Zaidi ya Vyuo Vikuu 100 Kushiriki
Nairobi, 1st December 2009.

Zaidi ya Vyuo Vikuu 100 vitawania maelefu ya Dola za Marekani katika mchuano wa msimu wa tatu wa Zain Africa Challenge (ZAC) unaotarajia kuanza mapema mwaka ujao.

Mchuano wa Zain Africa Challenge ndio mchuano pekee unaoonyeshwa kupitia Luninga unaokutanisha Vyuo Vikuu mbalimbali Barani Afrika. Mchuano huu umepanuka na unashirikisha Mataifa mengine mapya ambayo yameongezeka katika mchuano nayo ni Ghana, Nigeria, na Sierra Leonne na yatakuwa ya kwanza ya aina yake kuonyeshwa na Luninga Barani Afrika.

Katika msimu wa pili wa mchuano mwaka jana, Vyuo Vikuu vilivyokuwa vinashiriki vilikuwa vinatoka Tanzania, Kenya, Uganda, Malawi na Zambia.
Akitangaza programu ya msimu wa tatu ya mchuano huu, Ofisa Biashara Mkuu wa Zain Group, Tito Alai, alisema, ‘’ ZAC ni uthibitisho dhahiri wa nia yetu ya kuwaendeleza vijana ambao ndio hazina kubwa ya Afrika.
Mchuano huu sio tu unahusisha kushinda tuzo. Sisi hapa Zain tunawapa vijana fursa ya kujenda mitandao ambayo wataishi nayo milele. Na haya ndio mambo ya ulimwengu maridhawa wa Zain,’’

Zain Africa Challenge ni sehemu ya Programu ya Zain ya Ustawi ya Jamii inayoweka mkazo kwenye elimu.

Msimu huu wa tatu wa mchuano wa nchi zitakazoshiriki ZAC utaanza Januari 15, 2009 na kumalizika January 22, 2009. Mchuano wa nchi na nchi unalenga kuhakiki uwezo wa washiriki katika kuwakilisha vyuo vyao. Na nchi zao. John Sibi Okumu, anayefahamika kama Mwalimu ndiye ataendesha mchuano huo utakaoanza kuonyeshwa kwenye Luninga Afrika mwezi Machi.

Mambo Makuu msimu wa tatu wa ZAC ni pamoja na:
Vyuu Vikuu nchini Ghana, Nigeria na Sierra Leone vitaungana na vile vya Kenya, Malawi, Tanzania, Uganda na Zambia. Zaidi ya Vyuo Vikuu 100 vitashiriki katika mchuano kutoka nchi nane.

Kila nchi itakuwa na michuano ya kufusu kushiriki katika mchuano.
Timu 32 zitakazoongeza kitaifa zitasogea katika mchuano wa kimataifa Mjini Kampala, Uganda February 2009.

Vipindi 31 kutoka katika mchuano wa kimataifa utarushwa kenye luninga nchini Ghana, Kenya, Malawi, Nigeria, Sierra Leone, Tanzania, Uganda na Zambia.

Maswali yatakayoulizwa katika programu hii ya mchuano wa maswali ya haraka haraka yatagusa maeneo mbali mbali ikiwa ni pamoja na ; historia. Sayansi, Utamaduni wa Afrikan, geografia, fasihi, muziki na matukio ya wakati huo.
Kadhalika Zain Africa Challenge huonyesha fursa za elimu zinazopatikana katika vyuo husika pamoja na wasifu wa wanafunzi Barasa la Vyuo Vikuu la Kimataifa ni wabia katika programu hii.

Zain Africa Challenge inarushwa kama mchuano wa mtindo wa mtoano hadi kupatikana kwa bingwa. Vyuo vyote vinavyoshiriki na wanafunzi hupata tuzo kulingana na nafasi waliyopata.
Mwisho
For more inquiries contact
Beatrice Singano Mallya
0784 670 277
OR
Leticia Kaijage
0786 377847

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Mwaka huu nilipoteza network kabla mashindano hayajaisha. Naomba msaada kujua, Nani alikuwa mshindi? na Tz chuo gani kilifanya vuzri zaidi?

    ReplyDelete
  2. Ushauri kwa Vyuo toka Bongo, Uchaguzi wa wakilishi uwe na uwiano sawa wa masomo yaani sayansi, Art, Biashara N.K Pia wasisahau akina dada, huwa wapo fast san kuvuta kumbu kumbu. Upendeleo wa uchaguzi wa wawakilishi hutuua. Pia wakali wa darasani hutuangusha kwenye maswali yanyohusu Soka, Mbio, sinema, Literature (hadithi) kwani wao huwa hawajihusishi na dunia nyingine zaidi ya vitabu tu

    ReplyDelete
  3. Safi sana. Haya ndio mambo tunataka kuona yakipewa kipaumbele. Tumechoka publicity za miss Tanzania, miss ustakencheke, bongo star search, malkia wa sebene etc. Academic excellence has to be top priority. Kazi kwenu wana vyuo wa Bongo, jifueni kisawa....

    ReplyDelete
  4. Na waliogoma na kufanya fujo wamo?

    ReplyDelete
  5. Ukiangalia mashindano haya utagundua kuwa Watanzania hatuna exposure yakutosha. Hatusomi vitabu wala kutaka dunia inaendaje kwa upande wa kijamii,kihistoria, kisiasa najua tuko fiti. Ni kweli kama alivyosema mwenzetu hatuangalii mbali zaidi ya upeo wa macho yetu, na wenye akili sana mambo ya duniani(anasa na burudani) wao ni zero kabisa labda simba na yanga kwa hivyo kwa vijana ni changamoto tuamke tusome na yasiyo husu shule, safari hii tena kuna wanigeria itakuwa ni mpambano wa kuvutia sana Big up Zain kweli tumechoshwa na Umiss kindeki kila siku

    ReplyDelete
  6. KAMA TUNAVYOGOMEA EAC NA HILI NALO TUGOMEE, KWANINI SISI TU KILA MWAKA HATUSHINDI WAKATI SISI WATANZANIA TUNAVIPAJI TULIVYOPEWA NA MWENYEZI MUNGU? TUSIKUBALI, HAO WAJANJA WANATAKA WATUCHEKE KILA MWAKA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...