kikosi kamambe cha Bongo United FC
Skwadi la Houston Stars FC
Na Ripota wa Globu ya Jamii, Washington DC
Timu Ya Bongo United itawakaribisha kwa mara ya kwanza wapinzani wao wakuu,Houston Stars ndani ya Kapitali Washington Dc kwa mechi kali ya marudiano jumapili ya Mei 24.
Mara ya mwisho timu hizi zlicheza nov 29 mwaka jana na kutoka 3-3 kwa mechi iliyochezwa kwa dakika 120 kwenye sherehe za thanksgiving zinazofanyika kila november nchini Marekani.
Akithibitisha ujio wao timu hio,kocha mkuu timu hiyo ya Houston amesema timu itawasili washington Dc may 22 ijumaa usiku kwa ndege maalum na wanaendelea na mazoezi na mechi mbali mbali za kujinoa na mpambano huo.
Kwa upande wa Bongo United,kocha mkuu Gharib Latto,amesema timu imeanza mazoezi rasmi jana,na uongozi umeisha tuma barua za mwaliko wa mechi na timu za Senegal,Nigeria,Zambia na Malawi.
Amesema pia kutakua na mechi ya Simba na Yanga wiki mbili kabla ya mechi na Houston Stars na hii itakua mechi ya kwanza mwaka huu ya Simba kutaka kulipiza kisasi. Mechi hii pia itatumika kupima uwezo wa 'fundi' mpya waliyemleta toka Mlingotini, Bagamoyo, maalumu kwa kufunga vilomolomo.
Houston wanatarajia kuja na wachezaji 24, viongozi 2, 'mganga' mmoja na kocha mkuu wa timu hiyo.uongozi wa Bongo united fc unaikaribisha timu ya Housto stars fc kwa mikono miwili na kuwakumbusha wasisahau kuja na kombe atakalopewa mshindi wa mpambano huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Aah yaani hao DC wajiandae na kichapo kibaya sana kutoka kwe2 wazee wa D squad kwani sasa hivi 2po fiti kinoma na salaam 2meanza na watoto wa Kicongo na yoyote atakae tia timu ni kichapo tu.

    ReplyDelete
  2. MKUU WA WILAYA, TIMU HIZI NI KUONDOA MAUMIVU YA WIKI NA KUJARIBU KUPEANA MOYO KWA MAISHA MAGUMU NA UBAGUZI.ME NIPO ULAYA TUNAKITIMU KAMA HIVYO. TUNAISHI MAISHA YA UPWEKE SANA, BILA HIVYO HUPATI WA KUONGEA NAO UA HATA UMBEYA WA KIBONGO. KUPUNGUZA MAUMIVU KATIKA BARIDI KALI,BASI TWAKUTANA KAMA HIVYO. NI MAISHA YA KINYANI,LAKINI NDO HIVYO.
    HONGERENI WAPINZANI WWA HUKO ATI USA,POLENI KWA MAISHA MAGUMU USA.

    ReplyDelete
  3. hao houston valivyokuja wichita tuliwapiga goli 5 kwa mbili.ila to be honest wanajua soka.all the best guyz

    ReplyDelete
  4. Wanangu tuliyoyafanya ATL ,WICHITA.Pamoja na mazoezi yetu ya kitimu kila mtu afanye binafsi japo dakika 15 za kukimbia.Mpira mnaujua na mnafahamu kila mahali mkienda watu wanatulia,tutatoa starehe kama kawaida yetu.D SQUAD Moja moja

    ReplyDelete
  5. Timu ya Houston iko makini sana,nimeona wakicheza na wana uwezo mkubwa sana uwanjani.Kiutaalamu ukitaka kuona pambano zuri tafuta Game ya ATL na Houston.Wichita wana watu wachache wanaoujua,DC Kelele nyingi sana na ubishi usio na maana.Naamini DC ,watajirekebisha na kuelewa Game.

    ReplyDelete
  6. michezo ni furaha,ila gemu yetu na nyie ni ya kukata na shoka.Jiandaeni jamani!la sivyo ni mtachezea kichapo kibaya!!!

    ReplyDelete
  7. Hiyo Houston iliyokuja Wichita ni ya kujifagilia. Haikuwa timu ya Houston bali ni watu watatu tu waliokuwepo kutoka H-town mkaamua kusema mnacheza na Houston !! Vijana kwa daraja bado mpo chini,jaribuni njia nyingine !!

    ReplyDelete
  8. Huyo mwalimu mnayekuja naye ni mtaalam Shemdoe au?

    ReplyDelete
  9. nyie timu ya Houston mnacheza mpira na mdomo sana safari hii hamtoki mkija Dc msisahau kuja na ndege nyingine ya kubebea magori,na huyo mganga wenu tutaazima mganga wa simba kutoka mlingotini Bagamoyo amtie kilomolomo mganga wenu,mje vizuri Dc kiboko yenu

    ReplyDelete
  10. Houston,mnawafuata Bongo united kapitali mamaaa...mmekwisha hawa jamaa mnashindwa kuwafunga wanapokuja Houston na wanakua hawana lizevu hee...ushauri wa bure..msisahau kikapu cha magori hawa jamaa kila timu inayoenda Dc huondoka na mvua ya magoli,mwaka jana kwenye ligi africa cup wametolewa fainali na Nigeria tena kwa penati..haya kazi kwenu na goodluck

    ReplyDelete
  11. NYIE HOUSTON ONGEENI SANA FANYENI SANA MAZOEZI SISI DC TUNAKULA CHAMPAIGN TU NA TUNATUNGASHERIA. SI UNAJUA CAPITAL (CONGRESS) MKICHUNGULIA TU TATU (3). NAONA MMESAHAU MSIBA WA THNX GVN 2007 INDOOR MLIKUFA 8-4.

    SEE YOU MAY.

    IT IS WHAT ITS.

    ReplyDelete
  12. we anonymous wa tarehe 10 9.18am hicho ni kisingizio.nlicheza hiyo game na baada ya game nikaongea na wachezaji wa houston wakasema walitimia.kwa don't bring up excuses.tafuteni game tena kama vipi

    ReplyDelete
  13. HOUSTON MSHAELEKEA KIBLA ( MACCA) TUSHANOA KISU. DC TUNAKULA CHAMPAIGN TU SASA.

    ReplyDelete
  14. Jamaa wa Houston wanaumoja sana wakiwa uwanjani,wakiwa mazoezini utafikiri timu iliyo kwenye Ligi.Nilienda kutembea Houston nikaenda kuangalia mazoezi yao,kuna mtu mmoja nilimuona anapanga visahani,mara nikawaona wanakusanyika na kuanza mazoezi.Wako very organised

    ReplyDelete
  15. nijuavyo mimi mpira hautabiriki kwa kusema kuwa timu inayocheza nyumbani ni lazima iibuke na ushindi! hii sii kweli kila wakati!Mfano sisi houston tulikuwa nyumbani last year lakini tulilazimishwa sare na dc.Mwaka huu dc watakuwa nyumbani,sii ajabu wakashindwa hata kuambulia sare!(sitashangaa!)
    Mmeongea mengi ila kiundani yote ni majigambo tuu ndugu zangu... ooh mara mganga,...mara thanksgiving ya 2007,...ooh mara capital!yote hayo hayana uhusiano na mtu kumi na moja kwa kumi na moja,refarii mmoja na linesmen wawili!!
    Kuhusu ubora wa timu, ikumbukwe pia houston waishafika fainali ya mataifa ya Africa yaliyofanyika mara ya mwisho Houston 2006, na kupoteza mechi hiyo dhidi ya Cameroon(goli2-1)
    Naomba tusiibwabwaje sana ila tuombe uzima na inshallah! tutaonana graundi!

    ReplyDelete
  16. wote ni wapiga kelele tu si tunajua timu ni moja tu ATL Tanzanite Fc nyie wengine vitambi tu. ingieni kwenye ligi kama ATL sio kazi kucheza na wabeba mabox wenzenu. Tanzanite Fc tunawangoja kwa hamu nyumbani!! Mnafanya vizuri katika ligi.

    ReplyDelete
  17. ATL na nyie mna mcheza mpira na mdomo 85 north njia ya kuja Dc si mnaijua,karibuni oh ligi ligi,mmefungwa kwenye ligi mpaka mnaona uzia kuleta picha kwenye Glob ya Jamii na nyie Houston machinjioni panawasubili na tutaangalia passport ya kila mchezaji kabla ya mechi mambo ya kuchomekea wawest haitatokea tena

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...