nyumba za makabila mbalimbali kama zinavyoonekana kwenye mchoro ulioko kwenye geti la kilimanjaro national park

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Mbona za wabeba maboksi na waosha vyombo hawionyeshwi hapo? Au aibu kutuonyesha ni za kuzikodiswa tu...nasikia wengi wa wabongo wenzangu kule ughaibuni wanaishi kwenye 'Slums...hence,Slumdog millionaires...wakati wakija hapo kwa vekesheni!!!

    ReplyDelete
  2. are you kidding me what a bunch of bollocks..aliyeichora hii sio hata professional..we toka lini mzaramo akae kwenye nyumba hiyo..wangeandika mafisadi.wao wanasema hivyo kwasababu dar es salaam ni nyumbani kwa wazaramo na nyumba hizo zimejaa,hawajui hawapo hata mitaa kama ya mbezi au kunduchi..rarely..huko ni wachaga,wahaya,wanyakyusa..am disgusted na huyu mtu alietuzalilisha

    ReplyDelete
  3. Kimsingi nyumba hapo ya maana ni ya wahehe maana ni kama self contained za sasa mambo yote ni kama mnamalizana humo ndani. Sasa sijui hawa wengine na umaridadi wa kujiona wachagga na wahaya nyumba hata mwaka haihimili.

    ReplyDelete
  4. Sasa wazaramo walisimama wapi mpaka wakapitwa? Maana wao walikuwa na sevant kota long taim!

    ReplyDelete
  5. Nimeifurahia sana hii picha maana imekamilisha mawazo yangu tatizo ni kuwa mimi si mhandisi mchoraji(Architect).

    Inanisikitisha sana kuwa inaelekea tutasherekea miaka 50 ya uhuru katika nyumba ya mkoloni ambayo haina maudhui yeyote ya kitanzania.
    Mimi ningeshauri tume ya hawa watu waliobobea waandae mchoro wa Ikulu mpya au Nyumba ya Taifa ambayo itajumuisha mazuri ya nyumba za mtanzania.

    Ikulu ya sasa ibadilishwe iwe tu Kumbukumbu ya Rais na pia maktaba ya Uraisi(Presidential Library ambako tutaweka kumbukumbu mbalimbali za viongozi wetu wakuu kuanzia wakoloni.

    Ikulu ya sasa Haitufai kwa sababu:
    1. Ni ya wakoloni
    2. Haina maudhui ya nyumba ya Mtanzania
    3. Kiusalama haina ulinzi wa maana kutoka shambulio tokea baharini ukizingatia uwezo wetu kijeshi
    4. Kwa kuzingatia maafa yale ya Tsunami basi iwapo itatokea na kuathiri eneo letu basi itakuwa hatari kwa usalama wa Rais na kwa hivyo nchi.
    5. Kuwepo kwa Ikulu ndani au karibu na eneo la Biashara(Business City) kunasababisha misongamano isiyo ya lazima hasa misafara mbalimbali inapotokea ya Rais, viongozi wakuu na wageni.

    Naomba kutoa hoja wadau mchangie

    ReplyDelete
  6. Ninakubaliana kabisa na Anony wa Jan 09 2009 10:26 PM. Lakini ningependa kuongezea tu kwamba pengine hajui au amesahau - hili hayati JKN (pumzika kwa amani PKA) alikwishaliona na ndio maana aliamua kuwa makao makuu ya serikali yahamie Dodoma - uliwahi kusikia kitu iliyokuwa inaitwa CDA. Lakini kama ulivyokuwa kwa mawazo yake mengi mazuri, maafisa wake hawakutaka kuondoka dar (walifanya njama na pesa za CDA zikaishia kujenga maekalu Mbezi). Sio ajabu leo hii ajenda ya kuhamishia makao makuu Dom imefutika kabisa!!!!! Kwa kifupi watu wenye akili nyingi kama Mwl walikwishaliona hilo unalozungumzia na wakatoa mapendekezo muafaka. Kwa hiyo kama angetokea mtawala mwenye nia nzuri asingekuwa na kazi kubwa, ni kiasi cha kuamua kutekeleza sheria iliyokwishakubaliwa - kuhamishia ikulu DOM!!!!! nani ana ujasiri huo. DAR KUTAMU, HATOKI MTU. Nani alikwisha kuja Dar na akaondoka kwa hiari????????????

    ReplyDelete
  7. wahehe saaafi sana
    ni kweli ikulu ya Tz me ndo nilimwulizaga mwl wangu primary kidogo anichape makofi,mana sielewi ina maudhui ya kitanzania gani,usalama ziro kabisa-na ukitegemea Tz ni targeted nchi na terrosists,afu iko dar-buziest city na kero ya miundombinu,
    blah blah blah

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...