JK akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kutua dar leo akitokea addis ababa, ethiopia.
JK AMWEKEA NGUMU MUAMMAR GADAFFI
Na Mwandishi Maalum,
Addis Ababa, Ethiopia
RAIS Jakaya Mrisho Kikwete jana, Jumanne, Februari 3, 2009, alizima jaribio la kubadilisha msimamo wa Umoja wa Afrika kuhusu mapinduzi ya kijeshi katika Afrika, akisisitiza kuwa kamwe hakuna mapinduzi yoyote ya kijeshi mazuri duniani.
Katika mchango wake uliokatishwa zaidi ya mara nne kwa makofi na mamia ya wajumbe waliofurika katika Ukumbi wa UNCC-ECA mjini Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa 12 wa Kawaida wa Umoja wa Afrika (AU), Rais aliwaomba viongozi wenzake wa nchi za Afrika kuwa wakweli katika kujadili masuala muhimu ya maendeleo na ustawi wa Afrika.
Rais Kikwete aliungwa mkono katika hoja yake na baadhi ya viongozi waandamizi wa Afrika akiwamo Rais Idriss Deby wa Chad, Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda, na Waziri Mkuu wa Ethopia, Zenawi Meles na hivyo kukatisha mjadala huo.
Rais Kikwete aliingia kati kuzima jaribio hilo baada ya Mwenyekiti mpya wa AU, Kanali Muammar Gaddafi wa Libya, akiungwa mkono na Rais wa Senegal, Abdoulaye Wade kuwasilisha pendekezo kwenye mkutano huo wa kuzirejeshea tena uanachama nchi za Mauritania na Guinea, ambazo zimesimamishwa kwa sababu ya mapinduzi ya kijeshi.
Katika mchango wake, Rais Wade alisema kuwa mapinduzi hasa ya Guinea ni tofauti na mapinduzi mengine ya kijeshi, na kuwa utawala wa kijeshi wa nchi hiyo unaungwa mkono na wananchi.
Rais Wade alitoa uzoefu wake kuhusu utawala huo wa Guinea baada ya kuwa ametembelea nchi hiyo na kudai kuwa aliona jinsi wananchi wa nchi hiyo walivyozitokeza kwa wingi mitaani kumpokea na kuonyesha kuunga mkono utawala huo mpya.
Majeshi katika nchi hizo mbili yalitwaa madaraka katika Guinea na Mauritania mwaka uliopita wakati wa uenyekiti wa Rais Kikwete, ambaye mara moja aliamuru nchi hizo mbili kusimamisha uanachama wa AU kwa mujibu wa maamuzi ya viongozi wa nchi wanachama wa AU.
“Nawaombeni wenzangu tuwe wakweli katika kujadili mambo haya. Ni rahisi sana kwa jeshi kuwapanga watu mitaani na wakashangilia. Na hilo haliweza kuwa msingi wa kubadilisha uamuzi wa msingi kabisa wa Umoja huu,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:
“Unaweza kufanya lolote ukiwa na bunduki, na niamini mimi kwa sababu nilipata kuwa jeshini. Chini ya utawala wa kijeshi, unaweza hata kuitisha kura ya maoni na kupata asilimia 99,9. Ndugu zangu hebu tuheshimu misingi mikuu ya Umoja wetu kama tulivyokubaliana.”
“Hakuna mapinduzi mazuri ya kijeshi, na lazima tukomeshe utamaduni wa mapinduzi ya kijeshi. Tusirudi nyuma katika miaka ile ya 1960 na 1970. Mtu anayetaka kuwa rais anatakiwa aingie katika siasa na kuomba ridhaa ya wananchi,” alisema, akisisitiza:
“Kama unataka kuwa Rais, unajiuzulu kutoka jeshini.. kama mimi nilivyofanya tena nikiwa na umri mdogo na sasa nimekuwa Rais. Isitoshe, hawa ni watu wanaosema kuwa watakuwa madaraka kwa muda mfupi…lakini angalia yule Lassana Conte wa Guinea aliahidi miaka miwili, akaishia akishikilia madaraka kwa miaka 24.”
Rais Kikwete, kwa hisia na ufasaha mkubwa alielezea historia ya mapinduzi katika Afrika, akitoa mifano ya karibuni zaidi ya mapinduzi katika nchi za Ivory Coast, Guinea, Madagascar na Mauritania. Mwishoni mwa mjadala hata Rais Gaddafi alibadilisha msimamo na kuunga mkono msimamo wa Rais Kikwete na wenzake.
Rais Kikwete aliungwa mkono mara moja na Rais Deby wa Chad ambaye aliwaambia viongozi wenzake: “Kama alivyosema Rais Kikwete, hakuna mapinduzi ya kijeshi mazuri. Tunapoteza muda tu kujadili jambo hilo ambalo tulikwishakulichukua uamuzi….tuache kuzungumzia suala hili, tunapoteza muda tu…”
Naye Rais Museveni alisema kuwa kazi ya jeshi ni kulinda amani ya nchi. “Sasa hawa badala ya kulinda amani ambao ndio wajibu wao wanajaribu kutawala nchi. Hakuna mapinduzi ya kijeshi mazuri na hayajawahi kutokea katika historia. Mapinduzi ya kijeshi ni jam bo lisilokuwa na maana. Ni jambo lisilokuwa na thamani.”
Alisisitiza: “Tokea mwaka 1963, tumekuwa na watu hawa wa kustajabisha…akina Idi Amin. Tutauua Umoja huu kwa mawazo na mijadala ya ovyo na ajabu kama hii. Tuyakatae mapinduzi katika Afrika…na kwenye hili tuko tayari kutofautiana. Hatuwezi kamwe kuzikubali Guinea na Mauritania kurudisha wanachama mpaka zitimize masharti.”
Museveni alisema kuwa yeye ana uzoefu wa kutosha wa kuendesha Serikali zote mbili, ya kijeshi na iliyoingia madarakani kwa kuchaguliwa na wananchi.
“Niamini mimi. Nimekuwa hata mpiganaji wa misituni (rebel). Lakini mchakato wa uchaguzi ni mzuri, unawalazimisha viongozi kufanya kazi. Lakini watu kama Gaddafi wanaukejeli…Ni muhimu kuwapo uchaguzi. Mimi nimeongoza serikali zote mbili, ya kijeshi na isiyokuwa ya kijeshi, najua ninachokisema,” alisisitiza Rais Museveni.
Naye Waziri Mkuu Meles alisema: “Pengine masuala haya ni muhimu lakini siyo ya lazima. Sisi ni viongozi tuache kushinda tunazunguka tu kuhusu hoja zisizokuwa na msingi na kuhusu suala ambalo tayari limeamuliwa. Tuwe na ajenda, vinginevyo tutakuwa sawa na wasusi wa nywele wa jadi katika Ethiopia, ambao kwa sababu wana muda tokea asubuhi hadi jioni, na kwa sababu hawana ajenda, huzungumzia jambo lolote linaloingia kichwani.”
“Hii ni mikutano ya kuzungumzia mambo muhimu na ya maana. Siyo nafasi ya kuja na kupiga picha kwa baadhi ya viongozi,” alisema Meles.

VIONGOZI HAWA WANATIA MOYO KWELI, WANATAKIWA KUHAMISHIA MIJADARA YA AINA HIYO, ISIYOKUWA NA UNAFIKI KATIKA KUPIGA VITA RUSHWA, MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA NA WIZI YA MALI YA UMA.SIO SIKU NYINGI AFRIKA BORA KULIKO ULAYA INAKUJA, NA VIJANA WETU WANAOKIMBILIA KUWA WATUMWA WA WAZUNGU ULAYA WATARUDI NYUMBANI.
ReplyDeleteMUNGU IBARIKI AFRIKA
Kaka Kikwete hii ilikuwa POINT nakufagilia.
ReplyDeletesasa Afrika mkubaline juu ya Kuimarisha haki za Binadamu na kukuza misingi ya Demokrasia.
Pia wezi wa Kura kama akina Mwai na Robert Mgabe nao wafukuzwe kwenye Umoja wenu.
Huo ndiyo msimamo unaotakiwa kuonyeshwa na viongozi wetu wa Afrika na siyo kuwa kigeugeu. JK sasa muda unao, naona sasa ni wakati wa kumrudia CHENGE (mzee wa vijisenti) na wenzake kwani tayari ushahidi dhidi yao unatosha kuifanya serikali yako kuchukua hatua. Pesa walizoiba ni nyingi sana kiasi kwamba zikirudishwa tunaweza kununua matreka mengi tu pamoja na zana zingine za kilimo
ReplyDeleteHongera sana Rais Kikwete kwa kuwashushua hao mashabiki wa mapinduzi ya kijeshi. Hakika umetujengea heshima zaidi. Hawa akina Wade and Gadhafi wanataka kuturudisha katika Afrika ya Mobutu, Amini, Bokassa na wawauwaji wengine waliolikwamisha bara Afrika.
ReplyDeleteUmefika wakati wa kudumisha hawa wanaojifanya masultan wa Afrika kuanza kuheshimu demokrasia.
MBONA KILA MTU KACHUNA? xxxxxx tuuu!!!
ReplyDeleteJK ametoa point. Ukiwa na bunduki unaweza kufanya watu wafanye lolote unalotaka!!!
ReplyDeleteHiyo point ya JK mimi iko naunga mkono lakini hao waliochangia wote wanafiki tu. Deby, Museveni, Zenawi, wote waliingia madarakani kwa mapinduzi, na chunguzeni vizuri wanavyoendesha nch zao. Yaani hapo wamechangia tu kwa sababu wanafahamu fika nchini mwao kuna a lot of people ambao ni unhappy, kwa utawla wao wa kijeshi. Bora hata Ghadaffi hakua mnafiki. Huyo wa Senegal ndio namshangaa maana naskia ni mwanasheria mzuri tu, na pia amechagulia kidemokrasia. hivi kesho akipinduliwa atajiskiaje.
ReplyDeleteKuna wakati mapinduzi ya kijeshi yanasaidia kuondoa viongozi ving'ang'anizi kama kina Gadaffi, Museveni, Mugabe na wengineo wa dizaini hiyo. Bila mtutu wa bunduki wataendelea kubaki madarakani bila ridhaa ya wananchi kwa kujidai eti wamechaguliwa na wananchi.
ReplyDeleteHakika kipindi hiki tulipata bonge la President. Kumbuka kufikia hapo alifanya kazi ya ziada mpaka alikuwa mwanajeshi. Na sii hivyo tu kushikika nafasi mbali mbali katika serekali. Nilimvulia kofia kabisa Nyerere alipomnyima ushindi na kumwambia wakati wako bado na alisubiri. Mzee kwa hayo yote tunaku-admire na kukuvulia kofia. kwa mtu yoyote anayetaka kuwa kiongozi kuna mengi sana ya kujifunza toka kwa CV ya President wetu. Kuandika kiingereza kwenye blogs ni kitu kizuri kwasababu ni lazima tuwe level moja na wezetu duniani lakini pia actions speaks louder. Unaweza angalia CV ya president wetu from http://en.wikipedia.org/wiki/Jakaya_Kikwete
ReplyDeleteSasa Mzee JK tunaomba katika majukumu mengine muhimu ambayo yanalikabili hili taifa ni MAFISADI. Na hizi kesi zipewe umuhimu unaostahili ziende haraka.
jk umeonyesha msimamo,huo ni msima wa siku nyingi toka enzi za julius nafikiri nyerere jk angekupa 100 percents,tunataka misimamo kama hiyo idumu ktk siasa zetu,huyu gadafi asilete kutuburura na unafiki wake tena ana history chafu ktkt siasa za africa,dikteta,kitu kingine hapa lazima kiwekwe kielezwe bayana ktk mhula wake wa uenyekiti wa AU hasa huu muungano wa africa ni lazima viongozi wetu wawe makini katika kupitisha maiswada maana anaweza kuwatumia kama silaha yake dhidi ya maadui wake ,au kuwa support vibaraka wake kuweni makini wakina jk!!!
ReplyDeleteMAPINDUZI WAKATI MWINGINE NI LAZIMA KUONDOA MFUMO WA UONEVU KAMA MAPINDUZI YA ZANZIBAR 1964.ANGALIA WATU WANAKUFA KENYA NA ZIMBABWE CHINI YA NENO MOJA DEMOKRASIA MUGABE NA KIBAKI WAMEUA WATU WENGI ILI WAZIDI KUKAA MADARAKANI WAKATI GUINEA NA MAURITANIA HAKUFA HATA MTU MMOJA WAKATI VIONGOZI WALE WA KIJESHI WAKITWAA MADARAKA JE NI LIPI BORA?USHINDWE KWA KURA KISHA UIBE WATU WAFE AU MWANAJESHI WATWAE MADARAKA BILA KUMWAGA DAMU KUONDOA VIONGOZI DHALIMU?
ReplyDeleteHakuna lolote! Hawa viongozi wa Kiafrika wameamua kulindana tu..Mapinduzi ni kitu ambacho hakuna mtu duniani anakipenda lakini kuna wakati ni lazima.. Kama sivyo, basi nchi zaidi ya 40 za Afrika zisingepata Uhuru wake..
ReplyDeleteHaiwezekani Mapinduzi kuwa suluhu tu kwa kumwondoa mkoloni lakini kiongozi mshenzi wa kiafrika tutumie huruma na ujasiri kwa kutumia umwagaji damu.. Hao wazungu hawakuwa na damu?.. hao babu zetu waliopigana majimaji hawakuwa na damu..
Acheni ushabiki, mtu kama Mugabe anatakiwa kuondolea hata kama Mapinduzi ndio solution ya mwisho!..Na tutampongeza yewyote atakaye weza kumwondoa madarakani akam alivyoondolewa Ian Smith..
Congrats Mr.President.Your excellency.Mheshimiwa Rais nina uhakika unasoma hii blog.Hata mimi binafsi sipendi mapinduzi ya kijeshi lakini angalia sasa mtu kama Mugabe(Robert),rais wa Zimbabwe.Huoni kwamba hata baadhi ya nyie marais mnasababisha haya mapinduzi?.I am talking about kung'ang'ania madaraka.N
ReplyDeleteKwa kweli namfagilia sana rais wetu kwa msimamo wake katika kikao hicho cha Addis na kile kikao kilichofanyika SA kujadili mambo ya Zimbabwe. Inaonyesha wazi kwamba ukiwa mkweli na ukadiriki kusimama katika huo ukweli, basi wengine nao watakuunga mkono. Hongera sana baba JK!
ReplyDeleteNi ukweli pia kwamba mapinduzi yanaweza kuwa solution kwa kuwaondoa viongozi wanaong'ang'ania madarakani na kuwaumiza wananchi. LAKINI kinachosemwa na AU ni kwamba baada ya hayo mapinduzi, ni vyema hao askari wakakabidhi serikali kwa wananchi kwa kufanya uchaguzi wa kidemokrasia as soon as possible. Baada ya kufanya hivyo sioni kwa nini nchi hiyo haitakubalika AU.
Kwa sasa inabidi viongozi wetu wa Kiafrika kuwa macho sana na Mwenyekiti mpya wa AU maana ana tabia ya kutaka kuwaendesha watu kidikteta. Hata hongo atawapa! We ngoja utajaona...
Mkuu,
ReplyDeleteHabari hii vipi?
Kwanza, imeandikwa na mwandishi maalumu.
Pili, hailezi ni katika kikao gani cha AU ambacho malumbano haya yalitokea.
Tatu, ajabu ya ngamia kucheka nundu ya ng'ombe: eti Museveni na Melesi Zenawi wanampinga Gadafi? Halafu Chad leo inaweza kusimama kidedea kulumbana na Libya? Chad washasahau waliyofanyiwa na Libya?
Nne, malumbano hayakumakinikia mantiki nzima ya jeshi kuchukua madaraka Guinea na Mauritania? Je Guinea yalitokea mapinduzi?
Tano, si kila mapinduzi ya kijeshi ni haramu. Tukichukulia mifano ya mapinduzi ya Libya Gadafi alipompindua Mafalme Idris na Rawlings kule Ghana alivyowapindua kina Akufo na Limann na hata Liberia Doe alipompindua Tolbert na hata Ethiopia Mengistu alipompindua Haile Selasie kulikuwa na sababu za kimsingi kabisa za kufanya mapinduzi yale.
Sita, nanukuu
“Unaweza kufanya lolote ukiwa na bunduki, na niamini mimi kwa sababu nilipata kuwa jeshini. Chini ya utawala wa kijeshi, unaweza hata kuitisha kura ya maoni na kupata asilimia 99,9. Ndugu zangu hebu tuheshimu misingi mikuu ya Umoja wetu kama tulivyokubaliana.”
Nina mawazo tofauti na nukuu hii
kuwa na bunduki hakukupi nguvu ya kufanya lolote. Ujuzi wa kuitumia bunduki unaweza kukupa nguvu ya kuua, kuumiza, kutishia na hata kutuliza ghasia. George Jackson alisema the strong can rule the weak but the wise can rule the strong. Kwa hiyo unaweza kuwa na bunduki na ukawa si lolote wala chochote mbele yta wenye busara mfano wa Marekani na Vietnam.
Zaidi, wapo wanaopata kura za asilimia nyingi bila kuwa wanajeshi na waliingia madarakani kwa mapinduzi kama vile kina Omar Bongo wa Gabon au kwa demokrasia za kimtindo wa mbio za kupokezana vijiti wa Botswana wa kina Sir Seretsi Khama, Sir Kotimire Masire, Dr Festus Mogae halafu Generali Seretsi Khama Jr. Tukivuka mipaka ya Afrika tuna mifano ya kina Ayatollah Khomeini kule Iran na mapinduzi ya 1978 na Kadinali Sin dhidi ya Ferdinand Marcos kule Ufilipino.
Mkuu, ngoja niishie hapa. Kila la heri kwa siku ya kuzaliwa Azimio la Arusha na Chama cha Mapinduzi.
Ni mimi jamaa yako.
tumefurahi kusikia umoja wa afrika wamekubaliana kwa jambo1 hakuna mapinduzi mazuri popote. je katika kuchangia hilo,mbona tumesikia viongozi 4 tu wengine viongozi hawakuwa na la kusema?nadhani walikuwepo viongozi zaidi ya 40 mbona wengine hatukusikia msimamo wao? ni hilo tu swali langu nawashkulu sana kwa kutupa informaion ya addis
ReplyDeleteKaka Michuzi,
ReplyDeletemimi sichangii hoja maana JK ni Rais hilo halina ubishi na ameongea point.
Sasa shida yangu ni moja tu huyo "bodigad wake aliyevaa black hapo sio siri kila nimuonapo kwenye picha au television moyo yangu puuu!!! nisaidie. Kama ameoa basi mwache tu sina ujanja.