Mheshimiwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza na Ireland, Mama Mwanaidi Sinare Maajar, akitoa salam za Noeli na Mwaka Mpya
The Original Comedy, waalikwa wengine na Maofisa wa Ubalozi wakipata Msosi wa pamoja baada ya kupokea salam za Sikukuu ya Noeli na Mwaka mpya toka kwa Mh. Balozi Mwanaidi Sinare Maajar.

Ndugu Watanzania wenzangu,
Kwa mara nyingine tena tumepata fursa ya kufikia kipindi muhimu cha mwisho wa mwaka kwa kusherehekea kwa pamoja sikukuu ya Noeli na kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2009.

Kama ilivyo ada yetu, napenda kujumuika nanyi katika kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa nafasi hiyo.

Kwa niaba ya Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kwa niaba ya wafanyakazi wenzangu katika Ubalozi wa Tanzania London, na kwa niaba yangu binafsi napenda kuwatakia heri katika kipindi hiki muhimu.

Katika kipindi cha mwaka mmoja Watanzania waliopo Uingereza na Jamhuri ya Ireland wameshuhudia harakati zetu mbalimbali za kuhakikisha wanaimarisha ushirikiano kati yao. Pamoja na kasi ndogo katika harakati hizo, tumeshuhudia mafanikio yaliyotuwezesha kuanzishwa kwa Jumuiya za Watanzania sehemu mbalimbali, zikiwemo Birmingham na Edinburgh.

Huu ni mwanzo mzuri kuelekea kwenye ushirikiano thabiti wa Watanzania waliopo Ughaibuni (Diaspora). Aidha, mwaka 2008 umekuwa na mafanikio makubwa kwa kuweza kufanya Mkutano wa Diaspora hapo Mwezi Aprili.

Mkutano huo ulikuwa na mafanikio makubwa kwanza kwa kuweza kuwakutanisha zaidi ya Watanzania 400, wawakilishi wa kampuni zinazotoa ajira Tanzania na wawekezaji.

Ubalozi wenu unaendelea kufuatilia mapendekezo ya Mkutano huo na kwa kushirikiana na Tanzania Association (TA) tumeshaanza kufikiria kuandaa Mkutano mwingine wa Diaspora kwa kushirikisha washiriki wengi zaidi.

Tunaendelea pia kuwa na azma yenye imani kubwa ya kuwaunganisha Watanzania wote waliopo Ughabuni, si hapa Uingereza na Ireland tu, bali na Ulaya nzima na Amerika.

Tutafanikiwa endapo tutaendelea kuwa na mshikamano thabiti na ushirikiano wa kupigiwa mfano sisi wenyewe kwanza.

Natarajia mtaendelea kusherehekea pamoja fursa hii na kukumbushana kwamba Umoja ni nguvu na siku zote Tanzania itajengwa na Watanzania wenyewe.

Nawatakieni nyote Noeli njema na heri ya Mwaka Mpya.
Mungu Ibariki Afrika,
Mungu Ibariki Tanzania.

BALOZI MWANAIDI SINARE MAAJAR







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. api krisimasi andi api nyu iyaaa...rongu rivu mabeba boksi!

    ReplyDelete
  2. MBONA HATUALIKWA?ILIUWA SIRI?

    ReplyDelete
  3. hivi mabalozi wengine wako wapi

    ReplyDelete
  4. Joti Ukirudi Fala baki Ustue mitaa ya London hapo

    ReplyDelete
  5. Masanja umetoka ile mbaya.una maji ya nguo waswahili husema.Hongera origal komedi

    ReplyDelete
  6. Wajemeni, kumbe Joti mpole hivyo!!. Yaani amepozi kama vile siye.

    ReplyDelete
  7. Anon wa 10.31, ungehitajika hapo lazima ungekuwepo!

    ReplyDelete
  8. sio kila balozi lazima aweke kazi zake kwa balozi michuzi.wapo na wanafanya kazi. kuna lipi la ajabu mwanaidi kafanya?kula chakula pamoja?

    ReplyDelete
  9. anony december 27, 2008 11:07pm fafanua swali lako? yaani sababu hawajapiga picha na original komedi basi hawapo?

    ReplyDelete
  10. sina chuki na balozi mwanaidi anafanya kazi nzuri kama wengine. lakini nashangaa mdau hapo juu kusema kuwa mabalozini wengine wako wapi? ni kauli ya kizushi yenye majungu au kujipendekeza kwa balozi mwanaidi.siamini hata yeye kama atapendezewa na maoni ya huyu mtu juu kusema kuwa mabalozi wengine wako wapi?
    sio kila balozi ale na komedi. jeee hao comedy kama wakienda Brazil balozi wetu hatawakaribisha?
    Mwanaidi kaza buti wasikudanyanye hao wapambe njaa.ni wajibu wako kuwa karibu na watanzania wakati wakiwapo UK.sijui mwenzetu anaona nini special hapa kimetokea.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...