Hi Bro.Michuzi,
NAOMBA MSAADA TUTANI.
Kwanza kabisa napenda kutoa salamu zangu za maandalizi ya x-mas na mwaka mpya, kwa wadau wote wa blog hii ya jamii.

Pili nina pikipiki yangu huko Dar-Tz napenda kuiuza, maana imekaa tuu mda mrefu bila kuitumia, kwasababu mda mrefu mimi nipo huku, pia wanandungu zangu wanaiogopa kuitumia maana ni kubwa wanavyosema.

Ni CC 600 SUZUKI. Ipo Dar es salaam na ina hali nzuri.
Mtu anayeishughulikia mawasiliano yake ni: 0754-838369.
Mimi huku unaweza kunipata kwa simu: +39/380-3115382.

Asante sana kwa msaada wako mkuu wa Wilaya ya Nanihii na Balozi wa Zain.

Salamu sana kwa wadau wote!

B.F.CHIBIRITI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. CHIBILITI UTAKUWA UMEFIRISIKA TU WEWE HIYO TRICK MBONA NIYA ZAMANI SANA BADO INAITUMIA? KWA NINI HUKWENDANAYO ITALY UNATAKA KUMBAMBIKIZIA MTU KANYA BOYA? UZIRI WA MKAKASI NDANI KIPANDE CHA MTI LOH!SUBIRI UKIRUDI UFANYE MIPANGO YA KWENDA NAYO ITALY, USIACHE CHEMBACHAO KWA MSAALA UPITAO, UNAWEZA KUITUMIA UKIRUDI NA MY WIFE WAKO. AMA WEWE NDIYO WALE ETI MIMI NYUMBANI NINA BAROONI KUMBE PIKIPIKI. HATUTAKI PIKIPIKI BWANA SEMA TUKUTUMIE HUKO ITALY UENDESHE KWANZA NASIKIA HUNA GARI HUKO UNADANDIA TRENI KILA KUKICHA

    ReplyDelete
  2. bei ujatoa mambo yako mkato au ndio kanya boya
    usa

    ReplyDelete
  3. Yaonekana hao hawako Bongo dsm. Pikipiki cc600 ni kubwa mno Bongo?

    ReplyDelete
  4. bad timing chibi yaani mtu kafa kwa piki. we ndo unaweka tangazo la biashara?achieni wachaga biashara

    ReplyDelete
  5. Sasa mbona hata hiyo namba ya mtu uliyemkabidhi auize HAIPATIKANI na kama vipi sema ipo wapi na weka bei yako na ni ya mwaka gani?? imelipiwa ushuru na kusajiliwa hapa TZ

    ReplyDelete
  6. we chib ulifia wapo mzee wa vituko leo unatujia na kali ya kibajaji cha. kwani ulikujanacho au umekinunua bongo? hii mpya

    ReplyDelete
  7. Mashine imetulia. Suzuki pikipiki nzuri sana. Japokuwa cc 500 ni pikipiki kubwa mno na inakimbia sana. Labda usiindeshe DSM otherwise daladala zinakugonga mara moja. Vinginevyo, kule machimboni Merelani, Arusha hiyo itanunuliwa mara moja na kwa bei inayolipa. Mwambie huyo jamaa ulimwachia hiyo mali aipeleke Arusha.
    Mdau

    ReplyDelete
  8. KWANINI USIIPELEKE KWENYE KILE KITUO CHA WATOTO YATIMA,AMBACHO NA WEWE ULISEMEKANA UPO HUMO.NAFIKIRI INGESAIDIA SANA KULIKO KUIUZA NA UNGEPATA THAWABU NYINGI TU!AHSANTENI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...