Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi akiwa Ikulu ya Bujumbura na Miss East Africa, ClaudiaNiyonzima, mshindi wa tatu, Rahwa Ghebrehiwet na mshindi wa pili, AnneteMwakaguo ambaye anatoka Tanzania
Rais Nkurunzinza akiwa na Mkurungenzi wa Rena Events, Rena Callist(kushoto), Miss East Africa, Claudio Niyonzima (KULIA). Wengine kutokakushoto ni Serge Nkurunzinza, Annete Mwakaguo wa Tanzania ambaye nimshindi wa pili na Rahwa Ghebrehiwet wa Eritrea ambaye ni mshindi wa tatuRAIS wa Burundi, Mh. Pierre Nkurunziza amewaomba waandaji wa mashindano ya MissEast Africa kuyarudisha tena nchini Burundi hapo mwakani.
Akizungumza katika hafla aliyoiandaa Ikulu mjini Bujumbura jana, RaisNkurunzinza alisema serikali yake itatoa ushirikiano mkubwa kwa waandaji ambao ni kampuni Rena Events Limited ya Dar.
Alisema mashindano ya mwaka huu yaliyomalizika wiki iliyopita yalifanyikakwa mafanikio makubwa na amewapongeza waandaaji kwa kuyaandaa mashindanohayo kwa kiwango cha juu na kutangaza utamaduni na utalii wa nchi ya Burundi kwa kiasi kikubwa.
Rais Nkurunziza alikutana na Mkurugenzi wa Rena Events, Rena Callist, MissEast Africa 2008, Claudia Niyonzima, mshindi wa pili, Anette Mwakaguo waTanzania na mshindi wa tatu Rahwa Ghebrehiwet na mratibu wa Miss EastAfrica nchini Burundi, Serge Nkurunzinza.
Rais pia alimpongeza mrembo Claudia ambaye anatoka Burundi kwa kushindataji la Miss East Africa 2008.
Kwa upande wake Callist aliishukuru serikali ya Burundi kwa kuwezeshamashindano ya Miss East Africa 2008 kufanyika kwa ufanisi mkubwa.
Naye Miss East Africa 2008, Claudia alimweleza Rais Nkurunziza kwamba baada ya kushinda taji hilo, sasa ana wajibu mkubwa wa kutimiza lengo lamashindano hayo kwa kushiriki katika shughuli mbalimbali za ki jamii, nakwamba kwa mwaka huu lengo la mashindano hayo ni kusaidia watoto yatima nakuahidi kwamba atatimiza malengo yaliyokusudiwa.
Wakati huo huo, Miss East Africa imeandaa bahati nasibu itakayo chezeshwa katika nchi tanokuanzia mwezi ujao ili kusaidia watoto yatima, ambapo Rais Nkurunzizaameahidi kusaidia bahati nasibu hiyo na kuwaomba watu wote wa Afrika yaMashariki kuunga mkono bahati nasibu hiyo.



MUNGU IBARIKI BURUNDI.hiyo ni mwanzo tu
ReplyDeleteviongozi wa kiafrika siku hizi supa modo,supa travelar,supa man (wa kule zimb....)supa kroook,supa mafisadi...!
ReplyDeleteHuyu rais is mlokole huyu? Sasa na mambo ya urembo wapi na wapi!
ReplyDeleteKazi Nzuri Rena na Nkurunziza...hii imeipa Burundi sura mpy kuwa Imani itapatikana maana watu wengi walikuwa hawajui kama kuna weza kufanyika shindano kama hili.Harafu we Rais kama ni mrikore haijarishi yeye ni Raisi wa watu wote si Rais wa Warokore tu.Hata JK ni mwisramu ila hata Wakristo ni raisi wao.Acha ushamba
ReplyDelete