"Hasira za Wapemba kwa CCM Zinatokana na Kufeli kwa Chama Cha Mapinduzi"
Wapendwa Wanahabari,
Kufuatia ziara yake ya hivi majuzi kisiwani Pemba, Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mhe. Jakaya Kikwete, amenukuliwa akiwaambia Watanzania wa kisiwa cha Pemba kwamba huenda upinzani usiingie kabisa madarakani, na kwa hivyo ni vyema wakashirikiana na Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho ndicho kilichopo sasa madarakani.
Licha ya kuwa kauli hii ni ya kisiasa ambayo inaweza kutafsiriwa kwa muelekeo huo tu – kwani huyu ni mwenyekiti wa CCM ambaye kwa vyovyote asingetarajiwa kukitabiria chama chake kuondoka madarakani au kukiri kwamba kuna chama chengine ambacho kinaweza kuchukua nafasi ya CCM – sisi Kurugenzi ya Haki za Binaadamu na Mahusiano ya Umma ya The Civic United Front (CUF – Chama cha Wananchi) tunaona kuwa kuna haja ya kuitolea ufafanuzi.
Kwanza, kumekuwa na tabia ya viongozi wa ngazi za juu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuyatafsiri matatizo ya kisiwa cha Pemba kisiasa tu bila ya kuzingatia hali halisi ya kiuchumi ambayo wananchi wa kisiwa hicho wamekuwa wakipambana nayo.
CUF tunaposema kwamba hali ya maisha ni ngumu, ni kwa kuwa serikali zilizopo madarakani zimekisusa kisiwa cha Pemba na kukitenga kabisa kimaendeleo.
Serikali hizi, ambao zinaongozwa na CCM, zimekuwa zikifanya hivyo kama ni njia ya kuwakomoa wakaazi wa kisiwa hicho ambao tangu kuanzishwa tena kwa mfumo wa vyama vingi, mwaka 1992, wamekuwa wakionesha wazi msimamo wao wa kuipinga CCM.
Kwa hivyo, wakaazi wa Pemba wataendelea kuzipinga serikali zilizopo si kwa sababu ya chuki wala fitina, bali kwa sababu serikali hizo zimeshindwa kukidhi (have failed to deliver) matashi yao.
Pili, kwa kuwa Rais Kikwete na wenzake wanajuwa hasira walizonazo wakaazi wa kisiwa cha Pemba dhidi ya serikai hizi zilizoshindwa kuinua hali ya maisha ya mkaazi wa kisiwa hicho – kama vile pia zilivyoshindwa kwa wengine – basi wanatafuta kisingizio cha kuzielezea hasira hizo, kwamba eti ni viongozi wa vyama vya upinzani.
Huko ni kuwadhalilisha wananchi hao kwa kuwaona kama kwamba wenyewe hawana uwezo wa kuchanganua na kufahamu hasa lilipo tatizo lao, ambalo ni serikali za CCM zilizofeli, mpaka wachanganuliwe na viongozi wa upinzani. Hasira za wananchi wa Pemba ni muakisiko wa kufeli kwa CCM, na si chenginecho.
Tatu, ni vibaya kwa Rais Kikwete kutumia uzinduzi wa miradi ya maendeleo kuwasimanga wananchi wa kisiwa cha Pemba, kwani kwanza miradi hiyo inajengwa kwa kodi zao au kwa misaada ya wahisani ambayo huko ilikotolewa ilitolewa kwa ajili ya wananchi hao, na si kinyume chake.
Kama alivyosema mwenyewe, Serikali kujenga miundombinu ni jukumu lake na wala Rais Kikwete asijenge picha kwamba anawafanyia hisani wananchi wa huko; na hivyo akapata sababu ya kuwasimanga.
Mwisho, ikiwa kweli Rais Kikwete ana dhamira ya kuisaidia Zanzibar kuondokana na ule aliouita ‘Mpasuko wa Kisiasa’ anapaswa kuliangalia suala hili kwa uadilifu. Kuendelea kwake kupiga mifano ya watu ‘waliogomewa’ kupata huduma za kijamii kutoka kwa wenzao lakini asigusie kabisa sababu halisi zilizopelekea hao waliogomea kugomea, ni kuwabagua watu na ni kuendeleza mpasuko.
Tunakusudia kusema, ikiwa Rais Kikwete anaongelea kisa cha mwanachama wa CCM kususiwa biashara yake na wana-CUF, kwa mfano, basi pia na azungumzie kuwa mwana-CCM huyo aliyesusiwa ndiye aliyeshiriki kuwabaka watoto wa wana – CUF, kuiba mali zao na kuwaletea makundi ya Janjaweed kuwavunjia nyumba zao. Je, Rais Kikwete yuko tayari kuueleza ukweli huu pia?
Imetolewa na
Salim Bimani
Naibu Mkurugenzi,
Directorate of Human Rights and Public Relations
The Civic United Front (CUF)
Party Headquarters
P.O. Box 3637
Zanzibar
Tanzania
Tel. (+)255 (0)777 414 100 / (+)255 (0)777 414 112
Website: http://cuf.or.tz

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. we vipi?uctuwekee siasa humu!!!ahh

    ReplyDelete
  2. Hawa CUF hawana jipya JK kawapa ukweli wanabaki kupiga rojorojo..hhovyoooooooooooooo cuf.

    ReplyDelete
  3. huyu atakuwa us blogger tu..

    tafadhali usituchafulie tena hali ya hewa humu ndani....

    aisee km kuchafua hali ya hewa,ulichafua bwana mdogo...bonge la USHUZIIIIIIIIIIIIIIII!pakawa hapakaliki humu ndani...!sijui ulikula cheuro???mweeeeeh...

    tafadhali usije tena na siasa zako hatutakiiiiiii....

    ReplyDelete
  4. ndio mtindo wa utawala wa zama hizi. ukipinga ccm, serikali yake inakukomoa. ndivyo ilivyo kwa majimbo yote ambapo ccm imeshindwa. hata wanafunzi wa vyuo vikuu wanapodai haki yao wanawekwa kwenye kapu la upinzani na dawa yao kukomolewa. si mnaona watoto wa maskini walivyokataliwa kudahiliwa upya! walipinga sera za serikali ya ccm. serikali inapokuwa na mwelekeo wa kukomoa ni hatari tupu!! Wachangiaji wa kwanza watatu ninafikiri hamjui maana ya blogu. blogu si kuzungumzia tu kandanda, udaku na burudani. Ni uwanja wa kuburudishana na kubadilishana maoni juu ya masuala ya kijamii, burudani, siasa, elimu, udaku, nk.

    ReplyDelete
  5. Tamshi ya kurugenzi mbona imejaa contradictions tupu! Mara Pemba imesusiwa kimaendeleo mara inalaani Rais Kikwete hivi karibuni kutumia kisiasa fursa ya kuzindua miradi ya maendeleo huko Pemba! Mara Wapemba wanapinga Serikali za CCM kwa kushindwa kukidhi matarajio yao kama walivyoshindwa kwingine nchini!!Kikinzana huku kunatisha na kunadhihirisha kwanini this party - CUF - needs not only better leaders but better thinkers!

    ReplyDelete
  6. We mwana CUF he3bu acha hizo!!Mbona Karatu vipindi viwili iko na mbunge na halmashauri chini ya CHADEMA lakini hawana tabia zenu za kipemba za kuzira na kufanyiana hila la CCM. Siasa kule za kistaarabu kabisa. Lakini nyie mna nongwa sana. Alichowapasha JK size yenu haaswaa!!

    ReplyDelete
  7. Hoja ya Pemba kuwa na upinzani haina msingi kabisa. Kwani Pemba tu ndipo kuna upinzani dhidi ya CCM? Tarime, Karatu, Kigoma nk utasemaje? Fikiri zaidi!Acha uvivu wa kufikiri!

    ReplyDelete
  8. Ni aibu kubwa sana na fedheha kwa kiongozi wa ngazi ya juu, au kiongozi wa serikali kutoa kauli chafu kama aliyoitoa Mh. Rais Kikwete. Ni kauli inayoashiria kudumaza na kudumaa kwa demokrasia, lakini pia ukosefu na unyonge mkubwa kidiplomasia kwenye usuluhishi wa tatizo la kisiasa Zanzibar.

    Mimi kama mtanzania ninaeijua nchi yangu vema, ninayetambua mipaka ya kauli na ninaejali demokrasia nathubutu kusema Mh. Rais afute kauli yake au aweke mambo sawa kwamba alimaanisha nini maana amepalilia chuki. Zanzibar sio sawa na bara kwa sababu upinzani ni mkubwa, kiasi cha kuamini ulihujumiwa maika ya nyuma.

    Ni kauli inayokatisha tamaa, na ni doa kwake binafsi na kwa serikali anayoingoza. Ni doa kubwa kimataifa, na kwa vvyovote imechafua taswira ya nchi kimataifa hasa kwa wale wanaofuatilia masuala ya muungano.

    Niliposikia jambo hili sikuamini kama ni Kikwete ninayemuheshimu sana kwenye medeni hii ndiye ametamka hayo. Nathubutu kumtaka aombe radhi, au afafanue zaidi.

    Kikwete ameongeza mpasuko Zanzibar

    Edward
    DSM

    ReplyDelete
  9. TATIZO KUBWA LA WATANZANIA WALIO WENGI, WAKIWAMO VIONGOZI WA NGAZI ZA JUU HAWAJUI MAANA YA DEMOKRASIA. Ukiwauliza walio wenge watesema demokrasia ni uchanguzi huru na wa haki.

    Kadhalika, watanzania hao hao hawajui mwanadiplomasia anatakiwa awe vipi, na kauli zake ziweje, hawajui. So sad! Kauli ya Kikwete ilipaswa iza maandamano kote bara na visiwani. Ni kauli ya kulaaniwa hiyo!!! It should not be from a diplomatic person like Kikwete, hakika. I'm really sorry because I like the way he solves political problems, but in this last approach amezidi kumomonyoa demokrasia na kuongeza mpasuko Zanzibar. Inatisha sana. Sijui alilewa nini huyu bwana mkubwa.

    ReplyDelete
  10. CUF wasipobadilika haraka, basi safari yao huko mbele ni ngumu kuliko walikotoka.
    Kawaida kila jambo la kimaamuzi ni vema likawa na mpango mbadala (Plan B) sasa kwa hawa jamaa CUF inaonekana hakuna kitu kama hicho. Na hiiyote inachangiwa na mawazo finyu ya mtu mmoja tu nina uhakika huyo mtu akijiweka pembeni mambo mengi ndani ya CUF yatabadilika na kukiimarisha chama hicho.
    Alichowaambia Kikwete siyo jambo jipya, na kwa muelekeo huu walionao CUF ana haki ya kuwaambia ukweli ili muamke na kutafakari.

    ReplyDelete
  11. UGUMU WA MAISHA NA UMASIKINI SI PEMBA TU NI TANZANIA NZIMA, HIVI NYIE MMESHAENDA MIKOA YA KUSINI YA LINDI MTWARA MKAONA WATU WANAVYOPATA SHIDA, NENDENI NEWALA HATA MAJI YA KUNYWA NI SHIDA, YAANI BALAA TUPU HAPA HAPA DUNIANI WANAADHIBIWA NA HATA WAKIFA MUNGU AWAONEE HURUMA AWAPELEKE PEPONI NA KUWASAMEHE MADHAMBI YAO, SEREIKALI NATAKIWA KUTAZAMA NCHI NZIMA SI DAR ES SALAAM PEKEE YAKE HASWA OSTERBAY TU WAKATI KODI ZINALIPWA NA WATANZANIA WOTE WAKIWEMO WA NEWALA.

    ReplyDelete
  12. WAPEMBA WATU WANAOPENDA MANENO,WAVIVU ITAENDLEAJE PEMBE WAKATI HAO HAO WAPEMBA WANAONA WAO KUWA MAENDELEO MAKUBWA NI KUWEKEZA ILALA,KARIAKOO,MWANZA NA TANGA LAKINI HAWATAKI KUWEKEZA KWAO,HAPO HAPO WANAPIGA KELEL KILA SIKU PEMBA IPO NYUMA HAIDHAMINIWI WAMEZIDI MANNO HAWA HAWANA JIPYA,WAAMBIWE UKWELI MSHUKURU HUU MUUNGANO VINGINEVYO WENYEWE WANGELIKUWA WANAPINDUANA KILA SIKU KAMA COMORO...........Isma Kabengo-kampala,UG

    ReplyDelete
  13. nyie wabongo vp!, mnajua hali ya uko pemba au mnasikiliza habari za ccm na kuamini, siasa ya zanzibar na bara tafauti ilo lazima mlijue, znz wapinzani wengi kuliko wafuasi wa ccm, mwaka 1995 ccm wameshindwa na hawajataka kuitoa serikali, baada ya hapo wakaamua kupiga watu na kuwafunga kila ifikapo wakati wa uchaguzi, na kuchukua watoto wa wanaccm kuwafanya askari ili ikifika wakati wa uchaguzi wapige kura ishirini ishirini, hakuna hata mara moja uchaguzi wa znz ukawa huru na haki, ikifika wakati wa uchaguzi watu wa maeneo ya cuf wanapigwa kwa makusudi kwa kutumia maaskari na vikundi vya ccm vinavyojulikana km janjawiri, na sio pemba tu bali hata unguja sehemu za wanacuf, labda bara hakuna kitu km hichi ndo mana hamuelewi, so tafuteni habari mujue si mnakaa na kupiga zogo tu, 2001 wapemba wameuliwa km kuku na jeshi kutoka bara, na wengine wamewaona dada zao na mama zao na wake zao wanabakwa, kisa nini ni wapinzani, jee hayo yamefanyika bara?, wakisema mnasema oo wananongwa sijui wanahichi,km vp ccm iondoe vyama vingi n sote tuwe ccm, coz ukiwa mpinzani ushakua adui wa serikali, uchumi wa znz unategemea pemba kwa kiasi kikubwa tu, na bado huko pemba hakushuhulikiwi, ni serikali ndo ina wajibu wa kushuhulikia pahala na sio wananchi, wananchi wanachotakiwa ni kufuata mpango wa serikali. na hawa wengine wanalaumu eti wapemba wanafanya biashara ilala na kariakoo, wacha ujinga huo, serikali imepafanya dar pahala pa biashara ndio maana watu kutoka sehemu tofauti wanakuja hapo dar kwa ajili wafanye biashara, hasa uyo mpemba akifanya biashara yake dar atamuuzia nani? wakati serikali inazidi kuiua iyo pemba, funueni akili zenu izo, sio mnapiga zogo wala hali hamuijui, na sio pemba popote ambapo watu wanauna watupwa wanatakiwa wasema

    ReplyDelete
  14. Ninachosema wapemba watu wa maneno tu,hawawekezi kwao mbona wachaaga wanajenga kwao wakati wanafanya biashara kubwa mikoa mingine sasa kwa nini wapemba hawajengi kwao wanajenga ila,kariakoo,tanga mwanza wakati hao hao wanakalia maneno maneno,pemba nini ? inaukubwa gani ni ndogo hata kuliko wilaya ya bagamoyo hakuna maendeleo watu wachuki na fitina tu,mbona sasa serikali inawaletea umeme toka tanga nao ni CUF wameleta????? wekezeni kwenu jengeni kwenu fanyeni biashara bara lakini jengeni kwenu

    ..............Isma Kabengo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...