The Ngoma Africa Band

Bendi maarufu ya mziki wa dansi barani ulaya "The Ngoma Africa Band" inatarajiwa kuwadatisha washabiki wa mziki katika onyesho kubwa la "Fest Africa" litakalo fanyika mjini Tampere, Finland, siku ya tarehe 7 February 2009, katika ukumbi wa Klubi.

Bendi hiyo inayoongozwa na mwanamziki mashuhuri Ebrahim Makunja aka Ras Makunja"Bw.Kichwa Ngumu" yenye makao yake nchini ujerumani, itaupeleka "mzimu wadansi la bongo" huko Ufini.

Ngoma Africa ni maarufu kwa tabia za kuwadatisha akili washabiki kwa kutumia mdundo wao "Bongo Dansi".Bendi hiyo ambayo imetajwa katika maonyesho mengi ya kimataifa kuwa ni bendi bora kutokana na tabia zake za kuwaridhisha washabiki kwa kuwapa burudani ya kufa mtu!

Kikosi hiko cha Ngoma Africa kinatarajiwa kuruka kuelekea Tampere,Finland bila ya kuchelewa kwa ajili ya Onyesho hilo .

Ngoma Africa ambayo pia imepachikwa majina mengi ya kiusanii na washabiki kutokana na tungo zao na pia mdundo wake ambayo mara nyingi unawapeleka mchakamchaka washabiki!

majina kama FFU,wazee wa kuziwia rushwa, watoto wa uswahilini n.k hayakwepeki kwa bendi hiyo ambayo pia ina taji la "The Golden Voice of East Africa".

Ngoma Africa kwa mara ya kwanza kutumbuiza nchini Finland inatarajiwa kukonganyoyo za washabiki wote wa kimataifa katika mji wa Tampere.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. haya! hao vichaa wanakuja! na baridi hilo naona mtatona jasho kweli!!

    ReplyDelete
  2. ras Makunja vipi? safari hii madongo narushiwa nani? mie unanimaliza pale unaporushaga madongo yako! uwatazami usoni unao
    warushia! halafu hata noma huna!we mijiwe tu!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  3. Jamani chizi kapewa rungu sasa!nakuja sokoni Ufini.....

    ReplyDelete
  4. Hiiiii! Gwaride la FFU! kuchezwa katika barafu Ufini! kumekucha,naona mchaka mchaka kama kawaida na washabiki

    ReplyDelete
  5. Ras Makunja! vipi! mlimaliziana vipi? na baba wa kambo?

    ReplyDelete
  6. Do!Naona Kazi mnayo huko Tampere!
    mchizi aliyekomaa kichwa huyo anakuja na vichaa wake!

    ReplyDelete
  7. leo nina stress,,,
    ivi ukiwa scandinavian countries lazima ufuge nywele izo na kuvaa vilemba kama demu?ili wathungu wafoleni au?makumbusho ya Tz?na mabatiki?mana nijuavo hatuna utamaduni huo wala vazi la taifa
    hahahahaaa,,,anyway keep-up vijana tuwakilisheni vilivo ilmradi ubeba box huo mwapata cha kutuma kwenu bongo

    ReplyDelete
  8. Hi! mtoa maoni mwenye stress!!!
    maoni yako!yanaonyesha jinsi gani!kichwa chako kilivyojaa stress!!unazungumzia uhuru wa mavazi na nywere! bila kujua mambalozi wetu ni watu wa namna gani!pia wasanii hujichagulia mavazi na mtindo yao kiusanii!sio heti kivutio kwa wazungu!sidhani kati ya hao kama kuna anayembabahiia mzungu!?labda swali hio wajibu wenyewe,pia ngoma africa wanakaa Ujerumani sio scandinavia.

    ReplyDelete
  9. Hi! Peperusheni bendera kisawa sawa
    wenetu!!!!Ngoma Africa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...