
MPAMBANO WA UCHAGUZI GHANA NI MKALI SANA, MZEE MZIMA MR. NANA ADADANKWA OKUFO-ADDO kutoka chama tawala NPP alikuwa na matumaini makubwa sana ya ushindi maana amewekeza pesa nyingi sana kwenye kampeni yake.
Alipigwa bumbuazi kiasi cha kuamua kufukuza baadhi ya wajumbe wa timu yake ya kampeni.. Jamaa alikuwa anafanya kampeni ya uhakika kwa kutumia magari ya Kisasa ya Kiamerica FORD 4x4 za Kisasa kabisa kama 20 au 25 na vifaa vya music na vipaza sauti babukubwa huku akimwaga pesa na vitu kama Baisikeli but matokeo yamemshangaza kila aliyeamini kuwa jamaa atashinda…
Jamaa wa upinzani chini ya J.J Rawlings Raisi wa zamani wa Ghana ambaye ni maarufu sana huko nyumbani TZ na chama chao cha NDC mgombea Urasi akiwa Prof John Attah Mills walipishana na chama tawala kwa kura takribani laki moja tu style yao ya kampeni ilikuwa nyumba kwa nyumba na mtazamo wao ni MABADILIKO kwa WAGHANA Wote ( CHANGE FOR ALL) na NPP wao wanasema TUSONGE MBELE (MOVING FORWARD) kama si tafsiri sahihi mtanisamehe.
Uchaguzi unarudiwa Tar 28 Dec na jamaa wako busy wakipigana vikumbo kuomba ushawishi wa vyama vidogo vidogo vilivyoshidwa kwenye uchanguzi wa mwanzo viwasupport.
Chama kimoja kidogo kimekubali kusupport NPP vingine bado viko kimya…Uchaguzi wa mwanzo ulimtaka mshindi awe na zaidi ya alimia 50 ya kura zilizopigwa, lakini haikuwa hivyo hivyo ngoma inarudiwa tena.
Nimewakubali waghana kwenye suala la uchaguzi na umakini hakuna longolongo kama za kwetu hapo na kila mtu anaitamani na anasisitizia umuhimu wa yeye kwenye kupiga kura.. kuna watu wamesafiri kurudi kwenye miji waliyokuwa wanaishi zamani umbali kama wa Dar to Tanga hivikwenda kupiga kura tu……..WABONGO TUPO????
Zaidi ya yote...
JANA ZAIN GHANA IMEZINDILIWA RASMI NA IMEINGIA KWENYE KUNDI LA ZAIN FAMILY
muda si mrefu itajichanganya kwenye ONE NETWORK mambo yatakuwa swaaafi maana wale wanaoni-dip ama wanaonipa missed call from home wataweza kunitwangia moja kwa moja kwa gharama za chini kabisa!
Mdau wa GLOBU HII YA JAMII TOKA GHANA
Mwandishi hii makala tupe contacts zako huko Ghana.
ReplyDeleteMr Moderator can we have contact of this contributor. Tunaomba e mail au simu yake tuwasiliane nae. I can be of help in our project.
ReplyDeletenapenda kusema kuwa blog hi imekuwa mawasiliano ya hrka haraka katika jamii ya kitanzani popote pale ilipo. Unaonaje ukitoa nafasi hata ya kuwatafuta ndugu na jamaa ambao wamepoteza mawasiliano na kufanikiwa kuyapa kupitia glob yako? Asante Dikson Shirima. diksonshirima@yahoo.it
ReplyDelete