TAIFA STARS IMEFANIKIWA KUSONGA MBELE KWENYE MICHUANO YA CHAN KWA KUIBANJUA SUDAN JUMLA YA MABAO 5-2 YA AGGREGATE, BAADA YA KUSHINDA BAO 2-1 LEO HUKO KHARTOUM.
MPIRA UMEISHA NA TAIFA STARS KIDEDEAAAAAAAAAAAAAAA!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Jaji aonya kesi za EPA zisiwe kiini macho

    2008-12-12 13:23:44
    Na Joseph Mwendapole


    Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji Kiongozi mstaafu, Amir Manento, ameitaka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP)kupeleka ushahidi madhubuti na haraka mahakamani ili kuthibitisha mashtaka ya ufisadi uliofanywa katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ili kesi hizo zisionekane kuwa ni kama mchezo wa kuigiza.

    Alisema vinginevyo washitakiwa wote wanaweza kuachiwa huru na kesi hizo zinazowahusu viongozi na wafanyabiashara zikaonekana kama mchezo wa kuigiza machoni mwa jamii.

    Akizungumza kwenye hafla ya kilele cha miaka 60 ya tamko la haki za binadamu juzi, Jaji Manento alisema ushahidi huo lazima upelekwe haraka ili usaidie kufikiwa kwa maamuzi ya tuhuma hizo mapema.

    Alisema Jeshi la Polisi ambalo ndilo linahusika na upelelezi kwa kushirikiana na ofisi ya DPP wanapaswa kujizatiti kwenye ushahidi ili kinachofanyika sasa kisije kikaonekana kama kiini macho au mchezo wa kuigiza.

    ``Kupandisha watu mahakamani kisha mkakosa ushahidi wa uhakika wa kuwatia hatiani wakaachiwa huru kunaweza kuonekana kama mchezo wa kuigiza, lazima polisi na DPP wajizatiti kupeleka ushahidi wa uhakika,`` alisema Manento.

    Tayari watuhumiwa 20 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa madai ya kuhusika na wizi wa EPA. Jumla ya Sh bilioni 133 ziliibwa kilaghai katika akaunti hiyo.

    Tangu sakata la EPA liibuliwe nchini, kumekuwa na hisia tofauti miongoni mwa jamii juu ya utashi wa serikali wa kuwafikisha mahakamani wahusika wote wa wizi huo.

    Miongoni mwa hisia ambazo zimekuwa na msukumo mkubwa ni mustakabali wa kampuni ya Kagoda Agriculture Limited ambayo inatuhumiwa kujichotea kilaghai dola za Marekani milioni 30 sawa na Sh bilioni 40 kutoka EPA, lakini hadi sasa hakuna hata mtuhumiwa mmoja wa kampuni hiyo aliyefikishwa mahakamani.

    Kampuni ya Kagoda inahisiwa kuwa ndiyo muasisi wa wizi wa fedha za EPA; ikiwa imemharibia kazi Waziri wa Kwanza wa Fedha mwanamke wa Tanzania, Zakia Meghji, ambaye aliteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kushika wadhifa huo mara tu alipounda serikali Januari 2006.

    Meghji kwa kupotoshwa na aliyekuwa gavana wa BoT, Marehemu Daudi Ballali, aliandika barua kwa kampuni ya ukaguzi ya Deloitte Dutche akitetea uchotaji wa fedha uliofanywa na Kagoda kuwa zilikuwa ni kwa masuala ya kiusalama, kabla ya kuitengua barua hiyo.

    Waziri huyo hakurejeshwa kwenye baraza la mawaziri baada ya kuundwa upya kufuatia kujiuzulu kwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, kutokana na sakata la Richmond.

    Awali, akihutubia wananchi katika maadhimisho ya juzi, Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein, alisema serikali itaendelea kuimarisha idara ya mahakama kwa kuongeza bajeti ili ziweze kutekeleza majukumu yake kwa wakati.

    Alisema hali hiyo inaweza kusaidia kuhakikisha haki inatolewa kwa kila anayestahili.

    Akitoa salamu za Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, Kaimu Mwakilishi wa Umoja huo, Dk. Mohamed Belhocine, alisema matukio mengi ya uvunjifu wa amani yanayotokea sasa ni matokeo ya kudharauliwa kwa haki za binadamu na aliishauri serikali kutekeleza kwa vitendo maazimio na makubaliano ya mikataba ya haki za binadamu.

    Maadhimisho hayo yalitanguliwa na maandamano ya amani ambapo wananchi na wadau mbalimbali wa haki za binadamu waliandamana wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe unaopinga ongezeko la matukio ya ukandamizaji wa haki za binadamu.


    Post a Comment ~ Rudi Mwanzo ~ mtumie Rafiki

    ReplyDelete
  2. Hongera sana Stars na wahusika wote
    hii ndio inavyotakiwa,soka imepanda sana tz,iliyobakia ni kukaza buti ktk ligi zetu na kukuza kiwango zaidi,ikiwepo wafadhili kuwekeza na kusaidi madaraja ya chini pamoja na soka la watoto kwani wao ndio wanaojipanga huko chini kuja kushika hili linalofanyika sasa la kipandisha kiwango,kwani hawa wa leo baada ya muda sio mrefu watachoka na warithi ni watoto waliopo chini,pia vilabu vikubwa vianze kuchukuwa wachezaji kutoka mataifa mbali mbali duniani ili kuibadilisha sura soka yetu pamoja na kuleta ushindani zaidi na kukuza kiwango kwa wachezaji wetu kusoma kutoka kwa wachezaji wa nje,ikiwemo brasil,wapo wachezaji wengi vijana ambao wamechoka kimaisha na wanataka kupata nafasi hata hapo bongo kuja kusakata soka,aidha kualika timu za europer kuja kucheza games za majaribio na timu zetu kwani hii itapelekea vijan wetu kujiamini na kuona kuwa kiwango chao ni kikubwa sana na wanao uwezo wa kucheza soka pahala popote duniani,thanks,hongera sana stars

    ReplyDelete
  3. Asante Balozi kwa kuweza kutuunganishia matokeo ya Sudani jioni yaleo. Tunawatakia kila la kheri Taifa Stars. Sasa kazi kwao kujiandaa na Mtanange huu. Hiyo ni hatua moja mbele. Hongera Taifa Stars, Mungu Ibariki Tanzania

    Mdau
    Cardiff

    ReplyDelete
  4. wasikilizaji chakubanga ameipatia tanzania Bao la Final CHAN na kushinda kombe la CHAN kwa mara ya kwanza, mmesoma hapa kwanza.

    ReplyDelete
  5. hongera maximo na vijana wako wote. naomba huo ushindi uwe ni mwanzo sasa wa kuiweka Tz kwenye ramani ya soka duniani. sasa tupeleke vijana wanaouzika (umri na maumbile). ni wakati wa kina tegete, henri, ngasa, boban, kigi, uhuru na wengine. pia waongezwe vijana wachache wa under 20 kwa kuwaandaa na michezo mikubwa ijayo (mifano ya walcott na pato).

    hongera stars na vijana mmetupa rahaa.

    ReplyDelete
  6. C O N G R A T U L A T I O N S!!!
    H O N G E R A !!!

    ReplyDelete
  7. Maximo bonge la kocha, mambo ya kuchagua wachezaji kwa majina yao aliyaacha ona sasa mpira unavyopigwa. Mziray Upo? Kainoe simba..

    ReplyDelete
  8. Michuzi haya mamabo ya EPA tuwaachie wanasiasa kwangu mimi hayana maana yoyote. MAXIMO 11 oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.

    ReplyDelete
  9. Kesho J'Pili itangazwe kuwa siku ya mapumziko ya taifa.

    Mdau,zero

    ReplyDelete
  10. Hongera sana STARS, tuko pamoja ktk kushangilia ushindi huu. Ni hatua moja kubwa mbele tumepiga! Hongera sana!!!

    ReplyDelete
  11. JAJI AMIR MANENTO ANACHOFANYA NI USANII NA PILITICS, YEYE SHERIA AMESOMEA WAPI? HAPASHWI KUZUNGUMZIA KESI AMBAYO IPO MAHAKAMANI NJE YA MAHAKAMA HICHO NI KINYUME CHA SHERIA MAHALA POPOTE PALE DUNIANI, INAWEZA KUPELEKEA MALALAMIKO MBANDE ZOTE MBILI ENDAPO MAAMUZI YAKITOLEWA NA KUADHIRI UPANDE MMOJA NA KUONA WAMEONEWA, ANAPASWA KUZUNGUMZIA MAMBO HAYO MAHAKAMANI YEYE SI POLITICIAN. AACHE UMBEA WAKE, HAYA NI MAONI YANGU MIMI SI YAKO WEWE MICHUZI, WALA USIOGOPE KUYABANDIKE KWENYE BLOG, NAONA UMUOGA SANA KUPANDIKA MAONI YA WATU.

    ReplyDelete
  12. wewe michuzi mnafiki mkubwa najua hutaingiza hii comment jana tume tuma comment umezibaana mnafik mkubwa

    ReplyDelete
  13. واو! كيفية قراءة فقط ماكسيمو الحادية عشرة للم السودانية.

    http://www.sudansoccer.net/

    ReplyDelete
  14. Wee misupu,michezo na siasa wala haviendani.hayo maoni ya sisa ungeyaweka yanapohusika.ama ungeyabania ili wahusika wajue hapa si mahala pake na next time wapeleke ktk post inayohusu siasa.

    aniwaiziii, HUREEEEEEEE STAZ!!! i hpoe huu ndio mwanzo 2.more still 2 come.
    nashukuru wadau wengine wameacha kulialia juu ya kuachwa kwa wachezaji wanaowapenda.soka la siku hizi si la KUBEBANA kwa kuangalia majina.

    ReplyDelete
  15. HOGERA WADAU WOTE WALIOITIKIA WITO,NA KUICHANGIA STARS,NAWAPENDA SOKA WOTE.TUNAIMANI UONGOZI UTAKAO CHAGULIWA LEO, KUKAA CHINI NA MAXIMO AOGEZE MKATABA WAKE,AMEDHIHIRISHA NI KIASI GANI MWALIMU WA SOKA KWELI NA SIO MWALIMU MAJUNGU,ASANTE KWA KUWAWEKA SOKONI VIJANA WETU,SOKO LA MPIRA WA KIMATAIFA,MUNGU AKIPENDA HUENDA NA MAISHAO KUBADLIKA KWA JASHO LAO HONGERENI SANA STARS,PLEASE MSIBADILI JINA LA TAIFA STARSSSSSSSS

    ReplyDelete
  16. uyo annon aloandika lugha za watu wa nje (KIARABU) tusozielewa sie katika blogu ya jamii na wewe michu na roho zako za kwanini ukapost,,whyyyyyyyyyy?
    unatuboa sana post zingine waminya afu kiarabu coz kuna watu mtu mmekisomea madrasa mwabandika,,aaaghhaggh '~~**'#~.//" kabisa nyie
    BANA NA HII SASA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...