bosi wa kampuni ya air tanzania (atc) david mattaka ana kila sababu ya kufurahi kwani hatimaye shirika lake hilo la ndege limeanza tena safari rasmi baada ya kuzuiwa kurusha ndege zake kwa sababu za kiusalama. serikali imeipiga jeki atc kifedha na hivi sasa mambo mswano na safari za ndani za atc zimeanza rasmi leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hii Serikali yetu hapa nafikiri haijui inafanya nini.
    Waingereza wanasema, "Throwing Good money after Bad"

    Tunaelewa lengo la JMK kwamba nchi yetu iwe na shirika la Ndege kama Kenya na nafikiri ni nia yetu wote watanzania haswa ambao tuko nje. Na pia tunajua jinsi Shirika la ndege linaposaidia kuitangaza nchi na kusaidia utalii, na kurahisisha usafiri.

    Sasa hili swala la kutoa hela halafu uulize maswali baadae ni hasara kubwa kwa Taifa.

    Ili kampuni ifanikiwe inahitaji vitu vitatu vya msingi: Uongozi bora(Competent management), Mpango wa biashara(Viable Business Plan), na Mkakati sahihi( The Right Business Model).

    Sasa Serikali inamwaga tu hela bila kuyahakiki yote haya ikumbukwe hizi hela ni zetu na hivyo serikali haina budi itueleze wazi hii hela itarudishwa vipi.

    Katika hayo nilalifahamu kwa uhakika ni swala la uongozi bora ambalo ATCL halina.
    Wakati Bw Mataka mimi binafsi naamini alifanya Kazi nzuri pale PPF lakini muda ambao amekuwa nje ya kazi inanitia wasiwasi mkubwa.

    Mwenyekiti wa Boki ndio Kabisa hafai. Tukumbuke katika Serikali Ya Mwinyi Bwana Nyanganyi akiwa Waziri alisimamia ununuzi wa kivuko kile kilichoitwa UNIFLOTE ambacho kilikufa kabla hakijafanya kazi na matokeo yake maisha ya watu yalipotea pale kigamboni kwa kukosa usafiri.
    Pili hajawahi kusimamia kampuni yeyote kwa mafanikio sasa sijui ni sifa gani alizonazo kuendesha shirika hili sielewi. Au ndio wale Wateule??

    Business Plan na Business Model nina imani haipo maana serikali wamesema kuwa wametoa hii hela kwa imani halafu wakateua kamati ya kuchunguza. Wakimaliza kuchunguza hela itakuwa imeshaisha hivyo watataka nyingine.

    Mustapha Nyang'anyi alisema shirika linahitaji Tzs92bn ili liweze kuamka sasa wamepewa Tzs2bn baada ya kunywa tzs2.5bn.
    Hii ni sawa na serikali imechukua hela na kuitumbukiza shimoni.

    Mimi naona kabisa nia njema ya JMK kulinusuru shirika inatumiwa na wajanja kutapanya hela ya Serikali.

    Muda huu shirika liliposimama ungetumiwa kuifanyia marekebisho(restructuring) makubwa ATCL. Kuhakikisha ina professional management, Kuweka mtu anaeijua biashara ya ndege ya sasa awe Chairman na sio Nyang'anyi, Kuangalia uwezo wa wafanyakazi, Kuisafisha Balance Sheet, Kuhakikisha ina business Plan iliyohakikiwa na wataalamu wa mahesabu, na pia kuingalia upya business model yake kama bado inafaa kwa wakati huu(Mimi naamini haifai).

    Hii ni kampuni haina sababu yeyote kuundiwa kamati kuchunguza.
    It is a business company which needs a business solution not a political one.

    Kama Serikali ya Italy imekuwa na nia ya Kuikwamua Alitalia kwa malengo kama haya ya JMK lakini mwishowe iliridhia kwa kuwa ni business company the solution has to be business based.

    Kufanya kazi kwa imani ni kujihakikishia hasara.

    The market is very harsh and that is my only wish that our government should better realise that as soon as possible.

    Mungu Mbariki JMK,
    Mungu Ibariki Tanzania,
    Mungu iokoe Tanzania kutoka jamvi la wezi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...