Hi Mzee Michuzi,
Twin Tawazzzz ziko tu kila mahali. Hizi nimezikuta huku Sudan.

Email kapuni.
Cheers,
Aggrey

awa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hii habari imetoka kwenye gazeti la mwananchi 18/12/08 inahusu ujanja na unafiki wa wakenya katika kutekeleza makubaliano ya soko la pamoja. Wadau hebu itupieni jicho

    Ubinafsi wahofiwa kuhatarisha Jumuiya ya Afrika Mashariki
    Na Salma Said, Zanzibar

    WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Diodorous Kamala amesema Jumuiya ya Afrika Mashariki iko hatarini kuvunjika iwapo nchi wanachama zitaendekeza unafiki na ubinafsi.


    Akifungua mkutano wa siku moja ulioandaliwa kwa ajili ya wananchi wa wilaya ya Mjini kwenye hoteli ya Bwawani mjini hapa, Dk. Kamala alisema kuwa tatizo la ujanja na ubinafsi linaloonekana kuota mizizi katika jumuiya hiyo, litaipeleka pabaya ikiwa hatua madhubuti hazitachukuliwa kulikomesha.


    Dk. Kamala alisema mambo ya ukabila kwa baadhi ya nchi wanachama hayana budi kutafutiwa dawa na kukomeshwa na akazitaka nchi wanachama wa jumuiya hiyo kutoendekeza ukabila na badala yake kujali umoja na mshikamano.


    “Hatuwezi kuendesha na kuwa na jumuiya imara wakati kuna mambo ya ubinafsi, ujanjaujanja na

    ukabila... tukiendelea namna hiyo tutaiuwa jumuiya yetu…. Nasisitiza kuwa kamwe Tanzania sio kikwazo cha kuundwa kwa soko la pamoja kama wanavyodai wenzetu,” alisema

    Dk. Kamala.


    Alisema kuwa tabia ilyoanza kujitokeza kwa baadhi ya nchi wanachama kuweka vikwazo vya kibiashara, ikiwemo kukataa bidhaa fulani kuingia katika nchi zao ni mambo yatakayosababisha kuyumba kwa jumuiya hiyo.


    Alitoa mfano wa nyama ya Tanzania inayopelekwa na wafanyabishara kutoka Sumbawanga kuwekewa vizingiti nchini Kenya, maziwa yanayozalishwa mjini Musoma pamoja na magari ya mizigo kukataliwa kufanya kazi katika moja ya nchi za jumuiya ni mambo ambayo hayaonyeshi nia njema katika ushirikiano huo.


    Jumuiya ya awali ilivunjika mwaka 1977 kutokana na kutoaminiana.


    Dk. kamala alisema kuwa kutokana na kutokuwepo kwa dhamira njema na ubinafsi wa nchi wanachama, baadhi wamediriki hata kudai nafasi za ajira kama za uhudumu, udereva na ulinzi

    kwa zile taasisi za jumuiya zinazokuwepo katika nchi mwanachama, jambo ambalo alisema

    ni kinyume na mkataba wa kuanzishwa kwa jumuiya ya Afrika Mashariki katika

    eneo la taasisi na makao makuu yake.


    Alisema walikubaliana katika nchi wanchama sukari kutoka nje ya Afrika Mashariki ilipiwe kodi ya silimia 100, lakini makubaliano hayo hayakufanya kazi na badala yake sukari hiyo imesheheni katika soko la nchi wanachama.


    Pia alisema kuwa Kenya inaagiza mchele kutoka Pakistan kwa silimia 75 na ilipotakiwa kucha, ikatoa hoja kuwa nayo inauza chai kwa nchi hiyo hivyo itakuwa vigumu kukataa mchele wao na iliomba muda wa kutafuta soko jingine la chai lakini hadi sasa hakuna kinachoendelea.


    Hivyo alsiema kuwa ikiwa umoja wa forodha ambao ndio msingi wa soko la pamoja umeshindwa kutekelezwa kwa asilimia 100, uwezekano wa kuyumba kwa jumuiya hiyo ni mkubwa hasa ikitiliwa maanani kuwa sehemu kubwa ya utekelezaji wa makubaliano unafanywa na Tanzania wakati nchi nyingine zikisuasua.

    ReplyDelete
  2. Braza Misu, Hii habari ni muhimu sana. Hebu iweke ukurasa wa mbele wa blogi wadau wachangie

    ReplyDelete
  3. MTOA MAONI WA KWANZA SIJAMUELEWA HIYO KOMENTI YAKE NAONA KAMA HAIENDANI NA PICHA YA TWINI TAWAZZZZ

    ReplyDelete
  4. Hii inaonyesha hali halisi ya nyumba nyingi za waa-Africa zilivyo hasa vijijini.
    Ahsante brother Misupu kwa kutuhabarisha
    Mdau

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...