Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samwel Sitta akiongea na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa mikutano wa Karimjee mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa Kamati ya Bunge ya hesabu za mashirika ya Umma unaojadili utendaji na uwajibikaji wa mashirika hayo.
Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya hesabu za mashirika ya Umma Mh. Zitto Kabwe akitoa taarifa kuhusu mashirika sita ya Umma mara baada ya kamati hiyo kuyatembelea ili kutathmini utendaji na uwajibikaji wa mashirika hayo katika Ukumbi wa mikutano wa Karimjee leo jijini Dar es salaam. Kushoto kwake ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samwel Sitta akifuatiwa na Bw. Ludovick Uttouh Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali.

Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh: Samwel Sitta akifungua mkutano wa siku mbili wa kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma unaojadili utendaji na uwajibikaji wa mashirika ya Umma katika ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar es salaam , kushoto kwa spika ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali Bw. Ludovick Uttouh.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Jane Nyasuguta: "I made it a resolution to go down with as many men as possible


    Jane Nyasuguta*, 40, a former teacher living in Nyanza Province, western Kenya, thought she and her husband had a good marriage until she discovered he had a mistress in a neighbouring town. She told IRIN/PlusNews that after his death from an AIDS-related illness, and her discovery that she too was HIV-positive, she was filled with resentment.
    "When we first married, we were a very loving couple. We had started life together from scratch; we pooled together our little resources to build a wonderful family together because we were both receiving very little salary from the government.
    "I thought we were both very faithful to each other; I had no reason to suspect that my husband had a mistress outside our marriage. In 1999, he was promoted to be a head teacher and I thought that would make us happy even more, but it was never to be.
    "He started coming home late, drunk, and at times was very abusive both emotionally and physically. Then it became worse and he would stay away from home for close to one week.
    "I was dejected even more when I realised he had a mistress in Isebania township, near the Kenya-Tanzania border. He became sick around 2000 and he later died in 2002 of tuberculosis.
    "Immediately after his death, I went for an HIV test because I wanted to be sure. I was shocked when I realised I was positive. I knew I had got the disease from my husband and I made it a resolution to go down with as many men as possible, even very young boys in high school.
    "The disease finally put me down, and I was almost dead when a friend of mine took me to hospital, where I was introduced to ART [antiretroviral therapy].
    "When I regained strength, what I had done haunted me - I was destroying people's future and families, yet they never sent my husband out to go and get the disease.
    "I resigned from my teaching job, and together with my friend we formed a network of widows to sensitise people on the need to know their status, and even go public about it.
    "The past is behind me, but it still haunts me, especially the young boys I took to bed because of a problem within my family that they knew nothing about.
    "I pray every day that God will forgive me for what I did. But I also advise the young girls I talk to, if possible, to stay out of marriage because men can be sly."

    *Not her real name

    ReplyDelete
  2. Vikao viiingi vya kamati za Bunge na mijiposho kibao wanalipana lakini mbona hatuoni mabadiliko huku kwa wananchi??? Umaskini unaendelea kushika kasi...fedha za umma hazifiki kwenye zahanati za wananachi, maji taabu, umeme taaabu halafu wao wanaendeleaza vikao na suti zao KICHEFUCHEFU OVYOOOOO!!!

    ReplyDelete
  3. Kamati ingefanya utaratibu wa kuongea na wafanyakazi wa chini moja kwa moja kwa kushtukiza ili kupata ukweli wa mambo badala ya kuridhika na ripoti za kupikwa
    Wakati fulani tulishawahi kusikia wafanyakazi wa Dawaco wakiukataa uongozi wao hadharani kwa jinsi unavyowafanyia sijui ni hatua gani zimechukuliwa .
    Kuna watu wamegeuza mashirika haya kuwa ni makampuni yao binafsi wanafanya wanavyotaka kuna wizi mkubwa tu ndani ya haya mashirika
    Tatizo letu ni kwamba hatuna utamaduni wa kufuatilia mohi unaofuka ili kujua unasababishwa na nini mpaka pale hali inapokuwa mbaya kabisa kama kwa ATCL ambako kuna wakati wafanyakazi walishawahi kulalamikia uendeshaji wake
    Halafu kuna hizi zinazoitwa Bodi za uendeshaji mi sioni kama zinafanya lolote zaidi ya kuyatafuna mashirika kupitia maposho makubwa wanayojilipa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...