Brother Michuzi,

Kwanza tunakupongeza kwa kazi nzuri ya kufanya mawasiliano ya watanzania kwenye mitandao yawe rahisi kupitia blog yako. Na pia kutuhabarisha mambo mbali mbali ya nchini kwetu kwa njia ya taarifa na picha.

Sisi ni watanzania waishio jimbo la California katika eneo la Bay area (Oakland, San Francisco, Sacramento, San Jose na kadharika) Tunapenda kuwafahamisha watanzania wengine ambao wangependa kuungana na sisi mnamo tarehe 13 December mwaka huu kusheherekea sikukuu ya Uhuru wa Tanzania.
Tunafanya hivi kila mwaka. Tuna umoja wetu ulioimarika chini ya uongozi mashuhuri. Jina la Jumuiya yetu ni Tanzania Community Organization (TCO). Website yetu ni www.uzalendo.org. Mnakaribishwa kutembelea website na kuona shughuli zetu.

Siku ya sherehe hizi tutakuwa pia na mgeni wetu Mheshimiwa Balozi Sifueni atakuwa mgeni rasmi. Hii ni mara ya kwanza kujitambulisha kwenye blog yako, na ni heshima kubwa kwani sio siri, kupitia hapa tutakuwa tumejitangaza zaidi.

Ticket katika sherehe zetu hizi ni $45, na ni kila mtu anakaribishwa mwenye uwezo wa kuwepo tarehe hiyo. Sherehe zitafanyika mjini Oakland. Tunawakaribisha watanzania wote waishio USA na nje ya USA ambao wangependa kutuuga mkono.

Kama nilivyoeleza awali, website ina maelezo yote ya Jumuiya pamoja na njia za mawasiliano jinsi ya kutupata.

Erick Byorwango
Katibu Msaidizi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. nasikia huko california kuna majungu.wewe bwana eric mbona kwenye L unaweka R?halafu hiyo web yenu imekaa kishamba,animation za nini sasa well,hata kithungu ni kibovu.wachovu!

    ReplyDelete
  2. kama umekaribishwa nenda kama hutaki dont go usitafute sababu... why are you wary of Majungu if you are not the one making them....If you cant make it then do not come up with stupid excuse..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...