Bondia Francis Cheka ‘ SMG’ (shoto) amesaini mkataba wa kukubali kucheza na Rashind Matumla ‘ Snake Boy’ (kulia) katika mpambano unaoandaliwa na Mkurugenzi wa kampuni ya Best Man Promotion ya morogoro, Zumo Makame (kati) litalofanyika Februari mwaka huu mji kasoro bahari. picha na mdau john nditi
rashid matumla akimwaga wino juu na chini francis akicheka na karatasi


Kila jambo na wakati wake, lakini wakati hauwezi kufika kama haukuandaliwa vema. Na pengine ni "nature" ya mchezo inayoharibu watu. Kwanini hawa mabondia wanakuwa na upungufu wa kutambua muda wao wa kustaafu? Ni kwanini waheshimiwa hawa wanashindwa kuwekeza kwenye mambo mengine na kutumia muda mchache ambao wanakuwa wakikubalika na kupigana vema kujitengeneza maisha yao ya baadae? Ndondi si mchezo salama saaana kuucheza mpaka uzeeni na baada ya umri fulani unakuwa na nafasi ndogo ya kuondoa athari za masumbwi mwilini mwako. Wengine wanaanza wakiwa wadogo, lakini wangeweza ku-save ama ku-invest kwenye maisha mengine na kuyakimbia masumbwi baada ya muda mfupi ingekuwa heri zaidi. Kwa matumla kuendelea kupigana kwa namna apiganavyo na umri apiganao, nadhani ni KUMUOMBEA KILA LA KHERI maana siamini kama anapata pesa kama alivyokuwa akipata enzi zake na sidhani kama ana nafasi yoyote ya kugombea mkanda wenye hadhi kama alivyofanya miaka iliyopita. Pengine wanamasumbwi wajifunze toka kwa wakongwe hawa. Kina Evander ambao wanapigania dola eflfu kadhaa sasa baada ya kuingiza mamilioni kwa pambano. Kina Tyson waliolazimishwa kustaafu kwa kupigwa vibaya na mtu asiye na jina. Kina Hopkins (ambaye bado anafanya vema japo anaelekea 45) na wengine ambao kwa kutowekeza katika maisha yao ya "ujana wa mchezo" wanalazimika kupigana mpaka uzeeni.
ReplyDeleteMimi si mshauri wa Rashid lakini nadhani ni wakati ambao lazima akubali kuwa hataweza kuwa yule aliyekuwa na sasa ni wakati wa kutafuta wadhamini, kuanzisha Gym na kufunza chipukizi maana uwezo huo anao na atakuwa ameisaidia jamii.
Ni mtazamo wangu wa namna nionavyo tatizo, na yawezekana nionavyo tatizo ndio tatizo.
Blessings
hiki kikao mbona kimekaa kisanii sana...
ReplyDeleteNasikitika kumuoana Rashid Matumla bado anapigana. Its time for you to hang up gloves. Ngumi ni mchezo wa hatari na sio vizuri kabisa kuucheza after 35yrs of age. Unajikuta uko more vanurable to the punches kwasababu speed yako nayo inakuwa imepungua. Hata kama ni Ali, Tyson, Holyfied were not that good after 32.
ReplyDeleteRashid alikuwa ni bondia mwenye kipaji sana na angeweza kuwa bingwa wa dunia katika level ya kina De Lahoya, kama angepata chance. With all the admiration na kwa ajili ya afya yako itakuwa vizuri kuachia ngazi
That's right Anon 7:09PM. Nilikuwa nikimzimia sana Rashid lakini naamini wakati umefika ku-hang up na kusaidia vijana chipukizi.
ReplyDeleteBlessings
Jamani akina anon hapo juu nawashangaa sana. Iwapo Matumla ataning'iniza gloves maisha yatakuwaje? Bongo jamani hali ngumu. Hizo ngumi ndiyo ajira yake na ndiyo zinazompa mkate wa kila siku. Mwacheni apigane hata kama akifia ulingoni si basi bwana kitaeleka mbele za Mungu. Matumla, Rashid endelea kujipatia riziki. Mambo ya kuishiwa speed ni mengineyo.
ReplyDeleteMdau
Mi macho yangu yameona kwengine kabisaa, naona siku hizi kama anajichubua?! au ndo umaarufu tena?!
ReplyDeleteWanapigana lini. Manake inabidi warudi Gym haraka sana. Wote hao hawafananii hata kama wanazidunda ngumi. Hebu muone huyo mwenye shirt la bluu alivyokunja ngumi msuli haupo kabisa.
ReplyDeleteBila Gym show itakua kama ya amature fights tu.
Sasa jamani aanze kuwa mkabaji mitaani? si bora apigane hadi afie ulingoni. pengine hakupata ushauri huo wa kuwekeza tangu mwanzo. Waliojidai ni wadhamini wake waliishia kujitajirisha wenyewe. Ila mi naamini Mungu atamsaidia. Wenyewe wamwona jamaa aliesimama nyuma Rashid, jamaa anaonekana chapombe mzuri, hapo anasubiri mshikaji aingie ulingoni, uongo mbaya uhakika wa kutandikwa kilaji utakuwepo hata kama jamaa atapigwa, si atalipwa tu. ni mtazamo.
ReplyDeleteMATUMLA TUNAMPENDA ila SASA GLOVES CHINI bwana Aliyesema maisha, lazima wazamini wake wajue kumfundisha na kazi zengine bora atafute kazi nyengine hata kufunguwa sehemu kufundisha vijana alafu analipwa. kuliko umri huo kwendak upigana then mwisho matatizo ya akili naamini Umri wa matumla ni 42 kwenda juu najuwa nje Holyfield kina George mpaka 50 wamepigana ila wale mambo yao si mabaya sana na wanaowatizama. plz matumla tunakujali achia tu.
ReplyDeleteACHENI JILASI
ReplyDeletei hate this game (masumbwi)
ReplyDelete