mdau akipigwa pini na mgambo wa jiji kwa kupaki vibaya mtaa wa jamhuri, dar. nyuma kule ni mjengo wa kuegesha magari unaojengwa na nssf kusapoti shida ya kupaki jijini. nionavyo mimi wazee wa jiji waige mfano wa nssf kujenga maegesho kuondoa adha kama hiyo na pia kulazimisha kila mjengaji mpya aweke na sehemu ya maegesho. naomba kuwasilisha
mdau akipigwa pini na mgambo wa jiji kwa kupaki vibaya mtaa wa jamhuri, dar. nyuma kule ni mjengo wa kuegesha magari unaojengwa na nssf kusapoti shida ya kupaki jijini. nionavyo mimi wazee wa jiji waige mfano wa nssf kujenga maegesho kuondoa adha kama hiyo na pia kulazimisha kila mjengaji mpya aweke na sehemu ya maegesho. naomba kuwasilisha

Hii ni sawa kabisa, huwezi kuanza kupiga pini magari wakati unajua kabisa mjini hakuna parking za kutosha. Ni sawasawa na kumpa mtoto adhabu kwa sababu ya kwenda kubwa uani wakati wewe hujajenga choo. Ni wizi mtupu huu! Na hizi fedha wanazokusanya wanapelekaga wapi????
ReplyDeleteNamna hiyo ndo inatakiwa. Sasa hapo hata nikilipa hela sitakuwa na kinyongo kwa sababu mtu ka-invest hapo. Si huyu babu Kingunge na mgambo wake wanatuomba hela wakati magari yamepakiwa kwenye tope au mchanga tu. Mtaji wao ulikuwa ofisi pale Avalon na karatasi za ticket za kubandika kwenye magari tu. Lakini miaka nenda rudi wanakusanya mabilioni ya pesa lakini hakuna mabadiliko yoyote katika parking. Kweli bongo kuna ubabe jamani, sijawahi kuona nchi nyingine.
ReplyDeleteKweli kabisa misupu..badala ya wazee wa jiji kuhangaika na zabuni za jamaa wa kuweka pini kwenye ndinga zetu wangehangaika kutafuta wawekezaji na wabia kwenye ujenzi wa majengo ya kisasa ya kupaki magari! watu kama NHC, NSSF,PPF nk.wangeweza kutuondolea adha hii kama mfano unaoonekana dhahili kwenye picha...
ReplyDeleteHapo kiboko yaani kinachomsukuma mgambo kupiga pini hiyo ni ndoto ya Kaufisadi. Maana Kama gari imepaki vibaya yeye ndio anaisaidia isitoke hapo sasa kama jamaa akiamua asitoe kitu hao wengine watatokaje?? Yaani akili yake sijui iko wapi lengo lake si kuondoa kero bali anaizidisha mara mbili kwa kuhakikisha hilo gari haliondoki bali litaendelea kupaki vibaya.
ReplyDeleteAma kweli
Mzawa
Dah!! Hiyo safi sana Kaka. Maana jamaa kapigwa pini kwa kuwa kawazuia hao wengine. Sasa sina hakika kama huyo askari atakaa hapo mpaka dereva arejee ama la? Ama wataita Tow Truck (Breakdown) walipeleke kwenye yard yao ama la? Kama sivyo basi nadhani huyo askari atakuwa kaongeza matatizo maana hata dereva akirejea hatakuwa na namna ya kuwapisha hao waliopigwa pini.
ReplyDeleteKama ulivyoshauri, hao watu wa jiji wanawezesha kuwekeza kwenye sehemu za maegesho ili kuwapa watu nafasi ya kuchagua. Kwa hakika kuna sehemu unafika ambazo unakuwa hauna chaguo. Hakuna sehemu ya kupaki hivyo ni lazima umpige mtu pini hasa kama unaingia kuchukua kitu haraka haraka na kutoka.
Wakiwawezesha watu kuwa na sehemu za kuegesha naamini wataondoa wasiwasi wa usalama wa magari kwa wamiliki, vurugu za kukimbizana na wapigwa pini na pia watakusanya pesa nyingi na kirahisi tofauti na sasa.
Blessings
Jengo la TDFL pembeni ya barclays house ohio stree walikuwa na parking arcade yao, lakini sasa hivi wameibomoa na kuanza kushusha ghorofa jingine sijui nani alitoa kibali na baada ya jengo kuisha magari watapark wapi
ReplyDeleteminafkria kuanza kutembea na mkasi ule kukatia nondo sidhani kama utashindwa viminyororo vyao.maana sa zingine hawa jamaa wanafanya kukomoa vile raia,sijui watanishtaki kwa kipengele kipi?namimi sheria naijua(advocate) maana naona mjini ni uhuni tu!
ReplyDeleteSA NYINGINE KAMA JAMAA WANAMALIZIA HASIRA ZA MAISHA KWENYE GARI ZA WATU,HUYO JAMAA ALIVYOPAKI SIDHANI KAMA ANAKAA MUDA SEHEMU ALIYOENDA.LABDA DHARURA WATAJUAJE WASUBIRI KIDOGO HATA DK10.
ReplyDeleteTATIZO GAP YA MAISHA NCHINI KWETU NI KUBWA KWAHIYO WATEMBEA KWA MIGUU HUWA NA HASIRA SANA NA WENYE MAGARI,NAFKRI HAO JAMAA MARA NYINGI NI HIYO HASIRA YA MAISHA SA ZINGINE UTENDAJI WAO SIO SAHIHI!
ReplyDelete