Michuzi na Wadau,
NI MIMI STELLA
Nashukuru sana kwa wote mliochangia wengi mmenipa ushauri mzuri sana, na kunitia moyo na kuna ambao mnanikandia kuwa nilimtosa baba mtoto wangu.
Hivi nyinyi mnaosema eti nilikuwa na mapenzi ya kinafiki kwake sababu tu nilikataa kubadiri dini?sasa kama unampenda mtu kiasi gani sio kila atakachokuambia ufanye lazima ufanye sababu unampenda akikuambia muue mama yako au baba yako utafanya? eti sababu unampenda? waliposhindwa kwa wazazi wangu unajua wangepanga kunifanyia nini mimi?
Natoa ufafanuzi kwa hilo mimi sikumtosa hamjui ni kiasi gani nilikuwa napata presure kutoka kwa wazazi wake,mwanzo makubariano yetu na mwenzangu hayakuwa mimi nibadiri dini ilikuwa kila mtu ataendelea kuwa na dini yake, na hamjui kwa mtu aliyekulia katika familia isiyojihusisha na mambo ya ushirikina inapofikia mtu anakuja kwako na kukupa ushauri eti ufanye kitu kama hicho tena kwa wazazi wako mwenyewe?utajisikiaje wewe?
kilichonikasirisha mimi niyeye mwenzangu akawa upande wao na kunishauri nifanye hivyo hapo ndio nilipopata picha kuwa huko tunakoelekea sio kuzuri,sababu alianza kuegemea upande wa wazazi wake hata mtoto wangu alipozaliwa walimletea hirizi eti nimvarishe nikaichoma moto.
Sikilizeni yaliyomtokea mwenzangu sasa mdogo wake alipata mkristo kama mimi na yeye alikubari akawafanyia kaka zake waligoma na wazazi wao walifariki yeye akiwa mdogo, ameishi na huyo shemeji yangu huu mwaka wa 11 hawajawahi kupata mtoto wakawa wanampeleka kwa masangoma kuna kipindi alishika mimba nasikia ilikuwa ni mapacha sasa si mimba za waganga hayo madawa aliyokuwa anakunywa yalimzuru mimba ikatoka ndipo ndugu zake wakagundua kuwa kuna dawa alikuwa anatumia ndio zimesababisha, na hajashika mimba tena!
sasa nasikia wazazi hao hao wanamtaka mtoto wao aowe mke mwingine huyu mwanamke hazai, na huyo shemeji yangu anamtoto nasikia kazaa na mwanamke mwingine.
Huyu bwana niliyenae bado mapenzi hayajabadirika anajitahidi sana kujifanya kama hakuna kitu kinachoendelea na hata jana kuna marafiki zetu walikuja akawa anawaonyesha nyumba yetu inavyo onekana kwa sasa baada ya kumaliza ujenzi na kuwakaribisha wakitaka kuja holiday bongo.Lakini mambo yote nasubirij'3 kama wengi mlivyonishauri ntaongea nae tu kwa upole.
Asanteni saaana kwa ushauri wenu,
mwanzo nilipanick sana.
Mdau Stella

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 44 mpaka sasa

  1. Stela, unaongea manaeno ya mtaani ya uswahilini hasa. Kwa nini mambo kama hayo yanakupotezea muda?

    ReplyDelete
  2. Inaonekana umesoma lakini hutumii kisomo chako kufikiria.

    Tatizo kuna vijimambo vya manzese vina-consume akili yako bure (mara waganga, mara hirizi, mara sijui nini huu ni uswahili tuu)

    ReplyDelete
  3. Da stella nimesoma issue yako kwa makini na uangalifu mkubwa.Kitu ninachokushauri mimi ni kwamba don't make a decision based on your emotions feeling,unahitaji kuwa mtulivu sana then tafuta siku ambayo hata hisi kwamba unafanya vitu ambavyo huwa hufanyi example to be extra nice to him, sasa hiyo siku mwambie kwamba unajuwa kila kinachoendelea bila jaziba wala nini na ukishamaliza mwachie yeye ajikaange mwenyewe kama ni desion mwache afanye mwenyewe na baada ya kumwambia endelea kufanya kila ulichokuwa unafanya bila kinyongo nakuhakikishia atakuwa guity for the rest for his life na atafanya amendment for a broken heart.

    Mdau wa Gamboshi-Bariadi

    ReplyDelete
  4. Inabidi wanaume tuwe makini, especially vijana ambao hatujaoa...hii message ya huyu dada imenipa mawazo mengi kuliko majibu... YAANI HUYU DADA INTERESTS YAKE NI MALI TUU? Hana mapenzi na huyu baba..Honestly.....Inawezekana kweli na mwanaume kakosea..lakini wewe inaonekana interests yako ni hiyo nyumba na "container". Dada kama kweli una upendo wa dhati kwa huyo baba..ungemuuliza maana naamini kabisa na yeye ana upande mwingine wa story hii. ..kwani ni mara ngapi wapendanao hukosea? ila wewe unaogopa kisa..container halitashuka Dar?....wewe unaona uvumilie kusudi container liende..duh..nachoka na hizi ndoa za siku hizi!

    Anyway ni mitizamo tofauti ya kimaisha. Kwa hiyo container likishafika Dar? akileta za kuleta utampiga chini..after all uko wenu yeye ni foreigner? Inauma..najiweka kwenye viatu vya huyu mshkaji naona kabisa this is not fair! Maana mpaka kuamua kujenga kwenu ni kwamba "mnapendana" Unafikiri angeshindwa kukomaa mkajenge kwao? ila wewe unaona mambo yote ni nyumba na container..Dada Stella..maisha siyo mali tuu ndugu yangu..ni majumuisho ya vitu vingi.

    Nakutakia heri katika hiyo ndoa, kama itakuwepo.

    May the Good Lord Love YOU All!

    ReplyDelete
  5. Stella pole na hongera ulivyojitoa kwenye hiyo familia nikweli hata kama ningekuwa mimi kwa mtaji huo ningeshindwa.

    Sasa nyinyi hapo wachangiaji mnamsakama bure mimi nilivyomuelewa ni kwamba katoa ufafanuzi kutokana na kwamba watu wamemshambulia kuwa alimtosa yule kaka mmbongo, inaelekea hiyo familia ya huyo kaka wa kibongo niwashirikina sana,dada bora ulivyo mtosa sio kosa lako nakuunga mkono kabisa acha waosha vinywa waoshe lakini mimi nimekuelewa vizuri.
    mdau Canada.

    ReplyDelete
  6. Michuzi na wewe hebu wacha kuweka huu upuuzi tuwekee mambo ya maana sisi man huwa unatutafuta tusema uanze kuweka mkwala wa comment zetu kutoona mwanga wa jua kisa tuu wewe ni controller wa Blogu yetu, hebu achana na huyu dada Kubwa jinga ! Miaka 43 lakini anaact kama vile mwanangu wa miaka 7 lol!

    ReplyDelete
  7. DADA YANGU INAONESHA SIO MTU MZURI KABISA MAANA INAONESHA UNACHOJARIBU KUMJENGEA HUYO MWANAUME WAKO WA MWANZO TUMUONE NI MBAYA!!WEWE NIMTU WA KULIPA MAZURI KWA MABAYA!!SAWA UNACHOTAKA KUTUONESHA KUA HUYO JAMAA YAKO ALIKUA MSHIRIKINA NA NDIO SABABU YA WWE KUACHANA NAE!MBONA KATIKA KUANDIKA KWAKO MWANZO HUKUANDIKA ULIACHANA NAE KWA SABABU HIYO?HAKUNA LISILO PINGIKA KUA HASA KATIKA UISLAM MWENYEZI MUNGU AMEKATAZA SANA USHIRIKINA!HAPENDI WASHIRIKINA BUT JE WWE ULIMSHAURI NA KUMLINGANIA HUYO MPENZI WAKO?KAMA KWELI ULIKUA UNAMPENDA?
    INAONESHA ULIAMUA KUACHANA NAE KUTOKANA NA WWE KUA NA TAMAA YA MALI NA NDIO MAANA ULISUBIRI KWANZA UONDOKE NA UFANIKIWE
    PIA HAO WACHAGA WANAOKUSHAURI SUBIRI CONTANER,TUNAJUA KUNA JAMII ZA POLINI HAZINA UTU UTU KWAO NI MALI ULIZONAZO NA NDIOMAANA HAWAKUSHAURI KITU ZAIDI YA KUFIKILIA MALI KULIKO UTUWAKO
    PIA HAO WANAOMSINGIZIA YESU SIJUI KAFANYAJE!!UZUSHI MTUPU!MUNGU ALISHAKEMEA ZINAA KTK UISLAM ALISHAKEMEA HATA KUIKARIBIA ZINAA,ALISHASEMA MZINIFU ATAMUOA AU KUOLEWA NA MZINIFU MWENZIE,SASA WWE NI MZINIFU UMEMSALITI MPENZI WAKO WA MWANZO SASA MUNGU ANAKULIPA HAPAHAPA INGAWA HUKUTUSIMULIA NI JINSI GANI MWENZA WAKO WA MWANZO ALIUMIA KIASI GANI MAANA WWE NI SELFISH NA NDIOMAANA UNAJARIBU KUMJENGEA PICHA MBAYA KWETU!!KWAMAANA UNAJUA WAZI DINI ZINAVYOPINGA USHIRIKINA
    PIA HAO WANAOTAKA KUHALALISHA ZINAA ETIWANAUME WOTE WAKO HIVYO SIKWELI ILAJAMII NDIZO ZILIZO OZA HATUFATI MUONGOZO WA DINI YA KIISLAMU INAVYOTAKA NA NDIO MAANA MUNGU ANATULIPA HAPA HAPA ALISHASEMA ADHABU ZITAANZIA DUNIANI KABURINI NA AKHERA!!
    PIA USIUZE UTU WAKO KWA AJILI YA MALI,KAMA MWANAUME ANAKUPENDA ASINGETOKA NJE,TENA INAONESHA AMEANZA MUDA MREFU

    ReplyDelete
  8. Acha ujinga wewe kama umeamua ku-move on just do that!!
    Why discuss your issues hadharani?

    ReplyDelete
  9. KWA MTAZAMO WANGU ANONYMOUS WA KWANZA NA WA PILI HAPO JUU NASHINDWA KUWAELEWA YUHU DADA HAYO MAMBO YA USWAHILI NA UMANZESE MNAYOYASEMA SINDIO HAYO YALIYOMSHINDA?SASA HAPO MNAMLAUMU NINI?KAWEKA WAZI SABABU WATU WANASEMA ALIMKOSEA YULE BABA MTOTO WAKE,NAZANI MAELEZO YAKE YAMEJITOSHELEZA NI USWAHILI NA USHIRIKINA NDIO VILIMSHINDA.
    POLE SANA STELLA HUKUFANYA MAKOSA KABISA KUACHANA NAE ILA NAKUSHAURI MTANGULIZE MUNGU KWAKILA JAMBO ATAKUONGOZA TU.

    ReplyDelete
  10. eeeh dada wee,kutoa siri zote imehusu nini?

    ReplyDelete
  11. Nakubaliana na nyie akina anony hapo juu, huyu dada ana mambo ya uswahilini sana. Kama hukutaka kubadili (siyo kubadiri kama anavyoaandika) dini si ungeachana tu na huyo jamaa yako? Halafu stori yako haijatulilia kabisa kuna mahali unasema nyumba imekamilika hadi huyo basha wako akawa ana waonyesah amarafiki zenu halafu kwingineko unasema mnaendelea kujenga sasa hapa kipi ni kipi. Mwisho unasema ati bado ana mapenzi sasa unacholalamika ni nini? Ndoa si nikupenda na wewe unakiri anakupenda. Umeshakuwa mtu mzima umezaa watoto miaka mitano na mbongo miaka nane na huyo mgagigikoko jumla miaka 13 maana yake umesha onja maisha ya ndoa. Grow up girl (lady?)

    ReplyDelete
  12. Pole sana dada Stella kwa songo mbingo zote hizo. Pamoja na mwengi yaliyokupata na labda na kuchemsha wakati mwingine katika maamuzi yoko ila lile la kukataa kubadili dini ni jambo jema sana na la busara ulilofanya kuliko yote. Shika dini yako mama na hata haya yote yanayotokea sasa yakabidhi yote kwa YESU na ushike imani yako. Machafuko katika maisha yapo la maana ni kumtumaini MUNGU tuu. Kama MUNGU akikusimamia, jamaa atatulia na ndoa itakuwepo tena nzuri sana na watoto ataendelea kucheza nao kama kawaida. Rudi kwa MUNGU wako umlilie shida zako.

    ReplyDelete
  13. HEBU TOENI UPUUZI WENU HAPA!!WAJINGA NDIO WALIWAO NA NDIO MAANA MKIINGIA MJINI MNATAPELIWA KABLA HAMJAWA WAJANJA!!
    ETI NA WATOTO ATAENDELEA KUCHEZA NAO!!
    HAMJUI KAMA HIYO NI ACTING TU!!SIKU ZOTE MATAPELI NDIO WALIVYO WANAINGIA NA GIA NZURI SANA YA KUWALAGHAI WARUGARUGA KAMA NYINYI,MATAPELI SIKU ZOTE NI WAPOLE NA WANYENYEKEVU BUT NI BALAAA!
    SIKU ZOTE NDIPO MNAPO HARIBIKIWA WAKINA DADA WAKITANZANIA KUPENDA KUPEWA FADHILA NA NDIZO ZINAZO WACOAST SANA.
    KATIKA MAISHA YAKO MWANAMKE INABIDI UMWOGOPE SANA MWANAUME ANAYEHONGA NA KUKECARE SANA UJUE ANAKASORO.
    PIA HUYO DADA YAMEMPATA YA WHAT GOES AROUND WHAT COMES AROUND KATIZAMENI KWENYE BIBLE NA QURAAN TUKUFU!HAYO NIMALIPO ALIYOMFANYIA MWENZA WAKE WA MWANZO,MUNGU ANAJARIBU KUMWONESHA NAMNA ALIVYOMFANYA MWENZIE NAKUMPA PICHA AACHE USELFISH
    WAPUZI WAKUBWA MNAMSHAURI ABAKI KWENYE KABURI HILO!!LEO JAMAA ANATOKA HAKUPATA MARADHI KESHO AKIJANAYO JE?MKUMBUKE KAMA MMELIMIKA CONDOM HAIKING ASILIMIA MIA.
    KIMBIA DADA YANGU HATA NYUMA USIGEUKE!UNAJUA DADA YANGU KUNA JAMII HASA ZA NCHI NYENGINE WANAWAKE WENGI NI MATERIALIST NA NDIOMAANA NA WANAUME WAO WANAJENGEKA KTK MISING HIYO!!KWA HIYO DADA ZETU TULIOKUA NAO HUKU NA KUTOKUA NA EXPOSURE WANAONA WAMEFIKA!!KWA HIYO NAHUYO JAMAA INAWEZEKANA AMESHAISOMA SIKOLOGIA YA DADA YETU NAKUWAJUMUISHA WALEWALE

    ReplyDelete
  14. MIMI NAONA HUYO MWANAUME UMCHUKULIE KAMA ALIVYO. KWANZA ANAKUHESHIMU HATA KAMA ANAENDA NJE YA NDOA. NASEMA HIVI KWASABABU ULIMPATA AKIWA SI BIKIRA. ALIKUWA AMESHAMWACHA MKE MWINGINE. JE, ULIPATA UHAKIKA 100% WA KUWA YEYE HAKUWA MBAYA KWA KUACHANA NA MKE WA ZAMANI? KAMA UKIFIKIRIA HILO, UMOENDE KWA VILE ALIVYO. MAANA HAWEZI KUANZA UMALAIKA KWAKO TU WEWE. CHA MAANA ANAKUHESHIMU, ANAKUPA KINACHOTAKIWA. HALAFU KUWA NA KONDOMU NI VEMA TU, ANAONYESHA KUWA ANAKUJALI WEWE, NA YEYE PIA. JE, USINGEIONA KONDOMU WAKATI ANA WANAWAKE NJE, UNGESEMAJE. UNGEFURAHI UFE TU? PIA HATA WEWE NI MKE WA KUKUOGOPA, MAANA HUJAENDA NAYE KWA MSHAURI YEYOTE WALA NDUGU YAKE MSHAURIANE, NA UMELETA KWETU KWENYE BLOG HADI MAMBO YA KONDOMU. KUNA 'PRIVACY" HAPO KWELI? MTU MWENYEWE HAJASHINDIKANA UKIZINGATIA. WALAHI AKIJUA ULIVYOMFANYIA, NAYE HATAKUONA KAMA WEWE UNA BUSARA, ATAKUOGOPA NA KUKUACHA.

    DADA USIWEKE MKUKI KWA NGURUWE, IKIWA KWA BINADAMU MCHUNGU.....

    Mdau wa USA

    ReplyDelete
  15. Huyu dada utafikiri anatafuta deal ya kitabu.Majambooz umeshayaacha sasa kelele za nini,wewe changanya malapa yako na anza mbele.Siri ya mwenzio usiitoe kwani yeye hajatoa yako au wewe ni 100% perfect?.Kuishi pamoja ni kugumu na kunataka uvumilivu na kusitiriana, na kusameheana.Nakushauri umwombe msamaha kwa haya yote uliyoyasema.Mwisho nakuuliza wakati mnapeana raha mbona yote haya hayakuwepo?

    ReplyDelete
  16. Huyu dada angekuwa na akili alitakiwa baada ya kupata makaratasi amkumbuke mzazi mwenzie ambaye alimsaidia kwenda huko UK. Amvushe ili waachane na influence za wazazi.

    Ukitaka kujua ni wa pesa, kamsahau kwa ajili ya pesa. Na usikute hata hizo karatasi katengezewa na jamaa wake wa sasa ndo maana kamtosa jamaa wake wa zamani. Wanawake twawajuwa saana.

    We dada huna shukurani na fikra na usiponyooka kichawani utaishia pabaya.

    KUMBUKA WIMBO WA "KANITOROKA MPENZI WANGU"

    Mtoroke na huyo jamaa wa pili, maana we umeshafuzu katika hilo.

    Japo umejitahidi kuonyesha mzazi mwenzio wa mawanzo ni mbaya lakini inaonyesha ubaya wako huuoni.

    We dada ni komando saana. Hivi ulienda kusoma digrii au satifiketi tuu?

    ReplyDelete
  17. Dada Stella,
    Samahani kama narudia yaliyosomwa. Asubuhi nilisoma habari zako lakini kwa bahati mbaya nilikuwa natakiwa nifanye kazi. Kwa hiyo ndio namimi natoa mchango wangu. Mimi nakupa pole sana kwa yanayokukuta maishani mwako sana. ndoa ni jambo tamu na mimi niko ndani ya ndoa na ndio maana nasema ni tamu sana. kwanza nikupe pole kwa hayo ya huko kwa mpenzi wako muislamu. Yamewatokea dada zetu wengi na wameishia pabaya zaidi ya waliyokuwa wakitegemea. Wengi waliojiingiza kuolewa na waislam na kubadilisha dini, nina mfano wa dada wengi ambao badaka ya kuyafurahia maisha waliingiwa na mashetani. na usilamu mara zote umekuwa ukiendelezwa kwa kushurutishwa na kuogopeshwa. Ningeweza kukutumia resolution ya kuala lumpa ya mwaka 1998, utashangaa.
    Pili, unajua kwa vile huyo mtarajiwa wako alikuwa ashazaa na girl friend wa zamani, hata kama hawana mahusiano ya kimapenzi, kwa vyovyote watawasiliana tu. Hata mimi kabla ya kuoa nilikuwa na girl friend, na hatukuachana kwa vita, ni mambo fulani fulani ambayo hatukuelewana, na hata kama tungekuwa tumeachana kwa kugombana, so long we had shared good times together, we communicate. Mimi nakuambia sina mahusiano ya kimapenzi na mwanamke mwingine yeyote, lakini kusema kweli ili kuhakikisha kuwa mke wangu hapati presha na kutia doa ndoa yetu, mawasiliano ninayoyafanya na my ex girl friend yanafanyika kwa siri. Huenda mumeo mtarajiwa anajua kuwa una wivu sana na ndio maana anakuficha mawasiliano anayofanya na mpenzi wake wa zamani. Mimi nakushauri uolewe kwa sababu, hata yeye mpenzi wako anataka kupata heshima ya kuwa mume wa mtu kama na wewe unavyotaka heshima yako ipande kuwa wewe ni mke wa mtu na wala sio mtu wa kukaa na wanaume tu. Nina uhakika kuwa nawewe ukienda Daa unaweza ukawa unawasiliana na baba mototo wako ambaye ni mpenzi wako wa zamani huyu muislam. Na unaweza mawasiliano mengine ukayafanya kwa kujificha.
    Mwisho, napenda upuuze watu wanaokuvunja moyo kwa sababu wewe ninavyoona hoja yako wewe sio mhuni. Kuna watu wengine hapa wameshakuwa na wapenzi mia kidogo na hata waliotembea nao hawawezi kuwalist kwenye daftari la kurasa 100. Nakupa moyo, olewa na usije ukajifikiria kuwa wewe ni mhuni hata siku moja na hujakimbia mwanaume. By the way, marrying somebody who is not of your religion is unacceptable before God, because by doing so, you tell the world that there is somebody who is above Heavenly God. We commit sin everyday, but it is bad to commit sin openly as you will be the partaker of the sin that somebody else will commit because of your open sin.
    Be blest

    ReplyDelete
  18. Hela alizotumia mshefa wako wa zamani uli ukiwini nae awini utamlipa? Au unamwaga kimoja na kutuonyesha yeye ni mbaya saana kwa sababu hana imani kama yako?

    Kumbuka, anayekusaidia katika elimu ndo anakupa mtaji bora kuliko yote.

    MUNGU HUPENDA HAKI.

    Hata kama jamaa alikuwa an vitabia vya kishirikina, haiwi kwake halali kudhulumiwa. Kama ana dhambi, Mungu ndo atayemwadhibu siyo wewe.

    USIJEKUWA NDO UMESHAANZA ADHABU YAKO YA DHULMA.

    ReplyDelete
  19. bora umrudie jamaa wako wa zamani.

    Wacha siasa kali za kidini.

    ReplyDelete
  20. Msimlaumu Stella kuandika hapa habari zake...hatumjui naye hatujui ...tunamshauri na kumsahau...mara ngapi tumeshirikisha watu tunaofikiri tunawaamini/marafiki wa karibu kutaka ushauri wa mambo fulani halafu unayakuta yamezagaa kila kona?? Stella umefanya jambo jema.
    Haya yatapita !!! Ni mapito tuu...!!!

    ReplyDelete
  21. Kizuri cha jiuza kibaya cha jitembeza. Blah, blah, blah, blah miaka 43 bado ujaolewa unazalishwa tu. Oh, sitaki kubadilisha dini, una dini gani wewe. Ukristo ndio unakuruhusu kuzini zini.

    I'm really sorry for the guy, he is in the hook, you got all he earned back in Tanzania. Now you ask us to help you to finish him off.Pretending you are a victim looking for our sympathy.
    The sad thing is you painted your ex Bongo man and his family as the monsters, mmmmh , I smell fish here.

    You are materialist soulless individual, you duped the Bongo man,lied to him with your bad intention of running away from him.
    Now you tell us about this Mpopo of yours. Hey, this is karma, whatever goes around comes around. you're gonna be paid whatever you did to that ex tanzanian man of yours.

    Mdau USA.

    ReplyDelete
  22. STELLA MTU ALIYECHANGANYIKIWA HASEMI.

    HATA KUANDIKA KATIKA MTIRIRIKO KAMA HUU WAKO HAWEZI SEMA UNATAKA KUTUZINGUA TU.

    ReplyDelete
  23. We dada we. Chiriku si chiriku. Jamani wadao niambieni kama hii ni sentensi moja au vipi:
    ---------------------------------------
    "Sikilizeni yaliyomtokea mwenzangu sasa mdogo wake alipata mkristo kama mimi na yeye alikubari akawafanyia kaka zake waligoma na wazazi wao walifariki yeye akiwa mdogo, ameishi na huyo shemeji yangu huu mwaka wa 11 hawajawahi kupata mtoto wakawa wanampeleka kwa masangoma kuna kipindi alishika mimba nasikia ilikuwa ni mapacha sasa si mimba za waganga hayo madawa aliyokuwa anakunywa yalimzuru mimba ikatoka ndipo ndugu zake wakagundua kuwa kuna dawa alikuwa anatumia ndio zimesababisha, na hajashika mimba tena!
    ---------------------------------------

    Chonde chonde bibie.

    ReplyDelete
  24. Dada stela mi nakushauri mwombe sana Mungu, kuhusu hii ndoa yako unayoitegemea karibuni, Mungu anaweza yote.

    Ms GB

    ReplyDelete
  25. actual swala la imani ni sensitive sana kuliko watu wanavyodhani, uhusiano wa mtu na Mungu wake ni individual decison. huwezi vunja uhusiano wa mtu na Mungu wake kwa sababu flani flani za kidunia, yani umkosee Mungu umfurahishe mwanadamu, inatupasa tumtii Mungu sana,people hv to be careful with this.

    ReplyDelete
  26. POLE SANA DADA STELLA, PIGA GOTI MLILIE MUNGU ATAJIBU!!

    JIPE MOYO UTASHINDA!!! HAO WANAOKUPONDA ACHANA NAO, BADO HAYAJAWAKUTA KAMWE WASINGE ONGEA MAMBO HAYO!

    PAULO NA ANCILA WALIOMBA MILANGO YA GELEZA ILIFUNGUKA! OMBA BILA KUCHOKA MUNGU ANAJIBU MAOMBI!!! BWANA YESU AKUTANGULIE KATIKA KIPINDI HIKI. HAYO NI MAPITO TU NI KAMA MOSHI UPITAO ANGANI TU.

    FRIDA

    ReplyDelete
  27. nyie mnaosema analipwa hapa hapa kwa lipi? do we real know God? kama Mungu angekuwa ukifanya madhambi anakuangamiza papo hapo nani angebaki? ni rehema tu za Mungu ukitubu na kuungama basi Mungu anasamehe. ebu tuache mambo ya kusemeana mabaya hapa.its good kusema mazuri kwa wengine ndio blessings.

    mdau Dar

    ReplyDelete
  28. watu mnaupenda ukristo eeee??safi sana mana kila mtu ooooh ukristo sijui nini
    sasa na habari ndo iyo,,,

    ReplyDelete
  29. dada ya kikushinda huko njoo kwangu nipo Tanga mie mkristo nikuchune ulizochuna au vp nitamuwakilisha mbongo mwenzangu ulimtosa kwanza najua una mbongo pia huko UK anaekupa starehe huyo huja mtaja hapa au umemuacha tayari am wating for you madame

    ReplyDelete
  30. Huyu alyeandika: `kwanza nikupe pole kwa hayo ya huko kwa mpenzi wako muislamu. Yamewatokea dada zetu wengi na wameishia pabaya zaidi ya waliyokuwa wakitegemea. Wengi waliojiingiza kuolewa na waislam na kubadilisha dini, nina mfano wa dada wengi ambao badaka ya kuyafurahia maisha waliingiwa na mashetani.'' ana ajenda ya siri.

    Dini kama dini haijihusishi na mammbo ya kishirikina, ila sisi wanadamu kwa tamaa zetu ndio tunaofanya mambo hayo kwa kusingizia dini, na wakiona hayo, wale wenye mawazo finyu wanasema dini yao ndivyo inavyowatuma. Ni vyema tukasoma au tukauliza wasomi wa dini husika kabla ya kunyoshea kidole dini nyingine. Mashetani yanawatokea hata wasio Waislamu! Na kuna mifano yawaliolewa DINI NYINGINE, kutoka Uislamu wakapata matatizo kama hayo na mengine makubwa, hiyo yote ni mitihani ya Mungu.
    M3

    ReplyDelete
  31. Ushauri wangu kwa mlengwa ni kuwa umri ulio nao ni wakutumia busara. Umeishi na bwana wa kwanza, mkawa mnazini, na bahati nzuri alikutaka ufunge ndoa,ukakataa kwa kikwazo cha dini. Ni sawa, kwani hungeweza kuolewa na dini ya huyo bwana bila kuwa katika dini yake. Lakini cha ajabu kipindi chote mlichokuwa mkiishi naye hukulijua hilo mpaka ulipompata mwenye nazo!.
    Sasa umempata bwana wa imani yako, ulitakiwa basi, umshauri mapema kuwa unachotaka sio kuendelea kuzini, ila ndoa, lakini ukaona utamu wa zinaa ni bora kuliko ndoa. Nafikiri hata huyu jamaa uliyempata anaendekeza tabia hiyohiyo ya kuzini kwanza ndoa baadaye. Ogopeni sana tabia hii.
    Wengi wamekushauri `umwibie jamaa huyo halafu uishie’ Hilo sio jambo jema. Jambo jema ni kukaa na kuongea naye na kumpa ukweli na hali halisi, kwasababu miaka 45, unategemea nini tena? Ukatafute bwana mwingine mzini nayee, halafu baadaye mtafunga ndoa lini?
    Umri kama huo ni wakukaa na kutubu dhambi ulizozifanya mojawapo ni hiyo ya kusihi miaka mimgi bila ndoa. Sisi sote tuna dhambi ni ubora wa dhambi ni kutubia, au sio?
    Jingine, usimchukue bwana wako wa mwanzo kwa kuhalalisha hicho unachokifanya. Kwani hapo una dhambi za zinaa, dhambi za chuki, tama na sasa unataka kupata dhambi za wizi. Yeye kama binadamu anamakosa yake, likiwemo hilo lakuamini ushirikina, dini haikubali hilo. Kwa wanaojua Uislamu wanalijua hilo,ila kwa wale wenye ajenda za siri ambao huangalia matendoya wanadamu na kuyanasibisha na dini wanaweza wakasema yale waliyonayo kwa kujifurahisha, lakini wajue ipo siku watakumbana na Muumba.
    M3

    ReplyDelete
  32. Da Stella,
    Pole kwa yalikupata. Kwanza sali sana na ufunge kumuomba Mungu ufanye maamuzi mazuri. Pili, kama unampenda mchumba mwambie kila kitu ili ujue msimamo wako. Tatu, mwambie achague wewe au yule. Nne, kama ni wewe, je na wewe utaweza kusahau na kuvumilia? kama ni yule mwingine, carry on with ur life.ni ngumu lakini utafanikiwa.

    ReplyDelete
  33. STELLA ,IAM INTERESTED TO GET FEED BACK AFTER YOU DISCUSS WITH YOUR MAN,SO KEEP US INFORMED. ALL THE BEST

    NATI

    ReplyDelete
  34. KUNA WADAU WENGINE VICHWA MAJI SANA!YANI MTU ANAMSHAURI MWENZIE PUMBA MIKOJO KISA ETI DINI JE HIVYO NDIO UKRISTO UNAVYOFUNDISHA NA KUCHOCHEA ZINAA NJE YA NDOA?MAANA WENZETU WENGI WANAOJIITA WAKRISTO UKITIZAMA MAONI YAO YANAONESHA NGONO KWAO NJE YA NDOA NI KAWAIDA TU

    MFANO MCHANGIAJI WA TAREHE30 JAN SAA 4:05 AM.
    ETI NDO NI TAMU ALIEKWAMBIA KUA HUYO DADA KAOLEWA NINANI?
    ETI HATA AKITOKA NJE WE MVUMILIE,MPUUZI MKUBWA USIMLISHE PUMBA MWENZIO KISA UDINI AKIMLETEA UKIMWI JE?NYINYI NDIO MTAKUA WAKWANZA KUMKIMBIA NA KUMNYOOSHEA VIDOLE
    PIA SIO KWELI WAKINA DADA WALIOOLEWA NA WAISLAMU HUSHURUTISHWA UISLAM NDIO DINI YA KWANZA KUWAKOMBOA NA KUWAPA WANAWAKE HAKI ZAO;KABLA YA UISLAMU WANAWAKE NA WATOTO WAKIKE WALIKUA WAKIZIKWA WAZIMA NA KUNYANYASWA BUT UISLAMU ULIPOKUJA UKAKATAZA NA KUANZISHA HAKI ZAO
    PIA UISLAM UNAKATAZA VIKALI USHIRIKINA NA ZINAA IMEKATAZA HATA KUISOGELEA NA KUONESHA NI NJI ILIYOCHAFU KABISA,HAKIKA ALLAH ANACHUKIA WAZINIFU NA WASHIRIKINA
    MSIMPOTOSHE HUYO DADA KISA UDINI WENU MWAMBIENI ATUBU DHAMBI ZAKE!!
    ETI CONDOM PUMBAFU INAELEKEA HAMNA ELIMU KABISA ALIEWAAMBIA KUA CONDOM INAKINGA ASILIMIA MIA NI NANI
    WATS GOES AROUND WAT COMES AROUND MZINIFU ATAOLEWA AMA KUO MZINIFU MWENZIE.
    NYAMBAFU NA IMANI ZENU ZINAZO ALALISHA UZINZI NA KUTOKUA WAKWELI AMA KUTOKUA MASHAIDI WAZURI,HII TOSHA INAONESHA KAMA MNASHINDWA KUJAJI NA KUTOA MSAADA MZURI KWA DADA YENU MTAWEZA KUWA WAAMINIFU KWENYE NDOA ZENU?
    ALLAH ANACHUKIA WASHIRIKINA NA WENYE KUDHULUM NAFSI ZAO NA ZAWENZAO

    ReplyDelete
  35. Nakubaliana na Andy hapo juu. Nadhani stella watupotezea muda tu hapa. miaka 43 bado una haha na mapenzi, na wale wa adolescence age wafanyeje ikiwa umri huo bado unayumbishwa?
    wazazi wa bwana ulomtosa walikua na nia nzuri tu kua ubadili dini ili kuepuka kuzini. Ndoa za serikali hazitambuliwi mbele ya mungu ni hapa duniani tu my dear. kwa hiyo nia yao haikua mbaya, sasa wewe mpenda zinaa uliona kama ni tatizo. Kwani una shida gani wewe mpaka huyo chokoraa mlokutana kila mmoja akiwa na meno yake 32 akusumbue kichwa chako hadi kupelekea kusema mambo yako ya ndani kwa watu usowajua, mara uchawi, mara hiziri, mara mimba ya mapacha ikatoka, mara hajazaa mpaka leo, wewe pia mshirikana!!
    Naona wataka ukimwi kwa huyo unayeng'ang'ana naye sababu ya ma container na nyumba. Pole.

    ReplyDelete
  36. hivi dini au dhehebu linampeleka mtu kwa Mungu au peponi? i think not kama hatutendi mema mbele za Mungu ni upuuzi mtupu kukaa na kung'ang'ania dini zetu.

    ReplyDelete
  37. dini ya kweli ni kumcha Mungu na sio taasisi zilizosajiwa.

    ReplyDelete
  38. Nafikiri ulichotafuata umekipata "sympathy". Unajidai victim, victim ni yule aliyetumia hela zake kwako halafu ukamkimbia. Mkimbie na huyo.

    Halafu hao wanaosema utubu halafu utasamehewa. Je haki ya watu uliyokula iende bure?

    Japo wewe ni mkristo, uislamu unasema ukimkosea mtu katka mali, unamlipa na kumwomba msamaha ili asiwe victim wa vitendo vyako.

    ReplyDelete
  39. Stella Wacha unafiki Haina haja ya shemeji kafanya nini na kipi. Move on Endelea na maisha yako subiri uolewe na ambaye utaona atakufaa inaonesha hata wewe una problem si ndogo kuhusu hao mapacha kama si umbeya na ushirikina ni nini tena? kuwa kama mkristo nenda Kanisani omba soma unayoyaona yanafaa kama muislamu omba soma duwa omba swali fanya yanayofaa wacheni hisia fikra za ushirikina na unafiki manake hii topic uliyoweka ni UNAFIKI. Mungu akusaidie uwache kufikiria unaonewa.

    ReplyDelete
  40. we mama hivi huko uk hamna therapist? au huwezi kulipa mwenyewe mpaka mghana akulipie? tuondolee stress zako hapa. inaonyesha una stress na huna wa kumweleza. watu wamekueleza opinion za ss wewe unapandisha juu. kama hukutaka kuambiwa ukweli nenda kwenye therapist.

    ReplyDelete
  41. hivi huko uk ulikwenda ukasoma kweli? kujieleza hata kiswahili ni tabu. 43 yrs, elimu na kuishi majuu muda wote huo hujui good communication.

    wewe kila mmoja ni mbaya sijui ex gal hakupenda watoto, sijui hivi na vile wewe ndio mzuri tu.

    unatafuta sababu ya kumtosa huyo kama aliyesema hapo juu wewe umekufuzu na unachokua ni mali tu.....nilizania wewe mangi lakini na hiyo llll na rrrrr zako i doubt...

    watu wakipata makaratasi wanachukua wakwao wewe ulimtupa

    ongejiweka hadharani ili tuwashtue kaka zetu ...manale wewe sio black widow but you act like one

    ReplyDelete
  42. Anon wa January 30, 2009 10:57 AM, au M3. We unaonyesha ni mtu mwenye fikra na akili timamu. Unaangalia mambo kwa uhalisia.

    Watu wengi wanailaumu dini kwa sababu tu mtenda dhambi fulani kasema yeye ni dini hiyo.

    Lakini hamana dini inaamini mashetani, bali zinatambua mashetani wapo, na hakuna yeyote aliyepo ila aliumbwa (kwa hiyo ni kiumbe). MUNGU tuu ndo siyo kiumbe wengine woote hawakwepi hata kama ni malaika au mawe.

    TATIZO LA WATU WENGI NI USHABIKI NA UKOSEFU WA FIKRA.

    ReplyDelete
  43. UKIMWONA MWENZIO ANA HAFAI MANAKE HIYO NI TASWIRA ILIYOMO KATIKA UBONGO WAKE KUHUSU WEWE.UMESEMA SANA YA MWENZIO NA UNATAKA TUKUUNGE MKONO BILA KUSIKIA UPANDE MWINGINE.MYONGE ANYONGWE NA HAKI YAKE MPENI...KWANZA HAWA NDIYE ALIMDANGANYA ADAM AKALA TUNDA NA WEWE NI MWONGO TU TENA INABIDI TUKUPELEKE SOMALIA UKAJIBU MIMBA HIZO ULIZIPATA KWA UTARATIBU GANI.UNGEKUWA HUNA WATOTOT NINGEKUOA LAKINI SINA MIPANGO YA KUNUA MELI NA MABAHARIA WAKE TENA WA NAIJERIA,NUKSI TUPU!

    ReplyDelete
  44. hivi ninyi wanaume mnaomsakama kuwa anafuata mali mna akili kweli. mbona ninyi wengi wenu hamna mapenzi ya kweli.sasa mnataka afanyeje? acheni ujinga. mmezidi sana siku hizi. na hiyo ndio dawa yenu. mmekua mabahili kama nini siju.na mbado mtakoma. tutawachuna mpaka mifupa. maana mnajifanya vijogoo sana. waangalie kwanza. ovyooooooooo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...