hasheem thabeet doing his things
Michuzi,
Hasheem Thabeet amekuwa Player of the Week kwenye conference.
He is also considered for Player of the Year!
husky/hc-ap-mentop25,0,302695.story

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. IT'S ABOUT TIME JAMAA ATAPATA FEDHA KEDEKEDE HUYU

    ReplyDelete
  2. hongera sana hasheem mungu akubariki uzidi kupata shavu tunakuomba uongeze bidii sana kwenye hii fani yako maana ndo njia umeshapata ya kuwa milionea na kutupatia taifa letu sifa

    ReplyDelete
  3. Huyu chalii lazima atakuwa wa pili kuitwa na Commissioner David Stern siku ya NBA Draft kule NY, na hii ni kwa sababu Blake Griffin anayechezea Oklahoma University kama power forward anayetarajiwa kuwa drafted wa kwanza. Ame improve kimchezo (offense and defense) anapiga blocks “matawi” kama hana akili nzuri vile. Na kwenye offense kwa sababu ya size yake timu nyingi zina m double team kwa hiyo anachokifanya yeye ni kupokea pass na ku dish out kwa shooting guards kwenye perimeter ambao wanashoot three points au 2 point jumpers bila kuwa contested. Mfano mzuri ni ile mechi ya jana usiku dhidi ya Syracuse. Pia ukiangalia stats za ma best center wa college mwaka huu Hasheem ana average 4.2 blocks kwa game wakati center kama Luke Harangody wa Notre Dame ana average 1.0 block per game. Vile vile Hasheem ana average 11 rebounds kwa game. Ma analyst wa college basketball kama Dick V na Jay Bilas wote wa ESPN wanakubali kwamba kwa muda mrefu Hasheem amekuwa “underrated”. Ninatamani niwaone UConn na North Carolina wakicheza kwenye fainali za NCAA mwezi wa nne. Tyler Hansbrough vs. Hasheem Thabeet, na best coaches in college basketball Roy Williams vs. Jim Calhoun. Hii mechi itakuwa the best matchup. So Hasheem if you are reading this, we are routing for you and keep up the good work.

    ReplyDelete
  4. Kwanini picha zote anapiga akiwa mwenyewe, anacheza peke yake?

    ReplyDelete
  5. Hongera sana Hasheem kwa kuendelea kutesa huko. Wadau tunazidi kukuombea ufanikiwe zaidi na zaidi. Kumbuka usilewe sifa na inabidi ukaze buti zaidi ili uweze kupambana na vijana walioanza kucheza mchezo huo katika umri mdogo zaidi.
    NCAA ndiye msema kweli. Ukifanya kweli hapo na kuibeba timu yako ikatwaa ubingwa basi umejihakikishia moja kwa moja kuwa na pesa kama au kuliko mafisadi wa EPA au mzee wa vijisenti.

    ReplyDelete
  6. PhatLorenzo,

    Hashim ameiprove sana kwenye defense ila offense bado kidogo. Mie nataka arudi Senior year amalizie shule. Mwakani akirudi atakuwa ameongeza chances zake za kuwa #1 pick. Kumbuka Tim Duncan alivyofanya, alimaliza na kuja kuanza ku-dominate NBA right away.

    ReplyDelete
  7. jamaa kweli yupo juuu nimeanga game ya jana kipindi cha kwanza tuu ana block 5 na rebounds 7 ila kwenye offense bado kidogo ila akilifanyia hilo moja kwa moja hana mpinza kwenye draft. na huwezi kuongelea NCAA bila ya kutaja jina la thabeet. kijana anatisha na akipata body kubwa kama yakina BYNUM atatisha na atakua noma. anajua sana defense na ndio nguzo ya ushindi ni kukaba.
    mshikaji PHATLORENZO unayosema yote sawa sawa

    ReplyDelete
  8. Anapigwa picha peke yake sababu anayeongelewa ni yeye!! That's artwork!! Ulishawahi kuona wanasema Ronaldo kachaguliwa mchezaji bora wa Ulaya halafu zikatolewa picha za Kikosi cha Man Utd?

    ReplyDelete
  9. swali alouliza annon apo kwanini hashimu anapigwa picha pekee ni zuri tuuu!!
    yan atakama aongelewa yeye basi japo siku ingine apigwe ktk angle zote na wezie karibu.wee annon unaeuliza eti nani sijui akitangazwa mchezaji bora akiwa uwanjan lazima atatokea na wezie japo na akiwa ukumbini pale mbele atatoka kivyake,,,khaaa tutajuaje??
    HONGERA SAAAAANA HASHIMU THABITI ZIDI KUTUWAKILISHA TZ

    ReplyDelete
  10. Msemakweli,
    ninashukuru kwa insight yako lakini napenda kutofautiana na wewe kidogo. Ikitokea Hasheem akawa drafted wa pili, tofauti ya hela kati ya 1st draft pick na 2nd draft pick ni ndogo sana. Amesha prove kwamba he's a beast kwa hiyo ni nafuu aende kuuza NBA wakati yuko hot na wakati UConn ina timu nzuri. What happens akirudi mwakani halafu akaumia, tuseme akavunjika mguu? Do you think atakuwa drafted higher? Hapana? Ataenda kuishia wale wanaokuwa drafted round ya pili. Vile vile kuna young talent kila mwaka. Uconn wakiwa bomu mwakani unafikiri kuna mtu atakuwa anamuongelea Thabeet tena? Halafu kuna madhara ya kukaa shuleni muda mrefu. Muangalie mchezaji wa North Carolina Tyler Hansbrough..he's one of my favorites. Kama Tyler angeondoka Tar Heels kwenda NBA akiwa Sophomore angekuwa kwenye top 5 pick. Leo hii anaingia NBA as a senior hakuna anayevutiwa naye. He's likely to be a 20th pick. Angalia stock yake ilivyoshuka ndani ya miaka miwili. Kama unafuatilia college football nafikiri utamkumbuka yule Quarterback wa USC Matt Lainert aliyeamua kubakia shuleni baada ya kushinda National championship na Heisman trophy. Scouts walikuwa wanasema Matt kama angeamua kwenda NFL angekuwa 1st draft pick. Hakufanya hivyo akarudi college kwa senior year. Next year 2005 USC wakapigwa bao na Vince Young na Texas kwenye championship game..Vince Young na Reggie Bush wakaonekana ni better players kuliko Matt Lainert. Leinart akawa drafted 10th overall.
    Ninachokisema hapa..na sikatai kwamba ukikaa shuleni miaka 4 lakini ni wachache sana waliokaa shuleni miaka 4 wakawa successful kwenye professional sports. Tim Duncan mmoja wapo.

    ReplyDelete
  11. The Kid Averaging 31.0mins, 13.7pts, 11rbs, 4.2blks per game alafu mnasema he can't play offense? hivi nyie mnaangalia sources gani kupata hizi news? manake kama tupo kwenye same page hapa hii webseite ya kwao inaongelea vitu tofauti kabisa, sio kuna watu wanakurupuka tu wanaanza kuongea ya kwenu, anacheza big east conference, one of the toughest conference in the world of college basketball, and he provides those kind of numbers everynight he goes out there.. y'all must be watching either wrong sources or just hating. whoever is questoning the kid ability naona ungejaribu kwenda kucheza basketball hata hapo kwenye mtaa wenu kama kuna mgoli ya kikapu alafu kjaribu kucheza hata kwa dakika kumi na tano uone shughuli ilivyo pevu. coach wake anasema one of the best he ever coached alafu mtu anachezeshwa dakika 31 kati ya dakika 40 za game nzima. anapumzishwa dakika 4 kila half. hivi nyie mnajua kinachoendelea? mimi nishaenda kwenye game zake, naangalia tv kila siku wanayoyasema hao watangazaji ni scary kwa jamaa kuwa mtanzania. Mungu Ibariki Africa, Mungu Ibariki Tanzania.
    http://sports.espn.go.com/ncb/player/profile?playerId=31559
    Big Up Hasheem, Mdau wa Chicago.

    ReplyDelete
  12. PhatLorenzo,

    Nakubaliana na wewe na point ulizotoa ni nzuri. Hashim atazidi ku-improve unless aumie kama ulivyosema. Mie mtazamo wangu ulikuwa kwake kielimu angalau amalize shule apate Degree yake. Nakuelewa kwenye issue ya Matt Lainert. Ila si unaona Vince yupo wapi sasa? Collins anarudi next year as a starter.

    Kuhusu Tyler Hansbrough, jamaa ameiva (ready to produce on NBA level right away)yule huwezi kumfananisha na Hashim sasa hivi. Kama umeangalia game ya juzi walivyomchapa Duke. Ni mchezaji pekee ambaye yupo 4-0 ndani ya nyumba ya Duke chini ya kocha Krzyzewski.

    Final ikiwa Uconn VS Tar Heels itakuwa ngoma ngumu. Hashim akimprove kwenye hiyo game D na offense basi mwache aende NBA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...