picha za sikinde katika baadhi ya safari zao nyingi za ughaibuni.
mwanzo ilikuwa kama utani pale redio mbao zilipoanza kutangaza kwamba wamiliki wa bendi ya mlimani park orchestra wana sikinde ngoma ya ukae, shirika la mandeleo mkoa wa dar (DDC) wako njia moja kuivunja bendi hiyo kwa kile kilichosemekana kwamba ni mzigo kwa shirika hilo. wiki hii imethibitika kwamba habari hizo za kutia uchungu ni za kweli.
hivi tunavyoongea wanamuziki wa sikinde ama nginde nginde hawana ajira, ila inasemekana mwajiri wao amewapa mkono wa dhahabu kwa kuwakabidhi vyombo vya muziki wakajiajiri wenyewe, kama ilivyo msondo ngoma band ambao walijikuta katika jahazi kama hilo baada ya mwajiri wao, jumuiya ya wafanyakazi, kuitema.
Macho na masikio ya wapenzi wa muziki yanangoja nini kitachofuata, japo wengi wana imani kwamba sikinde haitokufa kutokana na kusheheni nyota wa muziki kama vile hassan rehani bitchuka 'super stereo, na mkongwe shaaban dede.


Kwa kweli kifo cha sikinde kinanitia machungu mno.Enzi zao hawa jamaa wakati wakipambana na watani wao wa jadi Juwata/Ottu Jazi, walikuwa wanatandika muziki sio mchezo. Kwa kweli mpambano ulikuwa mkali sana. Nikikumbuka nyimbo kama vile Najuta, Ukitakufurahi (wanasikinde), Mume wangu Jerry,Kipenzi changu Edita, Uzuri wa mtu sio sura,MV Mapenzi, Neema na nyingine nyingi kwa kweli sitamani kuona hii bendi ikifa. I hope some will take courage and invest on this band.
ReplyDeleteHebu jaribu kukumbuka wimbo kama huu:
"UKITAKA KUFURAHI KILA JUMAMOSI,
NJOO UBURUDIKE NA WANA SIKINDE OYEE
...HAYA NDIYO MAJINA YA WANASIKINDE TUCHEZE LEO NGOMA YA UKAE".
Wimbo kama huu mpaka leo ukiusilikiza natamani kama dunia irudi nyuma kama miaka 25 hivi nijikute pale DDC Mlimani au Kariakoo nikishuhudia akina King Enock wakiisakata Ngoma ya Ukaye. Sio hivyo tu, hata ukisilikiza nyimbo zao zaidi ya burudani zilikuwa na mafunzo mengi sana ukilinganisha na nyimbo zetu ningi za siku hizi. Sijajua ni kwanini baadhi ya nyimbo za siku hizi zinakuwa hazina mwelekeo.Labda wadau watanisaidia, inawezekana niko "biased" kutokana na vionjo vyangu. wakati mwingine unaweza ukajikuta tangu wimbo unaanza mpaka unaisha hujajua mtunzi alikuwa anataka kukupa ujumbe gani.
Mdau
Cardiff
Hima Watanzania wenzangu sote ni mashuhuda tunaoshuhudia mwisho wa muziki wa dansi wa KiTanzania. Bendi mbili za mwisho za muziki wa dansi wa KiTanzania Msondo na Sikinde tunaziona zinavyoterekea.
ReplyDeleteInasikitisha sana tena sana kuona hata muhusika mkuu wa kulinda alama yetu ya kimuziki ndiyo muagizaji wa kwanza wa muziki wa nje (Acudo Impact).
Imekuaje Zanzibar wameweza kuilinda Ikhwan Safaa kwa zaidi ya miaka mia moja (miaka 100) lakini Bara tunadidimiza Msondo na Sikinde zisizo hata na nusu ya umri wa Ikhwan Safaa?
Hebu tuangalie Guinea, Senegal, Ghana, Kongo, Kameruni, Kenya na hata South Africa (hata Kaburu hakudimimiza Kwela, Mbanqaca nk) jinsi wanavyolinda muziki wao wakati siye tunauua muziki wa dansi wa kwetu. Hapa tusirukie Ulaya, Marekani zote mbili au Visiwa vya Karibia ambako muziki umekuwa mwakilishi wa nchi za mabara haya kwa kila hali.
Wizara ya Utamaduni, Taasisi ya Mfuko wa Utamaduni Tanzania, Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania (CHAMUDATA), Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TASUBA) mko wapi na mnafanya nini kuulinda muziki wa dansi wa KiTanzania?
Katika hali ya sasa hapa bongo hakuna kiongozi wa shirika la umma anayemudu kuwa na bendi au timu ya mpira na mambo mengine yakaendelea, sikinde wamejitahidi kumudu wenzao walishindwa siku nyingi. Ushauri wangu kwa wanamuziki wa sikinde waichukulie hali hii kama changamoto na wajiandae kujitegemea kama wasipoteteleka nina hakika watafanya vizuri zaidi kwa kuwa hakuna mshahara, juhudi zao ndio zitawapa fedha zaidi. Mwanzo siku zote ni mgumu, fateni nyayo za baba zenu MSONDO!!!!
ReplyDeletesikinde sasa fanyeni kweli kwa kuzirudia nyimbo zenu kama 'salamu toka kwa mama' n.k ktk CD na VCD.
ReplyDeleteMaana sasa mko huru kufanya vitu bila kuzongwa na uongozi wa DDC.
Mimi nina imani kwamba sasa Sikinde itazaliwa upya na kufanya maajabu zaidi katika ulimwengu huu wa muziki hivi sasa wakiwa huru na wanajiendesha wenyewe.Sikinde imesheheni Wakongwe wa Muziki wenye Vipaji visivyomithilika!Wana uwezo wa kujiongoza wenyewe kama Bendi.Na kwa kweli wamekuwa wakijiongoza wenyewe kwa kipindi kirefu hivi sasa.Kwa Sikinde kuwa Bendi binafsi sasa watakuwa huru zaidi kupata Mikataba ya Kibiashara na Makampuni Makubwa hapa nchini kama TBL na mengineyo bila ya mizengwe ya kikampuni hususan kampuni za umma.Na la muhimu zaidi ni kwamba sasa watanufaika zaidi kutokana na jasho lao kwasababu watayadhibiti Mapato yao na kila atakaye fanya vizuri atazawadiwa ipasavyo.SIKINDE ITADUMU MILELE!
ReplyDeleteWapenzi wa SIKINDE,, Msiwe na shaka. SIKINDE IPO HAI. Kilichobadilika ni jina tu,, sasa hawatakuwa DDC MLIMANI PARK,, bali watakuwa kama walivyoanza kabla hawajachukuliwa na DDC yaani "MLIMANI PARK ORCHESTRA" Sikinde Ngoma ya Ukae. Kwa hiyo,, Sikinde Ngoma ya Ukae iko na itaendelea kuwepo. Hivi dakika hizi tu, wanamuziki wa MLIMANI Park wametoka kwenye press conference, kuelezea haya ninayoyasema. Hii ni neema kwao, kwani sasa watajienedesha wenyewe, na sas TBL wanatoa udhamini wa millioni 700 kwao. TBL walikataa kutoa udhamini kama huo kwa vile ilikuwa chini ya shirika (DDC) lakini sasa wametoa. Kwa hivyo tegeemeni mambo makubwa zaidi na jambo la msingi zaidi ni kwamba SIKINDE IPO.
ReplyDeleteKazeni buti mtashinda tu, irudisheni nginde enzi zile za mlimani park.pale mwenge silent inn palikuwa apatoshi.
ReplyDeletemabegi ya kariakoo mtaa wa kongo!!
ReplyDeletemmenikumbusha mbaaali hahaaaaaa