Hello Kaka Michuzi,
Heri ya Mwaka Mpya 2009!
Mimi nimekuja hapa Ujerumani kwaajili ya kusherekea Christmas na tulipoenda Supermarket kwaajili ya kununua bidhaa pamoja na mafataki kwaajili ya kusherekea kuukaribisha Mwaka mpya tukaona hili fataki lenye nembo ya Mlima Kilimanjaro.
Mimi nilifurahi sana kuona na tulinunua. Nimekutumia picha hii iliyokwenye nembo ya fataki lilo. Labda ni kawaida na labda mafataki ya aina hii yanauzwa Tanzania pia lakini mimi nimeshangaa sana kuona.
Tena utaona hata maneno yameandikwa kijerumani. Sina uhakika kama watu wengi huku Ulaya wanafahamu Mlima kilimanjaro uko Tanzania au wanajua tu uko Afrika. Picha ya pili ni baada ya kuliwasha fataki hilo lenye nembo ya Mlima Kilimanjaro.
Heri ya Mwaka Mpya 2009 kwa Watanzania wote.
Ni mimi
Andrew Ferdinands

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Mimi mkenya lakini nyie watanzania hamna chakufanya.
    Hata mkipewa huo mlima kilimanjaro na mombasa mtaendelea?
    Munasema mna kila kitu kuanzia madini mpaka sijui nini lakini uchumi wenu dororo na hamna mnakokwenda. Mwendo wa kobe una afadhali. kama hio shilingi yenu ndio iko taabani.
    Kenya mwatusema twauana kwa kabila sasa nyie mwauana kwa ngozi za kizerule, upuusi mtupu.
    mengine yakusema mnasahau mwaibiwa haki zenu lakini mwazisahau mnaoona ni mlima kilimanjaro tu ambao unaonekana kila siku na huwezi kuuhamisha ulipo.
    amkeni wenzetu.

    ReplyDelete
  2. Huyo jamaa wa kwanza anachefua lakini namshukuru, ametupa changamoto. Nachoweza kumwambi kwa haraka ni kwamba mjadala juu ya ardhi yetu na EAC tumefunga!

    Balozi, marketing strategies i.e ubunifu kwenye matangazo bado unatuangusha sana. Tunapiga kelele kila uchao kwamba nembo kama hiyo ya KILIMANJARO iwe na mahali panaonyesha TANZANIA.

    Hili ni tatizo sugu kwenye matangazo hasa ya kitalii. TANZANIA 'INYANYULIWE.' Ukisema Ngorongoro, ukasema Kilimanjaro, ukalia na Serengeti... kama hujaainisha kuwa viko TANZANIA bado zoezi la kuitangaza nchi yetu na kuinua pato kwa tasnia ya utalii bado ni tatizo.

    Heri ya Mwaka Mpya 2008.

    ReplyDelete
  3. Mwaka mpya wa 2008!?
    Mwenzetu unakwenda kinyumenyume

    ReplyDelete
  4. we mkenya unaumwa nini mbona juzi mmepigana wenyewe kwa wenyewe mpaka tukaja kuwasaidia , pua we

    ReplyDelete
  5. Tatizo lenu wakenya mnaukondea sana mlima kilimanjaro, na mmejaribu sana kuufanya uwe wa kwenu mmeshindwa,majangili wakubwa nyie kwanza ndio mnaongoza kuja kufanya ujambazi TZ kwetu.Shilingi yenu ipo juu huku mnazidi kuuana hamna lolote. Jamani hawa wadau wanatangaza hizi nembo wajaribu kuandika na nchi kama vile KILIMANJARO - TANZANIA. hizo ni salaam zako we mjaruo

    ReplyDelete
  6. Tatizo kubwa la wakenya wana uroho wa fisi, wakiona kitu chochote kwao ni biashara wale, imefikia washamaliza kila biashara sasa wananusa na kwa majirani tushike wapi ili tupate, kwani ile biashara ya wizi wa kupakia kwenye makontena maelfu na maelfu ya viumbe vitambaavyo na kupeleka nje iliishia wapi? au mmeshawamaliza wote sasa mnanusa na huku kudowea akiba zetu za vizazi vijavyo navyo mkombe. mwezi wa Sept. vyombo vya habari vilitangaza makontena yameshehenezwa wadudu mtu binafsi anawapeleka ujerumani kuwauza HaHaHaaaaaaaa. uroho kitu? mnajiibia hata wenyewe, toeni boriti kwanza kisha mje mkague kibanzi kwetu waroho wa kutupwa nyie. Nyerere alijisemea waache wenyewe watanzania watasoma na watajua namana ya kutumia rasilimali zao .Namalizi usemi wako POLEPOLE YA KOBE HUMFIKISHA MBALI, ukae ukijua Mmalagoli wewe.

    ReplyDelete
  7. Ni mimi tena mkenya
    Nasema mnashindwa issue ambazo ni muhimu kwa wana jamii mnaongelea tu Kilimanjaro
    Ey nyie watanzania huo mlima Kilimanjaro hatuwezi kuuiba nakuuhamisha Kenya nchi yetu nzuri, upo hapo hapo.
    Nikweli Kenya tuliuana wenyewe kwa wenyewe kwakutafuta haki yetu.
    Nyie mtakaa hivyohivyo mpaka suruali zenu zinatoboka matakoni huku mnaibiwa na wakubwa wachache.
    Kenya hio upuuzi hatuitaki. tunataka kwenda mbele na sio kurudi nyuma. nasema tena shilingi yenu na uchumi wenu umedumaa kwa kutojali haki yenu bali kuongelea Kilimanjaro tu ambayo hio mlima iko pale pale.

    Na kuhusu kuuana tuliuana kwa kutaka haki iwe Kenya.
    Nauliza hao mazerule mnawaua mpate haki gani?

    ReplyDelete
  8. yes Mkenya hapo umenena,
    we are always thinking about our mountain crying everyday that Kenyans are taking it and nothing is done with our tourism board to advertise what is rightfully ours...!!; natural resources and everything, in reality Tanzania has much more to offer than kenya but actually Kenyans are ahead of us and will remain there until someone put sense in our government to wake up and stop this loot maybe not the government but ourselves...., our blah blah, although gone are the days where we are fighting and killing in the name of democracy; but i like teh fact that Kenyans are bold enough to speak openly and furhtermore ministers in the same party can differ openly with the presdoo hakuna kulindana wala kujuana.. yes i like that for Kenyans, as for Albinos that is a national calamity which we all have to put a stop to it, it is a natioanl shame; like it or leave it, we are and i am shamed by this issue !
    now do i hear someone shout "traitor" at me ?? on this issue.. so be it.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...