Mratibu wa Maendeleo ya Biashara wa Zain Tanzania, Bryson Brighton (katikati) akikabidhi zawadi ya simu kwa Shecaly Shakiff aliyeshinda promosheni ya Sikia Kengele inayoendeshwa na Zain kwa kushirikiana na Tanzania Marketing and Communication (T-Marc), Dar leo. Zain ilitoa simu selula kwa washindi wanne. Kulia ni Ofisa Uhusiano wa Zain Tanzania, Celine Njuju.

Tanzania Marketing and Communication (T-Marc), Nelson Karanja (katikati) akikabidhi zawadi ya simu kwa Haji Mtulia aliyeshinda promosheni ya Sikia Kengele inayoendeshwa na Zain kwa kushirikiana na T-Marc, Dar leo. Kulia ni Ofisa Uhusiano wa Zain Tanzania, Celine Njuju.


Mtendaji wa Masoko wa Zain Tanzania, Maria Kimario (katikati) akikabidhi zawadi ya simu kwa Subira Chambuya aliyepokea kwa niaba ya Ombeni Nakolikonga aliyeshinda promosheni ya Sikia Kengele inayoendeshwa na Zain kwa kushirikiana na T-Marc, Dar leo




Mkurugenzi wa kampuni ya pikipiki ya Kazzar Ltd, Simbo Mushi akikabidhi ufunguo wa pikipiki aina ya Zongshen kwa Pius Gasper aliyeshinda promosheni ya Sikia Kengele

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Duh! kazi ipo jamani. Kuna mwafrika aliyezaliwa Afrika na anaitwa "Bryson Brighton"???!!!

    ReplyDelete
  2. lil mama in ze pink pink got some **s her.She fine though but I ma put rubberband on her.

    ReplyDelete
  3. CHUNVI CHUNVI,HAYA MZEE MKURUGENZI WA MAPIKIPIKI,
    NI MIMI KAMANDA WA VICHUPUKIZI..DOES IT CLICK? IFM MAN

    ReplyDelete
  4. Celine ana mipaja mweee!!

    Mdau,

    Boston, US

    ReplyDelete
  5. Huyo anayeng'ang'ania majina kuwa lazima yachanganywe na ya kikwao amepitwa na wakati...siku zote tumeshuhudia majina kama Daniel Yona...jina la kikwao liko wapi? Edward Hosea? Ramadhan Hussein, Abdul Baraka, Ali Hassan...haya ndiyo majina tunayohitaji kwani hizi siyo enzi za ukabila yaani mtu anasoma jina lako la ukoo kama linafanana na la kwake ndiyo linakuwa kwenye short list....
    Muda wa NIC kujaa majina ya Mwakasungura, Mwampamba, Mwandosya yameshapitwa na wakati.....huu siyo ule wakati wa akina Mwaikambo na na akina Nsekela. That ia gone!!!

    Watu waitwe wanavyotaka na hili litatusaidia kupunguza ujinga wa makabila, siyo lazima uitwe Kilontsi Mpologomyi ndo ujulikane unatoka Kigoma...unaweza pia ukawa Aman Warid Kabour na ukatokea Kigoma huko huko....siyo lazima uitwe Gerald Msangi ili ujulikane unatoka Upaleni...unaweza kuitwa Daniel Yona na ukatokea huko huko....siyo lazima uitwe Rugumyamheto ili ujulikane unatoka Ngala...unaweza kuitwa Idris Abdallah ukatokea huko huko, hivyo sioni sababu ya kushangaa Bryson Briton..it's his choice na hilo halimpunguzii uzalendo...kwani muhidini Issa Michuzi ni majina ya wapi!!! unataka Kikwete atamulazimisha Issa michuzi naye aitwe Jakaya iliwaonekane wote wanatokea Bagamoyo...siyo hivyo.

    Ndugu yangu unayechallenge majina siyo tu kama umeitwa na wakati bali unaatamia ukabila.

    Pole sana dunia hii utabaki mwenyewe...we're part of something bigger now.

    ReplyDelete
  6. Asante sana anony wa Desemba 13, 3:54 PM.
    Kuvamia majina ya watu ni dalili ya kujichukia, kujikataa na kutokujiamini. Na ukijikataa wewe mwenyewe basi hakuna atakayekukubali. Mataifa yenye nguvu Duniani hayatumii majina yasiyokuwa ya kwao na hawana matatizo hayo ya ukabila uliyoyazungumzia.

    Udhaifu wa mwafrika. Mwafrika ni mtu dhaifu kiasi kwamba haamini tena kama anaweza kusimama kama mwafrika na akahesabiwa kama mwanadamu. Udhaifu huu unamfanya ajipendekeze na kujipachika kwa "bwana" ambaye anadhania atampenda na kumtunza. Hii inamfanya aendelee kuwa dhaifu na mfuasi wa kudumu wa bwana wake. Kauli yako ya "we are part of something bigger now" inajieleza yenyewe.

    Kama huu ni ukweli,"we're part of something bigger now"
    kwanini ni waafrika peke yake ndiyo wanaovamia majina ya watu wengine?
    Unawajua wazungu wangapi au waarabu wangapi wanaoitwa majina kama Chamkaga Butele au Ndyanao Mokiwa au Sizwe Ofyang? Kwanini wazungu au waarabu hawaitwi Virendra Singh au Ranjeeta Kapur Khan? Are they not a part of the same something bigger?

    Kwanini wahindi na wachina siyo "part of something bigger now" na wanaendelea kutumia majina yao na wanatambulika kwa majina yao?

    Sitaki kuandika sana, ingawa kama unataka somo zaidi niandikie wanzalambongo@yahoo.com

    ReplyDelete
  7. safi wanzala nimependa kazi yako ahsante ubarikiwe!mkiwa 100 tu basi afrika itakuwa kitu kingin.

    ReplyDelete
  8. jina ni jina tu,,ila la asili lina maana saaaaana tu
    afu wee annon unayekashifu majina ya wanyakyusa na kigoma @@##~**">//,,zako sana wewe,utashushwa naniiii sasa ivi!!
    michu wee ndugu wa kikwete kumbe?dah sirikali imejaa wazaramo,wandengereko,wanakwerekwe nk nk watupu hahahaaaa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...