Michuzi,
Pole kaka na kazi za siku na pia zakutuweka update. Nilitaka nishare hii news na wadau kwamba Zimbabwe wametoa noti mpya ya million 500 dollar za kizimbabwe sawa na dollar 8 za marekani ambayo imetolewa mwezi huu wa desemba.
Asante na kazi njema

Mdua bantu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Kwa wale mafisadi wapenda npti nyingi nyingi,jipatie mabilioni ya Bob Mugabe , bado ya moto kabla pesa haijapoa!

    ReplyDelete
  2. kama sio unafiki nini? we unafikiri Mzee anahujumu nchi au Shiva anatumiwa kurudishia wakoloni ardhi ili ndugu zetu waendelee kuwa manamba? funguka macho sio kushabikia tu kila unaochoona kwenye hizo media zao, wacha watu wateseke watajifunza, au hujui historia, waisraeli wanapotoka utumwani Misri waliteseka hadi wakataka kurudi wakaendelee na utumwa lakini mambo latter yakawa safi. wache zim wajifunze the hard way soma kitabu cha mshindi wa tuzo ya Nobel ya Uchumi, Amartya Sen "Development as freedom" humo ndo utaona jinsi gani maendeleo ya kweli na uhuru wa ukweli unamaniasha nini. Sio kuleta dhihaka. Mbona Hata bongo hela thamani ya chini hata Kuliko the nch maskini kama Ethiopia kwenye vita na njaa kila siku.

    ReplyDelete
  3. Dola milioni 500 ama dola milioni 50, mbona unachanganya habari!!

    ReplyDelete
  4. I say'long live Mugabe'well... at least everybody is a millionaire!

    ReplyDelete
  5. Which is which hapo unaonyesha 50Mil Zimbabwean dollars na wewe umeandika 5OO Mil z dollars.

    ReplyDelete
  6. kaka naomba unitajie zimdollars ngapi ndio naweza kununua gari huko?

    ReplyDelete
  7. Duh! I think Mugabe doesn't get it. Million 500????!!!!!!!


    Heaven Almighty lets us not get there in this generation

    ReplyDelete
  8. Tena zina expire date,pengine ikadumu kwa miezi mitatu tu halafu isitumike tena,wataalaamu wenyewe wa uchumi wanasema kwa kuweka expire date inasaidia mzunguko wa pesa...
    bwana zimbabwe walipofikia asa hivi he he he!!!
    kaaazi kwelikweli!

    ReplyDelete
  9. Mdau Asante kwa taarifa, lakini nahisi kidole chako kimetereza hapo. Hiyo no noti ya dola hamsini milioni (Fifty million zimbabwe Dollar)
    Maana najua waosha vinywa watanza kukusakama. bora niwanyamazishe mapema.
    Mgabe inabidi akubali yaishe. La sivyo ataimaliza nchi

    ReplyDelete
  10. Damn!!! Even the late Mobutu Sese Seko Nkuku Ngbendu wa Za Banga didn't reach that boiling point. The highest was 1 million "New Zaire" bill during his regime...We Africans ought to unite and get rid of him as the situation doesn't get any better...

    Kabasele mwana Kin.

    ReplyDelete
  11. Hey! Kuna haja ya kuhamia huko! Nafikiri nami naweza kuwa millionaire in one day:-)
    Chakabanga

    ReplyDelete
  12. Wewe anony 9:54pm, mimi sioni unafiki ila nafikiri sasa imefika wakati Mugabe inabidi apishe damu mpya itakayokuja na mawazo endelevu ya kuwasadia wazimbabwe zaidi. Alipofika hivi sasa hawezi kuitoa Zimbabwe katika matatizo iliyonayo kwa kuwa ametawaliwa na jazba zaidi kuliko busara. Hata wewe umepata nafasi ya kuandika ulichoandika pengine kwa kuwa Julius alitawaliwa na busara zaidi kuliko jazba kwa uamuzi wake wa kuipatia Tanzania damu mpya ya uongozi...Vinginevyo majanga kama "kipindupindu" na mengineyo mengi yanayowatafuna wazimbabwe hivi sasa yangekupoteza kama Julius angekuwa na tamaa ya kuona kuwa yeye peke yake ndio anaweza kuifikisha Tanzania inapostahili kufika.

    Sina maana kuwa ampe "Shiva" ndio nchi itakuwa shwari hapana. Nina imani kuwa kuna watu miongoni mwa hao alio nao wenye uwezo wa kuitoa Zimbabwe hapo ilipofikia.

    Kama kweli anaipenda nchi yake asingekumbatia madaraka mbaka sasa hivi na kuona watu wake wanateketea...

    Mfano mzuri ni wakati Mwalimu alipoulizwa na watu mbalimbali kwa nini usiendelee japo kwa miaka mitano ili kuweza kufanikisha malengo yako... na yeye alijibu kuwa kama aliweza kuwepo kwa miaka 25 na hakufikia hayo malengo basi ni wakati muafaka kuwapisha na wengine wachukue na kuweza kukamilisha malengo.

    Na aliamua hivyo kwa nia nzuri tu. Nina hakika nia na malengo ya Mugabe ni nzuri kabisa lakini imefika wakati awapishe wenye uwezo wa kuitekeleza bila jazba wafanye hivyo.

    Aondoke mapema na wala asingoje mkewe akapigiwe magoti ya dhihaka kama alivyomfanyia mke wa Mwanawasa.

    Shona.

    ReplyDelete
  13. I knew it was bad but did not know it was this bad. Having been in Zimbabwe around 90's when $1USD was 6-8 ZWD it definitely came very far. Asante mdau you made me want to know more about this so I went and google and I also found:

    By July 4th, 2008 at 5PM, a bottle of beer cost $100 billion Zimbabwean dollars, but an hour later, the price had gone up to $150 billion.

    ReplyDelete
  14. Today's exchange rate:
    8 US Dollar = 1,825,402 Zimbabwe Dollar
    Don't exaggerate things guys.
    Mdau Bantu Ahsante kwa kutupa ujumbe, lakini tupe habari sahihi basi sio kutia chumvi. Hali Zimbabwe ni mbaya lakini kuna tofauti kubwa kati ya milioni moja na milioni hamsini au mia tano!!!!!

    ReplyDelete
  15. Wataalam wa finance hivi kwanini wasipunguze hizo zero,s? Kama bei ya beer moja ni 150 billion ZWD utanunua nini na 100,000 ZWD.

    Lakini Anony Dec 13,2008 8:21am, kama $1=220,000 ZWD, bei ya beer ya Zimbabwe itakuwa 150 billion/220,000
    ambayo itakuwa equivalent to $680,000
    Nani huyo anayenunua hiyo beer?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...