picha ya pamoja
Mama Salma Kikwete juu na JK (Chini) wakimpa mashada ya maua bin ti yao Dk. Salama Kikwete baada ya kula nondozz za ya Doctor of Dental Surgery Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili. Rais Mstaafu ambaye ndiye mkuu wa chuo hicho anashuhudia kwa pembeni




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. NI FURAHA ILIYOJE? KUSOMEA NYUMBANI INGAWA UWEZO WA KUSOMEA KOKOTE UPO? BABA OKOA VIZAZI VIJAVYO. WALIMU TUNAO WATEGEMEA HUKO VYUONI MUCH PCET(FOE) WAMEFICHA AU KUTUPA VIJITI VYA KUPOKEZANA (REALAYS)(PHDS,MS. BSCS) UPEO WAKO WA KUONA MWISHO (ZAIDI YA MBALI) NA KUTUJENGEA VYUO VINGI VIKUU HATUTO KUSAHAU KAMWE.CHUO KIKUU KAMA KISIVYO MAANA SASA VIMEKUWA VYUO VIKUU KILIPINGA SANA MAWAZO YAKO KWA MPOTOSHO WAUPEDO WAO KWAMBA ELIMU ITASHUKA, WAKATI WALITAKIWA WAJADILI WATAKIPANDISHAJE. MAANA VIJANA WAKO TUMEKUWATUNATANGA TANGA DUNIANI TUPUNGUZE MSONGO WA MAWAZO KWA KIJIMSHAHARA KILICHO JUU KIDOGO. HATA HIVYO BABA WAPO WALIO TAYARI KUFANYA KAZI KWA MAJI YA KUNYWA TUU NA MILO MIWILI KWA SIKU.UKOMBOZI WA NCHI HII UNAHITAJI KUJITOLEA KWANI MPAKA MWISHO WA DUNIA HAUTAWEZA KUPATA WATU WA KUUFANYIA KAZI BURE KAMA NCHI ZILIZOENDELEA ZILIPOPATA NAFASI HIYO MIAKA HIYO. WAPE CHANGAMOTO WANAO{ WAZALENDO} WAOKOE KIZAZI HIKI.UJUMBE WETU NI KWAMBA HATUOMBEI CHAMA AU SEREKALI IKOSEEILI TUONEKANE TUNAFAA KWA KUKOSOA.SIFA YETU NI KUTATUA MATATIZO YA WANANCHI MAENEO YA TUKIO KAZI YETU NI ELIMU TUU.KONDOO MMOJA AKIPOTEA 99 WANATELKEZWA MPAKA MMOJA APATIKANE.

    http://fie.engrng.pitt.edu/icee2006/papers/3399.pdf

    TUMAINI GEOFREY TEMU

    ReplyDelete
  2. Hii imetulia, jamani watanzania mna rais ambaye ni mfano wa kuigwa sio tu na watu wote uila sana kwenu nyinyi. Ametoa mfano mzuri kama mzazi kwa kusomesha watoto wake kwenye professions za nguvu na hivo basi hamna budi ila kuchukua changamoto hii na kufuata nyayo. ridhiwani ni wakili, salama ni dentist nk. Hii ndio mojawapo ya jinsi tanzania inaweza jikomboa dhidi ya "mamisheni" ambazo nchi jirani zinazo za kuiteka rasilmali yenu. Kwa kifupi, develop a highly skilled human resource that will enable tanzania protect and tap its own natural resources. this is where the future of bongoland lies yaani ndani ya ubongo. hongera salama na wazazi. shemeji Paulo Kamau, Mkenya mzalendo.

    ReplyDelete
  3. hongera salma.umefanya course tough na Mungu amekuwezesha kila kheri.Elimu isiwe kwa faida yako au yetu tu bali kwa nchi nzima.
    Jakaya proudiest dad two graduates at his home absolutely fantanstic .

    ReplyDelete
  4. Ni furaha iliyoje. Mzazi yeyote yule itampata furaha, awe yeye ni rais au mkulima wa kijijini kabisa.
    Hiyo ni ndoto ya kila mzazi.
    Hengera binti !

    ReplyDelete
  5. Hongera sana binti wa JK. Nondoz za dentistry sio mchezo. Huyu ndiyo binti wa kuoa sasa maana ana sifa zote za kuwa mke mwema. Kwanza kala nondoz kali na pili anatoka state house. Ukimpata ndiyo unakuwa umetoka. Brother Michuzi, naomba contact zake na ninaweza kumpata je huyo binti! Nataka nipeleke posa kwa JK.

    ReplyDelete
  6. salama hongera zako huyu binti mrembo kweli, anafaa kupata promotion, hongera mpendwa.

    ReplyDelete
  7. HONGERA BINTI, HONGERA WAZAZI. AHSANTE MICHUZI KWA KUTOA TAARIFA ZA KUJENGA. SALAMA NI ROLE MODEL KWA VIJANA WENZAKE NA WAZAZI NI ROLE MODEL KWA WAZAZI WENZAO. KILA LA KHERI.

    ReplyDelete
  8. ...wewe kalamba unayetaka contact kupeleka posa kwa JK,acha upuuzi wako hapo kwa kutaka vya mteremko,kwanza demu hawezi kukutaka mchovu kama wewe na mabox yako,wewe oa hiyo mizungu minene yako huko uliko usije kutuletea njaa zako...ebo!

    ReplyDelete
  9. Hongera Salama kwa kupata degree yako ya dentistry. Mwenyezi Mungu akujalie kila la kheri na akulinde na kila la shari. Akujaalie pia ujiendeleze zaidi katika masomo kwani elimu haina mwisho. Mwisho nawapongeza wazazi wake Bi Salama kwa malezi mazuri kwa binti yao.

    ReplyDelete
  10. Kaka Michuzi hiyo ngoma imeolewa au bado ipo ipo tu nataka kujaribu zali! ukipata namba yake nakupa zawadi ya fresh air

    ReplyDelete
  11. Salama hongera sana kwa kutuunga wasomi ingawa wengine kwa kweli uzalendo ulitushinda tukaenda nje ya nchi maana we could not stand ufisadi. At least hapo hata ukipewa kipaumbele kupata kazi na hautaangaika kama wahitimu wenzio tunajua kweli ulisoma sio kama watoto wa vigogo wengine wenye kazi za maana na nondozz za kununua nje ya nchi. Wanakuja huku kufanya ubishoohalafu wakirudi huko wanajua kazi zinawangoja mameneja masoko mabenki and you wonder why watu wanaona bora wahangaike na maboksi Ulaya. Lakini kwa kweli kwa hili Baba yenu ni mfano wa kuigwa na Mungu amjaalie he means well na ni Mzalendo wa kweli mimi ananikumbusha Mwalimi Nyerere Baba wa Taifa sema ulike Mwalimu yeye ameona umuhimu wa Globalisation and that these two things can work together somehow yaani sema tuu Washkaji na Wafuasi wake wanamuangusha simply because hizo tabia za ufisadi ndio ilikuwa kama life yao sas kumkunja samaki wakati kaishauka ni kazi sio mchezo sema JK Mungu akujaalie na anaona nia yako kwa Nchi yako despite na machache yako kwani binadamu wote hatuko perfect hivyo ya kwako tumekusamehe na tuko nyuma na wewe. Na wototo wa JKkwa kweli mmelelewa vyema Salam tulikuwa na kaka yako huku Ridhiwani yaani sijapa kuona most down to earth guy kama vile bab yake hajashika nchi he is vry easy going nashukuru nilipata nafasi ya kufahamiana nae alipokuwa Ukerewe na vilevile sio kama namsifia bali hata kwenye makundi ya ushororo alikuwa humuoni ni kitabu kamaliza shuguli iliyomlete kaanza bila makuu yeyote. TUnamuombea kila laheri na ndoa yake. Sema nasikia mna Dungaembe mmoja huko MRJ haha! Baba hii isikupe presha mana mtu wa hivyo tuko kwenye kila familia, as long as he is under control.
    Mdau hapo juu kaongea azma yako ya kujaza vyuo vikuu nchini kwa kweli I must say that will be the best move ever na legacy kubwa sana utakayoiachia vizazi vya Tanzania ukiweza kufanya hivyo. Kwa mchango wangu tuu mimi niko Ukerewe system ya huku ni kwamba at least kila mji una chuo kikuu kimoja ama zaidi na vyuo vingi vinajulikana kwa kuspecialize more kwenye kitu fulani mfano kama vile nyumbani tuna Mzumbe "sheria" na IFM "uhasibu" lakini bado vinafanya na kozi nyingine nyingi and in my opinion it is the best system ya kuleta maendeleao hata kwa hiyo miji kwani kwenye wasomi hakuharibiki neno na hata pakiharibika watu wanakuwa na plan B na hiyo ni kweli. So to start with sijui kama hii rubish yangu naandika kwa hapa itasomwa but why not kuanzisha changamoto ya kujenga vyuo au kwa kuanza tuu na college kila Mkoa badala ya kuconcentrate Mikoa mikubwa tuu. Na hii kazi Mheshimiwa ungewaachia hao Wakuu wa Mikoa ma RC wawe wa kuisimamia kwani hawana la maana wanalofanya wengi wao ! Wape mafungu ya hizo pesa za EPA zilizorudi wajenge Vyuo ya Usomi mikoani mwao , yaanze tuu hayo majengo and when it comes to furniture na vitabu library na nini jamani hapo sas ndio watu wa Mkoa mzima wachangie hata sisi tulio nje ya nchi tunaweza kuwasaidia kuraise funds but la msingi kitu kianze kwanza.Na hao Ma RC mzee JK asiyewajibika ni aruduishe hela yetu yote aliyokabidhiwa kwa hii project ama la tumfilisi mali zote then umburute mahakamani kwanza kabla ya kumfunga. Yaani haka ndio kawe kaproject kadogo uwape hao wakuu wa Mikoa from now mpaka uchaguzi ujao then tuone itakuwaje, zitengwe seheme Mikoa yote vijengwe vyuo tuone tushindwe wenyewe na hao wakenya wanaotusema sisi ma iliterate .Dr. Kikwete hongera kwa Nondozz Wanawake kama wewe ndio tunaowataka katika jamii yetu.

    ReplyDelete
  12. Hivi michuzi hawa wanasiasa unaoposti mambo yao kwenye hii blog ya jamii wanaposema hela yetu wanamaanisha nini? Naboreka kwelikweli.

    ReplyDelete
  13. Uwezo wa kusoma popote upo lakini sio Marekani.Utoke kwenye mfumo wa Elimu Tanzania halafu usome udaktari Marekani ni ndoto. Kwahiyo na mapesa yake lakini kusoma US ni nadra.
    Udaktari US una wenyewe.

    ReplyDelete
  14. Huyu ni raisi wa mfano bora. Maana maraisi waliopita sijasikia mtoto wake yuko chuo kikuu ukiacha Huseni Mwinyi.

    Haya ikulu ya kisomi hiyoooooo.

    ReplyDelete
  15. 1.ninampongeza Salama .Ni mfano bora.
    2.inapendeza kuwa hata mtoto wa Rais anasoma vyuo ndani ya nchi.
    3.Changamoto kwa JK:Iikiwa mwanao anaweza kusoma nchini pia inawezekana kujenga angalau hospital moja ya kisasa nchini Tanzania na kuokoa mamilioni ya pesa za walipa kodi pale ambapo viongozi wetu huenda
    kutibiwa Ulaya ,Marekani,Na India.Inawezekna.
    3.Sikujua kama DDS ni TOUGH COURSE.Ni kozo ya kawaida tu.Hakuna any toughness hapo.Ni mtazamo wangu.Yet,she deserves kupongezwa.
    {thesonofafrica}

    ReplyDelete
  16. KOZI ZOTE NI SAWA HAMNA CHA HII NI NGUMU AU RAHISI HUO NI MTAZAMO POTUFU NA UKALE/UTOPIA, KILA MTU HUCHAGUWA KUSOMA ANACHOTAKA, HAIWEZEKANI WATU WOTE WAKAENDA KOZI MOJA NI KITU YA KAWAIDA KABISA NA HAKUWA PEKEE YAKE ALIYEMALIZA HIYO KOZI NI WENGI TU AMEMALIZA NAO NA WENGI WAMEPITA KABLA YAKE NA KUWA RESOURCEFUL KATIKA JAMII SI LAZIMA UWE NA DEGREE, NA MAISHA PIA SI DEGREE, NA PENGINE YEYE AMEMALIZA KOZI KWA VILE ALIKUWA NA RESOURCES ZA KUMFIKISHA HAPO MASIKINI VIJIJINI WANASHINDWA KWA VILE HAWANA VITENDEA KAZI VYA KUWAMOTISHA KUFIKIA HAPO, HAMNA TAA ZA KUJISOMEA USIKU, MLO MARA MOJA KWA SIKU, MAJI YA KUOKOTA MTARONI, HAMNA UNIFORM WALA STATIONERIES KWA SHUGHULI ZA SHULE, WAZAZI MAZAO WANAKOPWA HAWALIPWI KWA MUDA MUAFAKA, NDUGU ZAO WALIOBAHATIKA KUPATA DEGREE HAWAPATI KAZI KWA VILE HAWAMJUWI MTU, SASA WATAKUWA NA MOTISHA GANI WA KUSOMA.

    ReplyDelete
  17. Hongera binti. Wenye mtizamo finyu wameshaanza kusema kozi yako ilikuwa rahisi. Unakumbuska msemo wa kiswahili unaosema: Mzigo wa pamba ni sufi kwa mwenzio? Mimi naona huyu binti wa JK ni lazima apewe heshima ya kumaliza kozi yake vizuri na pengine alipata na "awards" za honors ndugi michuzi unaweza kutofafanulia kama alipata honors. Na kama alipata - hiyo ni dalili kwamba kichwa cha huyo binti ni kina akili si mchezo. Tunakuombea mwanawetu uweze kutuokoa hapo nyumbani Tanzania. Jiulize sasa, kama alivyojiuliza mzee JK, nitaifanyia nini nchi yangu. Na wala usiseme nji yangu itanifanyia nini. nenda kajenge nji yetu sasa.

    Tumekupa nondo, jembe na panga kazi kwako mwanawetu.

    Ni mimi, mwalimu

    ReplyDelete
  18. Na yeye alikuwa anashiriki katika MIGOMO au alikuwa agomi je na yeye alikuwa anachelweshewa PESA za UDHAMINI?

    ReplyDelete
  19. Kwa Uzalendo JK umeshinda aisee. Unajua mtoto wake mwingine anasoma hapa ST. Patrick -Trust (Arusha) we acha tu. Wanasiasa wengine na waTZ wote huu ndio mfano wa kuigwa.

    ReplyDelete
  20. Anon Dec 14, 1:01 Je na wewe ni mume mwemaaaa? au unatoa udelele/udenda wa fisi hapa, ili ukatusumbulie binti na kumtumia vibaya kama mawazo yako yanavyolenga? Kama unataka kivuri jitunze pia nawe uwe mzuri Mume mwema, sio uwe mbaya kisha unataka vizuri, waswahili walisema "Usione vyaelea ujue vimeundwa" na pia usione vimemea ujue yuko anaepalilia mjomba.

    ReplyDelete
  21. Huyo anayesema kozi rahisi mbona yeye hakusomea hiyo akamaliza upesi akaja kutusaidia mtaani? Hivi kama ni rahisi hivyo mbona kuna madentist wachache sana ukilinganisha na madaktari wengine? Wivu tuu umewajaa watu, eti resource mbona sie tumesomea kwa kibatari na tumefika chuo kikuu? Hiyo wala sio sababu mtu kama ana nia ya kusoma atasoma tu kama anakimbia umande haijalishi yuko wapi atakimbia tu. Kwani vyuo vyote vimejaa watoto wa mjini na wenye uwezo? Kama hiyo ni kweli sasa mikopo ya nini?

    ReplyDelete
  22. duh binti sidhani ata atankumbuka siku nikimtokea,,,tulikua jirani pale vikawe street mikocheni hahaha
    na neema budodi je???shoga ako kamaliza?
    hongera binti JK afu unalipa ile mbayaaa duh!!!i wish
    ila jaman wadau watoto wa viongozi uwa wanafeli kweli,kukosa udhamini au wanajilipia private???ivi prof aweza tia mkasi ktk test yake,exams,take home nk-lower course work???hahaaaaa iko kaaazi kweli apa----NINA MFANO ULIO WAZI NYIE ACHENI KABISA
    Dr Salama ndo zuri sio kikwete alaaa

    ReplyDelete
  23. Hongera Mwenetu Salama. Umewatoa kimasomaso Wazazi na Nduguzo, na hasa kwako wewe mwenyewe kujikomboa kwa kuwa Msomi na kuwa na uhakika wa kazi ya maana. Mimi kama Mzazi ninapenda kukupongeza kwa dhati wewe na Wazazi wako. Kwani hiyo ndiyo ndoto ya kila Mzazi kuona Mwanae anafanikiwa. Umewapatia pia changamoto nzuri wadogo zako ambao bado wapo shule. Mungu akujalie kila la kheri katika majukumu yako.

    ReplyDelete
  24. gentle lady C
    Honesty ukishakua mtoto wa baba milango yote inafunguka

    ReplyDelete
  25. Hongera sana Salama JK. Umefanya kazi nzuri sana na unastahili kupewa sifa dada yetu. Shule imeisha sasa kinachofuata tafuta mme mzuri wa kufanana na wewe ili kupunguza matatizo unayoweza kukutana nayo mbeleni hasa ukikosea kuchagua. Wapo wanaume wengi tu wazuri wenye future na prospects na mimi pia naweza kuwa miongoni mwa hao. Ninachomwomba tu brother Michuzi anatoe contacts za Salama ili tujaribu bahati zetu.
    Honera sana Salama!!
    Mdau

    ReplyDelete
  26. ACHENI ROHO ZA KWANINI NYIE SI MKUBALI TU YAISHE,NDIO AMEWEZESHWA LAKINI SI AMEWEZA.WANGAPI WAMEJARIBU KUWEZESHWA WAMESHINDWA?
    HONGERA! KWA NONDOZZ

    ReplyDelete
  27. Mdau 'M' maneno yako yanagusa sana na ni mazuri. Mi naona kumbe kuna wengine wanaoona positive side of things. Hao watu wanaoponda kuwa ooh, mtoto wa baba mara ooh, sijui nini, ni kawaida katika jamii. Watu Hatulingani kwa njia yoyote ile. kubalini tu kisha mfanye bidii binafsi ya kufanikisha maisha yenu. Niliyoipenda zaidi ni ile JK kuacha urais wake pembeni na kuhudhuria event hii muhimu katika familia yake kama baba. Wapo mababa wengi tu wenzangu mie hawakuweza kufika eti wako bise "kumbe wapo kwenye starehe zao"

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...