Serikali imesema vitambulisho vya Taifa vitaanza kutolewa rasmi mwaka huu na mchakato wa kumtafuta mkandarasi unatarajiwa kukamilika baada ya miezi minne kuanzia sasa.
Pia katika hatua nyingine, imeahidi kufanya kila iwezalo kuhakikisha wauaji wa maalbino wanadhibitiwa, na hadi sasa watuhumiwa zaidi ya 100 wamekamatwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, juu ya mafanikio ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ya miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Nne, Waziri Lawrence Masha, alisema tayari michakato muhimu juu ya vitambulisho hivyo imekamilika
Habari kamili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Passport zetu wengine wanatuzengua na kuzipoteza tu moto utawaka kwa hivyo vitambulisho vya taifa.

    Anatajirishwa tu mtu hapa. Wale wa bibi wa kule mndenyi si wataibiwa vitambuliso vyao na wasomalia na wakenya?

    ReplyDelete
  2. Mimi naomba kutoa ushauri wangu kwa serikali, nasio serikali bali ni watanzania ambao wamepata dhamana ya kusimamia serikali yetu!

    Naomba kusema kwamba huundio wakati wakua makini sana! ikibidi watu waelimishwe nini maana yakua navitambulisho hivyo!

    pili,watu watakao kua wanaendesha hili zoezi wawe makini sana nasije kula rushwa, kwasababu kuna watu nje ya nchi yetu wanavitaka sana hivi vitambulisho kwahali na mali, mabalozi wa nyumba kumikumi, na makatibukata, inabidi waelimishwe sana kwasababu najua watatumika katika kumtambua mzawa na asye mzawa,especialy kwa wale ambao hawana vyeti vyakuzaliwa.
    tatu,kitengo kitakacho kabidhiwa zoezi hili, kifanye kazi kikijua kwamba kuna wakenya na waganda na watusi nchini kwetu na wata vitaka hivi vitambulisho!
    nne,hivi vitambulisho viwe na social security number kama wamarekani wanavyo fanya, ilikuja kubaini waarifu, na kubaini wazawa na wasio wazawa.

    Tanzania bado hatujawa makini katika swala la kusimamia,mambo yamsingi,watendaji waserikali bado hwajajijua kama wao niwatanzania na wanamajukumugani kama watanzania,kwahiyo huu niwakati wakua makini nasula hili.

    Wtendaji wakitengo kitakacho husika na hivi vitambulisho wasipokua makini watajikuata wanapatia waganda nawakenya na wanyaruanda hivi vitambulisho.

    SASA KAZIKWETU WOTE, WATUMISHI WA SERIKALI MJUE NYIE NI WATANZANIA NA MJUE MNAJUKUMU GANI KWA TAIFALENU.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...