Home
Unlabelled
mustafa hassanali kuuanza mwaka na malaika
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Naibu Gavana Reli atajwa kwenye EPA
ReplyDelete2009-01-29 10:10:19
Na Hellen Mwango
Shahidi wa pili katika kesi ya wizi wa Sh. bilioni 1.8 kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inayomkabili kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rajabu Maranda na mwenzake, amedai mahakamani kuwa Naibu Gavana wa Utawala wa benki hiyo, Juma Reli, aliithibitishia benki moja kwamba fedha hizo ni halali.
Shahidi huyo ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji na Huduma cha Commercial Bank Africa, (CBA), Ronald Manongi (49), alidai katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana kuwa Reli alithibitisha fedha hizo zilizoingizwa katika akaunti ya Maranda na Farijala Hussein zilikuwa halali.
Fedha hizo ziliingizwa katika akaunti ya Kampuni ya Kiloloma & Brothers ambayo ilidai kuwa ina jukumu la kukusanya deni la kampuni ya B.C.Cars Export ya India.
Kesi hiyo inasikilizwa mbele ya jopo la mahakimu watatu wakiongozwa na Naibu Mwenyekiti wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Cypriana Williana, Naibu Msajili Mahakama Kuu Tanzania, Phocus Bampikya na Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Saul Kinemela.
Akiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Boniface Stanislaus, shahidi alidai kuwa akiwa Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji na Huduma cha CBA wakati huo ikiitwa United Bank of Afrika, alipata mashaka baada ya kuona akaunti ya kampuni ya Kiloloma inayomilikiwa na washirika wawili, Farijala na Maranda, inaingiza fedha nyingi kwa ghafla, ndipo aliandika barua kupeleka ofisi ya Naibu Gavana.
Manongi alidai washitakiwa walifungua akaunti ya biashara CBA namba 0101305008, Agosti 31, mwaka 2005 ambapo waliingiza Sh. 500,000.
Shahidi huyo alidai Septemba 2, mwaka 2005 akaunti ya Kiloloma iliingiziwa Sh. 1,864,949,294.45 kwa njia ya mtandao wa kompyuta kutoka BoT kwenda CBA.
Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano kati ya Boniface na Manongi.
Boniface: Kabla fedha haijaingizwa katika akaunti kutoka BoT kuna mahali inapita?
Manongi: Mteja hana akaunti BoT, bali CBA inatuma maelezo kuwa fedha ni ya Kampuni ya Kiloloma.
Boniface: Ielezee mahakama nini kilitokea Septemba 2, mwaka 2005?
Manongi: Siku hiyo BoT waliingiza Sh. bilioni 1.8 kupitia akaunti ya kampuni ya Kiloloma.
Boniface: Baada ya fedha hizo kuingia ulichukua hatua gani?
Manongi: Kuna mambo kadhaa ambayo niliyafanya kwa sababu ilinipa mashaka ambapo niliandika taarifa kama mkuu wa kitengo kwenda BoT kwa kurugenzi ya usimamizi wa mabenki kueleza jinsi fedha ilivyoingia.
Boniface: Je, BoT walijibu taarifa yako ya mashaka?
Manongi: Walinijubu.
Boniface: Majibu yalitoka wapi?
Manongi: Nilijibiwa na ofisi ya Naibu Gavana wa BoT (wakati huo Juma Reli) ambapo alidai kuwa hakuna mashaka dhidi ya fedha hizo kuingizwa katika akaunti ya washitakiwa (Kiloloma).
Boniface: Uliridhika?
Manongi: Hapana, niliandika barua kwa mteja (Kiloloma) ili wanieleze fedha hizo ziliingizwa kwa madhumuni gani, chanzo chake ni nini, na mdeni ni nani?
Boniface: Je, ulijibiwa?
Manongi: Ndiyo, walinijibu walisema wanalipwa kwa niaba ya kampuni ya Cars Export ya India, na kwamba walidai wana kibali maalum cha kutumia sehemu ya fedha hizo ambazo zimelipwa na BoT.
Manongi alidai kuwa washitakiwa walichota fedha hizo kwa nyakati tofauti kuanzia Septemba 2 hadi Novemba 8, mwaka 2005 jumla ya Sh.1,150,249,294.45 na Sh. 714,700,000 (Paundi 350,000) walituma huko Uingereza.
Aidha, alidai kuwa hadi sasa akaunti hiyo imebakiwa na Sh. 115,394.64 tu. Kesi hiyo imeahirishwa hadi leo saa 3:30 itakapoendelea kusikilizwa.
SOURCE: Nipashe