Mwendesha mashitaka wa serikali Harun Matagane (kushoto) akimsomea mashitaka dereva Damian Aweda Lali (30) akiwa kitandani katika wodi ya majeruhi hospitali ya Mount Meru mjini Arusha kwa kusababisha vifo vya watu 16 na majeruhi 24.
Kwa mujibu wa hati hiyo ya mashitaka dereva huyo alisomewa makosa 47 ya kuvunja sheria za usalama barabarani.Kulia kabisa (mwenye miwani) ni hakimu mkazi wa mahakama ya mkoa wa Arusha anayesikiliza kesi anayesikiliza kesi hiyo George Hubert.
kweli hii kali..hi serikali ya tanzania ivi akili yake ina akili kweli, what if the man dies in bed before sentencing?? will the decease be the accused or wot? kwani hakuna subira mpaka apone? what kind of a law system is that? they need to have some kind of judiciary review, hata kama alisababisha vifo, still he needs a "fair trial" that country needs a LAW REFORM this is really insane and its funny too..
ReplyDeleteMdau
Hivi hii case au ni Orijino komedi?. Hawa watu wanaendeshwa sana na utashi wa kisiasa, huyo bwana kutokana na kuwa na hali hiyo ya kuumwa bado wanamsomea mashitaka yaani ni kama vile "Kwa nini wewe umepona" Tutakutia presha mpaka nawe ufe. Hapo ni hospitali na si mahakamani kwa nini wasingesubiri apone apate akili za kufikiri na kujua alichotenda ni makusudi au bahati mbaya tu?. Hakimu mwenyewe amekaa kama naye anasubiri kuchomwa sindano LOL!, bongo kweli nuksi wala si tambarale.
ReplyDeleteMi naona inabidi sasa twende kwa mtindo huu potelea mbali akifa kwa presha AJALI ZIMEZIDI madereva vichaa kama hawa ni kuwalaza hospital huku wamefungwa pingu kila siku wanaua tu EBO!! good job wadau wa sheria hakikisheni ananyea debe MUUAJI huyu.ili iwe fundisho kwa wengine weeeeeeeeeeeeengi kama hao.
ReplyDeleteNakubaliana hii ni kali ya kufungua mwaka. Je kama jamaa akili zake zimemruka kutokana na msikukosuko ya ajali itakuwa ni haki kweli. Mtu kama huyu alitakiwa kuwa chini ya ulinzi na atakapopata nafuu au kutoka ndiyo kusomewa mashtaka. Na inaweza isiwe big deal sana kwasababu hakukusudia. Na kama sheria hailazimishi magari kukaguliwa au kama gari lake lilikaguliwa utamhukumu vipi?
ReplyDeleteTATIZO LA KURIDHI SHERIA ZA KIKOLONI,KINACHOFANYIKA HAPO MSUKUMO WA ALICHOSEMA KIKWETE, LAKINI HAIONDOI UKWELI KWAMBA GARI LA DEREVA HUYO LILOGONGWA NA TELA LA KOKAKPLA, SASA DEREVA WA ROLI ATASHITAKIWA KWA KOSA LIPI.
ReplyDeleteTATIZO NI RUSHWA KWA KIKOSI CHA TRAFIKI,MAGARI YAKIKKAGULIWA ,HAYA YOTE YATAISHA.
msiwe watu wa kulaumu bila kuchambua mambo. Huyu jamaa anapaswa kusomewa mashitaka akiwa hapo na pia alindwe ili asikimbie. Watumishi wamefikia hatua hiyo baada ya aliyekuwa dereva wa basi la Tashrif lilioua watu 28 tanga kutoroka hospitali alikolazwa baada ya kupata nafuu kidogo ili kukimbia mkono wa sheria. Fikirieni kwanza kabla ya kuanza kuropoka hovyo hapa
ReplyDeleteMtazamo wangu ni kwamba huu ni ukiukwaji wa hakiza binadamu. Hata kama huyo dereve ni mtuhumiwa, nadhani bado ana nafasi sawa kama watu wengine siyo tu kujitetea lakini vilevile kuwa na mazingira mazuri ya kusomewa mashitaka. Sidhani kama watuhumiwa wakiwa wagonjwa magerezani huwa wanaburuzwa tu kortini ili mradi kesi ziishe. Ninafahamu kuwa kuna wengine wameathirika na janga hilo na ninatoa pole kwa hilo ila tukumbuke kuwa huyo ni binadamu kama sisi.
ReplyDeleteMafisadi wangekuwa wanasomewa mashitaka mapema kwa kasi, ari na nguvu hii basi inji hii ingefika mbali sana!
ReplyDeletekwanza ninapenda kuwapa pole watu wote walioumia na ndugu za marehemu kwenye hiyo ajali. kwakweli huu ni msiba mkubwa kwe watanzania. serikali isichukulie gazba kumuadhibu huyo jamaa kabla hawajafanya uchunguzi kama yeye alikusudia kufanya hiyo ajali au kulikua na makosa kwenye hilo gari. kama kulikua na makosa kwenye hilo gari mtu wa kwanza kufuatwa ni yule mwenye hilo gari. huyu jamaa ni dereva tu kazi yake ni kuendesha gari alilopewa na tajiri yake. je tanzania hukagua magari kabla hayajaruhusiwa kutumiwa. nchi nyingine huwa kila baada ya miaka michache kabla huja renew your licence ni lazima gari lako lichekiwe. kwasababu hii ajali huwa zinapungua. jee baada tu ya ajali walimchunguza huyo dereva kama alikua mlevi au la. alikua anasinzia kwa kuwa kazini kwa muda mrefu au la. alikua anaendesha vibaya hilo lorry au break zilikataa kushika. kama nyie serikali hamfanyi kazi zenu inavyo takiwa msikurupuke tu na kuwasomea watu mashtaka kabla hamjafanya uchunguzi. mimi ninaona sheria zetu zimeingiliwa na siasa au zinaupungufu mkubwa.
ReplyDeletePoleni wafiwa.
ReplyDeleteNingependa kuomba serikali iwalazimisha wafanyabiashara wa magari ya usafiri wanunue insurance ili katika ajali kama hizi, at least walioumia wapate fedha kutoka katika insurance.
Si ruhusa kufanya biashara nchi zilizoendelea bila ya kuwa na insurance ya kinga za ajali kazini kwa wafanyakazi wake na wateja. Na wateja waliofariki at least familia zao wanalipwa fedha kidogo. Kwa nini sisi tuko nyuma sana? Watu wangapi wamefariki katika ajali za mabasi?
Aluta Kontinua
Dah kweli kazi tunayo, yaani nimejaribu kusoma maoni ya watu hapo juu nimeona ni jinsi gani Tanzania ilivyo na watu wenye vichwa vitupu. Hii ndio maana madereva wanaendelea kutumaliza kila kukicha mabararani na hakuna anayeshituka.
ReplyDeleteYaani pamoja na huyo jamaa kusababisha ajali na kuua watu 16 eti kuna watu bado wanatetea..!!!??? Eti atasomewaje mashitaka kitandani...!!! acheni ushamba wacheni wanasheria wafanye kazi yao kama ingekuwa ni kinyume cha sheria hao jamaa wasingetilia suti zao na kwenda huko. huyu anon Tarehe January 23, 2009 9:12 PM anasema hiyo ni kinyume na haki za binadamu. Hivi huyo jamaa kuua hao watu 16 ni sawa na haki za kibinadamu...??? acheni mambo ya kipumb+++vu na muache wanasheria wafanye kazi zao.
Hakuna asiyejua karibu asilimia 80 ya ajali zote zinatokea zinatokana na uzembe na kutojali kwa madereva.
wacha jamaa atayarishiwe uniform akitoka tu Hospitali akanyee debe hiyo ndio dawa pekee. Wataheshimu tu sheria za barabarani kwa mtindo huu.
Nyie msiojua sheria, acheni kuonyesha ujinga wenu hapa. Eti kwanini wasisubiri mpake apone, that's a nonsense.
ReplyDeleteMimi hapa USA msichana wangu alisababisha ajali polisi walimwacha apelekwe hospitali, lakini walimfuta pale kitandani na kumuuliza maswali na kumpatia tiketi zake na siku ya kwenda mahakamani.
Hawa waendesha mashtaka wanafanya inavyotakiwa. Na kama ujui kitu, just shut up. Wacheni sheria zitumike kama zinavyotakiwa na acheni mambo yenu ya kienyeji kama mlivyozoea. Ambayo ndiyo chimbuko la matatizo ya kisheria bongo.
Mdau
USA.
wewe Mtoa Maoni wa January 24, 2009 1:09 PM,
ReplyDeleteUjui nini maana ya haki za binadamu ndio maana umeandika pumba kiasi hicho....
Kila mtu ana haki ya kujitetea na lazima apewe haki yake ya kujitetea hata sadam Hussein alipewa haki yake ya kujitetea hata watuhumiwa wa mauaji rwanda wanapewa haki sembuse dereva....
labda tajiri kakataa kutoa hela ya service....
Ukitembea duniani ndio utajua nini maana ya haki za binadamu nina uhakika ujatembea kwa hiyo siyo makosa yako
ni kweli waendesha magari ambao hawafuati sheria zilizopo na kuuwa watu wanatakiwa kushtakiwa. kabla hatuja muhukumu huyo dereva ni lazima ufanyike uchunguzi kujua hiyo ajali ilisababishwa na nini. hatuwezi kumlaumu huyo dereva bila ya kujua makosa ni ya nani. si vizuri kumtia mtu jela bila hujafanya uchunguzi. kwenye nchi zilizo endelea uchunguzi hufanywa kabla ya kumshtaki mtu. makosa yanaweza kuwe ya gari na sio dereva. nyie mlioguswa ni hii ajali kaeni tayari kumshtaki huyo dereva, mmiliki wa hilo gari na kampuni iliyokodi hilo gari na kama hilo gari llliruhusiwa kutumiwa kwenye barabara na idara inayohusika pia washtakini serikali. hivi ndivyo inavyofanyike kwenye nchi zilizoendelea. kesi kama hizi zikiwa zinakubaliwa kisheria kila mtu atakua careful.
ReplyDeletewewe MDAU WA JAN 24TH 7.14 WA USA, next time kasome vitabu kabla hujaanza kuropoka humu, the LAW in tanzania is the same as the whole of europe as its a commonwealth country, hayo mambo ya sheria zenu za USA haziingiliani kabisa na commonwealth countries ndo maana hata USA MNA DEATH SENTENCE but europe na africa there is no such thing, njoo usome law UK uelimike, na inawezekana huyo demu wako alisomewa mashtaka walijua atatoka nduki labda hana leseni, na makaratasi ofcouse, dont get me wrong im AN ASSERTIVE" person, sheria za marekani za ku bear amrs ulisikia ziko europe na african commonwealth countries? sasa kwa sababu demu wako alisomewa mashtaka kitandani ndo na wengine wasipewe haki zao sababu hiyo? hutaendelea daima ukiwa na fikra duni, ...i hope she managed to pay her fine and learn big time!
ReplyDeleteMDAU
uk
Sababu ya OJ kushinda kesi yake mara ya kwanza ni taratibu hazikufuatwa vizuri. Wewe Mdau wa Ohio mwenye binti ulichotakiwa ni kuita challenge(NFL)> Nenda mahakamani jitete vizuri ungeshinda vibaya sana. Unaishi US lakini inaonekana mkono wa sheria umekupita kushoto.
ReplyDelete