Home
Unlabelled
enzi za mwalimu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Nyerere road hapo mkuu, karibu na stendi ya daladala ya çhai ya 2'. Imekumbusha home mwanangu
ReplyDeleteNADHANI UFISADI NDO SUMU YENYEWE YA MSHIKAMANO
ReplyDeleteTanzania and Africa need to sustain and develop such nonviolence movement, the spirit that should be allowed to grow for nationalism and positive changes in our country and continent at large. Our democracy is suffering from malnutrition!
ReplyDeleteEnzi za mwalimu, kama zilivyokuwa enzi za Kwame (Ghana), Gandhi (India), Mandela na nduguze (SA) uzalendo na mshikamano vilitawala. Mipasuko kati ya 'walionacho' na 'wasionacho' haikuruhusiwa, hivyo kuleta amani ambayo hadi leo tunajivunia, japo definition ya demokrasi kwa taswira ya kimataifa bado Tanzania (na nchi nyingi za Afrika) tunasema ni "uchaguzi huru na wa haki." :)
Wanafunzi wakiandaa maandamano yanavunjwa! Walimu wakifanya yao wanabughudhiwa. Nakumbuka enzi za Mrema hata mabomu ya machozi, virungu vya polisi na mabuti yalitumika. Kwa sasa vitisho vya kisiasa i.e kauli tata na vurungu vinatawala.
Je, kama maandamano (as a powerful nonviolence strategy for changes) yanazuiliwa tutumie mawe? Tutumie matusi? Tutibuane na polisi? Tuchukie mamlaka iliyopo na kuiona kandamizaji ilhali sivyo? Kwa nini maandamano ya wanafunzi yaliyoandaliwa kwa misingi ya amani na utii wa sheria zilizopo yavunjwe?
Taifa limeshuhudia kwa kipindi kifupi kisichozidi miezi mitano kwa mfano, kumekuwepo na sera na vitendo vya kudumaza demokrasia, tofauti na ilivyokuwa enzi za Mwalimu! Gazeti likiandika ukweli linafungiwa; watu wakiandaa maandamano ya amani, yanavunjwa; na mbaya zaidi majuzi Dr.J.K. ametoa kauli tata huko Zanzibar ambayo sio njema kutolewa na manadiplomasia kama yeye.
Sisemi enzi za Mwalimu kulikuwa na mazingira mazuri kwa vyombo vya habari kutenda kazi zake, la hasha, bali kuna mambo mengi yalikuwa na unafuu ambao ulitufumba macho. Tulisoma bure; viongozi a.k.a vigogo waliwajibika kwa wananchi; ufisadi haukuwepo na kama ulikuwepo haukuwa mkubwa na wa wazi kama ilivyo hivi leo; wakubwa na wadogo waliheshimiana na ilijulikana wazi kuwa mamlaka (regime) ni ya raia.
We ought to invest on young people if we really need positive and lasting changes in our politics (and into other development arenas).
Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.
Tuwe wakweli wanakijiji kwa Nyerere watu hawakuandamana kwa hiari. Mnasahau mgambo na zile kodi wananchi walikuwa wanadhalalilishwa nalo. Nyerere hakuruhusu uhuru wa maoni hata kidogo wangapi waliwekwa kizuizi kwa kukataa kukubaliana nami.
ReplyDeleteNakubaliana na Nyerere kwa kupinga ufisadi, there i give him a credit
tuwe wakweli, nyakati hizo utake usitake ni utaandamana tu hata kama huelewi chanzo cha maandamano hayo.
ReplyDeleteHizo siku zimepita na wala hazirudi tena kulikuwa na mapenzi ya nchi na wananchi wakipenda kwa moyo na kusaidia kulikuwa na utu nasio kitu leo wapi?? ni mazungumzo tu ni vizuri tunakumbushana angalau kwa hizi picha
ReplyDeleteJapo sikuwepo lakini nafikiri enzi za Mwalimu watu walikuwa wanamapenzi ya kweli na nchi zao, sasa hakuna uzalendo kabisa kila mtu na lake waliopo tz na hata waliopo nje, tunahitaji kubadili fikra zetu ili turudishe uzalendo
ReplyDeletesiyo kweli kwamba tulisoma bure. tulisoma kwa kutumia fedha za misaada, mikopo toka nje, na kodi mbalimbali za wananchi.
ReplyDeleteHuwezi kuwa kama malaika, kama mwanadamu kuna makosa unafanya bwana. Nyerere alikuwa bonge la kiongozi. Ufisadi haukuwepo kipindi hicho na waliokuwa wala rushwa walifanyiwa haki yao. Watu walikuwa wanaipenda nchi yao. Kulipa kodi is a civil right na mtu ambaye anataka kutoroka kulipa kodi ni mbaya kuliko hata shetani mwenyewe.
ReplyDeleteWalioishi enzi zake kwa muda mfupi angalau kama mimi, wanamiss. Mimi yule mzee namiss saana.
Kila jambo na wakati wake. Hicho kilikuwa kizazi cha karne ya 19. Leo mambo ni mengine kabisa . ZIDUMU FIKRA ZA MWALIMU NYERERE!!!! Imebaki story
ReplyDeleteMwalimu bwana katurostisha , watu wanasoma lakini hawawezi waliowengi kuingia katika soko la kimataifa. Nakumbuka tukiwa chuo kikuu miaka ya 90s vitabu tulikuwa tunatumia vya miaka ya late 70s na early 90s. Sasa hiyo elimu inakuwaje hapo? Watanzania tukubali hicho kiswahili kime-turostisha na ajabu bado wabunge wanataka kitumike chuo kikuu.
ReplyDeleteMichuzi usiibane.
kama umekumbushwa mbali,hiyo nyerere road ungeiita jina lake la asili,...watoto wengine bana !
ReplyDeletebarabara ya nyerere,,,,
ReplyDeleteyani kweli nchi haibadiliki sehemu zingine asa mikoani,yan mwanza apo 1970 now iko ivo ivo kaaaazi kweli-kweli
mji wa kale
Annon wa 5:40PM, Jan. 25 tanua mawazo kidogo, fikirisha ubongo acha ubishi usio na maana. Kodi na mikopo ndivyo vilifanya tusome hivyo. Ukisikia elimu bure maana yake ndio hiyo.
ReplyDeleteNaunguana na muungwana hapo juu; Kiswahili kimeturostisha sana na bado kinaendelea kutudumaza kwenye kila nyanja!!
ReplyDeleteHivi, haiwezekani tukafundisha kwa kiingereza kuanzia vidudu na somo la Kiswahili likaendelea kuwa kama lilivyo? Tunafaidika nini kufundishwa kwa Kiswahili miaka saba, kisha kurudia mambo mengine Sekondari kwa kiingereza?
Tusidanganyane!!
Kiswahili hakina maana kwenye taaluma yetu, kinapoteza muda, kinadumaza taaluma, kinatufanya tusiwe washindani kazini ukilinganisha na wenzetu wa nchi za Kenya na Uganda ambako ndiko vigogo na wenye nazo wanakowapeleka watoto wao
Kama sivyo, kwa nini wanetu waende kusoma Uganda na Kenya?
Kiingereza ni dili, nawaapia. Na kusoma Kiswahili kama somo tu hakutatupotezea utamaduni wetu. Kilituunganisha enzi hizo, let's put it down and take another fastest boat, English!
Maasai
Michuzi, kuna ombi nimekuwa nataka kukupa kwa muda mrefu kidogo, lakini nimekosa sehemu ya kuweka.
ReplyDeleteNatafuta makala za zamani za magazeti ya kimataifa, ya U.K, USA etc. zenye articles zinazomhusu Nyerere wakati alipokuwa rais. Mimi ni mfuasi mkubwa wa Mwalimu na najua alikuwa anavutana nao sana miaka ile. Sijui unaweza kunidirect wapi panapoweza kunisaidia ili kujua ni propaganda gani walizokuwa wanazirusha kwenye media zao.
Nitashukuru kwa msaada wowote.
Mdau wa January 26, 8:24. Mwezi ule Nyerere alipokufa Daily Mail la Uingereza lilitoa article moja kuhusu maisha yake, basically ilimkosoa kwa siasa zake za ujamaa zilizofeli, uongozi wa kidikteta pia yule mwandishi aliishi Tanzania miaka ya 80 na alieleza kuwa thamani ya pesa yetu ilishuka sana na mwisho watu waliita chapa mwalimu meaning cha maana katika noti ilikuwa picha ya raisi tu. Pia alieleza jinsi maisha ya watu yalivyokuwa kwani waliokuwa na vitambi walikuwa viongozi wa chama tu! na wanawake waliovaa waliobadisha vitenge vizuri walikuwa viongozi wa jumuia za chama au wake wa viongozi.
ReplyDeleteHuyu jamaa anaitwa Max Hastings pia alieleza jinsi Nyerere alivyokuwa na akili za asili kuweza kumudu policy zenye nguvu lakini alikuwa mbishi kushaurika.
Muugwana.
Asante mdau wa January 27, 2009 1:08 PM, inawezekana nimeshaisoma hiyo article au ninayo. Lakini si unajua katika wakati kama ule, critics walikuwa kidogo measured kwenye statement zao ndiyo maana najaribu kupata hizo articles zilipokuwa released (in real time)wakati uchumi unayumba na kuanguka kama walivyokuwa wanasema.
ReplyDeleteNadhani lugha waliyokuwa wanatumia ilikuwa tofauti, labda critical zaidi kuliko waliyotumia wakati amefariki.