wadau sina zawadi ila naomba nichemshe bongo kidogo. unawakumbuka wakongwe hawa?


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Kaka huyo mrefu kati ni Mtemi Ramadhani.

    ReplyDelete
  2. Hivi waliwahi kucheza mpira hawa?

    ReplyDelete
  3. Ni Khalid Abeid aliekuwa simba, na wakati ni Mtemi Ramadhani wa simba na wa mwisho ni mchezaji wa cosmopolitan ya sikikuu kariaakoo kwa jina ni Jamil.

    ReplyDelete
  4. khalid abeid, mohamed bakari 'tall', abdul amasha.

    ReplyDelete
  5. DU MWANANGU MWENYEWE...UMENUKUMBUSHA MBALI..HAWA JAMAA WALIKUWA WANAPIGA MPIRA ILE MBAYA SIO KAMA WAKINA MWAIKIMBA WENU WA MIAKA HII..

    WELL KUTOKA KUSHOTO NI KHALID ABEID HUYU ALIKUWA NI KIUNGO WA SIMBA NAMBARI SITA..EBWANA JAMAA MPIRA ALIKUWA ANAUKANYAGA ILE MBAYA NA BAADAE ALIKWENDA UARABUNI.

    KATIKATI NI MTEMI RAMADHANI JAMAA ALIJIUNGA NA SIMBA AKITOKEA WAZIRI MKUU YA DODOMA..HUYU JAMAA ALITIA FORA KWANI ALIJISAJIRI TIMU NNE WAZIRI MKUU, PAN AFRICA, SIMBA NA YANGA NA MATOKEO YAKE AKAPIGWA LUPANGO HADI 1982 NDO AKAANZA KUKIPIGA SIMBA.

    KULIA NI JAMIL HIZAM "DENNIS LAW" JAMAA ALIKUWA ANAKIPGA YANGA NA COSMO ALIKUWA NI WINGA WA KULIA. YEYE ALIKUWA MDOGO SANA KULIKO WENZAKE NA ALIKUWA AKIONEWA SANA UWANJANI KWA KUPIGWA BUTI KWANI ALIKUWA NA CHENGA SANA ALIKUWA WINGA NO 7 NAE AKAENDA UARABUNI. HUYU JAMIL AMEMUOA DADA YAKE KHALID ABEID.

    NDIMI MZEE WA LIVERPOOL..WATU TUNA DATA MSIFIKIRI MPIRA TUMEANZIA UKUBWANI...AFU NYIE MAN KITI CHETU MTAACHIA WENYEWE

    ReplyDelete
  6. Swali? Khalid Abedi andi Haidari, mchezaji mwingine wa simba ambaye alitia fora ktk miaka ya sabini, ni ndugu? Yuko wapi huyu Haidari?

    ReplyDelete
  7. Hao ni michuzi na michuzi Jr na wakatikati ni Mjengwa wa kilolo-Iringa. Upo hapo?

    ReplyDelete
  8. Huyo ni balazo wa ze-nanii na mkuu wa wilaya ya kujipakazia. Na wa kulia ni Mgaya Kingobaa wa Masuguru, Muheza-Tanga.

    ReplyDelete
  9. kutoka kulia ni amuri azizi zamani alikuwa anachezea malindi zenji, kati ni twaa amidu (simba}kulia Rosta Ndunguru aliyekuwa anachezea nyota nyekundu,
    Mdau kariakidevu ahaa!!! sorry! kariakoo!!!!!

    ReplyDelete
  10. Huyu wa katikati anafanana na Pro J. na huyo wa kushoto ni Juma Nature. Au mnasemaje wadau?

    ReplyDelete
  11. Wengi mnaosoma blogu hii mlikuwa hamjazaliwa au labda mlikuwa bado mnavaa nepi wakati mababu walipokuwa wakikipiga ujanani mwao. kushoto KHALID ABEID (Simba), Kati ni HAJI LESO (Simba) na JAMIL HIZAM (Cosmopolitan).

    ReplyDelete
  12. Jamil Hizam yuko Dubai ameisha staafu mpira.Sasa ni kikongwe.Hakumuowa dada yake Khalid Abeid ! ! Amemuowa dada yake Abdul-Karim Mafish ambaye pia alikuwa mchezaji wa Cosmo lakini myaka mingi baada ya Jamil kuondoka.Haidar Abedi pia yuko Arabuni Sharja.Yeye pia ameisha acha mpira, umri wake mkubwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...