Nimepokea barua pepe toka kwa mhisani wetu mkuu, Mwanzo Park Lodges, sehemu ya barua pepe ile yasema hivi:


"Ndugu Mwenyekiti wa Fotobaraza, Salamu kwako.Napenda kutoa ofa/shavu/mwaliko kwa mmoja wa mwanakijiji wa kijiji chetu cha Waswahili mtandaoni, kushiriki nasi usiku wa Maakuli ya Kiafrika, siku ya tarehe 31/01/2008.

Mwanzo Park Lodges pia itagharamikia malazi ya mwanakijiji huyo mteule. Hii ni sehemu ya shukrani zangu kwa kijiji kwa kunipokea kwa mikono miwili, wa kulia na wa kushoto. Tafadhali nipatie jina la mwanakijiji huyo kabla ya Alhamisi jioni ili tujiandae kumpokea ipasavyo. Naomba kuwasilisha.

Peter Vava,
Mkurugenzi Mtendaji,
Mwanzo Park Lodges"

Fotobaraza inatoa shukrani nzito kwa Mwanzo Lodges. Nasi tunaweka 'kachumbari' kwa mwaliko huu. Kijiji kitagharamia usafiri wa kutoka Dar es Salaam hadi Mwanzo Park Lodges na kurudi kwa mteule wetu.

Pia tutagharamia vinywaji ila si vileo. Mteule pia atapata wasaa wa kukutana, kuzungumza, na kunyuka mifoto na Mkurugenzi wa Mwanzo, Mwenyekiti, pamoja na mama Mwenyekiti.

Pia atapata wasaha wa kufanya ziara kwenye mazingira murua ya Mwanzo Park Lodges, asubuhi ya tarehe 01/02/2008, kwa heshima ya Mkurugenzi mwenyewe.

Safari ya kuelekea Mwanzo Park Lodges itaanza saa nne asubuhi ya tarehe 31/01/2008 na mteule atarejea jijini siku ya tarehe 01/02/2008, saa sita mchana.

Tafadhali ndugu mwanakijiji, kwa heshima na taadhima, tunakuomba upendekeze jina la mwanakijiji ambaye ungependa achukue shavu hili la kwanza katika kijiji cha FotoBaraza. Jina litalako jirudia mara nyingi ndio litakalochaguliwa.

Mchakato utafungwa Jumatano ijayo saa sita usiku na mshindi atatangazwa Alhamisi ijayo saa tatu asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki.

Hairuhusiwi kupendekeza jina lako mwenyewe, ila kampeni ya nyumba kwa nyumba inaruhusiwa. Pendekezo la wanakijiji ni la mwisho. Pia ikumbukwe mashavu/ofa zingine kabambe ziko njiani.

Pamoja!
Mdau Bob Sankofa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Yes! Fotobaraza oyeeee!

    KILI
    Bulgaria

    ReplyDelete
  2. Nadhani tarehe iliyopo kwenye email imekosewa!

    ReplyDelete
  3. Aminia FOTOBARAZA,,,, babu big up

    VADONDE
    Kwa Chavez,,,,,,

    ReplyDelete
  4. Michuzi kitu unachonifurahisha ni kutokuwa na tabia ya kiswahili ya kuwabania bloggers wenzako.

    Kwa hilo nakupa big up sana Kaka.
    Ubarikiwe.

    ReplyDelete
  5. 2008 imepita ama mimi ndiyo nimelala???

    ReplyDelete
  6. Hivi wee mdau HUO NDIO UNONO HUO?au ndio umetoka tu usingizini kuamka ukaona kuna internet ukaamua ututumie tu ulichojisikia kukituma??anyway nina swali 1 tu kwako?SWALI..hii tunayoishi ni karne ya kumi na ngapi kwani huko ulipo mwenzetu?maajali yote haya ya barabarani leo UHONDO ikawe kusafiri na basi kutoka dar hadi mwanza kwenda na kurudi kisa ukalale hotel tu usiku mmoja.AMA KWELI UMETUCHOKA loool

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...