matokeo yanasubiriwa mchana huu na kama kawaida globu ya jamii itafanya mambo yake, ila kwa sasa minyeni kidoooogo kwani matokeo yanatangazwa muda si mrefu ujao....
Home
Unlabelled
mbunge mpya mbeya vijijini kujulikana punde
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
kweli Dunia imekwisha!! Wanaojiita watumishi wa Mungu a.k.a wachungaji wa kondoo wa Mungu wanavyojiingiza kwa wingi kwenye siasa ilhali twafahamu huko kumejaa uongo, ulaghai, ufisadi, utapeli na ushirikina. Mfano huyu mgombea wa Mbeya vijijini siku anahitimisha kampeni zake alisema wananchi wasimchague mgombea toka chama cha upinzani kwa vile atashindwa kufanya kazi zake ipasavyo maana waziri mkuu ni CCM, mawaziri wote ni CCM je akihitaji faili fulani atapewa na nani? Uongo mchana kweupeeee!!! Anataka kutuambia ndivyo hali halisi ilivyo au funika kombe mwanaharamu apite? Anataka kutuaminisha kwamba ndivyo Mizengo Pinda na mawaziri wote walivyo? Watu tunajua mambo-nenda katubu na uachane rasmi na uchungaji wake feki!!!!
ReplyDeleteMimi sijui lini tutajifunza demokrasia ya kweli. Ina maana ili ukae madarakani lazima ucheze rafu? Kwanini masanduku ya kura yalikutwa kwa viongozi na makada? sijui, lakini tujue tutakuja kuulizwa hicho ulichokipata ulikipata vipi? Kwani swali kubwa ni je nia ni kupata mkata au nikuwatumikia wananchi?
ReplyDeleteM3
Tunajua hii ni globu ya sisiemu, na kama kawa, tayari umekwisha kumtangaza! Asante kwa kutujulisha mshindi wetu!
ReplyDeleteBlaza Michuz, wacha unazi wa CCM, hii blogu ya jamii, picha uliyoweka kwa mwenye akli timatu anatambua kwamba, CCM kashinda, kama sivyo, kwa nini usiweke picha za wagombea wote. Any way, sikusudii kuponda hilo bali nataka kuungana na waliotangulia kuhusu rafu, wizi, utapeli, unyang'anyi na mchezo mchafu wa ccm wa kuiba kura. Hivi nauliza waungwa, demokrasia ndio hii? kwani CCM haiwezi kushinda bila mizengwe? mara masanduko yamekutwa majumbani mwa makada wa CCM, mara mchezo mchafu katika daftari la wapiga kura, mara majina ya watu hamuna, mara mamluki,,, eehee basiiiiii, inatosha, mtaiba mpaka lini. Kama hamuna insafu basi hata haya na soni pia hamuna?
ReplyDeleteBwana Michuzi mbona upo biased, au wewe CCM ipo kwenye damu. Nilitegemea ungeonesha picha za wagombea wa vyama vya upinzani, ili kujenga demokrasia ya kweli.Wewe kama mwanahabari unatakiwa usiegemee upande.
ReplyDelete