

    ReplyDelete
  4. Wewe anon wa December 24, 2008 8:48PM unafikiri supa staa lazima awe wa USA au UK tu? Hata TZ tunao masupa staa wetu ata kama hawajulikani dunia nzima.

    Na we Anon wa December 24, 2008 8:30 PM, we tangu ujua Victoria secret kuna vitu vya mademu basi unazani wanaume hawaezi nunua viitu au hawawezi kununulia wake zao viiitu vya victoria na kufungiwa umo? kwani kanumba haezi kupewa zawadi ya mkewe? au gal frendi wake?

    ReplyDelete
  5. Hiyo perfume ingenifaa mimi wakati huu wa xmas. Ungenipa hiyo (kazi kubwa) ya kukabidhi zawadi....hehehheheheheheh

    ReplyDelete
  6. Huyo mpokeaji si ulisema aje ameulamba mbona kaja kihasara hasara, na huyo kanumba kashaanza kuvaa shumizi ,shati gani hilo mwili wote nje.chini ana ndala. mnajoki ehhee.

    ReplyDelete
  7. M'Kiti & Mh.Balozi,
    Vitu vya 'pinki' huku Uingereza twaviogopa sana, otherwise Hongera! na shughuli ya kukabidhi zawadi kwa msomaji wa million 5 ktk blog hii inazidi kuboreshwa mwaka hadi mwaka.

    ReplyDelete
  8. Hizo gift alizopewa haina maana kwamba ni lazima atumie yeye.

    ReplyDelete
  9. yaaani huyu jamaa ananikumbusha mvuvi mmoja hivi wa nansio kwanza angalia sijui niite shati nahisi ntakuwa nimekosea ten angalia miguuni alichovaaa,

    ReplyDelete
  10. Kanumba umepaka nini usoni..this is a compliment brotha....au umetumia pro-active solution manake hata kina P.Diddy wanaisifu huku marekani.....it worked..
    Nachotaka kujua hapo kwenye hilo duka kuna products za Victoria Secrets??Manake Dar huwa natafuta sana body mist za Victoria Secrets na huwa sizipati...I'l be happy kama wanazo.

    ReplyDelete
  11. Wabongo wengi akili zenu zimekaa kubania bania tu. Mkiona picha moja kwa moja mnataka kukosoa. Sijui lini mtabadilika. Sasa hapo kuna nini kibaya hadi muanze kukosoa?

    ReplyDelete
  12. Mtu unaeongelea ndala mimi sioni kama ni ishu kubwa ya kumaindi mtu. Ukiwa sehemu za watu wenye hela mfano mzuri japan unaweza kukutana na mtu yuko na ndala zake hata especially sehemu za maana na ukiambiwa anamiliki nini na nini unaweza ukabaki mdomo wazi.Na usidhanie kuwa atakuwa anamiliki vitu eti gari etc....no no no yaani vitu vya uhahkika na visivyo hamishika na miradi iliyoshiba.Haya mambo ya ndala jamani yasiwafanye mdharau watu kwakweli.......

    ReplyDelete
  13. Hahaaahaaaaaaaaa eti amevaa shumizi!!

    Naona aliyetoa hii comment ni mmoja wa vijana wa ze comedy

    ReplyDelete
  14. Hivi ni lini watanzania tutasifia kwetu na wasanii wetu,kila mkiona celebrity wa Bongo lazima mumtoe kasoro,Tusipo i appreciate Nchi yetu wenyewe na watu wetu nobody will come from outside na kuisifia Nchi yetu,
    Kuishi Marekani si kujua kila kitu
    kwani wakitumia hiyo mifuko or wherever cha Victoria secret kunatatizo gani??????????
    Acheni hizo,shaurini kitu kilicho bora inchi yetu ibadilike na si kashfa ambazo zinazidi kuirudisha nyuma.

    ReplyDelete
  15. Me's Inglish is speak veere vere little but I is like to contribution my seeings. Whay is the superstar the Kanumba see inside the camera picture? Is not unnecessarily at all. Is forgive my Englishing is me am learning.

    Thank you.

    ReplyDelete
  16. Hii Blogu ya jamii haiishiwi na michango ya mawazo, maono n.k

    Tunashukuru supa staa wetu wa Basketball alielewa mchango wa hii globu ya jamii na akakubali kuwa mawazo mengi yamemsaidia ktk suala la supastaa yeyote anayeshiriki ktk mtoko,shughuli, uwakilishi, kazi n.k anayotakiwa kuonekana mbele ya jamii ikiweko washabiki wake, watanzania wenzake,watoto n.k tuliona alipotuwakilisha ktk shughuli ya Sullivan hapo A-Town.

    Hivyo Steven Kanumba usipuuzie mchango wa wanajamii wa globu hii, nakutakia kazi njema.

    ReplyDelete
  17. zawadi amepewa kanumba,sio mkewe ndo mana nashangaa of all the wraps why pink and victoria secrets? wenye duka walitaka show off na gift bags za victoria secret ,sema wamekosea kumpa mwanamme zawadi na kutumia gift bag ya victoria secret .

    lazima kieleweke kama kweli wanaume hawawezi pewa zawadi kwenye mifuko iliodisigniwa kifeminene na well known as sexy and feminene.

    wanaweza kwenda victoria secret kununuwa zawadi za wake /dada zao .lakini sio zawadi za kaka au baba zetu ziwekwe humo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...